Thursday, 9 April 2020

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Awataka Viongozi wa Dini Waepushe Misongamano Kwenye Nyumba Za Ibada Ili Kukabiliana na Corona

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa rai kwa viongozi wa dini nchini kuhakikisha wanaepuka misongamano kwenye nyumba za ibada hasa katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.

Waziri Ummy amewaomba viongozi hao kuhakikisha waumini wenye dalili za kikohozi, mafua na homa wanabaki nyumbani.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Aprili 9, wakati wa kikao cha kitaifa cha viongozi wa dini kilichozungumzia jinsi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.

Amesema hadi sasa kuna idadi ya wagonjwa 25 na taarifa nyingine ataitoa mchana baada ya kupata maelezo watalaamu waliopo maabara.

"Ugonjwa tumeletewa kutoka nje, hivi sasa takwimu za jana, juzi na wiki iliyopita tumeanza kuambukizana wenyewe kwa wenyewe. viongozi wangu wa dini naomba niliweke wazi its no longer imported cases, tumeanza local transmission.


"Ndani ya siku chache tutaingia katika community transmission. Maana yake tutapata mgonjwa ambaye hajui ugonjwa ameupata wapi? Sasa hivi amekuja mtu anamuambikiza fulani ndio maana tunafanya contact (muingiliano) kujua.

Amefafanua kuwa hatua ya maambukizi katika jamii ni ngumu aliyeambukizwa amepewa na nani na kwamba ndani ya siku chache inawezekana tukaingia katika hatua hiyo.


"Lazima niwaambia ukweli nisiwafiche soon (karibuni), tutaingia kwenye community transmission. Bado tunatakiwa kuchukua tahadhari na kuongeza juhudi za kukabiliana na ugonjwa huu," amesema Ummy.

Waziri huyo amesema ni wajibu wa kila kiongozi wa dini kuhakikisha wanaendesha ibada katika utaratibu na mazingira yasiyo hatarishi ili kujikinga dhidi ya virusi vya corona, akisema makongamano ya dini sio muhimu kwa wakati huu.


“Ni mategemeo yetu viongozi wa dini kuepuka mikusanyiko ya watu wengi, tunategemea kupata ushirikiano wenu kuhakikisha kuwa ibada zinaendeshwa katika mazingira ambayo si hatarishi, rais ameeleza kuwa serikali haitafunga nyumba za ibada lakini ni wajibu wetu kuangalia sasa tutafanya ibada kwa namna ambayo si hatarishi kwetu na kwa waumini.

“Kingine tunachoomba ni kuwepo utaratibu wa kupunguza waumini wakati wa kutoka na kuingia katika nyumba za ibada, kuwa na ibada fupifupi zinazofanyika mara kwa mara, kufanya usafi wa mara kwa mara kwenye nyumba za ibada na utakasishaji,” amesema.


Share:

Seneta Bernie Sanders ajiondoa katika kinyang'anyiro cha urais Marekani

Seneta Bernie Sanders amejiondoa katika kinyang'anyiro cha urais, huku akiahidi kushirikiana na Joe Biden, ambaye anapewa nafasi kubwa ya kushinda katika kura za mchujo katika chama cha Democratic.

Bw Sanders amewatolea wito wafuasi wa chama chake cha Democratic kushikamana vilivyo kwa kumshinda Donald Trump katika uchaguzi wa urais ambao umepangwa kufanyika mwezi Novemba.

Katika kuwatangazia wafuasi wake kwamba anajiondoa katika kura za mchujo za chama cha Democratic, Bernie Sanders amemsifu Joe Biden kama "mtu anayeheshimika sana" na kutangaza kwamba atashirikiana na mgombea mwenye msimamo wa wastani ili kuendeleza mpango wake uliozimwa na mrengo wa kushoto.

Baada ya kuelewa kuwa kuna mivutano kati ya kambi hizo mbili, Makamu wa zamani wa rais wa Marekani, Joe Biden, mwenye umri wa miaka 77, ameamua kuungana haraka na wafuasi wa Bernie Sanders mwenye umri wa miaka 78.

"Najua mtanipigia kura. Na najua inaweza kuchukua muda. Lakini nataka mjue kuwa ninawaona, ninawasikia, na kwamba ninaelewa kwa haraka mnachokitaka," ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter Joe Biden, ambaye atachuana na Donald Trump Novemba 3, 2020.

-RFI


Share:

TFS Kahama Waanza Uzalishaji Wa Mkaa Mbadala Ili Kudhibili Uvunaji Holela Wamisitu

SALVATORY NTANDU
Katika jitihada za kudhibiti uvunaji holela wa Misitu kwaajili ya Matumizi ya Mkaa wilayani Kahama Mkoani Shinyanga,Wakala wa huduma za Misitu (TFS) imeamua kujenga kiwanda Maalumu ili kuzalisha Nishati mbadala ya Mkaa unaotokana na pumba za Mpunga ambazo ni rafiki kwa mazingira.

Hayo yalibainishwa Jana na Meneja wa TFS wilaya ya Kahama, Ally Juma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Mradi wa utengenezaji wa Mkaa mbadala  unaotarajia kuanza kuuzwa Mjini Kahama hivi karibuni.

Juma alisema kuwa Ujenzi wa  kiwanda hicho umegharimu zaidi ya shilingi milioni 15 na kitakuwa kikizalisha tani tatu za Mkaa kwa siku ambazo zitakuwa na ubora wa hali ya juu kutokana na utengenezaji wake utakuwa wakitaalam zaidi ilikinganishwa na unaotokana na miti.

“Tutatumia pumba za mpunga, maranda ya mbao, magunzi ya mahindi,matenga ya miti yaliyoacha kutumika ambayo yanapatikana kwa wingi katika maeneo yetu ya Kahama hivyo tunaimani wakazi wa kahama watatuunga mkono pindi tutakapo anza kuuza mkaa huu”alisema Juma.

Aliongeza kuwa kiwanda hicho kitatumika kama chuo cha mafunzo ya wanachi kujifunza bure namna ya kutengeneza mkaa huo mbadala ambao ni rafiki wa Mazingira na kuwataka wawekezaji wilayani humu kuchangamkia fursa hiyo Muhimu.

“Nitoe rai kwa wafanyabiashara wa Kahama kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kutengeneza mkaa mbadala kwani Soko lipo na la uhakika,msiwe na hofu tumejipanga kuhakikisha wananchi wanachana na matumizi ya mkaa unaotokana na miti ambapo mpaka sasa tunaendelea na udhibiti wa watu wanaofanya biashara hiyo,”alisema Juma.

Sambamba na hilo Juma alifafanua kuwa katika Kanda ya Magharibi ya (TFS) serikali imesitisha shughuli zote za Uvunaji wa misitu ili kuwadhibiti watu wanaojihusisha na biashara ya mazao ya misitu kama vile mkaa,mbao na magogo ambao hapo awali zilikuwa zimeshamiri.

Mwisho.


Share:

Jiji La Dodoma Labadilisha Mfumo Wa Uuzaji Maeneo Tahadhari Ya Corona

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Kufuatia tishio la kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa Corona,Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi amelazimika kubadilisha mfumo wa uuzaji fomu kwa ajili ya maeneo kutoka njia ya kawaida na kuanzisha mfumo wa kidijitali.

Akizungumza na waandishi wa habari  April 8,2020jijini Dodoma Mkurugenzi  wa jijni hapa Godwin Kunambi amesema uuzwaji wa fomu hizo kwa njia ya mtandao utawapa fursa wale wote ambao hawapo Dodoma kujaza fomu hizo wakiwa kwenye maeneo yao badala ya kufunga safari hadi Dodoma.

Kuhusu wananchi waliokuwa tayari wamekwisha lipia na kuchukua fomu hizo KUNAMBI amesema wote wataingizwa kwenye mtandao ambapo pia mfumo huo utaanza kutumika rasmi April 14 mwaka huu.

Aidha  amesema muda wa uuzwaji wa fomu kwa njia ya mtandao utakuwa kwa muda wa siku saba na fomu moja itauzwa kwa gharama ya Sh20,000.

Awali zoezi hilo liliwalazimu wananchi kufika moja kwa moja katika Ofisi za iliyokuwa manispaa ya zamani lakini kutokana na mwitikio mkubwa imeonekana kukawepo uwezekano wa kusambaa kwa virusi vya ugonjwa wa Corona hivyo kulazimika kusitishwa kwa zoezi hilo na badala yake kutangazwa kufanyika kwa njia ya mtandao


Share:

Madson property limited, Inakuletea mkopo nafuu kabisa wa viwanja na mashamba usio kuwa na riba wala dhamana yoyote ile

HII NI OFA KABAMBE KWA WATEJA WETU. WATEJA 50 WA MWANZO WATAPATA PUNGUZO.

SAFARI ZA KWENDA KUONA VIWANJA ZITAANZIA OFISINI KWETU MWENGE TOWER MAPEMA SAA TATU KAMILI MPAKA SAA NNE NA NUSU JUMAMOSI HII YA TAREHE 11/04/2020


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamidi April 9




















Share:

Wednesday, 8 April 2020

HOTEL YA TANGA BEACH RESORT YAFUNGWA KUKABILIANA NA CORONA




 Meneja wa hotel hiyo Joseph Ngonyo akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kufungwa kwa hoteli hiyo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali kuzuia mikusanyi
Muonekano wa Hoteli Tanga Beach Resort
Muonekano wa Hoteli Tanga Beach Resort


 MENEJIMENTI ya uongozi wa hoteli yenye hadhi ya nyota tano ya Tanga Beach resort iliyoko jiji Tanga imelazimika kufunga hotel hiyo ili kuunga mkono jitihada za serikali za kuzuia mikusanyiko ili kujikinga na ugonjwa wa virusi vya Corona vinavyotokisa dunia kwa sasa.

Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari Meneja wa hotel hiyo Joseph Ngonyo alisema kuwa wameamua kufunga kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo hapa Tanzania pamoja na na kudhibiti mkusanyiko wa watu

Alisemam kuwa awali tayari biashara ya hotel ilianza kususasua kutokana na uwepo wa ugonjwa huo hivyo kulazima kufunga ili kuzuia mkusanyiko wa waty hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika msimu wa sikukuu.

“Dunia sasa hivi na hata nchini kwetu kumekuwa na tatizo la gonjwa la Corona hivyo tumeamua kusitisha huduma ili kuunga mkono kauli ya serikali ya kuzui mkusanyiko wa wau wengi pamoja hivyo ili kuwathibiti tumelazimika kufunga hotel hiyo”alisema Ngonyo.

Aidha aliwataka wananchi kuacha dhana potofu ambazo zimeanza kusambaa katika mitandao ya kijamii na kwamba wameamua kuunga mkono juhudi za serikali hivyo shughuli za hotel zinatarajiwa kuanza tena mwishoni mwa mwezi Mei.



Kwa upande wake mmoja wa wafanyakazi katika hotel hiyo Hadija Ramadhani alisema kuwa wamelazimika kuunga mkono maagizo ya serikali ili kupunguza maambukizi kwa wafanyakazi pamoja na wananchi ambao wanaweza kufika katika hotel kwa ajili ya kupata huduma.

“Tunaomba watu waachane na habari za mitandao kwani zinatuchafua lakini lengo letu ni kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wetu pamoja na wateja ambao wanakuja kupata huduma katika hotel yety”alisema Ramadhani

Naye kwa upande wake mfanyakazi wa Hoteli hiyo kitengo cha mapokezi Khadija Mcharo alisema kwa sasa huduma zao wamesitisha kutokana na uwepo wa virusi vya Corona na wanaiunga mkono serikali katika juhudi zake za kupambana kupunguza maambukizi hayo.
Share:

WAGONJWA WA CORONA TANZANIA WAFIKA 25....KIFO NI KIMOJA, WALIOPONA HADI SASA NI WATANO









Share:

Bunge la Kenya lafuta kikao chake kwa hofu ya virusi vya Corona....Wabunge 17 Wanadaiwa Kuwa na Virusi vya Corona

Kikao cha bunge nchini Kenya kilichokuwa kimepangwa kufanyika Jumatano ya leo katika mji mkuu wa Nairobi kilifutiliwa mbali kwa hofu ya virusi vya Corona.

Spika wa Bunge la Kenya Justin Muturi alivieleza vyombo vya habari kwamba kikao hicho kilifutwa baada ya rais Uhuru Kenyatta kuweka marufuku ya kutosafiri nje na kuingia Nairobi. 

Mji wa Nairobi na maeneo mengine katika eneo la Pwani yametajwa kuwa maeneo hatari ya virusi vya corona katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. 

Masharti hayo ya usafiri yanalenga kuzuia kuenea kwa virusi hivyo hadi maeneo mengine huku dunia ikitarajiwa kusherehekea siku kuu ya Pasaka wikendi hii. 

Hata hivyo magazeti mengi ya Kenya yamenukuu vyanzo vilivyosema kwamba baadhi ya wabunge walikutwa na virusi vya corona katika bunge hilo siku ya Jumatatu.
 
Tayari baadhi yao wamelazimishwa kwenda karantini baada ya kurudi kutoka nje ya nchi mapema mwezi Machi. Uongozi wa bunge hilo uliwataka wabunge kufanyiwa vipimo ndani ya bunge hilo. 

Magazeti hayo yanaripoti kwamba matokeo ya makumi ya wabunge waliopimwa wikendi yalitoka siku ya Jumatatu, yanaonyesha kuwa, kati ya wabunge 50 waliopimwa, 17 kati yao wamepatikana na virusi vya ugonjwa huo. 

Hadi sasa nchi ya Kenya imethibitisha visa 172 vya wagonja wa virusi vya corona vikiwemo vifo sita.


Share:

WHO Yakanusha Madai ya Trump Kwamba Inaipendelea China Kuhusu Corona

Maafisa wa Shirika la Afya Ulimwenguni - WHO wamekanusha leo kuwa shirika hilo linaipendelea China na kusema kuwa hatua hii hatari ya janga la virusi vya corona sio wakati wa kupunguza ufadhili, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema kuwa atasitisha ufadhili wake.

 Marekani ni mfadhili mkubwa wa shirika hilo lenye makao yake mjini Geneva ambalo Trump amesema lilitoa ushauri mbaya wakati wa mlipuko wa virusi vya corona. 

Mshauri mwandamizi wa Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dr. Bruce Aylward, ameutetea uhusiano wa WHO na China, akisema kazi yake na mamlaka za China ni muhimu katika kuuelewa mlipuko huo ulioanzia mjini Wuhan. 

Naye Mkurugenzi wa kikanda wa WHO barani Ulaya Dr. Hans Kluge ameuelezea mlipuko wa virusi vya corona barani Ulaya kuwa wa wasiwasi mkubwa na akazitaka serikali kutafakari vya kutosha kabla ya kulegeza hatua za kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo.


Share:

KIJANA ANUSURIKA KUFA KWA KUKATWA WEMBE SEHEMU ZA SIRI AKIOMBWA PESA NA MPENZI WAKE

Share:

Video mpya ya Alikiba – DODO

Video mpya ya Alikiba – DODO


Share:

Waziri Mkuu Uingereza Aendelea Kuwa ICU Kwa Siku ya Pili sasa Kwa Corona

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson ametumia siku ya pili akiwa chumba cha uangalizi maalum wa matibabu (ICU) akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Covid-19.

Boris ambaye alibainika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona Machi 27 alipelekwa katika hospitali ya St Thomas Aprili 5 kwa vipimo zaidi baada ya hali yake kubadilika na Aprili 6 akapelekwa ICU.

Kwa mujibu wa Shirikia la Utangazaji Uingereza (BBC) limeripoti Waziri wa Afya, Edward Argar amesema hali ya Boris inaendelea vizuri.

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Dominic Raab ambaye pia ana kaimu nafasi ya Boris amesema amekuwa akijiamini huku akimuita ni mpambanaji.

Raab amesema Boris amepatiwa matibabu ya hewa ya oxygen na akawa anapumua bila msaada wowote kama vile mashine ya upumuaji.

Raab amehakikisha kuwa Waziri Mkuu amekuwa akipata uangalizi mzuri wa kitabibu hospitalini hapo.


Share:

TAARIFA KUHUSU HUKUMU YA MAXENCE MELO NA MIKE WILLIAM

Share:

Chief of Party, Sub-Saharan Africa, Tanzania Development Alternatives, Inc. (DAI)

DAI is an international development company. For more than 45 years, we have worked on the frontlines of international development, tackling fundamental social and economic development problems caused by inefficient markets, ineffective governance, and instability. Currently, DAI is delivering results that matter in some 80 countries. Our development solutions turn ideas into impact by bringing together fresh combinations… Read More »

The post Chief of Party, Sub-Saharan Africa, Tanzania Development Alternatives, Inc. (DAI) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Livelihood Officer Job Opportunity at Save The Children – Morogoro Tanzania

Livelihood Officer Job Opportunity at Save The Children – Morogoro Tanzania Job Description Livelihood Officer- Morogoro – (2000024M) TITLE: Livelihood Officer- Morogoro TEAM/PROGRAM: Programme Operations LOCATION: Morogoro GRADE: 4 POST TYPE : NATIONAL CHILD SAFEGUARDING: Level 3: √ the post holder will have contact with children and/or young people either frequently (e.g. once a week or more) or… Read More »

The post Livelihood Officer Job Opportunity at Save The Children – Morogoro Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

DC WA SINGIDA AJA NA OPERESHENI TOKOMEZA CORONA


    Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili akiwa ndani ya basi la Kampuni ya Kiazi Kitamu akiwaeleza abiria mbinu za kujikinga na Virusi vya Corona (COVID-19) alipokuwa kwenye Operesheni maalum ya Tokomeza Corona Katika Manispaa ya Singida kwenye Kituo Kikuu cha mabasi. (Picha na. Peter Kashindye).
Madereva na Mawakala wa mabasi kwenye Kituo Kikuu cha mabasi ya Mkoa wa Singida (Misuna) wakionyesha jinsi ya kutumia vitakasa mikono ili kukabiliana na ugonjwa wa Corona (COVID-19) kwa Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili (Hayupo pichani) alipofanya Operesheni Maalum ya Tokomeza Corona Katika Manispaa ya Singida kuona utekelezaji wa maagizo ya Serikali ya kujikinga na ugonjwa huo (Picha na. Peter Kashindye).



  Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili (aliyenyanyua mkono) akihoji uelewa wa kujikinga na virusi vya Corona (Covid-19) mahali pa kazi kwenye maduka ya kuuzia nyama alipofanya Operesheni Maalum ya Tokomeza Corona Katika Manispaa ya Singida kwenye Soko Kuu la Singida Mjini. (Picha na. Peter Kashindye).




1.  Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili akiwasisitiza wafanyabiashara wadogo juu ya matumizi sahihi ya vitakasa mikono alipofanya Operesheni maalum ya Tokomeza Corona Katika Manispaa ya Singida kwenye Soko Kuu la Singida Mjini. (Picha na. Peter Kashindye).


1  Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili (aliyenyanyua mkono) akitoa maelekezo kwa madereva na mawakala kuzingatia miongozo iliyotolewa na Wizara ya Afya juu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona (Covid-19). (Picha na. Peter Kashindye).

Na John Mapepele ,Singida

Mkuu wa Wilaya ya Singida Injinia Paskasi Damian Muragili amefanya Operesheni Maalum kwenye maeneo mbalimbali ya Mji wa Singida kutoa elimu na kuona jinsi wananchi walivyotekeleza maelekezo ya Serikali kuhusu ya kujikinga na ugonjwa unaoambukizwa na Virusi vya Corona (Covid 19).


Licha ya kutoa elimu hiyo pia amewapiga faini za hapo hapo watu waliobainika kukiuka maagizo huku akisisitiza kuwa Serikali itawanyang’anya lesseni za biashara na kufunga biashara hizo wote ambao wataendelea kukaidi maelekezo hayo
 

Mhandisi Muragili amefanya Operesheni hiyo maalum akiwa na Kikosi Kazi cha wataalam mbalimbali kwenye Wilaya yake ambapo ilianza alfaji hadi usiku wa kuamkia leo ambapo alitembelea maeneo yote ya huduma katika Mji wa Singida iliyojumuisha maeneo ya Standi Kuu ya Mkoa wa Singida ya Misuna, Soko Kuu la Singida na maeneo ya biashara ya Bajaji.

Akiwa katika Soko Kuu la Singida, Mkuu wa Wilaya alifanikiwa kukuta maduka ya nguo ya Kikundi cha Ushonaji cha Singida yakiwa hayana vitakasa mikono lakini wauzaji walikuwa wakiendelea na shughuli za biashara na kuwatoza faini ya shilingi elfu 50 papo hapo.

Akilipa faini hiyo baada ya kukiri kosa hilo, Mwenyekiti wa kikundi hicho ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Soko Kuu Singida Amina Msaghaa aliomba samahani kwa Mkuu wa Wilaya na kuahidi kutoendelea kufanya kosa hilo na kwamba faini hiyo imekuwa fundisho kwao na kwa hiyo wao kama kikundi watakuwa mfano wa kuwafundisha wafanyabiashara wengini

“Mhe. Mkuu wa Wilaya naomba kukueleza kuwa tumetoa faini hii kwa masikitiko makubwa, lakini hii inatupa ujasiri wa kushirikiana na Serikali yetu kuhamasisha kuhusu kujikinga na ugonjwa huu, naahidi tutakuwa walimu wazuri” alisitiza Msaghaa

Mwenyekiti wa Waendesha Bajaji Mkoa wa Singida Hemed Juma amesema katika kupambana na ugonjwa wa Corona chama chao kimechukua tahadhari zote zinazoelekezwa na Serikali kuhusu ugonjwa huu na kwamba yoyote atakayekaidi atashughulikiwa kikamilifu na chama chao ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwenye Vyombo vya Sheria.

Akifanya ukaguzi kwenye mabasi yanayoingia na kutoka kwenye Stendi Kuu Mkuu wa Wilaya amesema abiria wanatakiwa kutumia vitakasa mikono wanapoingia na kutoka kwenye mabasi hayo kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa huu

Aidha amesema Operesheni hiyo imeanza na itakuwa endelevu na ya kushitukiza kila wakati hadi ugonjwa huu utakapoisha.

Amewataka kila mwananchi wa Wilaya ya Singida kuwa mzalendo kwa kuzingingatia maelekezo ya Wizara ya Afya ya kujikinga na ugonjwa huu kwa kujitenga na kuchukua hatua zinazotakiwa ili kujilinda na kuwalinda wengine na kwamba wanapohisi kuwa kuna mgeni ambaye ameingia na hajapimwa watoe taarifa kwenye Mamlaka zilizo katika maeneo yao

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi katika siku za hivi karibuni ameanza ziara maalum ya kuhamasisha wananchi wa mkoa wake kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huu kwa kufuata taratibu zote zinazotolewa na wataalam wa afya za kudhibiti na kujikinga na ugonjwa, wa Covid-19, kumwomba Mungu na kuendelea kuchapa kazi ili kunusuru kupoteza maisha na kushuka kwa uchumi wa nchi yao

Akiwa kwenye Soko maarufu la viazi lishe kwenye Kitongoji cha Kideka katika Kijiji cha Nkunikana aliwapongeza wafanyabiashara hao kwa kuzingatia maelekezo ya Serikali ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 kwa kuandaa miundombinu ya maji ili kunawa mikono kwa sabuni katika maji yanayotiririka wakati wote.


Aidha  aliwataka wakulima wa viazi lishe kuendelea kulima kwa bidii ili wananchi wapate lishe bora kutokana na viazi hivyo na majani yake ambapo alisisitiza kuwa katika kipindi hiki ni muhimu kusanitaizi mikono na kusanitaizi afya zao

“Naelekeza wakulima waache visingizio nao waendelee kwenda mashambani kujitenga na kulima kwa bidii katika kipindi hiki ili waweze kupata mazao mengi na wakati huo huo watekeleze matakwa ya Serikali ya kujitenga na mikusanyiko isiyo ya lazima ambayo ingeweza kusababishia maambukizi endapo mmoja ana maambukizi.”


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger