Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewatia hatia viongozi nane wa Chadema na aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho Dk Vincent Mashinji.
Washtakiwa hao wametiwa hatiani katika mashtaka 12 kati ya 13, yaliyokuwa yanawakabili ikiwemo la uchochezi.
Uamuzi wa kuwatia hatiani, umetolewa leo Jumanne, Machi 10, 2020 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka na ule wa utetezi.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya mahakama kuwatia hatiani washtakiwa hao, ndugu, jamaa na marafiki waliopo ndani ya mahakama hiyo walianza kulia kimya kimya huku wakifuta machozi.
0 comments:
Post a Comment