Saturday, 24 August 2019

Picha : BARAZA LA WAZAZI CCM KAHAMA LAMPONGEZA MAGUFULI KUWA MWENYEKITI WA SADC...SIMBA ATAKA WINGU LA MAKUNDI KUYEYUKA

Baraza la Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga limetoa tamko la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Tamko hilo limetolewa leo Jumamosi Agosti 24,2019 wakati wa kikao cha kawaida cha Baraza la Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Kahama kilichofanyika katika kijiji cha Magung'humwa kata ya Mwakata wilayani Kahama.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba, na Katibu wa CCM wilaya ya Kahama,Emmanuel Lameck Mbamange.

Akisoma tamko hilo,Katibu wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) wilaya ya Kahama,Disco Wabare amesema kuchaguliwa kwa rais Magufuli kuongoza SADC inaonesha dhahiri imani waliyonayo viongozi wa SADC kutokana na umahiri na utendaji kazi wake kwa wananchi wa Tanzania na Jumuiya ya SADC.

"Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa baraza la Wazazi la wilaya ya Kahama kwa pamoja tunatoa tamko la kumpongeza Rais wetu mpendwa,mwenyekiti wa CCM taifa,Amiri Jeshi Mkuu na mtetea wanyonge, Mhe. John Pombe Magufuli kuwa mwenyekiti mpya wa SADC",amesema.

"Sisi kama Baraza la Wazazi Kahama tunategemea kuona mabadiliko makubwa katika uongozi wake hasa katika kukuza uchumi wa nchi za SADC na kuondoa tatizo la ajira ambalo limekuwa kikwazo kikubwa kwa vijana wa nchi hizo",ameongeza Wabare.

Amebainisha kuwa Baraza la wazazi Kahama linaamini kuwa kwa kasi aliyonayo Magufuli katika kuendeleza nchi ya Tanzania kimaendeleo,ataitumia pia katika kuendeleza umoja wa SADC kwa kipindi cha mwaka mmoja aliochaguliwa kuongoza SADC.

Akizungumza katika kikao hicho,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba alisema pamoja na kumpongeza rais Magufuli ni vyema WanaCCM na Watanzania kwa ujumla kumuunga mkono kwa kufanya kazi kwa bidii. 

Simba ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ambapo mkoani Shinyanga zoezi la Uboreshaji Daftari la Wapiga Kura litaanza Agosti 26,2019 hadi Septemba 1,2019.

"Tusiishie kujiandikisha tu bali wakati wa uchaguzi ukifika,naomba tukapige kura,ili kuipa ushindi mnono zaidi naomba wanaCCM wajitokeze kwa wingi kupiga kura. Kila mwanaCCM ajitahidi kuwa na marafiki, wawashiwi wapenzi wa CCM wajitokeze kupiga kura.Tukumbuke kuweka wagombea wanaokubalika kwa kwa wananchi",ameongeza Simba.

"Uchaguzi wa serikali za mitaa ni msingi wa uchaguzi mkuu ujao 2020,ili tushinde kwenye chaguzi hizi,ni lazima tushikamane,tuwe na umoja kwani Umoja ni Ushindi.Naomba wingu la makundi liyeyuke,tushikamane,fitna kwetu ni mwiko",amesema Simba. 

Baraza hilo pia limepokea wanachama wapya kutoka vyama vya Upinzani akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Magung'humwa kata ya Mwakata,Salum Mohammed Salum (CHADEMA) ambaye ameahidi kutoa ushirikiano kuitumikia CCM ili ipate ushindi katika chaguzi mbalimbali zijazo.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba akizungumza wakati wa kikao cha kawaida cha Baraza la Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Kahama kilichofanyika katika kijiji cha Magung'humwa kata ya Mwakata wilayani Kahama leo Jumamosi Agosti 24,2019 .Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba akizungumza wa kikao cha kawaida cha Baraza la Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Kahama.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama,Disco Wabare akisoma tamko la Baraza la Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama,Disco Wabare akimkabidhi wenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba tamko la Baraza la Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba akionesha tamko la Baraza la Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba akiwasisitiza wanaCCM kushikamana na kuachana na makundi ndani ya chama. Simba pia aliwataka Makatibu wa CCM kuwapokea wanachama wapya wanaohitaji kujiunga CCM bila kujali kama wametoka vyama vya upinzani.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba akizungumza katika kikao hicho.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Masanja Salu akiwahamasisha wanaCCM kukijenga chama na kukitetea.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Masanja Salu akizungumza katika kikao hicho.
Katibu wa CCM wilaya ya Kahama,Emmanuel Lameck Mbamange akisisitiza kuwa CCM itaendelea kupokea wanachama wapya wanaotaka kujiunga CCM.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama,Sipilaus Bijampola akizungumza katika kikao hicho.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa kutoka wilaya ya Kahama Machimu Mshono Ndalo akiwashukuru wajumbe wa Baraza la Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama kumchagua kuchukua nafasi hiyo licha ya kwamba hakuwepo wakati wa uchaguzi huo.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji CCM mkoa wa Shinyanga kutoka wilaya ya Kahama, Greyson Tito Obata Okuku akizungumza wakati wa kikao hicho. 
Kikao kinaendelea.
Wajumbe wa kikao cha kawaida cha Baraza la Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Kahama wakiwa ukumbini.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji CCM wilaya ya Kahama na Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Wigehe, Marco Luswaga Shija akielezea mikakati mbalimbali ya uchaguzi. Shija aliwataka wanaCCM kuweka wagombea wanaokubalika.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Magung'humwa kata ya Mwakata,Salum Mohammed Salum (CHADEMA) akikabidhi kadi ya CHADEMA na kujiunga CCM leo huku akiahidi kutoa ushirikiano kuitumikia CCM ili ipate ushindi katika chaguzi mbalimbali zijazo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Magung'humwa kata ya Mwakata,Salum Mohammed Salum (CHADEMA) aliyejiunga CCM leo akielezea sababu za kujiunga CCM "Nimerudi CCM kwa sababu sasa kumenoga".
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

Toleo Jipya la Apple ni Pigo Kubwa kwa Watsapp, Facebook na Zingine Zinazokusanya Taarifa za Watu

Apple, watengenezaji wa Iphone wamesema mwezi wa Tisa mwaka huu watatambulisha teknolojia mpya ya IOS 13 ambayo inaonekana kuwa mwiba kwa Apps za Facebook, Whatsapp na zingine zinazotumia Internet  (voice over internet protocol – VoIP).

Katika toleo hilo,iOS haitaruhusu apps zisizotumika kuendelea kufanya kazi  kwa kificho(background) kwenye iPhone.

Apps zinazotumia teknolojia ya simu kwa njia ya intaneti kama vile Facebook na WhatsApp huwa zinaitaji apps hizo ziendelee kufanya kazi hata kama mtumiaji wa simu hazitumii kwa wakati huo. 

Wao wanadai kwa kufanya hivyo ni rahisi zaidi mtumiaji kupata ujumbe anaotumiwa kwa wakati au kuunganisha haraka call anayopigiwa.

Uamuzi huu wa Apple  umejikita zaidi katika suala la kulinda faragha ya watumiaji wa simu zake. 

Apple wanadai kuwa bado apps hizo zikiwa zinafanya kazi nyuma ya pazia zimekuwa zikikusanya  taarifa  kuhusu utumiaji wa simu wa mtu bila ridhaa yake.

Watengenezaji apps wamepewa hadi Aprili 2020 kuhakikisha apps zao zinafuata utaratibu huu mpya. 

Facebook kwa upande wao wamesema wapo katika majadiliano na Apple kuhusu utaratibu huu mpya.


Share:

Picha : MAFUNZO YA KUANDIKA HABARI KIPINDI CHA UCHAGUZI YAFUNGWA MWANZA,…RPC MULIRO ATEMA CHECHE






Mafunzo ya kuandika habari kipindi cha uchaguzi yaliyokuwa yakitolewa na Mtandao wa asasi za kiraia wa kuangalia uchaguzi Tanzania (TACCEO), chini ya kituo cha Sheria na haki za binadamu (LHRC), namna ya kuongeza tija katika kazi za uandishi ili kutoa elimu kwa umma ikiwemo elimu ya uraia na uchaguzi, yamefungwa rasmi leo Jijini Mwanza.


Akizungumza kwenye uhitimishaji wa mafunzo hayo,Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza Muliro Jumanne Murilo, wakati akiwasilisha mada ya usalama kwa waandishi wa habari, pale wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kuandika habari za uchaguzi, amewataka wanahabari pale wanapokuwa waki ripoti habari kwenye kipindi hicho, wazingatie maadili, Sheria, pamoja na miongozi ambayo hutolewa kwa ajili ya kiusalama, ili wapate kutoa taarifa zao bila ya kubughuziwa.



Amesema kwenye kipindi hicho cha uchaguzi kazi ya Jeshi la Polisi hua ni kulinda Amani kwa watu wote wakiwamo na waandishi wa habari, hasa pale wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kuhabarisha umma, lakini inapotokea hofu ya kiusalama hulazimika kuzuia mtu yoyote yule asipite kwenye eneo hatarishi, ndipo msuguano unapoanza kutokea baina ya Jeshi na waandishi wa habari.


“Tatizo ambalo husababisha msuguano kati ya Jeshi la Polisi na waandishi wa habari, ni pale tunapozuia mtu yeyote yule asipite kwenye eneo la hatari, ndipo wanahabari huanza kutoa vifungu vya kisheria kuwa wana haki ya kutafuta habari, na hatimaye kusababisha kutoelewana,”amesema Muliro.



“Mimi ninapo mweka Askari kwenye kituo cha Point “A”au “B” na kutoa agizo (Order), kuwa hakuna mtu yeyote asipite kwenye eneo hilo, ni vyema waandishi wa habari mkatii magizo hayo na siyo kulazimisha kupita tu, ndipo mtabaki kuwa salama na hakutakuwa na msuguano wowote ule baina ya Jeshi na Media, lengo siyo kuzuia habari bali ni kuhakikisha usalama unaendelea kutawala kipindi hicho cha uchaguzi,”ameongeza.


Pia amewataka waandishi wa habari kwenye kipindi hicho cha uchaguzi, waache kufanyakazi kimazoea pamoja na kutanguliza kujuana, bali wafuate misingi, sheria na miongozi ambayo hutolewa, na siyo kulazimisha kufanya kazi kwa madai kila mtu anatekeleza majukumu yake, ndipo kutaondoa misuguano hiyo, na kila mmoja kuwa salama.



Katika hatua nyingine amewataka waandishi wa habari, kipindi wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao wawe na vifaa kamili vya kazi, vikiwamo na vya kiusalama, kuwa na vitambulisho vya vyombo vyao vya habari, pamoja na kuvaa makoti yaliyoandikwa PRESS, ili wapate kutambulika wakati wa kutafuta habari na kutobughuziwa na mtu yoyote yule.

Naye Mwezeshaji Gasirigwa Sengiyumva ambaye ni mkurugenzi wa taasisi wa vyombo vya habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA), amewataka waandishi wa habari pindi wanapoandika taarifa zao kwenye kipindi hiki cha uchaguzi, wazingatie maadili pamoja na miiko ya taaluma yao ili wapate kutoa taarifa sahihi kwa umma.



Nao baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo, wameupongeza mtandao huo wa asasi wa kiraia wa kuangalia uchaguzi Tanzania (TACCEO), kwa kutoa mafunzo ambayo yatawasaidia kuandika habari kwa ufasaha za uchaguzi, pamoja na kuwa habarisha umma taarifa sahihi.



Mafunzo hayo yameshirikisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Geita, Mwanza, Simiyu, Kigoma, Kagera, Mara, pamoja na Mwanza, ambayo yamedumu kwa muda wa siku tatu kuanzia Agost 22 hadi 24 kwenye ukumbi wa mikutano wa Belmont Hotel Jijini Mwanza.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI



Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza Muliro  Jumanne Muliro akizungumza na waandishi wa habari walioshiriki mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi, na kuwataka wazingatie, maadili, miiko ya taaluma yao, pamoja na miongozo ambayo hutolewa wakati wakitekeleza majukumu yao kipindi cha uchaguzi ili wapate kuwa salama.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza Muliro Jumanne Muliro , akiwaeleza waandishi wa habari kuwa usalama wao wakati wa kuandika habari kipindi cha uchaguzi upo mikononi mwao kwa asilimia 70, endapo wakiti miongozo, Sheria, maadili, maagizo ambayo hutolewa, kuwa na vifaa vya kazi, yakiwamo mavazi ya kiusalama, pamoja na kuvaa vitambulisho na makoti yaliyoandikwa PRESS.

Mwezeshaji Gasirigwa Sengiyumva ambaye ni mkurugenzi wa taasisi wa vyombo vya habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA),akiwataka waandishi wa habari pindi wanapokuwa wakiandika habari za uchaguzi wazingatie maadili ya taaluma yao, ili wawe wanatoa taarifa sahihi za kuhabarisha umma.

Mwezeshaji Dastani Kamanzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Ujuzi Era, akiwataka waandishi wa habari pia wawe wabobezi wa kuandika habari ya mlengo mmoja(Specialized) mfano habari za afya tu, kilimo, uchumi, na siyo kuwa waandishi wa kuandika kila habari.

Mwandishi wa habari Ester Sumira kutoka Azam Tv Mkoani Geita akichangia mada kwenye mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi.

Mwandishi wa habari Paulina David kutoka Radio Free Afrika Jijini Mwanza akichangia mada kwenye mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi.

Mwandishi Salma Mrisho kutoka Star Tv Mkoani Geita, akichangia mada kwenye mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi.


Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali wakiwa kwenye mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi yaliyofanyika Jijini Mwanza.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi.


Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi.


Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi.



Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi.

Mratibu wa mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi Joseph Moses Oleshaghai kutoka kituo cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC), amesema wametoa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari, wakiamini kuwa waandishi wa habari ni wadau muhimu wa kufikisha elimu kwa umma ikiwemo elimu ya kiraia na uchaguzi.


Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali , wakiwa na wawezeshaji wa mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi, wakipiga picha ya pamoja na Kamanda ya Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza Murilo Jumanne Murilo mara baada ya kuhitimisha mafunzo hayo yaliyodumu ndani ya siku Tatu kuanzia Agost 22 hadi 24 kwenye ukumbi wa mikutano wa hotel ya Belmont Jijini Mwanza.


Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Share:

ALIYEDHANIWA KUWA NA UJAUZITO KUMBE UVIMBE WA KILO 28 AFANYIWA UPASUAJI SONGWE




Utumbo
Mama mmoja mkazi wa Mbozi mwenye umri wa miaka 43 amefanyiwa upasuaji katika hospitali ya mkoa wa Songwe na kutolewa uvimbe mkubwa kwenye kizazi wenye uzito wa zaidi ya kilo 28.

Upasuaji huo umefanyika katika hospitali hiyo ambayo kila wiki hufanya upasuaji wa uvimbe kwa zaidi ya watu watatu.

Akiongea na East Africa Television daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama mkoa wa Songwe na Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Dr. Lukombodzo Lulandala, amesema katika upasuaji aliowahi kufanya hajawahi kukutana na uvimbe mkubwa wa kiasi hicho cha kilo 28.

Aidha Dr. Lukombodzo Lulandala amewataka wananchi mkoani Songwe, wasikimbilie kwa waganga wa kienyeji badala yake waonane na wataalaam wa afya.

Mgonjwa wa tatizo hilo,amewashukuru madaktari wa Mkoa wa Songwe kwa kuokoa maisha yake na kwamba sasa baada ya kufanyiwa upasuaji huo anaendelea vizuri huku akisema kwa zaidi ya miaka mitano amekuwa akihangaika na tatizo hilo.

''Naomba elimu itolewe kwani ndugu zangu walijua ni ujauzito, wahanga wengine wamekuwa wakihangaika sehemu mbalimbali bila kwenda hospitali kumbe wanaongeza tatizo'', amesema.
Share:

Serikali Yajipanga Kuongeza Ushirikiano Na Sekta Binafsi-waziri Hasunga

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Serikali imesema kuwa imejipanga lkuongeza ushirikiano na Sekta binafsi  katika kuhakikisha kuwa kero na vikwazo vinaondolewa ili kuweka mazingira bora ya biashara na kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 24 Agosti 2019 wakati akimuwakilisha Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa kufungua Mkutano mkuu wa mwaka wa dharura wa TCCIA mwaka 2019 huku akiongeza kuwa serikali imefanya uamuzi mahususi mwaka huu wa kuondoa muingiliano wa utoaji wa huduma za mashirika ya TBS na TFDA ili kupunguza usumbufu kwa Wanyabiashara.

Alisema kuwa hizo ni hatua za awali na ametoa mwito kwa TCCIA kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanafuata sheria, kanuni na taratibu zote zilizowekwa ili kuondoa usumbufu wote unaoweza kujitokeza wakati wa kufanya biashara.

Alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli alizindua  Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP II) tarehe 4 Juni, 2018. Kwa kutambua umuhimu wa Sekta Binafsi, moja ya maboresho makubwa ya ASDP II ukilinganisha na ASDP I ni kuipa nafasi kubwa zaidi Sekta Binafsi.

Aliongeza kuwa ni wakati muafaka wa kubaini maeneo maalumu ambayo Taasisi hiyo ya TCCIA itaendelea kutoa mchango mkubwa katika kutekeleza programu hiyo ili iweze kufikia malengo yaliyowekwa.

Mhe Hasunga amesema kuwa ili kuhakikisha uboreshaji wa Mazingira ya biashara nchini, Serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi iliandaa andiko maalumu “Blue Print” ambalo lilikwisha zinduliwa, pia mpango wa utekelezaji wake umeandaliwa na umeanza kutekelezwa.

“Ni wajibu sasa wa kila pande yaani Sekta ya Umma na Binafsi kuhakikisha kuwa yale yote yaliyoainishwa katika andiko hilo yanatekelezwa ipasavyo” Alikaririwa Mhe Hasunga

Vile vile, amesema kuwa serikali imeendelea na jitihada za kuimarisha Mabaraza ya Biashara ya Mikoa na Wilaya ambapo tayari imeshaweka Mwongozo wa Mabaraza hayo ambayo TCCIA ni Sekretarieti.

Waziri Hasunga amewataka washiriki hao kuchangamkia  fursa zilizopo katika miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali nchini, hasa miundo mbinu ya reli ya Kisasa, mradi wa umeme wa bwawa la Nyerere, barabara za kisasa, bomba la mafuta, manunuzi ya ndege n.k.

Alisema kuwa Fursa hizo kwa kupitia sera ya “Local Content” nao wakiwa wazawa wana nafasi kubwa ya kunufaika nazo.

Amesema, Miradi hiyo ni mingi na itachukua muda mrefu ikitekelezwa kwa awamu tofauti. “Endapo kwa sababu moja au nyingine haukuweza kupata fursa ya kushiriki kazi kwenye mradi mmoja kwa sababu fulani zikiwemo sifa kadhaa basi, nakushauri ujipange vizuri kwenye miradi inayokuja, msikate tamaa” Alisisitiza Mhe Hasunga

Alisema kuwa serikali inatambua ushirikiano mzuri wa TCCIA na taasisi mbali mbali za Umoja wa Mataifa (UN) zikiwemo UNDP, UNIDO, FAO, UNV, UNESCO, ILO, na ITC, pamoja na Wadau wengine wa kimaendeleo kama Trade Mark East Africa.

Ushirikiano huo kwa kupitia mifumo ya kielektroniki ya kuripoti na kufuatilia vikwazo mbalimbali (NTBs Reporting and Monitoring System) na utoaji wa vyeti vya Uasili wa Bidhaa kwa njia ya kielektroniki (Electronic Certificates of Origin) umesaidia sana uondoaji wa vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiforodha (NTBs).

Pia, TCCIA imeshirikiana na Wadau wengine kama vile VSO, ENGEN, USAID, East African Trade Hub, BMZ, KOICA, JICA, TRIAS na DANIDA kupitia Local Investment Climate (LIC) kuimarisha biashara na mfumo wa majadiliano na sekta ya umma. Kwa kipekee ninawapongeza sana kwa mashirikiano hayo.

MWISHO


Share:

Mrembo Sylivia Sebatian Bebwa Ashinda taji la Miss Tanzania kwa mwaka 2019

Mrembo Sylivia Sebatian Bebwa toka kanda ya ziwa, ameshinda taji la Miss Tanzania kwa mwaka 2019, katika shindano lililofanyika ukumbi wa Kisena  Millennium Tower, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Jumamosi Agosti 24,2019 .
 
Sylivia anatokea  Jijini Mwanza akiwa ni mshindi wa Miss Mwanza 2019 lakini pia mshindi wa Miss Lake Zone. 

Kutoka na ushindi huo, Silvia ameondoka na kitita cha Sh10 milioni huku mshindi wa pili Grayres Amos akiondoka na sofa yenye thamani ya Sh2 milioni na mshindi wa tatu Qeen Antony akiondoka na Sh1 milioni moja.


Share:

Askofu Shoo Achaguliwa Tena Kuwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa kipindi cha miaka minne

Askofu Dkt Fredrick Shoo amechaguliwa kwa kipindi kingine cha pili kuwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa kipindi cha miaka minne .

Dkt. Shoo ametangazwa mshindi usiku wa kuamkia leo dhidi ya wagombea wengine katika uchaguzi huo ambapo ataliongoza kanisa hilo kwa kipindi kingine cha miaka minne (2019-2023). 

Askofu Shoo amepata kura 144 huku mshindani wake wa karibu, Dkt. Abednego Keshomshahara akipata kura 74 kati ya kura 218 zilizopigwa katika mzunguko wa mwisho baada ya kubaki wao wawili.


Share:

Vifo ajali ya lori la mafuta Morogoro vyafika 101

Idadi ya vifo vya majeruhi wa ajali ya lori la mafuta iliyotokea mkoani Morogoro, imefika 101 baada ya majeruhi mmoja aliyekuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kufariki dunia usiku wa kuamkia jana.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha, alisema aliyefariki dunia ni Sadiki ismail (31).

Alisema mpaka sasa kati ya majeruhi 47 waliofikishwa hospitalini hapo, waliobaki ni 14 ambapo kati yao 11 wako katika Vyumba vya Uangalizi Maalum (ICU) na watatu wako katika wodi za kawaida na hali zao zinaendelea vizuri.


Share:

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa, Dalili zake Hizi Hapa..Makala
51 minutes ago

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kulundia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.


Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.


Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.


Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.


Ugojwa huu wa ngiri unaweza kutibika

Mpate mpenzi wako unayempenda na kumfunga mume,mke mpenzi asitoke kwa mwingine .

Kwa Ushauri na Msaada wa Wasaliana na  0714006521


Share:

Mawakili 15 wa Serikali Wakabili Tundu Lissu Mahakamani

Mawakili wa Serikali 15 wakiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Clement Mashamba wamewasilisha pingamizi katika Mahakama Kuu kupinga maombi ya aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuhusu Ubunge wake.

Lissu amefunguka maombi Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya hati dharura, kupitia kwa Kaka yake Alute Mughwai, ambaye amempa mamlaka ya kisheria kufanya hivyo, ikiwa ni hatua ya awali kabisa ya kupigania kurudishiwa ubunge.

Dk. Mashamba amemueleza Jaji Sirilius Matupa kuwa mapingamizi hayo yana masuala manne ya msingi ikiwemo kuona kama mahakama hiyo ina mamlaka ya kusikilizwa maombi hayo kama yalivyoletwa.

Pia amedai wameangalia kama mleta maombi ambaye ni Allute Mughwai ana uwezo wa kuleta maombi hayo na kama maombi hayo yameletwa kwenye mahakama yenye mamlaka.

Dk.Mashamba amedai wanaangalia kama nafuu zilizoombwa kwenye mahakama hiyo ni sahihi kuletwa mahakamani au la.

Katika pingamizi hizo, hoja ya kwanza iliwasilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Abubakari Mrisha amedai yapo mambo sita ya kuzingatia kwa mleta maombi ikiwemo kuhakikisha maombi yanaletwa ndani ya miezi sita baada ya maamuzi, mahakama kuona haja ya kusikiliza maombi hayo na maombi kuletwa kwa nia njema si kwa lengo la kupotosha au kwa manufaa binafsi.

“Kati ya hayo, jambo moja pekee kwamba maombi haya yako ndani ya muda lakini mengine yamekosekana katika maombi haya. Maombi haya hayakidhi kwa sababu hakuna maamuzi yoyote yaliyoambatanishwa katika maombi haya ili iweze kuyapitia kama kuna haja ya kuilazimisha mamlaka iliyotoa maamuzi kuyaondoa,” alidai Mrisha.

Pia amedai kuwa hakuna maamuzi yaliyoambatanishwa ili mahakamani iweze kuyapitia na kutoa uamuzi kama kwenye kesi ya aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari dhidi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Alidai kwa mujibu wa Kanuni za Bunge zinaelekeza Mbunge ambaye ataathiriwa na maamuzi anatakiwa kuwasilisha mapingamizi kwa Katibu wa Bunge ambaye atayawasilisha mapingamizi hayo kwa spika.

Mrisha alidai kisheria walipaswa kuambatanisha maamuzi wanayolalamikia na kwamba katika kiapo kilichoandaliwa na Mghwai walichoambatanisha ni nakala za magazeti ya Mwananchi na Nipashe ambayo kimsingi hawawezi kuyaita maamuzi.

Katika mapingamizi mengine, Wakili wa Serikali, Lucas Malunde alidai alichokifanya Spika ni kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa NEC juu ya uwepo wa nafasi ya wazi ya kiti cha Mbunge kwa sababu hakuwepo na hatekelezi majukumu ndani ya Bunge.

Malunde alidai taarifa hiyo ilitangazwa kwenye gazeti la serikali hivyo hakutoa tamko la kumvua ubunge na kwamba Lissu hakujiudhuru wala hajafa.

“Hakuna mahali Spika alitoa tamko yeye alitoa taarifa ambayo inapopelekwa gazeti la serikali inakuwa mali ya serikali inayosambazwa na mtu yoyote anaweza kuipata akihitaji,” alidai Malunde.

Alidai maamuzi ya kutostahili kuendelea na ubunge hayatolewi na spika kwani katiba inaelekeza Mbunge atakosa sifa ya kuendelea kuwa kwenye nafasi hiyo endapo atakosa kuhudhuria vikao vitatu vya bunge bila ruhusa ya Spika.

Wakili wa Serikali Mkuu, George Mandepo amedai sheria inaruhusu madai kufunguliwa na mtu binafsi au muwakilishi ambaye ana nguvu kisheria kwa hivyo, maombi yaliyopo mahakamani yamewasilishwa na Lissu kupitia mwakilishi wake ambaye ni Mghwai.

Alidai katika kuomba ridhaa ya kuwasilisha maombi yanatakiwa kusainiwa na muombaji au muwakilishi wake pamoja na kuambatanisha hati ya kiapo na muhuri wa wakili.

“Katika maombi haya yanaonesha kuwa Julai 9, mwaka huu Lissu alisaini kiapo hicho akiwa nchini Ubelgiji na muhuri wa wakili Sadolf Magai alisaini kwa anuani ya Dar es Salaam,” alidai Mandepo.

Alidai ipo sheria inayosimamia maombi inayoeleza kiapo kinatakiwa kutolewa mbele ya msimamizi wako.

Mandepo alidai kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria za Tanzania kwa sababu kiapo kilichowasilishwa kimesainiwa na muhuri wa Tanzania wakati kiapo kilisainiwa nchini Ubelgiji hivyo, sio halali na maombi yaliyowasilishwa sio halali.

Alidai wanashangaa Julai 9, mwaka huu siku ambayo kiapo kiliandaliwa huko Ubelgiji hakioneshi ni kwa namna gani kilifika jijini  Arusha hivyo si kiapo cha kweli.

“Kiapo hiki kimebeba uongo kwa sababu moja wakili Sadolf hajaleta hati ya kiapo mahakamani wala maelezo ya kudhibitisha kwamba alikwenda Ubelgiji na hakuna kumbukumbu kwamba wakili huyo aliithinishwa kufanya kazi nchini Ubelgiji wakati aliapishwa na Jaji wa Tanzania,” alidai.

Kutoka na hoja hizo, aliomba mahakama iyatupe maombi kwani pamoja na mambo mengine aliyoyaleta, hana sifa ya kufanya hivyo.

Jaji Matupa jana alitakiwa kusikiliza maombi ya zuio la muda la kuapishwa kwa Mbunge Mteule, Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu na maombi ya kupinga kuvuliwa ubunge aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Tundu Lissu lakini haikuwezekana baada ya Jamhuri kuwasilisha pingamizi la awali.

Maombi ya kupinga kuvuliwa ubunge yalifunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa zamani wa Jimbo la Singida Mashariki, Lissu kupitia mawakili wake.

Amefungua shauri hilo chini ya hati ya dharura, kupitia kwa kaka yake Wakili Alute Mughwai, ambaye amempa mamlaka ya kisheria kufanya hivyo.


Share:

Wakimbizi Wa Burundi Walalamika Kuzuiwa Na Mashirika Kurejea Nchini Kwao.... Waziri Lugola Aagiza Wakamatwe Wanaoweka Vikwazo

Na Felix Mwagara, Kibondo (MOHA).
Baadhi ya Wakimbizi kutoka nchini Burundi wanaoishi katika Kambi ya Nduta, Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wamesema wanawekewa vikwazo na kucheleweshwa na baadhi ya watendaji wa mashirika ya wakimbizi kambini humo wakati wanapoomba kujiandikisha kurejeshwa kwao.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola na Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi, Pascal Barandagiye, wakimbizi hao wamesema wapo tayari kurudi nchini mwao kwa hiari lakini wanashindwa kujiandikisha kutokana na kukwamishwa na baadhi ya watendaji wa mashirika hayo.

Mkimbizi wa kambi hiyo, Nzoisa Bhainoje, alisema yupo tayari kurejea nchini Burundi lakini amefanya juhudi za kwenda eneo la kujiandikisha kambini hapo lakini hakufanikiwa kutokana na kusumbuliwa akiambiwa kuwa idadi wanaotakiwa kuondoka imekamilika.

“Nakumbuka nilifika eneo la kuondoka siku ya Jumanne lakini ilishindikana kujiandikisha kutokana na kukwamishwa, wengi tunataka kuondoka lakini tunashindwa kuondoka kwasababu tunakwamishwa,” alisema Bhainoje.

Bhainoje aliongeza kuwa, wanaomba watendaji hao wawaruhusu kwa wale wanaotaka kurejea nchini mwao kwa hiari, lakini kwa wale ambao hawataki kuondoka wanaweza kubaki kwa mipango yao.

Baada ya wakimbizi hao kutoa kero zao kwa Waziri Lugola na Waziri Barandagiye, ndipo Lugola aliagiza kufanyika uchunguzi katika kambi hiyo kuwakamata wale wote ambao wanakwamisha wakimbizi hao kurejea nchini kwao kwa hiari.

“Naagiza uchunguzi ufanyike haraka iwezekanavyo kwa yeyote atakayehusika anakwamisha zoezi hili la kuwarejesha wakimbizi hawa ambao wapo tayari kuondoka nchini kwao kutokana na amani iliyopo, awe Afisa kutoka Wizarani, awe afisa wa shirika lolote, awe yupo hapa kambini, lazima tutamkamata na kumpeleka mahakamani,” alisema Lugola.

Aliongeza kuwa, muda umefika kwa wakimbizi wa Burundi kurudi nchini mwao, kwasababu zile sababu ambazo zilikuwa zinazuia zoezi la kuwarudisha kwao wakimbizi hao kwa sasa havipo tena kwasababu nchi hiyo ina amani.

Alisema Serikali ya Tanzania chini ya Rais John Magufuli imejiridhisha sababu kubwa iliyowaleta wakimbizi hao wa Burundi nchini ya kutowepo kwa amani haipo tena na kwamba kwa sasa Burundi ipo salama kiulinzi na kiusalama pia kisiasa hivyo wakimbizi hao wanapaswa kurudi nchi mwao wote bila kuwepo kikwazo chochote.

“Wanaosema Burundi haina amani wanaipaka matope nchi hiyo kwani jambo hilo halina ukweli wowote na Tanzania imefanya uchunguzi wa kutosha na kujiridhisha kuwa amani ya kudumu ipo nchini humo, Oktoba Mosi tutaanza kutekeleza mkataba wa pande tatu wa kurudishwa kwa wakimbizi 2000 kila wiki wa Burundi kwenda nchini mwao”. Alisema Lugola.

Naye Waziri Barandagiye, kwa upande wake alisema Burundi iko tayari kutekelezwa kwa makubaliano ya pande tatu ya kuhakikisha wakimbizi wote wa Burundi wanaohifadhiwa kwenye makambi mbalimbali ya wakimbizi mkoani nchini wanarudi Burundi lakini wanashangazwa na namna Shirika la Kuhudumia Wakimbizi linavyoendesha zoezi hilo kwa kasi ndogo.

"Tuko tayari kupokea wakimbizi 3000 kila wiki zaidi ya takwimu ya wakimbizi 2000 iliyotolewa kwenye makubaliano ya pande tatu, maandalizi na matayarisho ya kupokea wakimbizi hao yapo vizuri na wengi wanaorudi wamekuwa wakipata misaada mbalimbali ikiwemo miradi ya kiuchumi kwa ajili ya kuendesha maisha yao,";Alisema Barandagiye.

Barandagiye amewataka wakimbizi hao kutokubali kudanyanywa na maneno ya wanasiasa kwamba hakuna amani nchini Burundi lakini kuwa na tamaa ya kwenda kuishi Marekaani, Canada kuwa huo ni uongo hivyo wanapaswa kurejea nchini mwao kwakuwa ipo amani na pia mazingira
yanaruhusu kuppokelewa.

Waziri Lugola na Barandagiye walitembelea Kambi ya Nduta, Wiliyani Kibondo na Mtendeli iliyopo Wilayani Kakonko mkoani humo, kwa lengo la kuhamasisha wakimbizi katika kambi hizo kurejea nchini kwao kwa hiari.


Share:

Atupwa jela miaka 30 kwa kubaka mtoto wa miaka 10

 Mahakama ya Wilaya ya Lindi imemuhukumu mkazi wa kata ya Rutamba, Issa Mpanyanje (51) kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 10.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa mahakama hiyo, Liliani Rugalabamo, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo mshitakiwa alipewa nafasi ya kujitetea ambapo aliiomba mahakama hiyo imuonee huruma kwani ni mkosaji wa mara ya kwanza pia anayo familia akiwemo mke na watoto wanaomtegemea hivyo iwapo atapata adhabu kali itawafanya wakose huduma zake.

Hakimu Rugalabamo akitoa adhabu katika kesi hiyo namba 34/2019, kupitia vifungu 130 kifungu kidogo (1) na (2) (e) na 1321 kifungu kidogo Sheria sura ya 16 kama ilivyofanywa marejeo mwaka 2002 alisema amesikia maombi ya pande zote mbili,lakini kutokana na Sheria kumshika mikono, amemuhukumu kwenda jela miaka 30 na atakapomaliza adhabu yake amlipe mlalamikaji fidia ya Sh milioni mbili.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na mwanasheria wa Serikali, Rabia Ramadhani kuwa mshitakiwa huku akitambua anachokifanya ni kosa, Aprili 14 mwaka huu maeneo ya mashambani bila huruma alimbaka mlalamikaji na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.

Inadaiwa mshitakiwa alipata mwanya huo baada ya kumshawishi mlalamikaji waende shambani akamsaidie kuvuna karanga na baada ya kufika huko alianza kumtomasa kisha kumbaka huku akimsisitiza kutomwambia mtu yeyote.

Hata hivyo kutokana na maumivu makali aliyokuwa akiyaona Mtoto huyo waliporejea Nyumbani alilazimika kukiuka maagizo aliyopewa na kumweleza mama yake ambapo naye alitoa taarifa kituo cha Polisi ambapo alikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi 24 August



















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger