Wednesday, 11 March 2020
Bashe: Vijana Limeni Na Kuuza Popote, Serikali Haitowaingilia
“Tunataka Shughuli za Uchaguzi Mkuu 2020 zifanyike Jengo Jipya la NEC” - Mhagama
JAJI MUTUNGI: ZOEZI LA UHAKIKI WA VYAMA HALIFUTI CHAMA CHA SIASA
WAZIRI MKUU AZINDUA MKAKATI WA KUPAMBANA NA UNYANYAPAA WA VVU NCHINI
Tuesday, 10 March 2020
FULL POWER, ZATI 50 NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO
Mbowe na Wenzake Wakutwa Na Hatia Kwenye Mashitaka 12 Kati ya 13
Washtakiwa hao wametiwa hatiani katika mashtaka 12 kati ya 13, yaliyokuwa yanawakabili ikiwemo la uchochezi.
Uamuzi wa kuwatia hatiani, umetolewa leo Jumanne, Machi 10, 2020 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka na ule wa utetezi.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya mahakama kuwatia hatiani washtakiwa hao, ndugu, jamaa na marafiki waliopo ndani ya mahakama hiyo walianza kulia kimya kimya huku wakifuta machozi.
Looking for Gender Expert at AAN Associates
Looking for Gender Expert AAN Associates is looking for ”Gender Expert” for UNICEF Tanzania opportunity of “Evaluation of the Simplified Birth Registration System in mainland Tanzania”. Required Skills and Experience Education: Master’s Degree in social science especially gender studies, or relevant discipline Experience: 5-9 years of increasingly responsible professional experience in the substantive area, of which five years… Read More »
The post Looking for Gender Expert at AAN Associates appeared first on Udahiliportal.com.
Lodge Assistant Manager at Four Seasons Hotels and Resorts
Lodge Assistant Manager This position is for a local Tanzanian, If you are not Tanzanian we can not consider your application. The Ideal candidate should have luxury hotel / lode experience and previous management experience. Basic Purpose Oversees the Front Desk operations and acts as the Front Office Manager and manager on duty in the Lodge when senior… Read More »
The post Lodge Assistant Manager at Four Seasons Hotels and Resorts appeared first on Udahiliportal.com.
Western Tanzania Regional Manager at Water Mission
What is the opportunity? Working under the direct supervision of the Water Mission – Tanzania Country Program Director, this position is responsible for applying sound project and program management techniques, engineering principles, and excellent written and verbal communication skills to manage a regional office in Tanzania. This position oversees large, solar powered water projects in multiple locations. The… Read More »
The post Western Tanzania Regional Manager at Water Mission appeared first on Udahiliportal.com.
Project Manager at Sandvik
Sandvik is a high-tech and global engineering group offering products and services that enhance customer productivity, profitability and sustainability. We hold world-leading positions in selected areas – tools and tooling systems for metal cutting; equipment and tools, service and technical solutions for the mining industry and rock excavation within the construction industry; products in advanced stainless steels and… Read More »
The post Project Manager at Sandvik appeared first on Udahiliportal.com.
Key Customer Manager at Sandvik
Sandvik is a high-tech and global engineering group offering products and services that enhance customer productivity, profitability and sustainability. We hold world-leading positions in selected areas – tools and tooling systems for metal cutting; equipment and tools, service and technical solutions for the mining industry and rock excavation within the construction industry; products in advanced stainless steels and… Read More »
The post Key Customer Manager at Sandvik appeared first on Udahiliportal.com.
Workshop Supervisor and Technical Trainer at Sandvik
Sandvik is a high-tech and global engineering group offering products and services that enhance customer productivity, profitability and sustainability. We hold world-leading positions in selected areas – tools and tooling systems for metal cutting; equipment and tools, service and technical solutions for the mining industry and rock excavation within the construction industry; products in advanced stainless steels and… Read More »
The post Workshop Supervisor and Technical Trainer at Sandvik appeared first on Udahiliportal.com.
Data Assistant at STEP
Consultancy opportunity: Data Assistant About the consultancy: The consultant will provide administrative and technical support to STEP’s programs through data entry, data management, data quality verification, data analysis and reporting. Responsibilities: Data management To conduct data entry and data quality checking for a range of projects To process camera trap and other photographic data according to existing protocols… Read More »
The post Data Assistant at STEP appeared first on Udahiliportal.com.
Waziri Mkuu Akagua Daraja La Muda La Kiyegeya Morogoro.....Abaini Meneja Wa Tanroads Mkoa Bado Hajateuliwa, Aliyemhamisha Akutwa Bado Yuko ‘site’
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesisitiza kuwa Mameneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wa mikoa yote nchini wanapaswa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa madaraja yote siyo kwa juu tu bali hadi chini ya madaraja ili kujiridhisha na usalama wake.
“Nilitoa agizo kwa mameneja wa TANROADS ambao wana highways, wazikague kila mara kwa sababu hatuhitaji kuwa na highways zilizobomoka.”
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Machi 10, 2020) wakati akizungumza na watendaji wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na viongozi wa Mkoa wa Morogoro, mara baada ya kutembelea eneo hilo na kukagua ujenzi wa barabara ya muda ili kurejesha mawasiliano na mikoa mingine.
“Nimekuja kuona kazi inaendeleaje, nimekuta msongamano wa magari hakuna kama ilivyokuwa wiki iliyopita. Ile diversion (barabara ya mchepuko) imesaidia kuondoa msongano uliokuwepo,” amesema Waziri Mkuu.
“Mahitaji yetu ni kuwa na daraja la kudumu, kwa hiyo mharakishe ujenzi wa daraja hilo, Mmesema sasa hivi mnapanga kuweka daraja la zege ili maji yakija kwa wingi yaweze kupita juu ya hii barabara ya muda, msisitizo ni kukamilisha kazi ya daraja la kudumu,” amesema wakati akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale.
Katika ukaguzi huo, Waziri Mkuu alibaini kuwa Meneja wa TANROADS, mkoa wa Morogoro, Mhandisi Godwin Andalwisye ambaye aliagiza arejeshwe wizarani na nafasi yake ijazwe na mtu mwingine, bado alikuwepo kwenye eneo la tukio akiendelea na kazi.
“Uamuzi niliochukua wa kumhamisha Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro ulikuwa sahihi kwa sababu huyu Bwana anaonekana hawezi kazi ya kusimamia wengine. Fedha ya ukaguzi ipo, ya ujenzi ipo, halafu kazi haifanyiki. Kazi ya kusupervise haiwezi, kwa hiyo, ateuliwe Meneja mwingine,” alisisitiza.
“Nilimuuliza meneja aliyekuwepo kama wana fedha za ukaguzi, akasema anayo. Nikamuuliza kama anayo fedha ya spot maintenance, akasema anayo. Fedha hizi zote zilipaswa zitumike kwa kazi iliyopangwa, lakini hilo halikufanyika.”
Akijibu hoja hiyo, Mhandishi Mfugale alisema amemuacha Mhandisi Godwin Andalwisye aendelee kuwepo pale site kwa sababu ya utalaamu wake kweye madaraja. “Ulishatoa maelekezo kuwa aondolewe, na wa kumhamisha ni mimi, tunatumia tu utaalmu wake.
Alipoulizwa kama ameshateua Meneja mwingine wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Mfugale alikiri kwamba bado hajamteua mtu mwingine.
Jumatano iliyopita, (Machi 4, 2020) Waziri Mkuu alikatisha ziara yake mkoani Tanga na kutembelea eneo hilo ambako alishuhudia mlundikano wa magari na abiria hali ambayo haikumfurahisha.
Aliagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Morogoro, Mhandisi Godwin Andalwisye arejeshwe wizarani na nafasi yake ijazwe na mtu mwingine mara moja kwa sababu ya kuzembea kutimiza wajibu wake.
Waziri Mkuu ambaye alisafiri kwa magari kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, pia alisimama Morogoro na kukagua ujenzi wa uzio wa makaburi ya Kola Hill ambako walizikwa wahanga wa ajali ya lori la mafuta lililopinduka na kulipuka Agosti 10, 2019 na kuua watu 115, kati yao wanaume walikuwa ni 109 na wanawake ni sita.
Akiwa makaburini hapo, Waziri Mkuu aliuagiza uongozi wa Manispaa ya Morogoro uweke utaratibu wa kuwa na mtu maalum atakayesimamia masuala ya mazishi yote yatakayofanyika kwenye makaburi ya Kola Hill.
Amesema mtu huyo ahakikishe makaburi yote yanachimbwa katika utaratibu na mpangilio utakaoliwezesha eneo hilo kuwa na nafasi ya kuzika watu wengi. “Utaratibu wa sasa wa kuchimba makaburi kiholela utalifanya eneo hili lijae haraka huku likiwa halina mpangilio maalum.”
Waziri Mkuu pia aliridhia maombi ya uongozi wa mkoa wa Morogoro ya kutaka akubali makaburi hayo yajengewe ili yawe na muonekano mzuri kazi ambayo itagharimu zaidi ya sh. milioni 12.
Uongozi huo pia uliomba rdhaa ya Waziri Mkuu kutengeneza mandhari ya ndani ya uzio (Landscaping) kazi ambayo itagharimu sh. 1,682,500/- pamoja na kujenga mnara wa kumbukumbu kwa gharama ya sh. 4,173,125/-.
(mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu Majaliwa Kufungua Mkutano wa Mawaziri SADC kwa Njia ya Video
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa anatarajiwa kufungua kikao cha Baraza la Mawaziri wa Nchi wanachama wa jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wanaoshughulikia Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Fedha Uchumi pamoja na viwanda na Biashara Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Machi kwa njia ya Video kufuatia tishio la virusi vya Corona.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Kanali Wilbert Ibuge katika kituo cha mikutano Mwalimu Nyerere (JNICC) baada ya kutoa taarifa fupi ya kikao cha dharura cha Mawaziri wa SADC sekta ya Afya kilichojadili hali halisi ya Ugonjwa wa Corona (CODIV- 19) katika Nchi za SADC.
Amesema Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na kuendeshwa kwa njia ya mfumo wa Video (Video Conference) kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Corona (CODIV-19) ulioikumba nchi ya Afrika ya Kusini ambayo pia ni Nchi mwananchama wa Jumuiya ya SADC.
“Kufatia Ushauri uliotolewa katika maazimio ya kikao cha Mawaziri wa Afya wa SADC, kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC sasa hivi kitafanyika kwa njia ya video tofauti na ilivyozoeleka, hivyo kila Nchi mwanachama wa SADC atakuwa nchini kwake huku tukijadili kwa njia ya video” alisema Balozi Ibuge.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mtendaji wa Maswala ya Ushirikiano wa Kikanda (SADC) Thembinkosi Mhlongo amesema kuna haja ya Nchi wanachama wa SADC kutumia hati ya kusafiria (Pasport) inayoweza kukumruhusu kila Mwanachama kusafiri na kufanya Shughuli za maendelo katika umoja wa SADC bila bugudha.
“Umoja wa Mataifa na jumuiya nyingine mengine wana Hati zao za kusafiria, na sisi tunahaja ya kuwa na hati zetu za kusafiria tukiwa kama SADC, katika jumuiya yetu kuna watu watafanyakazi kwa muingiliano wa kikanda hivyo ni muhimu kutumia hati moja” Alisema Mhlongo.
Miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa katika mkutano huo ni mazingira wezeshi ya maendeleo ya viwanda, masuala ya fedha na Michango ya Jumuiya, hati za kusafiria za SADC, na uanzishwaji wa shirika la utalii kwa nchi za kusini mwa Afrika.
Mwisho.