Wednesday, 5 February 2020

Programme Officer Job (Labour Migration) – P2 at IOM – UN Migration Arusha, Tanzania

Position Title : Programme Office (Labour Migration) Duty Station : Arusha, Tanzania, United Republic of Classification : Professional Staff, Grade P2 Type of Appointment : Special short-term graded, Six months with possibility of extension Estimated Start Date : As soon as possible Closing Date : 16 February 2020 Established in 1951, IOM is a Related Organization of the… Read More »

The post Programme Officer Job (Labour Migration) – P2 at IOM – UN Migration Arusha, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

80 Health Jobs at The Benjamin William Mkapa Foundation February 2020

80 Health Jobs at The Benjamin William Mkapa Foundation February 2020 The Benjamin William Mkapa Foundation has been accredited by the Ministry of Health, Social Development, Gender, Elderly and Children to implement the Reliability and Sustainable Health System (RSSH) Project through funding from the World Fund for AIDS, Tuberculosis and Malaria (Global) Fund). This project aims to strengthen health… Read More »

The post 80 Health Jobs at The Benjamin William Mkapa Foundation February 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUTATHMINI UCHUMI WAKE BILA KUTEGEMEA MASHIRIKA YA KIMATAIFA PEKEE


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akipeana mkono na Kiongozi wa Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Bw. Sikhumbuzo Dlamini, baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao, Jijini Dodoma.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) na Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ukiongozwa na Bw. Sikhumbuzo Dlamini (kushoto), wakiwa katika Mkutano katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akielezea umuhimu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), kutathmini ukuaji wa uchumi, wakati wa Mkutano wa Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ulioongozwa na Bw. Sikhumbuzo Dlamini kutoka Eswatini, Jijini Dodoma
Kiongozi wa Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Bw. Sikhumbuzo Dlamini akifafanua jambo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani), ambapo aliipongeza Serikali kwa kazi nzuri inayofanya katika kukuza uchumi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto), akimuongoza mgeni wake ambaye ni kiongozi wa Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Bw.  Sikhumbuzo Dlamini, ulipotembelea katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), uliongozwa na Bw. Sikhumbuzo Dlamini (wa nne kulia), pamoja na viongozi wa Wizara hiyo na wajumbe kutoka SADC, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ukiongozwa na Bw. Sikhumbuzo Dlamini (katikati), wakifuatilia mada  zilizokuwa zikiwasilishwa katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wakifuatilia mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ukiongozwa na Bw. Sikhumbuzo Dlamini (hayupo pichani) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
(Picha na Peter Haule, WFM, Dodoma)

Na Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dodoma

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa nchi za Afrika hasa zilizopo chini ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) zinatakiwa kujitazama na kushauriana kuhusu mwenendo wao wa uchumi badala ya kuyaachia Mashirika ya Kimataifa pekee.

Rai hiyo imetolewa Jijini Dodoma wakati wa Mkutano kati yake na Ujumbe wa SADC unaoongozwa na Bw. Sikumbuzo Dlamini, ambao umetembelea nchini kwa ajili ya Mpango wa kujitathmini kiuchumi kwa mwaka wa Fedha 2019/20.

Dkt. Mpango alisema kuwa nchi za Afrika zimezoea kuona Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) au kuja kuangalia namna gani Uchumi unavyoendelea ili hali   Afrika hasa nchi za SADC zina fursa pia ya kutembeleana na kushaurina namna bora ya kuendeleza uchumi na kuwahudumia wananchi ikizingatiwa kuwa nchi hizo zinafahamiana vizuri.

“Madhumuni ya ujumbe wa SADC kutembelea nchini ni kuangalia hali ya ukuaji wa uchumi, ubadilishanaji wa fedha za kigeni, mauzo ya bidhaa ndani na nje ya nchi na kushauri mahali ambapo Tanzania haijafanya vizuri au kutumia fursa ipasavyo’’, alieleza Dkt. Mpango.

Alisema kuwa nchi za SADC zilikubaliana kuchagua ujumbe ambao utakuja nchini kufuatilia namna uchumi Mkuu unavyoendelea, hivyo ametumia fursa hiyo kueleza utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya Umeme wa Maporomoko ya Mto Rufiji, ujenzi wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) na miundombinu mingine ya barabara.

Kwa upande wake Kiongozi wa Ujumbe wa SADC, Bw. Sikumbuzo Dlamini, ambaye pia ni Meneja wa Sera za Uchumi na Takwimu wa Benki Kuu ya Eswatini, ameipongez Tanzania kwa maendeleo makubwa iliyofikia baada ya kujionea miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya Reli, miradi ya maji ambayo itasaidia ukuaji wa uchumi Uchumi Mkubwa na kuiwezesha kufikia Malengo ya Maendeleo endelevu.
Share:

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KATIBU MTENDAJI WA SADC, BALOZI WA UMOJA WA ULAYA (EU) NA BALOZI WA CHINA NCHINI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) hapa nchini Balozi Manfredo Fanti aliyeongozana na Balozi Emilio Rosetti alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam Februari 5, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) hapa nchini Balozi Manfredo Fanti aliyeongozana na Balozi Emilio Rosetti alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam Februari 5, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea  na Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) hapa nchini Balozi Manfredo Fanti aliyeongozana na Balozi Emilio Rosetti alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam Februari 5, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza baada ya mazungumzo Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam Februari 5, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) hapa nchini Balozi Manfredo Fanti baada ya kukutana naye Ikulu jijini Dar es salaam Februari 5, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Dkt. Stergomena Tax alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam Februari 5, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Bw. Mkundi Mutasa aliyeongozana na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Dkt. Stergomena Tax aliyekutana naye kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam Februari 5, 2020. Kulia ni Mkuu wa Itifaki Kanali Wilbert Ibuge
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo  na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Dkt. Stergomena Tax aliyeongozana na Afisa wake mwandamizi Bw. Mkundi Mutasa alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam Februari 5, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Dkt. Stergomena Tax baada ya kukutana na kufabya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam Februari 5, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang Ke alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam Februari 5, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang Ke  alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam Februari 5, 2020. Kulia ni Mkuu wa Itifaki Kanali Wilbert Ibuge.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang Ke alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam Februari 5, 2020
PICHA NA IKULU
Share:

Masauni: Polisi haina pesa ya kufunga CCTV

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amewataka Wabunge kushirikiana na wadau mbalimbali katika maeneo yao kwa lengo la kuhakikisha wanachangia upatikanaji wa CCTV Camera, zitakazofungwa katika vituo vya polisi nchini ili kuepusha malalamiko ya wananchi.

Hayo ameyabainisha leo Februari 5, 2020, Bungeni Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Tauhida Gallos, lililohoji umuhimu wa kufunga CCTV Camera katika vituo vya polisi, zitakazomuwezesha Mkuu wa Kituo kufuatilia na kujua ni nini kinachoendelea kituoni.

"Jeshi la Polisi halina bajeti ya kuwezesha ufungaji wa CCTV Camera vituoni, hivyo Wabunge mshirikiane na wadau ili Camera hizo zinunuliwe zifungwe na kupunguza malalamiko ya huduma isiyo na weledi ya askari kwa wananchi" amesema Mhandisi Masauni.


Share:

Vigogo Wengine 6 Wa Jeshi La Zimamoto Wawasili TAKUKURU Makao Makuu Dodoma Kuhojiwa

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waliokuwa wajumbe wa kamati ya utekelezaji  wa makubaliano  iliyosainiwa tarehe 22,Agosti ,2019  kati ya jeshi la zimamoto na uokoaji  na kampuni ya ROM Solutions  Co.LTD leo Feb.5,2020 wamewasili ofisi za  Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa [TAKUKURU]makao makuu jijini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na kashfa ya kufanya mkataba mbovu wa Trilioni Moja bila kupitishwa na  bunge.

Idadi ya  wajumbe waliofika katika ofisi hizo leo  ni sita ambapo walifika  ofisi za TAKUKURU pamoja na kompyuta mpakato [Laptop]walizopewa na kampuni ya ROM SOLUTIONS CO.LTD.

Wajumbe hao pia walikuwa wakilipwa posho za vikao USD 800   na kampuni hiyo  wakati wakiwa wanakutana katika vikao vyao  vya majadiliano.

Wajumbe hao ni pamoja na Kamishna wa zimamoto  Mbaraka Semwanza,Naibu Kamishna  wa zimamoto Fikiri Salla,Naibu Kamishna wa Zimamoto  Lusekelo Chaula’.

Wengine ni Naibu Kamishna  zimamoto Ully Mburuko,Mchumi zimamoto Boniface Kipomela  na Mchumi  wa jeshi hilo la zimamoto na uokoaji Felis Mshana.

Ikumbukwe kuwa sakata hilo  la mkataba mbovu  wa Trilioni moja limesababisha aliyekuwa waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola kuachishwa wadhifa huo na kuteuliwa mwingine  hivi karibu George Simbachawene.


Share:

Dkt.Abbasi Asisitiza Mageuzi ya Kiutendaji kwa Menejimenti

Na Anitha Jonas – WHUSM
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt.Hassan Abbasi amewataka viongozi wa menejimenti wa Wizara hiyo kufanya mageuzi kwa kuwa sekta za wizara  hiyo zimebeba ushawishi mkubwa kwa nchi  na dunia.


Dkt.Abbasi ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma baada kuwasili katika ofisi ya wizara hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba na kufanya mazungumzo na viongozi wa Menejimenti kwa lengo la kupata taarifa fupi ya kisekta na makabidhiano ya ofisi.


“Wizara hii imebeba sekta muhimu sana katika nchi ambazo ni soft power na smart power mfano sekta ya Sanaa na Michezo ni burudani na sekta hizi zikisimamiwa vizuri taifa hili litazidi kuwa la amani  na furaha pamoja na uchumi utaongezeka,tutaandaa matamasha ya kitaifa ya burudani kama JAMAFEST ambayo yatashirikisha wasanii na wachezaji sisi ni watumishi wa umma lazima tuoneshe wananchi utendaji wetu na ningependa tuache kufanya kazi kwa mazoea,”alisema Dkt.Abbasi.


 Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho, Dkt. Abbasi alisema kuwa anatarajia kuona utendaji wa pamoja (team work) na utendaji wa kujituma pasipo kuchoka,pia alisisitiza anategemea kutumia vipaji na ubunifu.


Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt. Ally Possi alipokuwa akifanya makabidhiano alimweleza Dkt. Abbasi changamoto mbalimbali za wizara ikiwemo ya uhaba wa fedha katika uendeshaji wa Uwanja wa Taifa na pamoja na Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kuwa na changamoto katika uendeshaji, umuhimu wa  programu hiyo sababu kuwa ni ya kimataifa na faida zake utakaposimamiwa vyema na kukamilika.


“Nakupongeza kwa mapinduzi makubwa unayoyafanya katika Idara ya Habari hakika kazi ni nzuri haswa katika kuisemea Serikali ningeomba kwa upande wa usimamizi wa taaluma ya habari na Vitengo vya Mawasiliano Serikalini huko nako nguvu inahitajika ili kuwa na utendaji wenye usawa katika uwajibikaji wenye tija,’’alisema Dkt.Possi.


Aidha, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw.Marceline Patrick alimpongeza Katibu Mkuu huyo na kumweleza kuwa watumishi wote wamefurahia uteuzi wake na wana imani nae katika kusimamia mabadiliko ya sekta za wizara na wapo tayari kumpa ushirikiano ili kufanikisha hilo.


Halikadhalika  mmoja wa wafanyakazi wa wizara hiyo kutoka Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, Bibi Hadija Kisubi alisema anamshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt.John Pombe Magufuli kwa kumteua Dkt.Abbasi kuwa Katibu Mkuu katika wizara hiyo sababu ni mchapakazi na anaamini kuwa atafanya mabadiliko makubwa katika wizara katika maeneo yote yenye changamoto.


Share:

Mpasuko Mkali Wainyemelea Marekani....Trump Agoma Kumpa Mkono Spika, Spika Naye Kaamua Kuichana Hotuba Yake

Rais Trump kususia mkono wa Spika Pelosi na Pelosi kumjibu kwa kuichana hotuba yake ni baadhi tu ya vitimbi vilivyodhihirisha mgawanyiko mkali wa kisiasa nchini Marekani, wakati Trump alipotoa hotuba kuhusu hali ya nchi.

Tofauti na ilivyozoeleka kuwa hotuba ya rais wa Marekani kuhusu hali ya nchi ni muda wa maridhiano kisiasa, mazingira katika kikao cha Congress kilichowaleta pamoja wajumbe wa baraza la wawakilishi na maseneta yaliakisi mpasuko mkali wa kisiasa muda wote wa saa moja na dakika 18 wa hotuba ya Trump.

Zoezi zima lilianza vibaya pale Rais Trump alipokataa kuupokea mkono alionyooshewa na spika wa baraza la wawakilishi Bi Nancy Pelosi na kuuacha ukining'inia hewani. 


Na lilimalizika kwa hatua ya Pelosi kumjibu Trump mtindo wa jino kwa jino, alipochana vipande vipande nakala ya hotuba ya Trump aliyokuwa amekabidhiwa, mara tu Trump alipomaliza kuzungumza. 

Rais Trump ametumia sehemu kubwa ya hotuba yake kwa majigambo, ya namna alivyofanikiwa kuukarabati uchumi wa Marekani, na hadhi ya nchi hiyo, ambavyo amedai vilikuwa vimewekwa rehani na watangulizi wake. 

Masuala mengine aliyoyamulika Trump katika hotuba yake, ni makubaliano ya kibiashara kati ya China, na mengine ya eneo huria la kibiashara katika nchi za Amerika Kaskazini, akisema hayo ni mafanikio makubwa ambayo yatarejesha maelefu ya viwanda nchini Marekani.

Amezungumzia pia sera za kupunguza kodi na kumaliza kuhusika kwa majeshi ya Marekani katika mizozo ya Mashariki ya Kati, kama ushahidi wa kutimiza ahadi alizozitoa kwa wapiga kura.

Hotuba yake ilishangiliwa mara kwa mara na wabunge wa chama chake cha Republican waliosimama kumpigia makofi, huku wademocrat wakibakia katika viti vyao, baadhi wakizomea, na wengine hata kutoka nje.


Share:

Shilingi Bilioni 1.5 Kujenga Chuo Cha Veta Tabora(Uyui)

Na Daud Tiganya
Halmashauri ya Wilaya ya Tabora(Uyui) limeishukuru Serikali kwa kuwapatia kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA)  cha  kisasa kitakachojengwa  eneo la Isikizya wilayani humo.

Fedha hizo zitasaidia katika ujenzi wa majengo ya fani mbalimbali iiwemo ushonaji, ufundi umeme, uhazili na komputya  na uchomeleaji vyuma (welding)

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Ntahondi katika kikao cha  Baraza la Madiwani wa kupitia taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alisema kukamilika kwa Chuo hicho cha VETA kutasaidia vijana ambao wamemaliza elimu ya Shule za Msingi na Sekondari kusomea kozi mbalimbali ambazo zitawawezesha kujiajiri wenye kwa ajili ya kuondokana na umaskini.

“Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo alisema Hospitali ya Wilaya ya imeanza kufanya kazi kwa kutoa huduma za matibabu ya wagonjwa wan je.

Alisema kuwa hatua hiyo imefikia baada ya agizo la Mkuu wa Mkoa wa Tabora la kumtaka Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo kuanza na utoaji wa huduma za awali katika majengo ambayo yamekamilika ili kuwapunguzia adha za wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za matibabu.

Alisema kwamba kuanza utoaji wa huduma kwa Wagonjwa wa Nje(OPD) kumesaidia kupunguza usumbufu kwa wananachi wa wilaya hiyo kwa kupata huduma za matibabu kuwa karibu na wananchi.

Wakati huo huo Ntahondi alisema kuwa Halmashauri hiyo imetenga shilingi milioni 60 kwa ajili ya ujenzi wa majengo katika Sekondari saba ili kupunguza mrundikano wa wanafunzi wa Kidato cha kwanza.

Alisema sanjari na hilo wanaomba Ofisi ya Kanda ya Udhibiti ubora kuwasaidia ili Shule ya Sekondari ya Idete iweze kupokea wananfunzi wa Kidato cha Tano mwaka huu.

Ntahondi alisema wanaendelea na wanaandalizi kwa ajili ya uanzishwaji kwa Kidato cha Tano kama watakubaliwa ili Wilaya hiyo iweze na Shule za sekondari za Kidato cha tano na sita mbili ikiwemo ya hivi sasa ya Ndono.


Share:

LIVE: Mkutano wa 18 wa Bunge la 11, Kikao cha Saba

LIVE: Mkutano wa 18 wa Bunge la 11, Kikao cha Saba


Share:

Viwanja Vizuri Vinauzwa Bagamoyo Road ....Bei Yake ni Nafuu sana, Karibuni

VIWANJA VIZURI  BAGAMOYO ROAD  -KARIBUNI.......Viwanja vipo km2 kutoka bahari ya Hindi na km 2 kutoka lami yaan unaingilia Mapinga upande wa baharini , Tayari Kuna majirani

Ukubwa wa Heka ni Tsh mil 20 na kwa kiwanja Cha 20/20 ni Tsh mil 3.5 , kiwanja 20/30 mil 5.5 , kiwanja Cha 20/40 ni Tsh mil 7  

Pia Vipo vya Mapinga center Vimepimwa sqmeter Tsh 17000 na vya jirani na shule ya Baobab Bei Tsh Bei mil 9,.

Unaweza kulipa kwa awamu mbili....kwa maelezo zaidi piga 0677705808 Tuongee, Karibuni sana


Share:

Mahakama ya Iran yamhukumu kifo jasusi wa CIA

Msemaji wa Idara ya Mahakama nchini Iran Bw. Gholam Hossein Esmaili, amesema Mahakama Kuu ya nchi hiyo imemhukumu kifo raia mmoja wa Iran ambaye ni jasusi wa Shirika la Upelelezi la Marekani, CIA.

Shirika la habari la Iran Fars limemnukuu Bw. Esmaili akisema kuwa, Amir Rahimpour, ambaye alikuwa mpelelezi wa CIA, alipewa kiasi kikubwa cha pesa ili kutoa baadhi ya taarifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran kwa idara ya ujasusi ya Marekani.

Ameongeza kuwa watu wengine wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka 10 kila mmoja gerezani kwa tuhuma za kufanya upelelezi kwa ajili ya Marekani.


Share:

Raia Burkina Faso kupatiwa silaha kupambana na wanamgambo wenye uhusiano na makundi ya kigaidi

Wabunge nchini Burkina Faso wamepitisha kwa kauli moja muswada utakaowezesha raia wa kupewa silaha ili kupambana na makundi yenye ya waasi.

Muswada huo ambao sasa unasubiri kutiwa saini na Rais unalengo la kupunguza mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo wenye uhusiano na makundi ya al-Qaeda na Islamic State.


Muswada hu unasema kuwa, uwezo wa jeshi wa kupambana na wanamgambo na makundi ya wabeba silaha hautoshi kutokana na idadi yao kuwa ndogo na kuna ukosefu wa mafunzo yanayofaa.

Burkina Faso, kama zilivyo nchi jirani za Mali na Niger imekuwa ikiandamwa na mashambulio ya kigaidi ya mara kwa mara, ambapo tangu mwaka 2015 hadi sasa watu 750 wameshauawa na wengine zaidi ya 560,000 wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mashambulio hayo.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, mashambulio ya kigaidi yaliyofanywa katika eneo la magharibi mwa Afrika katika mwaka uliomalizika wa 2019 yameua raia elfu nne wa nchi za eneo hilo.

Hata hivyo, hatua hiyo imepingwa na baadhi ya wadau wa haki za binadamu kwa madai kuwa ni hatari kwa usalama wa raia.


Share:

Iraq: Maandamano Yasababisha Vifo 536 Ndani Ya Miezi 4

Kamati ya haki za kibinadamu ya bunge la Iraq imetoa taarifa ikisema, maandamano yaliyotokea katika sehemu mbalimbali za Iraq katika miezi minne iliyopita, yamesababisha vifo vya watu 536 na wengine elfu 23 kujeruhiwa. 

Taarifa hiyo imesema kuanzia Oktoba mosi mwaka jana hadi Januari 30 mwaka huu, maandamano hayo yamesababisha vifo vya waandamanaji 519 na wengine elfu 20 hivi kujeruhiwa, huku askari 17 wakifariki na wengine elfu 3.5 wakijeruhiwa kwa upande wa kikosi cha usalama.


Share:

Palestina yakaribisha uungaji mkono wa EU na AU kukataa mpango wa amani wa Marekani kuhusu Mashariki ya Kati

Palestina imepongeza Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika kwa uungaji mkono wao kwa Palestina kukataa mpango wa Marekani kuhusu amani ya Mashariki ya Kati.

Waziri wa mambo ya nje wa Palestina Bw. Riyad al-Maliki amepongeza taarifa zilizotolewa na mwakilishi mwandamizi wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki ambazo wamekataa mpango wa Marekani.

Habari nyingine zinasema mwenyekiti wa baraza la utawala la Sudan Bw. Abdel Fattah al-Burhan amesisitiza tena msimamo wa Sudan kuiunga mkono Palestina na haki za watu wa Palestina kuanzisha nchi yao huru. 

Bw. Al-Burhan amesema hayo baada ya kukutana na waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu nchini Uganda.


Share:

Watu waliofariki dunia kwa virusi vya Corona wafikia 425 nchini China

Idadi ya watu waliofariki dunia kwa ugonjwa unaotokana na virusi vya Corona imefikia 425.

Kabla ya hapo viongozi wa idara ya afya nchini humo walikuwa wametangaza kuwa idadi ya wahanga wa ugonjwa huo ni 360. 

Hata hivyo ripoti iliyotolewa jana imesema kuwa jumla ya watu elfu 990 wamelazwa katika mkoa wa Hubei na kwamba 576 kati yao wana hali mbaya. 

Virusi vya Corona viliibuka kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka uliopita katika soko la vyakula vya baharini la mji wa Wuhan nchini China.

Hata hivyo mbali na mji huo, virusi hivyo sasa vimeenea katika nchi 18 za dunia. Hii ni katika hali ambayo mashirika mengi ya ndege likiwemo Shirika la Ndege la Qata, Air Canada, Air France, Air Seoul, American Airlines, British Airways, Lufthansa, Turkish Airlines na mengine kadhaa, yamesimamisha safari zao kuelekea China kutokana na hatari ya virusi hivyo.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano February 5











Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger