Saturday, 24 August 2019

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi 24 August



















Share:

NEC Yamteua Anna Kajigili kuwa Diwani Viti Maalum CHADEMA




Share:

Ndege ya Air Tanzania yazuiwa kuondoka Afrika Kusini kwa amri ya mahakama

Ndege ya Air Tanzania iliyokuwa inatoka Afrika Kusini kwenda jijini Dar es Salaam, Tanzania imezuiwa kuruka kwa amri ya Mahakama Kuu ya Gauteng, Johannesburg nchini humo.

Taarifa iliyotolewa Ijumaa   Agosti 23, 2019 na katibu mkuu Wizara ya Ujenzi,  Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Leonard Chamuriho inaeleza kuwa Serikali ya Tanzania kupitia ofisi ya mwanasheria mkuu inafuatilia suala hilo ili ndege hiyo iachiwe na kuendelea na safari zake kama kawaida.

"Waziri wa Ujenzi,  Uchukuzi na Mawasiliano anaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa abiria wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) waliokuwa wanasafiri leo kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oliver Tambo,  Johannesburg kuja Dar es Salaam kufuatia ndege hiyo kushindwa kufanya safari kama ilivyopangwa, " inaeleza taarifa hiyo.




Share:

Friday, 23 August 2019

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo

SUPER MORISIS; nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-85)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wala kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 18-45

SUNUPER;   Hurefusha na kunenepesha maumbire madogo ya uume uliosinyaa ,  matatizo haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguruma na kujaa gesi hatimae kinyesi kuwa km cha mbuzi, ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia nidawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

ONDOA MATATIZOYAKO YOTE  ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,  kurudisha mali iliyopotea au kuibiwa 

Kwahuduma na msaada wasiliana na DR. GALIMBO  0759208637   /  0620510598


Share:

Naibu Katibu Mkuu Ofisi Ya Makamu Wa Rais Akutana Maafisa Mazingira Wa Mikoa Ya Tanzania Bara Jijini Dodoma.

Maafisa Mazingira Nchini wametakiwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais ili kuhakikisha Katazo la mifuko ya plastiki linafanikiwa na kutekelezeka vema.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine alipokutana na Maafisa hao kutoka mikoa ya Tanzania Bara katika Warsha iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais katika ukumbi wa Nyaraka jijini Dodoma.

Alisema kuwa Warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais ina lengo la kujenga uelewa wa pamoja kuhusu utekelezaji wakatazo la mifuko ya plastiki na namna ya kuboresha ushirikiano na uratibu katika hifadhi ya mazingira kwa ujumla.

“Kwa ujumla, katazo la mifuko ya plastiki limeleta sifa na heshima kwa nchi yetu katika ngazi ya Kitaifa na Kimataifa. Tanzania inakuwa miongoni mwa nchi 60 duniani ambazo zimepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki. Hii ni hatua kubwa na ya kujipongeza kwa dhamira na msimamo wa Serikali katika kukabiliana na changamoto za hifadhi ya mazingira” alisema Balozi Sokoine.

Aliongeza kuwa changamoto iliyopo kwa sasa ni kuibuka kwa matumizi ya mifuko ya plastiki ya kubebea bidhaa ambayo ni “transparent” na kupelekea mifuko hiyo kuzagaa na kutumiwa kama vibebeo vya kubebea bidhaa. Hivyo basi amewaagiza Maafisa hao wa Mikoa kuanza kufanya ukaguzi kwa kushirikiana na Baraza la Usimamizi wa Mazingira katika mikoa yao waliotoka.

Pia aliwasisitiza kuendelea kujenga uelewa kwa walio chini yao kuanzia ngazi ya mkoa mpaka ngazi ya chini(kata,Tarafa,vijiji) ili elimu ya katazo la matumizi ya mifuko ya plstiki ifike mpaka ngazi ya chini.

Katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki lilianza rasmi tarehe mosi ya mwezi juni 2019, ikiwa ni kufuatia agizo lilitolewa na Mh. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bungeni jijini Dodoma.

Ofisi ya Makamu wa Rais ni wasimamizi wakubwa katika kampeni hiyo ya marufuku ya mifuko ya plastiki.


Share:

Benki Ya Dunia Yaahidi Kuongeza Fedha Mpango Wa TASAF

Na. Peter Haule, WFM, Dar es Salaam
Benki ya Dunia imeahidi kutoa fedha zaidi kwa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini- TASAF, unaofadhiliwa na Benki hiyo kwa kushirikiana na Tanzania kwa kuwa awamu ya kwanza na ya pili ya mpango huo umeonesha matokeo chanya kwa kuboresha maisha ya watanzania kiuchumi.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi 22 zilizopo Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, wakati alipofanya ziara ya kuangalia utekelezaji wa TASAF awamu ya kwanza na ya Pili katika Mtaa wa Keko Machungwa Kata ya Miburani, Jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa ameshuhudia mwenyewe wanawake wakiwa wamezalisha bidhaa mbalimbali vikiwemo viatu, vikapu, shanga, mikoba, vyungu, urembo na nguo zilizotengenezwa kupitia mpango wa TASAF, jambo linalodhihilisha manufaa ya mpango huo kwa Kaya masikini katika kukuza uchumi wao.

“Kwa kuwa nawakilisha nchi za Afrika ikiwemo Tanzania katika Benki ya Dunia, Washngton Marekani, nimejionea kwa macho yangu bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa hasa na wanawake, hivyo naenda kupeleka ujumbe huo muhimu ili Benki iweze kuongeza fedha zaidi kwa awamu zingine kwa ajili ya mpango huu wa TASAF kutokana na manufaa yake katika kupunguza umasikini nchini Tanzania”, alieleza Bi. Kabagambe.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa  Mtaa wa Keko Machungwa, Bw. Uwessu Misanga, alisema kuwa kuanzia mwaka 2015 hadi Februari, 2019, fedha walizolipwa walengwa wa Kunusuru Kaya Masikini katika eneo lake ni takribani Sh. milioni 86.1.

Alisema manufaa ya mpango huo ni pamoja na upatikanaji wa  mahitaji muhimu kama Chakula, kuongezeka kwa mahudhurio ya wanafunzi shuleni na  kuhudhuria Kliniki kwa watoto chini ya miaka mitano kutoka Kaya Masikini.

Mafanikio mengine ni pamoja na kuongezeka kwa kipato kwa walengwa kutokana na biashara ndogondogo zinazofanywa na kaya hizo lakini pia kuboreshwa kwa mahitaji muhimu ya wanafunzi kutokana na ruzuku.

Aidha Bw. Misanga, alibainisha changamoto za utekelezaji wa Mpango wa TASAF kuwa ni pamoja na ukosefu wa elimu ya ujasiriamali, baadhi ya Kaya kukosa fursa ya kuingia kwenye mpango, uhaba wa maeneo ya kufanyia shughuli za kuongeza kipato na pia uhaba wa mitaji katika vikundi vya wajasiriamali vilivyoanzishwa na Kaya hizo.

Alisema kuwa katika kukabiliana na changamoto hizo Serikali inafanya tathmini na mapitio ya mpango kwa awamu ya kwanza ili kuwezesha Kaya zilizoachwa kuingizwa katika mpango huo na pia Ofisi ya Halmashauri ya Temeke Jijini Dar es Salaam, imewaelekeza wanakikundi wa ujasiriamali kuwasilisha mahitaji ya eneo kwa kuzingatia shughuli wanazotaka kufanya ili kutatua changamoto zao.

Baadhi ya wanufaika wa TASAF waliotoa shuhuda zao mbele ya Mkurugenzi huyo wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, wameishukuru Benki ya Dunia kwa kuwawezesha kujikwamua kimaisha na pia wameomba kuendelezwa kwa mpango huo kwa kuwahusisha watu wengi zaidi na kuwatafutia masoko ya bidhaa zao.

Mwisho.


Share:

Waziri Mkuu Aagiza Apelekewe Taarifa Za Utendaji Wa DED Lindi

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Bw. Shaibu Ndemanga ampelekee taarifa za utendaji kazi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Bw. Waryoba Gunza baada ya kushindwa kutoa maelezo kuhusu utekelezaji wa mradi wa maji kata ya Rutamba.

Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Agosti 23, 2019) wakati akizungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Rutamba akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za maendeleo na huduma za jamii mkoani Lindi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya kumtaka Mkurugenzi huyo atoe maelezo ya namna gani walivyojipanga katika kutekeleza mradi wa maji kwenye kata hiyo ambayo wakazi wake wanakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa maji na kushindwa kutoa maelezo.

Kwa mujibu wa Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Lindi, Bw………alisema mradi wa kata hiyo unakabiliwa na tatizo la uchakavu wa miundombinu na ukarabati wake unahitaji bajeti sh. milioni 75 ambazo wameziomba kutoka Wizara ya Maji.

Waziri Mkuu amesema miradi yote ambayo gharama zake ziko chini ya sh. milioni 100 inatakiwa itekelezwe kwa kutumia fedha za ndani ya halmashauri husika. “Miundombinu hiyo ilitakiwa iwe imebadilishwa. Mradi wa sh. milioni 75 unaomba fedha wizarani ni uvivu.”
Waziri Mkuu amesema suala la huduma ya maji limewekewa msisitizo na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuanzisha kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani, inayolenga kuwawezesha wananchi kupata maji safi na salama karibu na makazi yao.

Waziri Mkuu aliwaambia wananchi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kuondoa tatizo la maji kote nchini ili kusaidia wananchi hao hasa wanawake kutumia muda mwingi kufanya kazi za maendeleo kuliko kutafuta maji.

Hata, hivyo Waziri Mkuu amewahakikisha wananchi hao kwamba licha ya kuagiza mradi huo wa ukarabati wa miundombinu ya kusambazia maji ufanyike kwa haraka, pia Serikali inatekeleza mradi mwingine wa maji wa Milola ambao ukikamilika maji yatafikishwa hadi Rutamba.

Wakati huo huo,Waziri Mkuu amewaagiza Wakuu wa Wilaya nchini wahakikishe wanawasimia vizuri watumishi wa umma na kuwachukulia hatua wote watakaobainika kushindwa kutekeleza majikumu yao ipasavyo.

“Rais Dkt. John Pombe Magufuli ana nia njema ya kuwapa huduma safi wananchi wote hadi wanyonge na ameelekeza wahudumiwe vizuri bila ya ubaguzi. Wananchi kama kuna mtumishi asiyewahudumia vizuri msisite kumtaja kwa sababu Serikali hii haitomvumia.”

Waziri Mkuu asema ni lazima kila mtumishi wa umma anayelipwa mshahara kwa kutumia kodi za wananchi ahakikishe anatekeleza ipasavyo majukumu yake kwani asipofanya hivyo hatokuwa na nafasi ya kuendelea na kufanya kazi ndani ya Serikali.

“Watumishi fanyeni kazi kwa bidii na msitarajie kuundiwa tume pale mnapofanya vibaya, ukiharibu kazi tunakushughulikia hapo hapo na huu ndio msimamo wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli.”

Waziri Mkuu amesema kuwa watumishi wanatakiwa wafanye kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni za kazi na pia watambue dhamana kubwa waliyonayo, ambayo ni kuwahudumia wananchi wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Amesema watumshi wa umma hawapaswi kukaa maofisini bali wanatakiwa wapange siku nne katika juma kwa ajili ya kwenda kutembelea wananchi hususani waishio maeneo ya vijijini kwa ajili ya kuwasikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi.

Waziri Mkuu amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za jamii ambazo zilikuwa zikiwakwaza wananchi zikiwemo za miundombinu ya barabara, tatizo la maji, elimu na afya, lengo likiwa ni kuwawezesha Watanzania wote waishi vizuri.

Awali, akizungumza kwaniaba ya wabunge wa mkoa wa Lindi, Mbunge wa Viti Maalumu, Riziki Lulida alisema wakazi wa kata ya Rutamba wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji licha ya kuwepo kwa vyanzo, hivyo aliiomba Serikali iwasaidie.

Hata hivyo alilalamikia kuwepo kwa uharibifu mkubwa wa mazingira katika maeneo hayo ikiwemo uvamizi katika vyanzo vya maji pamoja na ukataji hovyo wa misitu unaohatarisha kuibuka kwa jangwa, ambapo Waziri Mkuu ameagiza viongozi wa wilaya hiyo kuzishughulikia suala hilo.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,        
IJUMAA, AGOSTI 23, 2019.


Share:

Albert Msando amlipia Rais Magufuli deni Muhimbili

Alberto Msando ambaye ni Wakili wa kujitegemea amefika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kulipa MILIONI 5 ambazo Rais John Magufuli aliahidi kuzitoa kumlipia Mama aliyemlilia akitaka alipiwe gharama hizo ili apatiwe mwili wa Mama yake.



Share:

Picha : WAANDISHI WA HABARI WAPIGWA MSASA KUANDIKA HABARI ZENYE TIJA




Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, wamepewa mafunzo namna ya kuandika habari zenye tija ndani ya jamii, ambazo zitatatua matatizo yao na kuleta furaha kwa wananchi.


Mafunzo hayo yametolewa leo Agosti 23,2019 na Mwezeshaji Dastani Kamanzi kwenye mafunzo ya waandishi wa habari, ambayo yanaendelea Jijini Mwanza kwenye ukumbi wa mikutano Belmont Hotel, yanayoendeshwa na mtandao wa asasi ya kiraia wa kuangalia uchaguzi Tanzania (TACCEO), Chini ya kituo cha Sheria na haki za binadamu (LHRC).


Mafunzo hayo yana husisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita, Mara, Kagera pamoja na Kigoma, yenye mlengo wa kuongeza tija kwa waandishi hao, katika kuandika habari zenye kutoa elimu ya uraia kwa umma pamoja na uchaguzi.


Kamanzi ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Ujuzi Era la Jijini Dar es salaam, amesema Mwandishi mwenye tija ni yule ambaye ana andika habari zenye mguso ndani ya jamii na kuweza kuwatatulia matatizo yao pamoja na kuleta, uhuru, haki, amani pamoja na udungu.


“Mwandishi wa habari mwenye tija ni yule ambaye ana andika habari zenye mguso ndani ya jamii pamoja na kutatua matatizo yao, na kuleta furaha kwa umma pamoja na Serikali,”amesema Kamanzi.


“Ili uwe Mwandishi wa habari mwenye tija lazima uzingatie maadili ya taaluma yako, mjuzi katika teknolojia inayotawala taaluma yako, Mwadilifu, pamoja na kujua habari unayotaka kuandika inafaida gani ndani ya jamii, na siyo kujiandikia tu habari bila ya kujua matokeo yake,”ameongeza.


Naye Mwezeshaji Ndimara Tegambwage ambaye ni Mwandishi Mwandamizi hapa nchini, amewataka waandishi wa habari za uchaguz wazingatie Shajala ya Ripota (dairy), ili wawe na kumbukumbu za uchaguzi, na kuweza kuandika habari nzuri, kipindi kabla ya uchaguzi, kipindi cha kupiga kura, na kipindi baada ya uchaguzi.

Anasema Mwandishi wa habari anapokuwa na Shajala hiyo ya Ripota, itamsaidia kujua historia ya uchaguzi kwenye eneo husika ama jimbo, na kuweza kuandika habari za uchambuzi, kisiasa, kiuchumi, kiusalama. Chakula, miundombinu, pamoja na kuweza kuwabana wagombea juu ya ahadi walizoahidi kabla ya uchaguzi.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Dastani Kamanzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Ujuzi Era, akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari namna ya kuandika habari zenye Tija kwa jamii na kutatua matatizo yao. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde1 blog 

Mwandishi wa habari mwandamizi Ndimara Tegambwage ambaye pia ni mhariri wa gazeti la Mwananchi akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari namna ya kuandika habari,kipindi kabla ya kupiga kura, kipindi cha kupiga kura, na kipindi baada ya kupiga kura.

Mwandishi wa habari mwandamizi Ndimara Tegambwage ambaye pia ni mhariri wa gazeti la Mwananchi, akitoa mafunzo wa waandishi wa habari kuwa na Shajala Ripota ambayo itamsaidia kuandika habari vizuri za uchaguzi.

Mwezeshaji Jimy Luhende akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari namna ya kuandika habari za uchaguzi katika nyanja mbalimbali.

Mwandishi wa mitandaoni Nicholaus kirunga kutoka Kigoma akichangia mada kwenye mafunzo ya waandishi wa habari Jijini Mwanza namna ya kuandika habari za uchaguzi.

Mwandishi wa habari Aidani Mhando wa Chanel Ten kutoka Mkoani Simiyu akichangia mada kwenye mafunzo ya wana habari Jijini Mwanza.

Mwandishi wa habari Rhoda Ezekiel kutoka Gazeti la Uhuru mkoani Kigoma akichangia mada kwenye mafunzo ya waandishi wa habari Jijini Mwanza yanayohusu uandishi wa habari za uchaguzi.

Mwandishi wa habari Joel Maduka kutoka Storm FM Mkoani Geita, akichangia mada kwenye mafunzo ya waandishi wa habari Jijini Mwanza.

Waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mwanza, Simiyu, Geita, Kigoma, Kagera, Mara, na Shinyanga, wakiwa kwenye mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi na zenye Tija kwa umma.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.

Mafunzo yanaendelea.

Mafunzo yanaendelea.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo Jijini Mwanza.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde1 blog 

Share:

Benki Ya Dunia Yaipongeza Serikali Kwa Kujenga Reli Ya Kisasa Kwa Fedha Zake Za Ndani

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kutekeleza Mradi Mkubwa wa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) kwa kutumia fedha zake za ndani.

Bi. Kabagambe anayewakilisha nchi 22 za Kanda ya Afrika katika Benki hiyo yenye Makao yake Makuu Washington DC nchini Marekani, ametoa kongole hiyo kwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, baada ya kutembelea na kukagua sehemu ya ujenzi wa miundombinu ya Reli hiyo, kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro.

Alisema kuwa amefurahishwa na kiwango cha kiufundi kilichotumiwa na Kampuni ya Yapi Merkez iliyopewa kandarasi ya kujenga Reli hiyo na kwamba mradi huo sit u utakuwa na manufaa kwa Tanzania peke yake bali katika ukanda wa nchi za Afrika ambazo hazipakani na bahari.

“Nimekuja kujionea hatua kubwa zilizochukuliwa na Serikali ya Tanzania kujenga Reli hii ya kisasa na ninampongeza sana Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kwa kutekeleza mradi huu mkubwa na wa kielelezo kwa kutumia fedha zake za ndani” alisisitiza Bi. Kabagambe.

Aliahidi kuwa wakati Benki ya Dunia ikiangalia namna ya kuongeza ufadhili wa miradi kwa Tanzania, ataishawishi Benki hiyo pamoja na  taasisi nyingine za Kimataifa zinazotoa misaada na mikopo kutoa fedha ili Tanzania iweze kutimiza malengo yake ya kukamilisha ujenzi wa Reli hiyo ambayo itafungua fursa za kiuchumi na kijamii katika ukanda wa Afrika.

Mkurugenzi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Reli, Kutoka Kampuni ya Reli-TRC, Mhandisi Felix Nlalio, aliezea kufurahishwa kwake na ziara ya kiongozi huyo wa Benki ya Dunia pamoja na ahadi aliyotoa ya kuipigia debe Serikali kwenye taasisi za kimataifa ili zitoe fedha za kukamilisha mradi huo.

Aliahidi kuwa kazi yao kubwa kama Kampuni ya Reli na Serikali kwa ujumla ni kuchapa kazi usiku na mchana ili kuhakikisha kuwa ujenzi wa reli hiyo unaokwenda kwa kasi uweze kukamilika kwa wakati na kuiletea faida nchi pamoja na nchi jirani.

Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa unaohusisha awamu mbili, Kipande cha kwanza kati ya Dar es Salaam na Morogoro (kilomita 300), ambacho kilianza kujengwa Mei 2, 2017 na kitakamilika ifikapo Novemba 2, 2019 kwa gharama ya Sh trilioni 2.7, wakati kipande cha pili kinachoanzia  Morogoro –Makutupora (Manyoni, Singida) (kilomita 422), kilianza kujengwa Februari 26, 2018 na kitakamilika baada ya miezi 36 yaani Februari 25, 2021 kwa gharama ya Sh trilioni 4.4.

Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kuongeza mapato katika Bandari ya Dar es Salaam na pia kutaimarishara biashara hususani kati ya Tanzania na nchi zinazopitiwa na ushoroba wa kati (Central Corridor) za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Uganda na Rwanda.

Mwisho

 


Share:

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa, Dalili zake Hizi Hapa..Makala
51 minutes ago

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kulundia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.


Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.


Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.


Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.


Ugojwa huu wa ngiri unaweza kutibika

Mpate mpenzi wako unayempenda na kumfunga mume,mke mpenzi asitoke kwa mwingine .

Kwa Ushauri na Msaada wa Wasaliana na  0714006521


Share:

BALOZI SEIF AWAPONGEZA WABUNGE,AZZA HILAL NA NCHAMBI KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO SHINYANGA

Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi 

Na Annastazia Paul - Malunde1 blog

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad na Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Mhe. Suleiman Nchambi wamepongezwa kwa utendaji kazi wao mzuri hasa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayowanufaisha wananchi wao wanaowaongoza.




Pongezi hizo kwa wabunge hao zimetolewa jana Agosti 22,2019  na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Somagedi wilayani Kishapu ambapo amesema kwamba wabunge hao wanafanya kazi nzuri kwa maendeleo ya wananchi.


Akimzungumzia Mbunge Azza Hilal, Balozi Seif amesema kuwa "Kazi kubwa umeifanya maana mkoa huu ni mkubwa sana huna hata mfuko unaokusaidia, mwenzako huyu ana mfuko wa Jimbo unamsaidia saidia, nikuombe Mheshimiwa Azza jitahidini huko bungeni mpate mfuko maalum utakaowasaidia zaidi katika utendaji wenu, unafanya kazi nzuri sana". 

Aidha amempongeza Mbunge wa Jimbo la Kishapu,Mhe. Nchambi kwa kutekeleza vyema  ilani ya CCM na kukamilisha miradi iliyoanzishwa na wananchi na ikiwemo kutoa mifuko 1200 ya saruji na mabati 400 kwa ajili ya kuikamilisha miradi ambayo inaendelea, iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi katika kata zote 25 za wilaya ya Kishapu.

Balozi Seif amewaomba wananchi wasirubuniwe na badala yake wawangalie vizuri wabunge hao kwani wanafaa na ni chachu katika maendeleo yao.

"Niwapongeze sana kwa kupata wabunge hawa wazuri na katika uchaguzi wa 2020 muwatizame vizuri",amesema Balozi Seif.

Katika hatua nyingine amewataka Wabunge wote kujijengea desturi ya kutembelea majimbo yao na kuzungumza na wananchi ili wazijue kero zao.

"Kaeni kwenye majimbo yenu ili muwe karibu na wapiga kura wenu, msikilize kero zao na mjue mahitaji yao". Amesema Balozi Seif.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji Mbunge wa viti maalum Mkoani Shinyanga,Mhe.Azza Hamad amesema kuwa jumla ya shilingi Milioni 130.8 zimetumika katika miradi ya sekta mbalimbali wilaya Kishapu ikiwemo afya, elimu na vikundi vya wanawake.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Mhe. Suleiman Nchambi
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad.
Share:

MKURUGENZI WA BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA APONGEZA MAFANIKIO YA TASAF


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe (aliyeshika mkoba) akilakiwa na Mmoja waMaafisa wa TASAF, Bi. Tatu Mwaruka wakati wa ziara ya kukutana na Walengwa wa TASAF katika Mtaa wa Keko Machungwa wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam. 
Bi. Anne Kabagambe (picha ya juu na chini) akiwa katika mkutano na walengwa wa TASAF katika mtaa wa Keko Machungwa ,wilaya ya Temeke, jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Walengwa wa TASAF wakiwa na bidhaa walizozitengeneza baada ya kupata ruzuku kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini-PSSN.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe akikagua bidhaa zilizotengenezwa na Walengwa wa TASAF mtaa wa Keko Machungwa,Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DuniaBi. Anne Kabagambe katika picha na Walengwa wa TASAF baada ya kukagua bidhaa wanazozitengeneza kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato kkupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. 
Na Estom Sanga -TASAF 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi.Anne Kabagambe amepongeza mafanikio ya Serikali ya Tanzania Kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF katika kuboresha maisha ya Wananchi wanaokabiliwa na Umaskini. 

Bi. Kabagambe ambaye yuko nchini kwa ziara ya Kikazi , ametoa pongezi hizo baada ya kukutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF,na kujionea bidhaa wanazozalisha katika Mtaa wa Keko Machungwa ,Wilaya Temeke, mkoani Dar es salaam. 

Amesema kutokana na ubora wa Utekelezaji wa Miradi ya TASAF, Benki ya Dunia imekubaliana na Serikali ya Tanzania kuidhinisha kiasi cha Shilingi Trilioni Moja kwa ajili ya Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Sehemu ya Pili , fedha ambazo amesema zitasaidia zaidi juhudi za Serikali katika kuwahudumia Wananchi wanaokabiliwa na Umaskini. 

‘’Tumejiridhisha pasi na mashaka kuwa utekelezaji wa Shughuli za TASAF katika awamu zote tatu umekuwa wa mafanikio makubwa hivyo Benki ya Dunia imeamua kuendelea kusaidia juhudi hizi’’ amesisitiza Bi.Kabagambe. 

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika amesema kiasi hicho cha fedha kitatolewa mwezi Ujao wa Septemba na kuwataka Walengwa na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kuendelea kuboresha miradi ya kiuchumi ili kuongeza tija na hatimaye waweze kuboresha zaidi maisha na kuondokana na umaskini wa kipato. 

Kwa Upande wao Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wameishukuru Serikali kupitia TASAF kwa jitihada za kuwaondolea kero ya umaskini wa kipato na kuomba juhudi zaidi zielekezwe katika kuwapatia elimu ya Ujasiriamali ili waweze kuboresha shughuli za uzalishaji mali na kukuza kipato chao. 

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF umekuwa ukitekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao unahudumia takribani Kaya Milioni Moja na Laki Moja Kote Tanzania Bara,Unguja na Pemba na hivi sasa uko katika maandalizi ya utekelezaji wa Sehemu ya Pili ya Mpango inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni baada ya taratibu muhimu kukamilika.
Share:

WALIOPATA SIFURI MTIHANI WA ‘MOCK’ KIDATO CHA NNE SIMIYU KUWEKWA KAMBI MAALUM YA KITAALUMA

Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka amesema wanafunzi kidato cha nne waliopata daraja sifuri katika mtihani wa Mkoa wa Kujipima ‘Mock’ watawekwa  katika kambi maalum ya kitaaluma na kufundishwa na walimu mahiri  kwa lengo la kuwasaidia kuongeza ufaulu na kufikia  daraja la nne na kuendelea,  katika mtihani wa Taifa mwaka huu 2019.

Mtaka ameyasema hayo Agosti 22, 2019  katika kikao cha tathmini ya matokeo ya mtihani wa Mock kwa wanafunzi wa kidato cha nne na matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha sita mwaka 2019, ambapo mkoa wa Simiyu umekuwa miongoni mwa mikoa kumi bora Kitaifa.

Mtaka amesema lengo la Mkoa ni kuona wanafunzi wote waanafanya vizuri na hakuna mwanafunzi wa kidato cha nne anapata daraja sifuri hivyo wanafunzi wote wenye daraja sifuri na wale walipata daraja la nne alama za mwisho watawekwa pamoja na kutafutiwa walimu mahiri ili wawasaidie kupanda kitaaluma na kupata ufaulu mzuri.

“ Tutaweka kambi ya wanafunzi wote waliopata sifuri kwenye mtihani wa ‘Mock’ lakini pia hata wale waliopata daraja daraja la nne alama zinazoashiria kuelekea kwenye sifuri, Siku sitini kabla ya mtihani wafundishwe masomo manne tu, Civics(Uraia), Kiswahili, Kiingereza na Historia ngalau wapate alama D ili wapate cheti; nia yetu kama mkoa ni kuona kila mwanafunzi anafanya vizuri" alisema

Katika hatua nyingine Mtaka amewahimiza wakuu wa shule kusimamia kwa karibu ufundishaji na kuhakikisha katika kipindi hiki kuelekea katika mitihani wa Taifa wa Kidato cha nne, kuongeza ufaulu kutoka nafasi ya tisa ya mwaka 2018 kwenda kwenye nafasi nzuri zaidi.

Afisa elimu wa mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju  amewataka wakuu wa shule na maafisa elimu kata na wilaya  kuendelea kusimamia ufundishaji ili wanafunzi waweze kufanya vizuri na wale ambao shule zao hazikufanya vizuri waimarishe usimamizi ili kuongeza ufaulu.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Itilima amezungumzia kambi maalum za kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata sifuri kwenye mtihani wa Mock ambao wapo takribani  2000 kati ya wanafunzi zaidi ya 9000, kwamba zitakuwa msaada kwao na wanatarajia kuzifanya kwa ufanisi ili mkoa uwe kati ya mikoa tisa bora Kitaifa mwaka 2019(Single digit).

Mkuu wa mkoa ameahidi kutoa shilingi elfu 30 kwa mwalimu katika kila alama A itakayopatikana kwenye somo lake, shilingi milioni tano kwa shule itakayoingia kumi bora kitaifa, Milioni tano kwa Halmashauri itakayoingia kumi bora kitaifa, na milioni mbili kwa mwanafunzi atakayepata ufaulu  daraja la kwanza pointi saba na kuwa katika kumi bora kitaifa na ikiwa hatakuwa miongoni mwa wanafunzi bora kitaifa atapewa shilingi milioni moja.

Mkutano wa tathimini ya matokeo ya kidato cha sita mkoani Simiyu unawakutanisha wakuu wa shule za sekondari,maafisa elimu wilaya ,wakurugenzi watendaji, wenyeviti wa halmashauri za wilaya na wenyeviti wa Kamati za Elimu za Halmashauri lengo likiwa ni kuangalia walipo na wanapoelekea katika maendeleo ya elimu mkoani Simiyu

MWISHO.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger