Saturday, 7 December 2019
Milioni 11 Zatumika Kulipia kadi za bima ya afya iliyoboreshwa (CHF) Kwa Wazee Kahama
Mazingira Ya Uwekezaji Katika Sekta Ya Mifugo Na Uvuvi Yaboreshwa Zaidi
Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Na Kidato Cha Kwanza 2020 Mkoa Wa Njombe
Mdogo wa Marehemu Steven Kanumba, Seth Bosco Afariki Dunia
“Mdogo wangu Seth alikuwa anasumbuliwa na uvimbe kwenye uti wa mgongo akafanyiwa upasuaji na tukawa tunamuuguza nyumbani kwa Mama hapa Kimara Temboni, Jana jioni akalalamika maumivu yanazidi tukampeleka Muhimbili akapata afadhali tukarudi nae nyumbani
“Tuliporudi nyumbani kutokea Muhimbili alikuwa yuko vizuri tu, akaomba alale kidogo kisha tumuamshe aangalie TV kuna kipindi anakipenda, akiwa kitandani akafariki, tulikuwa na Daktari nyumbani anasema Seth alipata shida ya kupumua, pumzi zilimuishia
“Mwili wa Seth kwa sasa umehifadhiwa Muhimbili na shughuli zote za Mazishi zinafanyika hapa Kimara Temboni DSM, nyumbani kwa Mama Kanumba” - Amesema Abela (Dada wa Maremu)
Friday, 6 December 2019
Kyela Mbeya Form One selection 2020
Kyela Mbeya Form One selection 2020 The List of Selected Candidates is available for each Ward Education Coordinator, Each Board’s Advertising Boards and the Office of the Regional Head Office, Check it here http://Mbeya.go.tz/ Form one selection for the academic year 2020 The following Kyela Mbeya students have been selected to join form one for the academic year… Read More »
The post Kyela Mbeya Form One selection 2020 appeared first on Udahiliportal.com.
Chunya Mbeya- Form one selection 2020
Chunya Mbeya- Form one selection 2020 The List of Selected Candidates is available for each Ward Education Coordinator, Each Board’s Advertising Boards and the Office of the Regional Head Office, Check it here http://Mbeya.go.tz/ Form one selection for the academic year 2020 The following Chunya Mbeya students have been selected to join form one for the academic year… Read More »
The post Chunya Mbeya- Form one selection 2020 appeared first on Udahiliportal.com.
Mbeya Jiji – Form one selection 2020
Mbeya Jiji – Form one selection 2020 The List of Selected Candidates is available for each Ward Education Coordinator, Each Board’s Advertising Boards and the Office of the Regional Head Office, Check it here http://Mbeya.go.tz/ Form one selection for the academic year 2020 The following Mbeya Jiji students have been selected to join form one for the academic… Read More »
The post Mbeya Jiji – Form one selection 2020 appeared first on Udahiliportal.com.
Busokelo Mbeya – Form one selection 2020
Busokelo Mbeya – Form one selection 2020 The List of Selected Candidates is available for each Ward Education Coordinator, Each Board’s Advertising Boards and the Office of the Regional Head Office, Check it here http://Mbeya.go.tz/ Form one selection for the academic year 2020 The following students have been selected to join form one for Busokelo Mbeya Secondary schools… Read More »
The post Busokelo Mbeya – Form one selection 2020 appeared first on Udahiliportal.com.
Form One Selection 2020 Mbeya Region
The List of Selected Candidates is available for each Ward Education Coordinator, Each Board’s Advertising Boards and the Office of the Regional Head Office, Check it here http://Mbeya.go.tz/ Form one selection for the academic year 2020 The following students have been selected to join form one for Mbeya Secondary schools for the academic year 2020. HALMASHAURI YA BUSOKELO.pdf… Read More »
The post Form One Selection 2020 Mbeya Region appeared first on Udahiliportal.com.
Procurement Officer Job Opportunity at Aga Khan University
Procurement Officer The Aga Khan University empowers the people of the developing world with the knowledge and skills to realize their highest goals. We provide a transformative education that prepares our graduates for local and global leadership. We generate solutions to problems that affect millions of people through pioneering research. We strive to achieve world-class excellence, inspiring individuals… Read More »
The post Procurement Officer Job Opportunity at Aga Khan University appeared first on Udahiliportal.com.
Programme Officer Infrastructure Job Opportunity at European Development Fund
Programme Officer Infrastructure European Development Fund – Programme Support Unit (EDF – PSU) is within the Ministry of Finance and Planning, established under the External Finance Division. The European Development Fund (EDF) is the European Union’s (EU) main instrument for providing development aid to African, Caribbean and Pacific (ACP) countries and to Overseas Countries and Territories (OCTs).The activities… Read More »
The post Programme Officer Infrastructure Job Opportunity at European Development Fund appeared first on Udahiliportal.com.
Finance Officer Job Opportunity at European Development Fund
Finance Officer European Development Fund – Programme Support Unit (EDF – PSU) is within the Ministry of Finance and Planning, established under the External Finance Division. The European Development Fund (EDF) is the European Union’s (EU) main instrument for providing development aid to African, Caribbean and Pacific (ACP) countries and to Overseas Countries and Territories (OCTs).The activities of… Read More »
The post Finance Officer Job Opportunity at European Development Fund appeared first on Udahiliportal.com.
Call for Interview at District Council -December 2019
Call for Interview at District Council -December 2019
The post Call for Interview at District Council -December 2019 appeared first on Udahiliportal.com.
Mifuko Mbadala Isiyokidhi Viwango Marufuku Nchini
Serikali imesema kamwe haitaruhusu uzalishaji, uingizaji na matumizi ya mifuko mbadala aina ya Non-Woven isiyokidhi viwango vya 70 Gram Per Square Metre (GSM) kutumika nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mussa Sima katika Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashara na Wawekezaji uliolenga kusikiliza na kutatua changamoto zao, Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Kibaha mkoa wa Pwani.
Awali akiwasilisha taarifa ya Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amesema kuwa kumekuwa na uchelewashaji wa utoaji wa vibali vya kuingiza mifuko mbadala nchini kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira hali ambayo inaleta vikwazo kwa wafanyabiashara na wawekezaji.
Akitoa ufafanuzi wa ucheleweshaji wa vibali hivyo Mhe. Sima amesema kuwa Serikali imepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki nchini tangu Juni Mosi 2019 na kutoa fursa kwa wakezaji kuagiza na kuzalisha mifuko mbadala ili kukidhi soko la ndani.
Hata hivyo changamoto imejitokeza kwa wafanyabiashara wasio waaminifu kutaka kuingiza mifuko isiyokidhi viwango aina ya Non-Woven. “Kumeanza kujitokeza uvunjifu wa sheria katika uzalishaji na uingizaji wa mifuko mbadala aina ya non-woven. Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeweka vigezo vya mifuko mbadala aina ya non-woven inayoweza kutumika nchini ikiwa ni pamoja na Uzito usiopungua GSM 70 (Gram per Square Metre), iweze kurejelezwa, Ioneshe uwezo wa kubeba, anuani ya mzalishaji na iwe imethibishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS)” Sima alifafanua.
Amesisitiza busara itumike katika kumaliza mgogoro uliopo baina ya mfanyabiashara aliyeagiza bidhaa hiyo huo bila kuathiri upande wowote kwa kutoa mapendekezo kwa mfanyabiashara mwenye mzigo husika kuurejereza ama kuusafirisha nje ya chini ya uangalizi maalumu na kuagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Shirika la Viwango nchini (TBS) kumaliza suala hilo mapema iwezekanavyo.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Sima amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imefanya mapitio ya Kanuni za Taka Hatarishi za mwaka 2009 na kutunga Kanuni mpya ya mwaka 2019 ambazo zimezingatia Mkataba wa Basel yaani Basel Convention for transboundary Movement of Hazadous Waste ambao Tanzania imeridhia baada ya awali biashara hiyo hairatibiwi ipasavyo
“Kwa mujibu wa Mkataba huu, mfanyabiashara anapotaka kuingiza Hazadous Waster ikiwemo chuma chakavu pamoja na masharti mengine ni lazima nchi ambapo chuma chakavu kinatoka kupata kibali cha Serikali ya nchi husika ili kuthibitisha kuwa nchi hiyo imeruhusu usafirishaji huo” Sima alisisitiza.
Amefafanua kuwa malighafi inayotumika na Viwanda vya ndani imekuwa ikipelekwa nje, hivyo Serikali imeweka masharti magumu kwa lengo la kulinda viwanda vya ndani na kuruhusu kusafirishwa kwa malighafi ambayo haitumiki hapa nchini.
Naibu Waziri Sima amewahimiza wawekezaji kuwekeza katika Mkoa wa Pwani na kutumia nishati ya gesi kwa wingi. “Ni viwanda 48 tu nchi nzima ndio vinatumia nishati ya gesi, wawekezaji wekeni nia ya matumizi ya Gesi ili TPDC waweke miundombinu stahiki, nawasihi ndugu zangu tulinde mazingira yetu”
Siku ya pili ya mkutano wa Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashara na Wawekezaji umefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Kibaha mkoa wa Pwani na kuhudhuriwa na washiriki kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Pwani.
Temporary jobs (Tume ya Taifa ya uchaguzi) at Iringa Municipal council-December 2019
Temporary jobs (Tume ya Taifa ya uchaguzi) at Iringa Municipal council-December 2019 BVR Kit Operators.
The post Temporary jobs (Tume ya Taifa ya uchaguzi) at Iringa Municipal council-December 2019 appeared first on Udahiliportal.com.
Rais Dkt. Magufuli apata tuzo kwa kuimarisha Diplomasia ya Uchumi wa nchini.
Shirika lisilo la Kiserikali la Kuinua Diplomasia ya Uchumi Tanzania (TEDEF) limetambua juhudi na kuthamini kazi anazofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. John Pombe Magufuli kuhakikisha azma ya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025 inafikiwa.
TEDEF imemtunuku tuzo Rais Dkt. Magufuli na kuwa miongoni mwa Watanzania 10 waliofanya vizuri kwa kutoa mchango wao katika kuimarisha Diplomasia ya Uchumi wa nchini.
Akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Rais Dkt. Magufuli na kuwakabidhi tuzo hizo watanzania wengine waliomstari wa mbele kuinua diplomasia ya uchumi nchini Desemba 5, 2019 katika ukumbi wa Karimjee uliopo jijini Dar es salaam, Naibu Waziri Wa Habari, Utamaduni, Sanaa Na Michezo Juliana Shonza ameishukuru TEDEF kwa uamuzi wao wa kushirikiana na Serikali katika kuimarisha diplomasia ya Uchumi nchini.
“Diplomasia ya Uchumi ni Muhimu kwa ustawi wa Taifa. Mataifa yote makubwa duniani yameupa umuhimu wa kwanza Diplomasia ya Uchumi ambao umekuwa ni muhimili wa kukuza mataifa hayo. Nanyi TEDEF mmekuwa wazalendo kwa kutambua na kuthamini mchango wa viongozi na wananchi mbalimbali katika kuhakikisha nchi yetu inafikia azma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati” alisema Naibu Waziri Shonza.
Miongoni mwa kazi zilizomfanya Rais Dkt. Magufuli kupewa tuzo hiyo mchango wake katika kujenga miundombinu ya kufanikisha Diplomasia ya Uchumi Tanzania ikiwemo miradi ya reli ya kisasa (SGR), kuimarisha shirika la ndege, ujenzi wa barabara na madaraja mbalimbali nchini pamoja na Mradi wa umeme Bwawa la Nyerere.
Watanzania wengine waliopata tuzo za kushiriki kujenga diplomasia ya uchumi ni mawaziri wawili ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi kwa kuongoza majadiliano ya Biashara ya Kimataifa baina ya Tanzania na Kampuni ya Madini ya Barrick kwa mafanikio makubwa kwa Tanzania pamoja na Wiziri wa Mambo ya Ndani nchi Kangi Lugora ambaye anasimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao kwa kutambua amani iliyojengeka ni muhimu kwa kufanikisha Diplomasia ya Biashara na Diplomasia ya Uchumi.
Tuzo hizo pia zimeenda kwa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi ambao nao wametambuliwa kwa mchano wao katika kujenga diplomasia ya uchumi; Ubalozi wa Tanzania Nchini Rwanda ukiongozwa na Balozi Ernest Mangu ambao umeongoza kwa mauzo ya nje katika nchi za Afrika Mashariki, Ubalozi wa Tanzania nchini China ukiongozwa na Balozi Mbelwa Kairuki kwa kwa kuongoza katika uwekezaji mitaji nchini pamoja na Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani ukiongozwa na Balozi Wilson Masilingi ambao umeongoza kwa kuleta watalii nchini.
Mbali na viongozi hao, Mkoa wa Dar es Salaam ambao unaongozwa na Mkuu wa mkoa huo Paul Makonda nao umepata tuzo hiyo kwa kuongoza kwa miradi ya uwekezaji ambapo takribani miradi 109 imesajiliwa.
Aidha, Watanzania wengine ambao wametambuliwa kwa mchango wao katika kushiriki katika kuitangaza Tanzania kimataifa katika diplomasia ya uchumi na kupewa tuzo hiyo ni mchezaji wa mpira wa miguu Mbwana Samata kupitia sekta ya michezo, mwanamuziki Nasibu Abdul (Diamond) kupitia sekta ya muziki pamoja na mtangazaji wa TBC Elisha Elia anayetangaza kipindi cha Kishindo cha Awamu ya Tano na kusaidia kutangaza miundombinu ya Diplomasia ya Biashara na Diplomasia ya Uchumi kupitia sekta ya habari.
Kwa upande wake Mkurugenzi na Makamu Mwenyekiti Bodi ya TADEF Dkt. Wilbroad Mtabuzi ameyataja baadhi ya majukumu ya msingi ya shirika hilo kuwa ni pamoja na kuvutia uwekezaji hasa kwenye viwanda, Kuhamasisha biashara ya kimataifa kuhamasisha utalii, kutangaza sifa njema za nchi yetu ambayo ni amani, utulivu na umoja wa Kitaifa ambapo majukumu hayo yatasaidia kuchangia kasi yakuufikia uchumi wa kati.
Dkt. Mutabuzi amesema kuwa TEDEF imefanikiwa kuunda vyama vya ushirika kwa wahimitimu wa elimu ya juu nchini ambao wamejiajiri katika katika sekta ya kilimo-biashara kwenye mikoa ya mikoa ya Dare es salaam, Pwani, Dodoma, Kigoma, Mbeya na Mwanza.
Wahitimu hao wamefanikiwa kuanzisha vikundi vya ufugaji samaki kibiashara katika mkoa wa Pwani eneo la Ruvu wilayani Bagamoyo pamoja na kuwasaidia wakulima zaidi ya 2000 wanaojishughulisha na kilimo wamenufaika na huduma za TEDEF nchini.
Sera ya Diplomasia ya Uchumi Mwaka 2001 nchini ilianza kutekeleza kufuatia idhini ya Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa mwaka 2000 ikitambua kuwa Diplomasia ya Uchumi ni Ustawi ambapo ushiriki wa TEDEF katika diplomasia hiyo una mchango katika kuleta ustawi katika nchini.
-Mwisho-




















