Thursday, 19 March 2020

Polisi Nchini Kenya Yausaka Mtandao wa Watu 85 Unaohusishwa Na Mgonjwa Wa Corona Aliyetoroka hOSPITALI

Serikali Nchini Kenya inawasaka watu 85 wanaohofiwa kuambukizwa virusi vya corona baada ya kuambatana na mgonjwa wa virusi hivyo katika hospitali ya Mbagathi. 

Mgonjwa huyo anasemekana kutoroka katika wodi iliyotengewa wagonjwa wa Corona katika hospitali hiyo ila alikamatwa baadaye na maafisa wa ulinzi. 

Katibu mkuu wa muungano wa wauguzi nchini, Seth Panyako alithibitisha kisa hicho kupitia kwenye hotuba yake na wanahabari Jumatano, Machi 18.

 " Kuna mgonjwa aliyepelekwa katika hospitali ya Mbagathi akiwa na virusi hivyo, aliondoka hospitalini humo bila kupewa ruhusa lakini maafisa wa ulinzi walifanikiwa kumkamata . Kwa sasa tunawasaka wagonjwa wengine 85 waliotangamana naye". Panyako alisema.


Share:

Kesi ya Tundu Lissu Yakwama Tena

Kesi inayomkabili aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na wenzake imeshindwa kuendelea baada ya Upande wa Mashtaka kushindwa kuwasilisha jalada la kesi hiyo

Mahakama hiyo jana ilitarajia kusikiliza maombi yaliyowasilishwa na wadhamini wa mshitakiwa huyo wakiomba mahakama kutoa hati ya kumkamata mshitakiwa huyo kwa kuwa wao wameshindwa.

Wakili wa Serikali, Ester Martin alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa mwendesha mashitaka anayesikiliza shauri hilo hayupo hivyo anaomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kusikilizwa.

Baada ya Upande wa mashitaka kuwasilisha hoja hiyo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 23, 2020 kwa sababu ya Upande wa Mashitka umeshindwa kuwasilisha jalada la kesi hiyo mahakamani hapo.


Share:

Burkina Faso yaripoti kifo cha kwanza cha Corona

Burkina Faso imetangaza kifo cha kwanza cha mtu aliyekuwa na ugonjwa wa Corona nchini humo, hii ikiwa ni kesi ya kwanza ya kifo kilichotokana na ugonjwa huo kuripotiwa katika eneo la chini ya jangwa la Sahara barani Afrika.

Profesa Martial Ouedraogo, mkuu wa jopokazi la kupambana na virusi vya Corona nchini humo amewaambia waandishi wa habari kuwa, aliyeaga dunia kwa Corona ni mwanamke wa miaka 62, aliyekuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi. 

Amesema mwanamke huyo ambaye pia alikuwa anaugua ugonjwa wa kisukari, aliaga dunia usiku wa kuamkia jana Jumatano.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi March 19






















Share:

Wednesday, 18 March 2020

UDSM YATOA SAA 48 WANAFUNZI WOTE WAONDOKE CHUONI

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) nchini Tanzania kimewataka wanafunzi wote kuhakikisha ifikapo Ijumaa Machi 20, 2020 wawe wameondoka kurejea nyumbani.

UDSM imetoa taarifa hiyo leo Jumatano Machi 18,2020 ikiwa ni saa chache kupita tangu Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa atangaze kuvifunga vyuo vyote kutokana na kujikinga na virusi vya ugonjwa wa corona (CODIV-19).

Agizo hilo la Majaliwa amelitoa baada ya wagonjwa wawili zaidi raia wa kigeni kubainika kuwa na virusi vya corona wakiwa Dar es Salaam na Zanzibar hivyo kufikisha idadi ya waliobainika nchini humo kuwa watatu.

Katika taarifa ya Makamu mkuu wa UDSM, Profesa William Anangisye imesema katika kutekeleza maelekezo na ushauri wa Serikali kwa lengo la kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo, shughuli zote za masomo chuoni hapo zimesitishwa kuanzia leo Machi 20 2020 hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.

“Kutokana na masomo kusitishwa, wanafunzi wote, wa programu zote, walioko likizoni wanatakiwa kubaki nyumbani huko waliko, hadi hapo watakapotaarifiwa kurejea chuoni,” amesema Profesa Anangisye

Makamu mkuu huyo wa chuo amesema, “wanafunzi wote wa programu zote, ambao kwa sababu mbalimbali bado wapo katika kampasi yoyote ya chuo wanatakiwa kuwa wameondoka chuoni ifikapo Ijumaa Machi 20, 2020, kwenda nyumbani hadi hapo watakapotaarifiwa kuwa chuo kimefunguliwa tena.”

Amesema shughuli nyingine zote za Chuo zitaendelea kama kawaida kwa kuzingatia maelekezo kuhusu udhibiti wa kuenea kwa ugonjwa wa corona.
CHANZO- MWANANCHI
Share:

Wizara ya Afya Yasema Uvaaji Holela wa Mask ni Hatari Kwa Afya Yako

WIZARA ya afya imesema kuwa  kuwa si kila mtu anatakiwa kuvaa kifaa cha kuziba uso ‘mask’ ili kujikinga na homa inayosababishwa na virusi vya corona.

Akitoa maelekezo kuhusu watu wanaotakiwa kuvaa mask, Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Udhibiti na Ufuatiliaji wa Magonjwa Mlipuko, Dk. Janeth Mghaba amesema kifaa hicho kinavaliwa si zaidi ya saa nne tu na mtu ambaye tayari ana maambukizi kusudi asimuambukize mwingine.

Amesema hiyo ni kwa sababu siyo rahisi mtu akakohoa aidha kwa kutumia kiwiko au mkono atakuwa na maji maji na mara nyingi ataweza kumuambukiza mwenzie.

“Kwa hiyo yule ambaye ni mgonjwa tu, tunasema kwamba ukijisikia dalili za kukohoa basi wewe vaa mask yako nenda kwenye kituo cha afya karibu au hospitali.

“Mask pia zinaweza kuvaliwa kwenye sehemu za msongamano au sehemu zenye watu wengi lakini kwa sababu tayari serikali imeshapiga marufuku hii misongamano, hatutegemei kukuona wewe unavaa mask unapita sehemu ambako hakuna msongamano na wewe ni mzima huna maambukizi,” amesema.


Share:

Walioambukizwa corona Kenya wafika 7

Waathiriwa wa kirusi cha corona nchini Kenya wamefikia watu saba baada ya watu wengine watatu kuthibitishwa kuambukizwa kirusi hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano, Waziri wa Afya wa Kenya, Mutahi Kagwe amesema kuwa, watu wote hao saba wametoka nje ya Kenya. 

Wawili kati ya wagonjwa hao wametokea Madrid Uhispania kupitia Dubai na mgonjwa wa tatu ni raia wa Burundi aliyewasili katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi akitokea Dubai pia.


Share:

Serikali yataja sababu sampuli za Virusi vya Corona kupimwa Dar es Salaam

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amesema kuwa sampuli za washukiwa wa virusi vya Corona zinapimwa maabara ya taifa iliyopo jijini Dar es Salaam pekee kwa sababu ndiyo inayokidhi vigezo vya kupima virusi hivyo nchini.

Ummy Mwalimu ametoa kauli hiyo leo kufuatia wananchi wengi kuhoji sababu za serikali kusafirisha sampuli kutoka maeneo mbalimbali kuelekea Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi badala ya kupimiwi huko huko zinapotokea.

“Kirusi hiki ni ‘highly infectious’ (kina ambukiza kwa kasi), kinapimwa katika maabara maalum ambapo ina ngazi inaitwa ‘biosafety level 3.’ Kwa nchini Tanzania ni Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii tu ambayo ipo ngazi ya tatu katika upimaji wa sampuli za virusi ambavyo vina hatari ya kuambukiza kwa kiasi kikubwa,” amefafanua waziri huyo.

Ameongeza kuwa kabla ya Februari 15 mwaka huu Kusini mwa Jangwa la Sahara maabara mbili tu (Afrika Kusini na Senegal) ndizo zilikuwa na uwezo wa kupima kirusi cha Corona, hivyo kwa Tanzania kuwa na maabara inayoweza kupima kunaonesha kuwa kazi kubwa imefanyika.

Aidha, amewatoa hofu wananchi kuwa wamechukua hatua madhubuti pamoja na kusaini mikataba kuhusu namna ambavyo sampuli zitasafirishwa kuelekea Dar es Salaam, kama ambavyo ilikuwa ikifanyika hata wakati wa Ebola.


Share:

Waziri Mkuu Majaliwa: Nchi Za Sadc Tuendelee Kupaza Sauti Kuondolewa Vikwazo Zimbabwe

Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kutumia majukwaa ya kikanda, kitaifa na kimataifa kwa ajili ya kupaza sauti zao ili kusaidia kuondolewa kwa vikwazo kandamizi vya kiuchumi kwa Jamhuri ya Zimbabwe.

Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC leo Jumatano (Machi 18, 2020) Jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Majaliwa alisema Tanzania kupitia nafasi yake ya Uenyekiti wa SADC imeendelea kupaza sauti kwa ajili ya kuisaidia Serikali ya Zimbabwe.

Aliongeza kuwa mwezi Oktoba mwaka jana Tanzania ilifanya kongamano kubwa la kihistoria lililowaleta pamoja wadau mbalimbali wa kitaifa na kimataifa, ambapo katika kongamano hilo wadau hao walitoa, ambapo Serikali ya Tanzania inaamini kuwa ujumbe wa mkutano huo uliwafikia walengwa.

Aidha Majaliwa alisema kuwa wakati Nchi Wanachama wa SADC wakielekea kuitekeleza ya mwaka 2020 (SADC Post 2020 Agenda), mataifa hayo hayana budi kuungana pamoja na kupaza sauti zao hadi hapo vikwazo hivyo vitakavyoondolewa kwa Jamhuri ya Zimbabwe, vikwazo ambavyo athari zake zimekuwa kubwa kwa uchumi wa wananchi na Nchi ya Zimbabwe.

‘’Vikwazo hivi vya kidhalimu, athari zake ni kubwa kwa ustawi wa uchumi wa Zimbabwe na wananchi wake kwa ujumla, hivyo hatuna budi kuungana pamoja katika kupaza sauti zetu ili kuisaidia Jamhuri ya Zimbabwe kuondolewa vikwazo hivi’’ alisema Majaliwa.

Kuhusu mafanikio ya SADC, Majaliwa alisema tangu Januari mwaka huu Tanzania kupitia nafasi yake ya Uenyekiti wa SADC, inaendelea na jitihada mbalimbali za kuimarisha jumuiya hiyo ili kuweza kufikia malengo, ambapo imefanikisha kufanyika kwa mikutano mitano ya kisekta ikiwemo Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Mawasiliano, Uchukuzi, TEHAMA na Hali ya Hewa.

Anaitaja Mikutano mingine ni pamoja na Mkutano wa Mawaziri wa sekta za Maliasili na Utalii, Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Afya, Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Kazi na Ajira, Mkutano wa Mawaziri wa Menejimenti ya Maafa katika SADC.

Aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka 40 tangu kuanzishwa kwa SADC, Jumuiya hiyo imeendela kupata mafanikio mbalimbali ikiwemo miradi ya miundombinu, viwanda, elimu, mazingira na jinsia na kuzitaka Nchi wanachama kuchukulia changamoto zinazojitokeza kwa sasa ikiwemo kisera, bajeti, ushiriki hafifu wa sekta binafsi kuwa sehemu ya maandalizi ya Mpango Mkakati wa miaka 10 ya Jumuiya hiyo wa 2020/2030.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi alisema Tanzania kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Jumuiya hiyo, imewezesha kwa kiasi kikubwa kufanikisha mafanikio ya mkutano huo uliofanyika kupitia njia ya mtandao (Video Conference) kutokana na tishio la uwepo wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya COVID 19.

Prof. Kabudi alisema Tanzania kupitia nafasi yake ya  Uenyekiti imeendelea kuhakikisha kuwa ajenda ya utengamano wa Jumuiya hiyo inafikiwa kama ilivyoanishwa katika Mkataba wa Uanzishwaji wa SADC inayoongozwa na nyaraka mbili za kimkakati amazo ni Mkakati Elekezi wa Kanda 2015-2020 na Awamu ya Pili ya Mpango Mkakati wa Asasi za Siasa, Ulinzi na Usalama.

Aliongeza kuwa kupitia maazimio na mikakati hiyo, SADC imewezesha kuleta mchango na maendeleo makubwa ndani ya ukanda huo kwa kuhakikisha kuwa nchi wanachama zinakuwa na mtazamo mpya wa kimkakati na kupata matokeo chanya yatakayoakisi maendeleo jumuishi na endelevu kwa ajili ya ustawi wa wananchi wa jumuiya hiyo.

Kwa mujibu wa Waziri Kabudi alisema katika mkutano pia, Baraza hilo linatarajia kupokea na kujadili taarifa ya maandalizi ya Dira ya Jumuiya ya 2050 pamoja na Mpango Mkakati wa utekelezaji wa malengo ya dira hiyo na kutoa mtazamo mpya wa kimkakati unaotoa mwongozo kwa ajili ya kuimarisha mtangamano.

Naye Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo, Dkt. Stergomena Tax alisema Jumuiya hiyo imeendelea kupiga hatua za maendeleo katika nyanja mbalimbali za kiuchumi ikiwemo viwanda, nishati, maji kupitia utekelezaji wa maazimio na mipango mbalimbali ya utekelezaji iliyowekwa katika mwaka 2019/2020 na 2020/2021.


Share:

Kampuni za mawasiliano ya simu zinavyosaidia kuinua wanawake nchini Tanzania

Wiki iliyopita wanawake barani Afrika walisherehekea Siku ya Kimataifa ya Mwanamke. Siku hii muhimu husherehekea mafanikio ya mwanamke kijamii, kiuchumi, kiutamani na kisiasa na kuchagiza mjadala wa usawa wa kijinsia.  

Nchini Tanzania usawa wa kijinsia umeongezeka katika miaka ya karibuni kutokana na nguvu za serikali, taasisi na watu binafsi kuweka mazingira ya upatikanaji wa elimu kwa mtoto wa kike na haki ya mwanamke kumiliki na kutumia ardhi.Licha ya maendeleo hayo, yapo mengi ambayo inabidi kufanywa kuendelea kumpa nafasi zaidi mtoto wa kike. 

Eneo mojawapo ambalo kuna mengi ya kufanya ni katika teknolojia na mawasiliano. Takwimu na hivi karibuni zinaonyesha katika suala la umiliki wa simu za mkononi Tanzania kuna pengo la asimili 9 kati ya wanawake na wanaume, wanaume wakiwa juu. 

Takwimu zinaonyesha pia kwamba hata katika upatikanaji wa mtandao wa intaneti, wanaume wako juu zaidi kwani kuna pengo la asilimia 13 kati ya wanaume wenye uwezo wa kupata na kutumia intaneti ukilinganisha na idadi ya kundi hilo upande wa wanawake. 

Sote tunafahamu kwamba mtandao wa intaneti ni moja ya njia bora za kuinua aina ya maisha ambayo mtu anaishi. Mfano, intaneti inatoa nafasi ya kupata huduma za fedha, bima za afya na hata nafasi za kazi. Hii leo, mtandao wa intaneti na kuunganishwa kidijitali kunawapa nafasi wanawake ambao zamani hawakuwa na fursa nyingi, fursa mpya ya kufaidi hayo yote.  

Bahati nzuri, hapa Tanzania sekta ya mawasiliano ya simu imeleta namna mpya na za kibunifu kupata faida za kuuganisha kidijitali kwa wanawake.


 Kampuni kama Tigo imeunda apps zinazosaidia wanawake kuendesha na kusimamia mipango yao ya fedha. Mfano Tigo Pesa App inawapa wanawake nafasi kuweka fedha, kufanya malipo na hata kupata mikopo.

 Mbali na hiyo, Tigo pia inasaidia kuhakikisha kwamba wanawake wanapata ujuzi ili kufurahia fursa hizi. Katika hili, Tigo Tanzania wamezindua programu kama “Apps and Girls” ambapo wanawafunzi wa kike wanafundishwa mbinu za kuvuna fursa katika dunia ya kidijitali. 

Katika haya yote, lazima kukumbuka kuwa programu kama hizi za kampuni za simu zimewezekana kutokana na miaka mingi ya uwekezaji wa kampuni hizi. 


Uwekezaji huo umejenga msingi wa mipango kama hii ambayo inawapa nguvu na kuwainua wanawake pamoja na jamii kwa ujumla. Ili kuhakikisha kwamba kampuni hizi zinaendelea na mipango ya namna lazima taifa letu liendee kuunga mkono ukuaji wa sekta hiyo kwa kuipa mazingira bora ya uwekezaji na sheria bora za kiuendeshaji. 

Tuendelee kufanya kazi pamoja kuunga mkono mipango kuwainua watoto wa kike na wanawake kwa ujumla.


Share:

MUFTI WA TANZANIA, SHEIKH ABUBAKAR ZUBERI AAGIZA MADRASA ZOTE NCHINI KUFUNGWA ILI KUKABILIANA NA CORONA


Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi amewaagiza walimu wa madrasa kufunga madrasa zote hadi utakapotangazwa utaratibu mpya. Aidha amewataka waumini wote kuchukua udhu nyumbani wanapokwenda msikitini, ikiwa ni tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Akizungumza  leo Jumatano Machi 18, na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam Sheikh Zubeir amesema agizo hilo linapaswa kutekelezwa haraka iwezekanavyo na kwamba taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Amesema kuhusu Swala ya Ijumaa na ile ya Jamaa zitaruhusiwa kwa sasa na huenda itabadilishwa kulingana na mazingira ya ugonjwa huo.

“Kuanzia sasa swala za Jamaa zinapaswa kuswaliwa kwa kuachiana nafasi na kuzingatia usafi ili kupunguza maambukizi,” amesema Sheikh Zubeir.

Amesema kwa maeneo ambayo yanawashukiwa wa ugonjwa huo na yamewekwa karantini hairuhusiwi kuendelea na swala hizo kwani hata vitabu vya dini vinaelekeza kuwa ni dhambi kumuambukiza ugonjwa mwenzio kwa makusudi

Amesema muislamu yeyote atakayepata na maradhi haya ni haramu kwake kuhudhuria swala za Ijumaa na Jamaa kama ambavyo ni haramu kwake kuchanganyika na wengine kwani kufanya hivyo ni kuisambaza na kueneza ugonjwa huo kwa wenzake.


Share:

Mgonjwa wa kwanza wa Virusi vya corona awaomba msamaha Watanzania

Mtanzania wa kwanza kuthibitika kuwa na ugonjwa hatari unaosababishwa na Virusi vya Corona, anayejulikana kwa jina la Isabella Mwampamba, amezungumza leo kwa njia ya simu na kuwataka watanzania wasiwe na hofu na kikubwa wazidi kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo.

Akizungumza leo Jumatano Machi 18, 2020 kwa njia ya simu katika mkutano wa wanahabari ulioandaliwa na Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu uliofanyika katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha,  Mrisho Gambo amesema, “ninaendelea vizuri, namshukuru Mungu kwa kunilinda nawaomba msahama watanzania kwa maana kuwa mgonjwa wa kwanza kuugua corona iliyoleta  taharuki nchi nzima na watu wengi wanaona kwamba mimi ni kisababishi."

Isabela amesema kwa sasa hana dalili zozote za ugonjwa huo na kwamba hana homa wala mafua.


Aidha, Waziri Mwalimu amesema mtandao wa watu 26 walioshirikiana na mgonjwa huyo wako chini ya uangalizi na vipimo vya sampuli vimeshapelekwa jijini Dar Es Salaam na majibu yatatolewa wakati wowote kuanzia sasa.

Machi 16, 2020, Tanzania ilithibitisha kisa cha kwanza cha mgonjwa wa Corona, aliyetokea nchini Ubelgiji na kutua katika Uwanja wa Ndege wa KIA.


Share:

Mkurugenzi wa wilaya Babati awaondoa wafanyabiashara Mnadani kuhofia Corona

Na John Walter-Babati
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Babati Hamisi  Malinga amezuia mnada maarufu wa Maole uliokuwa ufanyike leo Machi 18,katika kijiji cha Maweni kata ya Magara mkoani Manyara.

Malinga amesema baada ya agizo lililotolewa na serikali kupitia kwa waziri Mkuu Kasim Majaliwa kwa sasa wanachofanya wao ni utekelezaji wa agizo hilo na kwamba asubuhi ya leo wamesisitiza tangazo hilo kwa wafanyabiashara.

Amewataka wafanyabiashara hao kutii agizo la serikali na kujali Ubinadamu kuliko biashara zao na kusubiri hadi hali ya maambukizi ya Virusi vya Ugonjwa wa Corona itulie na kusubiri tangazo lingine la serikali litakapotolewa.

Amesema anatambua fika kuwa mnada huo unaingiza kipato kikubwa kwa Halmashauri ya wilaya ya Babati na mkoa kwa ujumla,lakini afya na maisha ya watu ni muhimu kuliko mapato yanayopatikana.

Mnada huo maarufu uaofanyika kila jumatano, huwakutanisha wafanyabiashara mbalimbali kutoka Mkoa wa Arusha na Manyara .

Jana Machi 17,2020, Serikali ilisitisha mikusanyiko yote mikubwa ya ndani na nje isiyo ya lazima ikiwemo shughuli za michezo, matamasha ya muziki, mikutano mbalimbali ikiwemo ya shughuli za kisiasa, mahafali na shughuli nyingine za kijamii na kufungwa  shule zote za awali, msingi na sekondari kwa siku .

Pia Waziri mkuu aliwataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya wahakikishe maeneo yote yaliyobainishwa na kutengwa (vituo vya huduma na ufuatiliaji) kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa endapo watajitokeza katika maeneo yao yanakuwa na mahitaji yote muhimu na yanahudumiwa ipasavyo.

Mpaka sasa serikali imethibitisha kuongezeka kwa wagonjwa wawili wa Corona na kufanya idadi ya walioambukizwa kufika watatu.


Share:

Fahamu Dalili na Jinsi ya Kujikinga na Virusi Hatari vya Corona

Ugonjwa wa homa ya virusi vya corona (COVID-19) unasambaa kwa kasi duniani kote hivyo ni muhimu ku kuchukua tahadhari kutokana na mwingiliano mkubwa uliopo kati ya Watanzania raia wa China ambako homa ya virusi hivyo ilianzia, na wa nchi nyingine zilizoathirika na ugonjwa huo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limekua likitoa taarifa za mara kwa mara za maendeleo ya mlipuko wa virusi hivyo na pia kuelimisha njia ambazo zinatumika kujinga na maambukizi ya ugonjwa huo .

Dalili kuu za ugonjwa huu ni homa kali, uchovu na kikohozi kikavu na zinatokea taratibu. 

Dalili inayotia hofu zaidi ni kukosa pumzi ingawa taarifa za kitaalamu zinasema mtu mmoja kati ya watu sita walioambukizwa ndiyo hufikia dalili hiyo. 

Shirika la Afya Duniani (WHO) inasema wazee na watu wenye magonjwa ya kudumu kama vile shinikizo la damu, kisukari, matatizo ya figo ndiyo walio katika hatari kubwa kuathirika wanapopatwa na virusi vya corona.

Virusi vinaweza kusambaa kupitia maji maji kutoka kwenye pua au mdomo wa aliyeathirika. 

Kugusa mafua, mate na makohozi ya mwenye virusi na kisha kujigusa mdomo, macho na pua kunaweza kusababisha kupata virusi vya corona.

 Ili kujikinga virusi vya corona, inapaswa kunawa kila wakati mikono kwa maji ya vuguvugu, sabuni au dawa za kuua vijijidudu. Kaa umbali wa angalau hatua mbili kutoka mtu anayepiga chafya au kukohoa.

Epuka kushika macho, pua na mdomo kwa mikono isiyo safi kwa sababu mikono ni rahisi kubeba vimelea vya maradhi. 

Zingatia ustaarabu wa kuzuia pua na mdomo wakati wa kukohoa au kupiga chafya. 

Iwapo una mafua makali, homa, kikohozi na kushindwa kuhema nenda hospitali kupata msaada wa kitaalamu. 

Epuka kuwa sehemu yenye msongamano kama vyombo vya usafiri, maduka na maeneo yenye mgandamizo wa hewa. 

Tumia kifunika mdomo na pua na ukivae kwenye mikusanyiko.


Share:

Taasisi Za Manunuzi Ambazo Hazitajiunga Na Mfumo Wa Taneps Kutoshiriki Zabuni

Na Peter Haule WFM, Dodoma
Serikali imezitaka Taasisi zote za Manunuzi ambazo hazijajiunga katika Mfumo wa Ununuzi ya Umma kwa njia ya Mtandao (e-Procurement System) ujulikanao kama TANePS kufanya hivyo kinyume na hapo zitakuwa zimejipotezea nafasi za kushiriki katika Zabuni zinazojitokeza.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Balozi Dkt. Matern Lumbanga, wakati wa Ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa PPRA, jijini Dodoma.

Balozi Lumbanga amewataka Watumishi wa  PPRA, kuhakikisha kuwa wanasimamia kikamilifu matumizi ya mfumo wa TANePS kuhakikisha kwamba taasisi zote za umma ambazo hazijajiunga na mfumo zinaunganishwa kwenye mfumo na kuanza kuutumia katika manunuzi yake kabla ya kufunga mwaka huu wa fedha 2019/2020.

”Ni imani yangu kuwa mfumo huu utakuwa mwarobaini wa changamoto ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kwenye ununuzi ya umma kama vile, michakato ya zabuni kutumia muda mrefu na gharama kubwa, kukosekana ushindani, uwazi na usawa kwenye michakato ya zabuni  na pia bei kubwa za bidhaa na huduma ikilinganishwa na bei halisi ya soko”, alieleza Balozi Lumbanga.

Pia Dkt. Lumbanga amewakumbusha watumishi wa PPRA kuzingatia kanuni zilizotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya juu ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya ugonjwa wa Corona ambao ni tishio kwa Dunia.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo, alisema kuwa Taasisi Nunuzi na Wazabuni, wanaendelea kupatiwa mafunzo ya jinsi ya kuutumia na kujiunga kwenye mfumo wa TANePS na hadi sasa Taasisi Nunuzi 511 kati ya 540 zimepata mafunzo na zimeanza kuutumia mfumo huo.

Mhandisi Kapongo alieleza kuwa, Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa PPRA ni cha tatu tangu kuanza kwa Baraza hilo la Wafanyakazi wa PPRA na ni kikao cha pili katika mwaka huu wa fedha wa 2019/20.

Alisema kuwa Mamlaka imejiwekea utaratibu wa kufanya vikao viwili ya Baraza la Wafanyakazi katika kila mwaka wa fedha ili kujadili kwa pamoja njia za kuboresha mafanikio yanayokuwa yamepatikana na njia za kutatua changamoto zinazoikabili Mamlaka.

Mhandisi Kapongo alisema kuwa katika Kikao cha Baraza hilo la Watumishi watapokea, kujadili na kupitisha taarifa ya nusu mwaka ya utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2019/2020, na kujadili na kupitisha Bajeti inayopendekezwa ya mwaka 2020/2021.


Share:

Kamati Ya Bunge Yaiagiza Thbub Kupeleka Mapendekezo Ya Kutungwa Sheria Ya Matumizi Ya Mitandao

Na  Mbaraka Kambona,
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imeiagiza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa kushirikiana na Taasisi ya Haki Maendeleo kuandaa mapendekezo yatakayosaidia kuanzishwa kwa mchakato wa  kutungwa kwa sheria ya kulinda haki za mtumiaji wa huduma za mifumo ya kimtandao na kuyawasilisha kwa kamati hiyo ili waweze kushawishi bunge na mamlaka nyingine husika ili sheria hiyo iweze kutungwa.

Maelekezo hayo yalitolewa na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Emmanuel Mwakasaka, Mbunge wa Tabora Mjini kufuatia mada kuhusu haki za binadamu na Mitandao iliyowasilishwa vyema na Mwenyekiti wa Bodi ya Haki Maendeleo, Dk. Abdallah Mrindoko katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kushirikiana na Taasisi ya Haki Maendeleo kwa wabunge wa kamati hiyo Iliyofanyika Mkoani Morogoro Machi 16, 2020.

Akiongea baada ya kuwasilishwa kwa mada hiyo, Mwakasaka alisema kuwa kuna haja ya kuwa na sheria itakayolinda usiri wa taarifa za mtumiaji wa huduma zinazotumia mifumo ya kimtandao kwa kuzingatia kuwa mifumo hii inachakata taarifa za mtumiaji na kuzisambaza jambo ambalo linaibua haja ya kutungwa kwa sheria hiyo.

Mapema wakati akitoa mada hiyo, Dk. Mrindoko alitaja changamoto kubwa inayowakumba watumiaji katika kipindi hiki cha maendeleo ya teknolojia ya mtandao ni uwepo wa taasisi nyingi zinazojihusisha na utunzaji na uchakataji wa taarifa katika mfumo wa kidijitali bila kuwepo na sheria ya kulinda haki hizo za mtumiaji.

Dk. Mrindoko aliongeza kuwa ili thamani ya matumizi ya mitandao iweze kutambulika vizuri ni muhimu kuwa na sera na sheria itakayosimamia ulinzi wa haki  za mtumiaji nchini.

Aliendelea kusisitiza  kwamba mapinduzi ya huduma ya kifedha kwa njia ya mitandao ya simu imeibua changamoto nyingi zinazohusiana na ulinzi wa haki za mtumiaji, akisema kuwa jukwaa hili limeleteleza muingiliano kati ya kampuni za mawasiliano na taasisi za kifedha, mazingira ambayo yameibua hoja ya kuwepo sheria ya kusimamia masuala hayo.

“Mazingira yaliyopo sasa yametengeneza ombwe la kisheria kufuatia kuwepo kwa pande  mbili ambazo ni kampuni za simu na taasisi za kifedha zinazosimamia masuala ya kifedha mitandaoni ambapo kila mmoja ana mipaka yake kiutendaji”, alisema Dk Mrindoko

“Wakati matumizi ya simu katika kutuma na kupokea pesa kumepelekea ukuaji na urahisi wa mzunguko wa masuala ya kifedha, bado kuna changamoto nyingi zinazohusu mustakabali wa mtumiaji ambazo zinahitaji kupatiwa ufumbuzi, aliongeza Dk. Mrindoko

Aidha,  alieleza kuwa maendeleo katika matibabu ya afya ya kimtandao na kitambulisho cha uraia vimeleteleza maswali mengi kuhusiana na ulinzi na usiri wa taarifa za mtumiaji, akipendekeza kuwa mambo yote haya inabidi yawe katika mfumo mmoja ambao utalinda usiri na taarifa za mtumiaji. 

Akichangia majadiliano katika warsha hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome alikiri kuwa ni muhimu kuwa na sheria zinazolinda usiri na taarifa za mtumiaji huku akisema kuwa mchakato wa kutunga sheria hiyo hivi sasa ipo katika mchakato wa kutungwa ili iweze kutumika.


Share:

Breaking: WAGONJWA WA VIRUS VYA CORONA WAFIKA WATATU TANZANIA ......VYUO VIKUU VYOTE VYAFUNGWA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa idadi ya wagonjwa wa Virusi vya Corona nchini imeongezeka na kufikia watatu, ambapo mmoja amepatikana Zanzibar ambaye ni raia wa Ujerumani na mwingine Jijini Dar es Salaam ambaye ni raia wa Marekani.

“Tuna ongezeko la wagonjwa wawili ambao wamethibitika kuwa na corona Tanzania, mmoja kutoka Zanzibar yeye ni Mjerumani ana miaka 24 na tayari yupo kwenye uangalizi, na hapa Dar tuna Mmarekani mwenye miaka 61 amebainika kuwa na corona pia” -Amesema Waziri Mkuu Majaliwa

Pia amesitisha masomo kwa vyuo vikuu na vya kati nchini kuanzia leo March 18, 2020 ili kukabiliana na Virusi vya Corona.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger