Sunday, 12 July 2020

Angalia Picha : RAIS MAGUFULI AKIWA NA WASANII MBALIMBALI IKULU CHAMWINO DODOMA...DIAMOND, ALIKIBA, HARMONIZE...


Na Alex Sonna,Dodoma
WASANII wa mziki wa Bongo fleva wamempagawisha Rais John Magufuli katika hafla ya chakula cha mchana na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) iliyofanyika Ikulu ya Chamwino.

Katika hafla hiyo, wasanii mbalimbali akiwemo Alikiba, Daimond Platnumz, Hamonize, Nandy, Zuchu, MwanaFA, Lavalava, kundi la Magufuli Gang likiongozwa na Shetta, Dogo Janja, Mrisho Mpoto, Bob Haiza,Rayvanny, Mbosso,Marioo, kundi la TOT na wasanii wengine, ambapo walipata fursa ya kutumbuiza na kukonga nyoyo za wajumbe wa mkutano huo.

Akizungumza namna alivyofurahishwa na mziki wao, Rais Magufuli amesema yeye ni shabiki sana wa nyimbo na huwa anafurahi sana.

“Nawashukuru sana wasanii kweli nimejisikia raha, unapomuona Alikiba amekaa pamoja na Daimond wamekaa pamoja unaiona nguvu ya CCM, leo unapomuona Harmonize aliyemkimbia Daimond anamsifia hadharani huu ndo utanzania ninao utaka, nawashukuru sana wasanii, asanteni sana kwa kuunga mkono Chama cha Mapinduzi,”amesema.

Amewataka waendelee kuitangaza Tanzania wasikate tamaa na kuwahakikishia siku zijazo mambo yatakuwa vizuri.

“Huwa nafurahi na nafuatilia kweli sijui nyimbo za Nandy za nani, endeleeni kuitangaza Tanzania, msikate tamaa tupo pamoja na nyinyi, endeleeni kukinadi Chama cha Mapinduzi, nataka kuwahakikishia siku zinazokuja mambo yatakuwa mazuri zaidi, nawashukuru mameneja wenu wote nawashukuru na waigizaji na wanamichezo wote kwa kazi kubwa ya kutangaza nchi yetu,”amesema.

Ameongeza “Kitendo mlichoonesha leo mkaoneshe hivyo hivyo, mapatano mliyofanya leo yakapate na nguvu ya Mwenyezi Mungu, ninyi ni vijana mmeanza vizuri nendeni hivyo na Mungu atawajalia zaidi.”

Tazama hapa chini Matukio katika picha ,Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya kumbukumbu na wasanii waliofika pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho kutembelea Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Julai 12, 2020


 

Share:

SIMBA SC YAITAFUNA YANGA UWANJA WA TAIFA...SASA KUKUTANA NA NAMUNGO FC FAINALI


Kiungo wa timu ya Simba, Gerson Fraga akishangilia kwa kunyoosha mikono juu baada ya kuifungia timu yake bao la kwanza.

Na Damian Masyenene -Shinyanga Press Club Blog
TIMU ya Simba SC leo imefanikiwa kusonga mbele na kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) maarufu kama Kombe la FA, baada ya kuwachapa watani wao wa jadi, Yanga SC kwa mabao 4-1 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa leo saa 11 jioni katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba wamengia kwa nguvu kubwa katika mchezo huo wakihitaji kulipiza kisasi cha kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu Machi, mwaka huu, ambapo wameutawala mchezo huo wakitandika kandanda safi na kupoteza matumaini ya wapinzani wao kupata ushindi.

Mabao ya Simba yalifungwa na Gerson Fraga mnamo dakika ya 14, Cloutous Chama (49), Louis Miquissone (51) na Mzamiru Yassin (88), huku bao la kufutia machozi la Yanga likipachikwa nyavuni na Feisal Salum ‘Fei Toto’ katika dakika ya 70.

Kufuatia ushindi huo, Wekundu wa Msimbazi Simba watakutana na Namungo FC ya Lindi katika mchezo wa fainali wa michuano hiyo mwanzoni mwa mwezi Agosti, 2020 katika uwanja wa Nelson Mandela, mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Namungo FC ambao ni msimu wao wa kwanza kwenye Ligi Kuu, walitinga hatua ya fainali jana Julai 11, 2020 baada ya kuwanyuka Sahare All Stars kwa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.

Share:

Mkutano Wa Baraza La Mawaziri Wa Fedha Nchi Za SADC Kuanza Kesho Dar Es Salaam

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, anatarajiwa kuongoza Mkutano wa Mawaziri wanaohusika na masuala ya Fedha na Uwekezaji wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jopo la Mapitio ya Uchumi Mpana (Peer Review Panel) unaotarajiwa kufanyika tarehe 15 Julai 2020 kwa njia ya mtandao kutokea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Dar es salaam.

 Mkutano huu utatanguliwa na kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara za Fedha na Benki Kuu wa SADC, utakaofanyika kwa siku mbili kuanzia kesho tarehe 13-14 Julai, 2020.

Mkutano huu ambao utawakutanisha Mawaziri wenye dhamana na masuala ya Fedha na Uwekezaji na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi 16 wanachama wa SADC, utajadili masuala ya Fedha na Uwekezaji pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji wa maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji katika mkutano uliofanyika mwezi Julai 2019, Windhoek, Namibia.

Vilevile mkutano huu utajadili kwa kina na kutoa maamuzi ya kisera kuhusu athari za Kiuchumi na Kijamii za COVID-19.

Mkutano huu ulipangwa kufanyika ana kwa ana kuanzia tarehe 13-17 Julai, 2020 lakini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19), utafanyika kwa njia ya mtandao kuanzia tarehe 13 hadi 15 Julai, 2020 .

Mkutano huu ni utekelezaji wa maelekezo ya Mkutano wa dharura wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika tarehe 18 Machi 2020, Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, ulimuelekeza Mwenyekiti wa Baraza kwa kushirikiana na Sekretarieti ya SADC kusimamia zuio la kufanyika kwa mikutano ya ana kwa ana kutokana na mlipuko wa COVID-19.

Imetolewa na
Benny Mwaipaja
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO


Share:

Wizara Ya Ardhi Yawasilisha Taarifa Ya Vijiji Vyenye Migogoro Maeneo Ya Hifadhi Kwa MARC

Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewasilisha taarifa ya utekelezaji maagizo ya kutoondolewa vijiji 920 kati ya 975 vilivyokuwa katika migogoro maeneo ya hifadhi nchini kwa Wakuu wa mikoa wa Tanzania Bara.

Uwasilishaji taarifa hiyo umefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo jijini Dodoma mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Wataalamu kutoka wizara za Ardhi, Ofisi ya Raisi TAMISEMI, Kilimo, Mifugo, Maliasili na Utalii, Maji na Makamu wa Raisi ambazo Mawaziri wake walitembelea maeneo yenye mgogoro na kuja na mapendekezo yaliyosababisha Rais kuchukua uamuzi huo.

Awali wananchi waliokuwa wakiishi kwenye vijiji vya hifadhi walionekana wavamizi wakati serikali ilitoa hati za usajili kwa vijiji na wananchi wake kushiriki shughuli mbalimbali zikiwemo za uchaguzi jambo lililomfanya Rais John Pombe Magufuli kuchukua uamuzi wa kuvibakisha vijiji 920 baada ya kupata ushauri wa mawaziri wa sekta husika.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha taarifa hiyo kwa Wakuu wa Mikoa ya Tanzania Bara Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo alisema, utekelezaji maamuzi ya kutoondolewa vijiji 920 ni wa awali huku kazi kwa vijiji 55 vilivyosalia ikiendelea ambapo alisema itahusisha Wakuu wa mikoa, wilaya na wataalamu wengine.

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi William Lukuvi aliwaambia wakuu hao wa mikoa kuwa, uwasilishaji taarifa ya utekelezaji maagizo yaliyofikiwa kuhusiana na vijiji 920 unafanyika kwa kwa lengo la kuwafahamisha ni vijiji gani vimefutwa na ipi ya kupunguzwa katika maeneo yao.

‘’kazi ya kubakisha vijiji kwenye maeneo ya mgogoro katika hifadhi imeanza na lengo hapa ni wananchi wasiishi kwa hofu na ninyi kama Wakuu wa mikoa lazima mfahamishwe ili kujua ni misitu gani imefutwa na ipi imepunguzwa’’ alisema Lukuvi

Kwa mujibu wa Lukuvi, wizara yake imeona ni wakati muafaka kuiwasilisha taarifa ya utekelezaji maagizo hayo kwa wakuu wa mikoa kutokana na wao kuwa na mamlaka katika maeneo yao na kuongeza kuwa pamoja na Wizara hiyo kushughulika na migogoro kwenye maeneo ya hifadhi lakini itaendelea kushughulikia migogoro mingine kwa utaratibu wa serikali.

Hivi karibuni Waziri Lukuvi alisisitiza kufanyika uchambuzi wa kina wakati wa utekelezaji maagizo hayo ili kuja majibu yatakayokidhi malengo ya uamuzi uliofanyika ambapo alisema  wakati kazi ya uchambuzi ikiendelea wasimamizi wa sheria wanapaswa kuendelea kusimamia sheria na kuwatahadharisha kuwa makini wakati wa utekelezaji majukumu yao ili kuepuka uvunjifu wa amani.

Kwa muda mrefu wananchi wa Vijiji 975 vilivyo katika hifadhi wamekuwa katika mgogoro kwa kudaiwa kuwa wavamizi na kusababisha nyumba zao kuchomwa moto huku baadhi yao wakiwa wameishi maeneo hayo kwa zaidi ya miaka ishirini.

Mgogoro huo ulisababisha Rais John Pombe Magufuli kuingilia kati na kuridhia vijiji 920 kubaki maeneo ya hifadhi sambamba na kufutwa misitu ya hifadhi saba yenye ukubwa wa ekari 46,715 ili ipangwe upya. Pia Rais Magufuli alifuta mapori tengefu 12 yenye ukubwa wa ekari 707,659.94 na ardhi hiyo kugawiwa kwa wananchi kwa ajili ya makazi, kilimo na shughuli za ufugaji.


Share:

HOTELI MPYA YA KISASA 'SHY SPARK HOTEL' KUFUNGULIWA RASMI AGOSTI,2020 SHINYANGA MJINI...NAFASI ZA KAZI ZATANGAZWA

Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu ‘SHY PARK HOTEL’ ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 2020;  Mkurugenzi wa SHY PARK HOTEL anawatangazia nafasi za kazi wale wote waliosomea na wenye uzoefu wa Masuala ya Usimamizi wa Hoteli.

SHY SPARK HOTEL IKO WAPI?
SHY PARK HOTEL inapatikana Lubaga Mjini Shinyanga karibu na Ikulu pembezoni mwa Barabara ya Old Shinyanga.

HUDUMA ZINAZOPATIKANA SHY SPARK HOTEL
Shy Park Hotel inatoa huduma za malazi ‘vyumba vya kulala’ ,vyakula ikiwemo nyama choma, vinywaji, kumbi za sherehe/harusi na mikutano, Swimming pool kwa watoto na watu wazima, michezo mbalimbali ya watoto, Sauna, Massage, Gym, Car wash, Car Parking n.k

NAFASI ZA KAZI
Shy Park Hotel inakaribisha maombi ya kazi kwa waliosomea masuala ya Usimamizi wa Hoteli ‘Hotel Management na wenye uzoefu wa kutoa huduma tajwa hapo juu.

SIFA ZA WAOMBAJI WA KAZI
Sifa za muombaji awe na umri wa miaka kuanzia 20, awe na taaluma ya Usimamizi wa Hoteli ‘Hotel Management’ au mwenye uzoefu wa usimamizi wa hoteli. Watume maombi wakiambatanisha na barua ya udhamini iliyopitishwa na serikali ya mtaa.

KUTUMA MAOMBI
Barua za maombi ya kazi ziwasilishwe ofisini, Fika SHY PARK HOTEL
Au kupitia  Email info@shypark.co.tz  au Whatsapp namba 0759096494
Kwa Mawasiliano zaidi piga simu namba 0621288344 

Mwisho wa kutuma maombi ni Julai 17,2020 saa sita mchana, usaili ‘Interview’ itafanyika Julai 18,2020

Karibu SHY PARK HOTEL
Picha mbalimbali muonekano wa majengo ya Shy Spark Hotel iliyopo Mjini Shinyanga.

Muonekano wa vitanda
Muonekano sehemu ya Sauna

Share:

Maendeleo ya teknolojia ya kidijitali na umuhimu wake kwenye kukuza uchumi Tanzania

Duniani kote suala la matumizi ya teknolojia ya kidijitali linakua kwa kasi kubwa sana na kwa kiasi fulani kunachagizwa na matumizi ya intaneti/data kupitia simu za mkononi.

Kwa mujibu wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa  wa Biashara na Maendeleo, matumizi ya data duniani kote yanatarajiwa kuongezeka kufikia ujazo wa 150,700GB kwa sekunde mwaka 2022. Ukuaji huo ni mkubwa sana ndani ya miaka michache ambapo mwaka 2017 ujazo ulikuwa 46,000BG kwa sekunde.

Sehemu ya mafanikio haya imechagizwa na matumizi ya data barani Afrika kwa mfano, katika mtandao mmoja utumiaji wa data umekua kwa asilimia 52 mwaka 2019.Takwimu hizi za karibuni zinaonesha habari njema kwa uchumi wa Tanzania.

Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia sekta ya dijitali nchini Tanzania ni moja ya kichochea kikubwa cha ukuaji wa uchumi. Pia, kuzidi kusambaa kwa matumizi ya intaneti kwenye simu na ubunifu wa teknolojia ni moja ya njia bora za kuhakikisha Tanzania inafikia maendeleo ya kijamii katika miaka ijayo.

Kwa mfano, Sekta ya mawasiliano ya simu imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na sekta ya afya nchini Tanzania kuja na njia ya ubunifu ambayo itarawarahisishia wazazi kusajili watoto wao wanapozaliwa. Huduma kama hizi zinaweka misingi kwa wazazi kuweza kupata huduma mbalimbali kama huduma za afya na programu za chanjo.

Miaka si mingi ijayo, usajili wa vizazi utawasaidia watu juu ya kile kinachofahamika kama utambuzi wa kidijitali ambao utawezesha watu kupata kazi pamoja na kulipa kodi kwa urahisi.

Tigo Tanzania- moja ya watoa huduma wakubwa wa mawasiliano ya simu imechangia sana katika utoaji wa huduma. Programu tumishi ya Tigo inawawezesha wazazi na wakunga kusajili taarifa za kuzaliwa kwa watoto wao kwa kutumia simu ya mkononi. Mbali na kutoa huduma kwa urahisi na uharaka kwa wateja wengine, programu hii inawezesha kuhakikisha watu wanaweza kunufaika kwa mambo yote ya kijamii miaka ijayo. 

Ili kuzisaidia kampuni za mawasiliano ya simu kuendelea kuleta utofauti wa kibunifu ni vyema kutilia maanani mahitaji yao na kuwasaidia kukua zaidi. Hii itasaidia Watanzania kuendelea kupata huduma bora na za uhakika na kukuza uchumi wetu.


Share:

KAMATA MCHONGO KUTOKA JAMBO!! TUKUPIGIE TUKUPE MCHONGO!!


Iwe Shinyanga, Mwanza, Dar es salaam, na Tanzania nzima kuwa wakala wa bidhaa za Jambo ujipatie Ubora wako kwa Bei ya MWANANCHI.

Wasiliana nasi leo kupitia namba +255 622 666 692. #ᴊᴀᴍᴜᴋᴀʏᴀ
Share:

FULL POWER, ZATI 50 NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO

Zati 50
Full Power
Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume:


⇒Ngiri,

⇒Henia

⇒Kisukari

⇒Tumbo kujaa gesi

⇒Kutopata choo vizuri

⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu

⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi

⇒Msongo wa mawazo 



⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko  na kufanya kuwa na muda  mrefu na nguvu za kutosha.



FULL POWER



⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.



⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa

⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.

Zati 50


⇨ Inarutubisha maumbile ya uume  na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4


⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.



Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama



Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger