Wednesday, 29 April 2020

WAGONJWA WA CORONA KENYA WAFIKA 384


Idadi ya walioambukizwa virusi vya Corona nchini Kenya yafikia 384, ni baada ya wagonjwa wapya 10 kuongezeka ambapo tisa ni kutoka Mombasa na mmoja ni kutoka Nairobi.



Akiongea na Waandishi wa habari leo, Aprili 29, 2020 Katibu wa Afya Mercy Mwangangi amesema katika saa 24 zilizopita sampuli 580 kutoka kaunti 24 zilipimwa dhidi ya homa hiyo.
 


Share:

MUME NA MKE WACHARANGWA MAPANGA NA MKWE WAO AKILIPIZA KISASI WAMEMBANIA KURUDIANA NA MKE WAKE

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwanaume aitwaye Mwandu Chalya (75) na mke wake aitwaye Gigwa Kwangu (70) wamenusurika kufa wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao baada kukatwa na kitu chenye ncha kali na mkwe wao Masele Boniface akilipiza kisasi walivyokataa asirudiane na mke wake kutokana na kupeana talaka mahakamani. 

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Aprili 29,2020 majira ya saa nane usiku katika kitongoji cha N'halange, kijiji cha Mwamasololo, kata ya Sekebugoro, tarafa ya mondo, wilaya ya Kishapu. 

Amesema Mwandu Chalya (75) pamoja na mke wake aitwaye gigwa Kwangu (70) wote wakazi wa Mwamasololo walijeruhiwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za miili yao na mtu aliyetambulika kwa jina la Masele Boniphace ambaye ni mkwe wao wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao. 

“Chanzo cha tukio hili ni chuki /kulipiza kisasi baada ya wazazi hao wa mke wake aitwaye Emiliana Mwandu (31) mkazi wa Mwamasololo kumkataza kurudiana na Masele Boniface baada ya kutengana kwa kupeana talaka mahakamani mnamo tarehe 06/05/2019 kwa sababu za ukatili aliokuwa akifanyiwa na mtuhumiwa kwa kupigwa hadi kupoteza fahamu kipindi hicho 2019”,ameeleza Kamanda Magiligimba. 

Amesema majeruhi wanapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga na hali zao zinaendelea vizuri. 

Kamanda Magiligimba amesema mtuhumiwa alikimbia mara baada ya tukio hilo na juhudi za kumtafuta na kumkamata zinaendelea. 



Kamanda Magiligimba ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuacha kabisa tabia ya kujichukulia sheria mkononi na inapotokea kutoridhika na maamuzi ya mahakama ni vyema kuchukua hatua ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya mahakama badala ya kujichukulia sheria mkononi.
Share:

BUNGE LAAHIRISHWA KUFUATIA KIFO CHA MBUNGE WA SUMVE, RICHARD NDASSA


Spika wa Bunge, Job Ndugai, leo Aprili, 29, 2020, ameahirisha Mkutano wa 19, Kikao cha 9, cha Bunge hadi kesho, kufuatia kifo cha Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa.



Ndassa anakuwa mbunge wa pili wa CCM, kufariki dunia wakati Mkutano huu wa Bunge la 19 ukiendelea, baada ya Mbunge wa Viti Maalumu Mchungaji Getrude Rwakatare kufariki dunia wiki iliyopita.

“Waheshimiwa wabunge, ninaomba kuwajulisha kuwa bunge letu limepata na msiba mwingine mkubwa wa kuondokewa na mbunge mwenzetu wa Jimbo la Sumve  ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo hapa Dodoma.

“Kufuatia msiba huo, taratibu mbalimbali za mazishi zimeanza kufanyika kwa mawasiliano kati ya Ofisi ya Bunge na familia ya marehemu na serikali na kila tukipata taarifa zadi za kuwataarifu tutafanya hivyo,” amesema.

Aidha, akimueleze Ndassa, Spika Ndugai amesema; “Marehemu Ndassa ni mmoja wa wabunge waliokuwa wanaitwa senetors, alikuwa ni mmoja wa wabunge waandamizi walioingia bungeni tangu mwaka 1995, amekuwa mbunge wa Sumve kwa vipindi vitano na miezi… hii inaonyesha imani kubwa waliyokuwa nayo wananchi wa Sumve na wabunge wengi tunaweza tukajifunza uongozi bora kwa kufuata nyayo zake.

Pamoja na mambo mengine, Spika Ndugai amesema kwa mujibu wa Kanuni ya 151 ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la 2016, kwa siku ya leo hawataendelea na kikao cha bunge badala yake watakuwa na maombolezo ya msiba wa mbunge huyo.

“Tutajitahidi sana iwezekanavyo kuhakikisha kwamba ndugu yetu anazikwa kule Sumve kesho jioni, tutajitahidi sana sana… kwa sababu kwa mila zetu za Kiafrika kwa kweli kumzika mtu popote pale ni jambo linalotupa ugumu fikiria wote tuliopo hapa upate jambo kama hilo halafu  unawekwa popote, kwa hiyo tutajitahidi sana. Kwa hiyo ofisi yangu itashirikiana na serikali kuona kila kinachowezekana kinafanyika,” amesema Spika Ndugai.


Share:

Serikali ya Uganda yatathmini uwezekano wa kulegeza masharti ya watu kutembea...Museven Katoa Masharti Kwa Madereva wa Malori

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema hivi karibuni atatangaza iwapo atalegeza masharti ya watu kukaa nyumbani kutokana na mamabukizi ya Corona, katika taifa hilo ambalo limeshuhudia maambukizi ya watu 79.

Wakati huo huo rais Yoweri Museveni ametangaza hatua mpya za kudhibiti mienendo ya madereva wa malori yanayoingia nchini humo kutoka mataifa jirani baada ya zaidi ya madereva 20 kupatikana na ugonjwa wa Covid-19.

Hatua hizo ni pamoja na kila lori kuwa na mtu mmoja - dereva pekee yake ambaye hataruhusiwa kulala hotelini wala nyumbani kwa watu.

Katika hotuba yake kwa taifa usiku wa Jumanne rais Museveni amebaini kwamba madereva hao ni tishio katika mapambano ya nchi hiyo dhidi ya Corona akitoa mfano wa janga la Ukimwi la miaka ya 1980 na miaka ya tisini wakati ambapo madereva wa malori katika kanda hiyo waliaambukiza watu virus vya HIV katika kila miji waliyopitia wakiwa safarini. Muda wa watu kubaki nyumbani unamalizika tarehe 5 Mei 2020.

Wakati hayo yakijiri Shirika la Kimataifa la Kutoa Misaada (IRC) limeonya kuwa watu bilioni moja huenda wakaambukizwa virusi vya Corona kote duniani, huku likisema nchi zisizojiweza zinahitaji usaidizi wa haraka.


Share:

Idadi ya Vifo Vya Corona Nchini Marekani Yazidi Idadi ya Wamarekani Waliofariki Wakati wa Vita Vya Vietnam

Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani imeongezeka na kufikia zaidi ya Milioni moja, huku idadi ya watu walipoteza maisha ikifikia zaidi ya 58,000.

Takwimu za kiafya zinaonesha kuwa kwa sasa Marekani ina visa vya maambukizi 1,035,765  huku idadi ya watu walipoteza maisha ikifikia zaidi ya Elfu 59.

Wachambuzi wa mambo nchini humo wanasema idadi ya watu walipoteza maisha sasa inazidi ile iliyoshuhudiwa wakati wa vita nchini Vietnam.

Kulingana na ripoti ya Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, watu 59,266 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa Covid-19 nchini Marekani, nchi iliyoathirika zaidi ulimwenguni, wakati askari 58,220 wa nchi hiyo walipoteza maisha wakati wa vita vya Vietnam (1955-1975), kulingana na ripoti rasmi iliyochapishwa kwenye Jalada la kitaifa.

Ongezeko la maambukizi na vifo linatishia hatma ya kisiasa ya rais Donald Trump ambaye atatetea kiti chake wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Novemba.


Share:

Waziri Mkuu Majaliwa: Tutaendelea Kuboresha Huduma Za Afya

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekabidhi magari 10 ya kubebea wagonjwa kwa wabunge ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za dhati za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora za afya karibu na makazi yao.

Magari hayo 10 ni kati ya magari 50 ya kubebea wagonjwa yenye thamani ya sh. bilioni sita yaliyonunuliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Global Fund. Kati ya magari hayo, 18 yatapelekwa kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa na 32 ni kwa ajili ya hospitali za Halmashauri pamoja na vituo vya afya.

Waziri Mkuu amekabidhi magari hayo leo (Jumatano, Aprili 29, 2020) kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Ambapo amesema mbali na magari hayo kutolewa kwa ajili ya kuboresha huduma za mama na mtoto pia yatatumika kuwahudumia wagonjwa wa corona ili kuokoa maisha ya wananchi.

“Eneo hili tumeliwekea nguvu za kutosha na Watanzania wote ni mashahidi kwa namna ambavyo Serikali imejitahidi sana katika kupunguza vifo vya mama na mtoto kwenye jamii zetu. Magari haya yatakwenda kutumika kwa ajili ya mama na mtoto lakini kwa kuwa gari litakuwepo kituoni litawahudumia na wagonjwa wengine.”

Waziri Mkuu amewashukuru wabunge wote kwa namna wanavyoishauri Serikali katika kufanya maboresho ya sekta mbalimbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na sekta ya afya ambapo leo wameshuhudia matunda ya ushauri wanaoutoa.

“Magari haya yatakwenda kufanya kazi ya kuokoa maisha ya Watanzania wengi kwa kuwasafirisha wagonjwa wa rufaa kutoka kituo cha afya kwenda hospitali ya wilaya na hospitali ya wilaya kwenda hospitali ya rufaa.”

Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema ununuzi wa magari hayo ni utekelezaji wa ahadi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuboresha zaidi huduma afya kwa wananchi.
 
Waziri Ummy amesema Wizara imenunua magari hayo ili kuimarisha huduma za rufaa kwa wagonjwa hususani kwa akina mama wajawazito hata hivyo kutokana na changamoto ya ugonjwa wa corona pia magari hayo yatatumika kwa ajili ya kubebea wagonjwa wa corona.

“Watanzania wameshuhuduia kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli, wameshuhudia upatikanaji wa dawa, wameshuhudia maboresho makubwa katika upatikanaji wa vifaa tiba, ujenzi wa vituo vya afya, ujenzi wa hosptali za halmashauri pamoja na hospitali za rufaa za mikoa na uboreshwaji wa miundombinu ya kutolea huduma za afya.”

Akizungumza kwa niaba ya wabunge waliopokea magari hayo, Mbunge wa Ileje, Janneth Mbenne amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kitendo hicho cha kihistoria. “Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa mawazo na maono makubwa ya maendeleo ya Taifa. Magari haya yatakwenda kuboresha huduma za afya katika majimbo yetu.”

Naye Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2015-2020 kwa vitendo. “…moyo usio na shukurani hukausha mema yote na heri wale wanaowajali wagonjwa kwa maana ufalme wa Mungu ni wao.”

Pia, Mbunge wa Nyasa na Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Stella Manyanya amesema kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Nyasa wanamshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa msaada huo kwani walikuwa na changamoto kubwa na gari la kubebea wagonjwa.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Breaking : MBUNGE WA SUMVE RICHARD NDASSA AFARIKI DUNIA


Habari zilizotufikia hivi punde zinasema Mbunge wa Jimbo la Sumve Mhe. Richard Ndassa (CCM) amefariki dunia leo Jumatano Aprili  29,2020.

Page Liked · 30 mins 

Miaka hii mitatu imenikumbusha sana namna tulivyo viumbe dhaifu hapa duniani na kwamba hakuna jambo moja lililo la uhakika kwenye maisha yetu. Maana leo upo, na kesho haupo. Sekunde hii Mzima, na ijayo hujui nini kitatokea. Tuswali sana na kuomba radhi za Allah ndugu zangu. RIP Mzee wangu, Mhe. Ndasa.

Tutawalete taarifa kamili hivi punde..
Share:

Picha : WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKABIDHI MAGARI 50 YA KUBEBEA WAGONJWA KWA WABUNGE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa  kwa wabunge yenye thamani ya  shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020.


Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na wa tatu kulia ni Mbunge wa Nyasa ambaye pia ni  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi, Stella Manyanya.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) wakifurahia wakati  Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta (kulia) alikionyesha ufunguo wa gari la kubebea wagonjwa baada ya kukabidhiwa wakati Waziri Mkuu alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa  kwa wabunge yenye thamani ya  shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto (kulia) wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa  kwa wabunge yenye thamani ya  shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Wa pili kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa  kwa wabunge yenye thamani ya   shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Share:

WAGONJWA WA CORONA TANZANIA WAFIKIA 480 ....KUNA ONGEZEKO LA WAGONJWA WAPYA 196


Na.WAMJW,Dodoma
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametoa taarifa ya mwenendo wa Ugonjwa wa Corona nchini ambapo amesema kuwa kuna maambukizi mapya ya ugonjwa huo kwa watanzania 196 ambapo kati yao; kutoka Bara ni 174, Zanzibar 22 na kufanya jumla ya watu waliopata maambukizi kuwa ni 480.

Aidha,Waziri Majaliwa amesema kuwa idadi ya wagonjwa waliopona imeongezeka kutoka 48 hadi kufikia 167, (Zanzibar wako 36, Bara ni 83). 

Hali kadhalika vifo 6 vimetokea na kufanya jumla ya waliofariki kwa ugonjwa wa Corona kufikia 16 hadi sasa. 

Waziri Mkuu ametoa rai kwa Watanzania kuacha kutoa taarifa za uzushi za vifo kuwa kila Kifo kinachotokea hakisababishwi na Ugonjwa wa Corona.
Share:

NAIBU WAZIRI NYONGO AONGOZA KIKAO CHA MARIDHIANO NA KUPOKEA OMBI LA MWEKEZAJI


NAIBU Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Nzega ili kusikiliza maombi na kutatua  changamoto za wachimbaji wadogo wa madini Aprili 27 mwaka huu
NAIBU Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo kulia akihoji jambo kwa wachimbaji waliokuwa wakilalamika kutopewa leseni kwenye eneo ambalo waliliomba jambo ambalo RMO alipaswa kukaa na pande hizo kutafuta muafaka
NAIBU Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza na waandishi wa habari juu ya makubaliano yaliyofikiwa mara baada ya wajumbe kujadili maombi ya mwekezaji ya kutaka kupunguziwa gharama ya ununuzi wa madini ya dhahabu baada ya uchenjuaji wa marudio wa mchanga wa dhahabu ulioachwa na mwekezaji mkubwa wa madini wa kampuni ya  Resolute iliyokuwa ikifanya shughuli zake wilaya ya Nzega kufunga mgodi      
NAIBU waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Nzega kulia Godfrey Nyapula wakati wa kikao na wachimbaji wadogo wa madini kilichofanyika kwenye ofisi za Mkuu huyo wa wilaya Aprili 27 mwaka huu
KATIBU Mtendaji wa Tume ya Madini Proffesa Shukrani Manyaa akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua zinazofuata baada ya kikao cha kuridhia ombi la mekezaji ili utekelezaji wake uwekwe katika utaratibu unaokubalika kisheria


Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, akiongoza kikao kilichohudhuriwa na Katibu Mtendaji wa TumeyaMadini, Prof. ShukraniManya, MkuuwaWilayayaNzega, Godfrey Ngupula, Afisa  Madini Mkazi wa Mkoa waTabora, Mhandisi Mayingi Makalobela, Mkuu wa Chuo cha Nzega, Nuru Shaban Kamati ya Ulinzi na Usalama  wilaya ya Nzega pamoja na mwekezaji wa uchenjuaji wa marudio, RashedShabout Said.

Afisa Madini Mkazi wa Mkoa waTabora, Mhandisi Mayingi Makalobela akitoa maoni yake juu ya ombi la mwekezaji Rashed Shabout Said wa uchenjuaji wamarudio ya mchanga ulioachwa na kampuni ya resolute baada ya mgodi huo kufungwa.


SERIKALI  imeridhia ombi la kupunguza gharama ya ununuzi wa dhahabu unaofanywa na mwekezaji Rashed Shabout Said wa kampuni ya Ashery Construction &Matinje gold Extraction yauchenjuaji wa marudio ya mchanga wa dhahabu ulioachwanakampuniya Resolute iliyofunga shughuli zake za uchimbaji mkubwa wa madini ya dhahabu mwaka 2014.

Makubaliano hayo yalifikiwa Aprili 27, 2020 wakati wa kikao kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus  Nyongo kilicholenga kujadili ombi la mwekezaji Rashed Shabout Said anayechenjua dhahabu kwenye mabaki hayo ya mchanga wa dhahabu ulioachwa na kampuni ya Resolute iliyokuwa ikichimba dhahabu wilayani Nzega,MkoaniTabora.

Pamoja na NaibuWaziri Nyongo kikao hicho kiliwahusisha Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini,Profesa Shukrani Manya, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tabora Mayingi Makalobela, Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupula, Mkuuwa Chuo cha Madini kampasi yaNzega, Nuru Shabani, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Nzega pamoja na  ujumbe ulioambatana na mwekezaji huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho, Naibu Waziri Nyongo alisema, kikao kimeridhia ombi moja kati ya matatu yaliyowasilishwa na mwekezaji ikiwa ni kushusha bei ya kumwuzia dhahabu kiasi kilichopunguzwa kimsaidie kulipia  gharama nyingine anazozitumia katika uwekezaji huo.

Nyongo alisema Rashed aliomba kupunguzi wa gharama ya dhahabu anayoinunua serikalini mara baada ya uchenjuaji, kuondolewa gharama za watumishi wanaoshiriki katika kusimamia mchakato mzima wa uchenjuaji wa mchanga huo pamoja na kuondolewa malipo ya mrabaha nakurudishiwa pesa zilizolipwa kama mrabaha kwa awali mbili za uchenjuaji zilizopita.

Nyongo alibainisha kuwa Wizara kwa kushirikiana na Tume ya madini zimeridhia kupunguza gharama ya kuuza dhahabu kwa  mwekezaji huyo na kwamba huduma nyingine na malipo ya mrabaha yatapaswa kulipwa kama kawaida  kwa mujibu wa sheria.




Kwaupande wake, KatibuMtendajiwaTumeyaMadini, Prof. Shukrani Manya alisema ombi la mwekezaji limepokelewa na kwamba hatua inayofuata nikwenda kupitia na kurekebisha mkataba ikiwani pamoja na kupeleka maoni yaliyofikiwa na kikao hicho kwa mamlaka nyingine ili kumwezesha mwekezaji huyo kufanya kazi yake kwa tija na bila manung’uniko.


Akizungumza na waandishi wa habari mwekezaji Rashed, aliishukuru serikali kwa kupokea na kufanyia kaziombi lake na kukiri hakutegemea kuwa angesaidiwa kw aharaka namna ilivyofanyika nakukiri kwamba hakika Serikali ya Awamu ya Tano inasikilizana kutatua changamoto za wananchi.


“Nashukuru sana kwa serikali hadi Naibu Waziri kuja kunisikiliza kwa kweli Wizara ya madini nisikivu sana, nashukuru sana” Rashed alikazia.

Akizungumzia changamoto wanazokutana nazo kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona Rashed alisema kumekuwa na changamoto ya usafirishaji wa madini kutokana na ndege nyingi za nje kusitisha safari zanje hivyo inakuwa ngumu kwa kuendesha biashara.

Share:

Digital Support Executive at Vodacom Tanzania

Digital Support Executive Posting Country:  Tanzania, United Republic of Date Posted:  28-Apr-2020 Full Time / Part Time:  Full Time Contract Type:  Permanent Joining Vodacom is more than a job, what we do matters. We don’t just carry minutes, texts and data – we carry people’s lives. And that’s a huge responsibility. If you think for a minute about the people you rely… Read More »

The post Digital Support Executive at Vodacom Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

KIJANA AMUUA BABA YAKE KWA KUMKATA PANGA AKIDAI URITHI WAKE

NB- Picha haihusiani na habari hapa chini

Na Israel Mwaisaka, Sumbawanga
Jeshi la Polisi mkoani Rukwa linamshikilia kijana mmoja mkazi wa Kijiji cha Mtenga Tarafa Namanyere wilayani Nkasi, kwa tuhuma za kumuua kwa kumkata kata mapanga kichwani baba yake mzazi aitwaye Ntemi Seni (65) akidai urithi wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masejo amesema kuwa tukio la kuuawa kwa mzee huyo lilitokea Aprili 25, mwaka huu majira ya saa 09:30 usiku huko Kijiji Mtenga wilayani Nkasi.

Amesema, kijana huyo mwenye umri wa miaka 36 jina linahifadhiwa inadaiwa alikuwa akitaka baba yake mzazi ampe urithi wa mali alizonazo ili ziweze kumsaidia kupata kuendesha maisha yake pasipo utegemezi.

Masejo amesema, baada ya kijana huyo kushinikiza mara kadhaa apewe sehemu ya mali ya mzazi wake kama urithi na baba yake kukataa kufanya hivyo kulizuka vurugu baina yao ndipo kijana huyo alipochukua panga na kuanza kumkimbiza na kisha kumkamata na kuanza kumkata kata na mapanga kichwani.

Kamanda amesema, Baba huyo alivuja damu nyingi katika sehemu ya kichwa na kufariki dunia muda mfupi baadae kutokana na kukosa msaada wa haraka wa kufikishwa hospitalini kwa matibabu.

Amesema, mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa awali kukamilika.

Share:

DAKTARI WA WAGONJWA WA CORONA AJIUA


Dr. Lorna M. Breen ambaye aliamua kujiua, picha kubwa ni hospitali aliyokuwa anafanya kazi.

VIRGINIA, Daktari Mkuu katika chumba cha dharura katika Hospitali ya Manhattan nchini Marekani ambaye aliwatibu wagonjwa wengi wa virusi vya corona (COVID-19), Dkt.Lorna M. Breen amejiua kwa kujinyonga.

Kwa mujibu wa The New York Times, baba yake mzazi na Jeshi la Polisi mjini Charlottesville, Virginia wamethibithisha kifo hicho.

Dkt.Breen ambaye pia alikuwa ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Dharura katika Hospitali ya NewYork-Presbyterian Allen alijinyongea mjini Charlottesville, Virginia ambapo alikuwa anaishi na wazazi wake.

Msemaji wa Jeshi la Polisi mjini Charlottesville,Tyler Hawn ameeleza kupitia barua pepe kuwa, maafisa wa jeshi hilo siku ya Jumapili iliyopita walipokea simu ya dharura ikihitaji msaada wa kitabibu.

“Mgonjwa (Dkt.Lorna) alichukuliwa na kupelekwa Hospitali UVA kwa matibabu, lakini baadae aliamua kujijeruhi mwenyewe,”amesema Hawn.

Baba yake Dkt.Lorna Breen, Dkt.Philip C. Breen amesema, baada ya binti yake kubaini hali yake si njema aliamua kufanya uamuzi ambao si wa busara.

“Alijaribu kufanya kazi yake kwa kadri ya uwezo wake na ikamuua,”amesema Baba mzazi wa marehemu huyo.

Dkt.Philip Breen amesema, binti yake awali alikuwa ameambukizwa virusi vya corona, lakini alikuwa amerejea kazini baada ya kupona wiki moja na nusu iliyopita.
Share:

AKAMATWA KWA KUSAMBAZA UONGO MTANDAONI KUWA DAWA YA COVID 19 NI KUNYWA NA KUJIPAKA PILIPILI NA UPUPU

Na Amon Mtega - Songea 
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)Ibrahimu Bukuku (26)kwa tuhuma za kusambaza ujumbe unaodaiwa kuwa ni wa upotoshwaji kwenye mitandao ya kijamii uliohusu dawa ya ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya Corona.
 

Akizungumza ofisini kwake jana Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Simon Maigwa amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa katika kijiji anachoishi cha Lunyele (Darpori) kata ya Tingi Wilaya ya Nyasa mkoani humo.

 Kamanda Maigwa amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza Chuo Kikuu cha Dodoma anayesomea shahada ya Sayansi fani ya Biolojia (Bachelor of Science in Biology) amesambaza ujumbe kupitia simu yake ya kiganjani usemao 'Dawa ya ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya Corona ni kutumia upupu pamoja na pilipili.

Maigwa amefafanua kuwa ujumbe huo ambao umesambazwa kwenye makundi mbalimbali ya kijamii ya Whatsap kuwa "Dawa ya Covid 19 ni kuchukua pilipili kichaa sufuria moja iliyotwangwa halafu changanya na maji vikombe vitano kisha kunywa kutwa mara saba kwa muda wa siku tatu na siku ya nne chuma upupu na kujipaka mwili mzima" jambo ambalo linadaiwa kuwa upotoshwaji mbele za jamii na linachukuliwa mchezo kwenye gonjwa hili la Covid 19.

 Amesema kuwa jeshi la Polisi litaendelea kuwatafuta wale wote wanaofanya mchezo na ugonjwa huu wa Covid 19 unaosababishwa na Virusi vya Corona na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kujibu mashistaka yanayowakabili.
Share:

TULONGE AFYA YAZINDUA KIPINDI CHA 'WASHA KIDEO NA SITEREREKI' LIVE MTANDAONI KUELIMISHA VIJANA MASUALA YA AFYA 'COVID- 19'

Ili kukabiliana na changamoto za COVID-19 ambazo zimeathiri shughuli mbali mbali Nchini Tanzania, Programu ya USAID Tulonge Afya imezindua kipindi maalum cha TV cha moja kwa moja (yaani live) "Washa Kideo na Sitetereki" kipindi ambacho pia kitakuwa kikirushwa moja kwa moja kupitia mitandao ya kijamii. 


Malengo ya kipindi hiki cha Washa Kideo na SITETEREKI ni kushughulikia changamoto za kiafya zinazohusiana na vijana na jinsi wanavyoweza kukabiliana nazo katika kipindi hiki cha janga la COVID-19 ambapo mifumo yote ya kila siku imevurugika kwani watu wote wanahimizwa kukaa nyumbani.

Programu ya SITETEREKI ni jukwaa la kubadilisha tabia na mienendo ya kila siku (SBC) linalolenga vijana. Jukwaa hili linasaidia kukuza Muingiliano wa vijana nchini Tanzania ili kujua vyema, kuhamasisha, na kuwezesha vijana kuchukua tabia njema ambazo zitaboresha ustawi wao kwa jumla. SITETEREKI imeundwa kusaidia moja kwa moja vipaumbele vya kimkakati kwa vijana katika Serikali ya Tanzania na inafadhiliwa na serikali ya Marekani kupitia USAID.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa programu hiyo, Mkurugenzi wa USAID nchini Tanzania Andy Karas alisema kuwa kipindi cha Washa Kideo na SITETEREKI kimebuniwa kusaidia vipaumbele vyaSerikali ya Tanzania kwa Vijana.. 'Sote tunaelewa kuwa sasa vijana wetu hawawezi kwenda tena kwenye mikusanyiko ya kijamii, Luninga pamoja na mitandao ya kijamii sasa imekuwa ndio kimbilio la vijana wengi.

 Kwa sababu ya idadi kubwa ya watu wanaokaa nyumbani kwa sasa, utumiaji wa vyombo vya habari na hasa Luninga pia umeongezeka kwa kiasi kikubwa. Vijana wetu wamekuwa wakivutiwa na mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na YouTube, Instagram, pamoja na vyombo vingine vya habari vinapokuwa vikirusha taarifa zao moja kwa moja. 

Kwa sababu hiyo, tumezindua kipindi "Washa Kideo na SITETEREKI" ili kutoa fursa ya kipekee ya kufikia mamilioni ya vijana wa kitanzania kwa njia ambayo huwashawishi wakati wa kutoa ujumbe muhimu wa afya ili kuwasaidia kuwalinda wao na familia zao, na nchi kwa ujumla kwa wakati wote na janga la COVID-19. "Karas alisema.

Aliongeza, ‘COVID-19 inajaribu kutikisa mienendo yetu ya maisha lakini kupitia muendelezo wa ufadhili wa serikali ya Marekani na uwekezaji wake katika afya ya Watanzania na taasisi za afya, na kuwa na mienendo mizuri ya kiafya ambayo tunashirikiana pamoja leo hii, vijana wa Kitanzania “hawata - tetereka”. 

Serikali ya Marekani inaendelea kusaidia kupambana na mlipuko wa COVID-19 kwa kuchukua hatua za haraka kupitia taasisi zake mbalimbali hapa nchini. Serikali ya Marekani inashirikiana na wafanyakazi wa Tanzania walio mstari wa mbele katika kupunguza maambukizi, kutoa huduma kwa waathirika, na kuandaa jamii kwa kutoa vifaa muhimu vinavyohitajika kupambana na COVID-19.

Akizungumza kuhusu kipindi cha Washa Kideo na SITETEREKI, Mkurugenzi wa Miradi Tulonge Afya Waziri Nyoni alisema kuwa Kipindi hicho Kina lenga kufikia vijana zaidi ya milioni 20 wenye umri kati ya miaka 14 mpaka 25 hapa nchini.

Tamasha hilo litaunga mkono juhudi za kupambana na janga hatari la COVID-19, na VVU, afya ya uzazi na malengo ya mkakati wa uzazi pamoja na kukuza tabia chanya kwa vijana.

‘Tamasha la Washa Kideo na SITETEREKI litakuwa likirushwa kila Ijumaa kwa masaa mawili kuanzia saa tatu mpaka saa tano usiku huku wasanii wakitumbuiza moja kwa moja kupitia Clouds TV na Clouds Radio. Vile vile, litakuwa likirusha moja kwa moja kupitia mitandao ya kijamii ya Clouds Media. Wasanii, ma DJ pamoja na waendesha kipindi hicho pia watakuwa wakirusha moja kwa moja kwenye mitandao yao ya kijamii na hivyo kuweza kuwafikia zaidi ya wafuasi wao milioni 22.4 kwenye mtandao wa Instagram. Watazamaji wataweza kuwasiliana moja kwa moja na wasanii’ Nyoni alisema.

Tamasha la kipindi cha Washa Kideo na SITETEREKI litawaleta pamoja wasanii mbali mbali ikiwa ni pamoja na Maua Sama, jux na G-Nako, pia watakaoshiriki kwa njia ya mtandao watakuwa Harmonize, Nandy, Dogo Janja na Nikki wa Pili. Aliongeza kuwa watangazaji wa programu hiyo watakuwa Nickson George na Mina Ally wakati DJ’s watakuwa DJ D-Omy na DJ Sinyorita.

Mradi wa Tulonge Afya, ni mradi wa miaka 5 unaofadhiliwa na shirika la Marekani la USAID, miradi ya Tulonge afya ina lengo la kukuza shughuli chanya za afya katika kaya na jamii nchini Tanzania huku ikilenga wanawake na vijana. Mradi wa Tulonge Afya unatekelezwa na FHI 360 Wizara ya Afya , Maendeleo ya Kijamii, Wazee na Watoto pamoja na washirika wengine.
Share:

DOWNLOAD - PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG ...TUKUTUMIE HABARI ZOTE BURE KWENYE SIMU YAKO

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.


Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa
Share:

Serikali Itaendelea Kuwakinga Watumishi Wa Afya Ili Wasipate Maambukizi Ya Ugonjwa Wa Covid – 19

Na WAMJW – Dar es Salaam
Serikali itaendelea kuwalinda watumishi wa afya ili wasipate maambukizi wakati wakiwahudumia wagonjwa wenye Virusi vya Corona (COVID-19) kwa kuwapa vifaa kinga na mafunzo ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa hao.

Hayo yamesemwa jana  jijini Dar es Salaam  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (WAMJW) Ummy Mwalimu wakati wa kikao baina yake na wamiliki wa Hospitali binafsi na viongozi wa vyama vya kitaaluma vya afya.

Waziri Ummy alisema ni jukumu la Serikali kuhakikisha linawalinda watoa huduma za afya kwa kuwapa vifaa kinga ili wawahudumie wagonjwa waliopata  maambukizi ya ugonjwa wa COVID -19.

“Ninaomba mzifikishe shukrani zangu za dhati kwa wahudumu wa afya  ambao wako mstari wa mbele katika kuwahudumia  wagonjwa waliopata maambukizi ya ugonjwa wa Corona ambao ni janga la kimataifa’’,alisema Waziri Ummy.

Waziri huyo pia aliwashukuru viongozi hao  kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kuhakikisha Hospitali zao zinatoa huduma kwa wagonjwa.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi alisema nguvu za pamoja zinahitajika ili wagonjwa wenye maambukizi ya ugonjwa wa Corona na wale ambao hawajapata maambuzi waweze kupata huduma za matibabu kwa wakati.

Prof. Makubi alisema jambo la muhimu kwa  watoa huduma za afya ni kujilinda wakati wanahudumia wagonjwa pia wamiliki wa Hospitali watoe elimu ya jinsi ya kujikinga na maambukizi ya COVID -19 kwa wafanyakazi wao.

 Naye Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) Dkt. Elisha Osati aliipongeza Serikali kwa hatua iliyochukuwa ya kupambana na ugonjwa wa Corona nchini.

“Mkutano huu ni wa muhimu kwetu kwani tumekaa kwa pamoja na kujadili mambo mbalimbali kuhusiana na ugonjwa wa COVID-19, ninaamini baada ya mkutano huu kila mmoja wetu ataenda kuyafanyia kazi”, alisema Dkt. Osati


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger