Friday, 23 August 2019

BALOZI SEIF AWAPONGEZA WABUNGE,AZZA HILAL NA NCHAMBI KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO SHINYANGA

Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi 

Na Annastazia Paul - Malunde1 blog

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad na Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Mhe. Suleiman Nchambi wamepongezwa kwa utendaji kazi wao mzuri hasa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayowanufaisha wananchi wao wanaowaongoza.




Pongezi hizo kwa wabunge hao zimetolewa jana Agosti 22,2019  na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Somagedi wilayani Kishapu ambapo amesema kwamba wabunge hao wanafanya kazi nzuri kwa maendeleo ya wananchi.


Akimzungumzia Mbunge Azza Hilal, Balozi Seif amesema kuwa "Kazi kubwa umeifanya maana mkoa huu ni mkubwa sana huna hata mfuko unaokusaidia, mwenzako huyu ana mfuko wa Jimbo unamsaidia saidia, nikuombe Mheshimiwa Azza jitahidini huko bungeni mpate mfuko maalum utakaowasaidia zaidi katika utendaji wenu, unafanya kazi nzuri sana". 

Aidha amempongeza Mbunge wa Jimbo la Kishapu,Mhe. Nchambi kwa kutekeleza vyema  ilani ya CCM na kukamilisha miradi iliyoanzishwa na wananchi na ikiwemo kutoa mifuko 1200 ya saruji na mabati 400 kwa ajili ya kuikamilisha miradi ambayo inaendelea, iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi katika kata zote 25 za wilaya ya Kishapu.

Balozi Seif amewaomba wananchi wasirubuniwe na badala yake wawangalie vizuri wabunge hao kwani wanafaa na ni chachu katika maendeleo yao.

"Niwapongeze sana kwa kupata wabunge hawa wazuri na katika uchaguzi wa 2020 muwatizame vizuri",amesema Balozi Seif.

Katika hatua nyingine amewataka Wabunge wote kujijengea desturi ya kutembelea majimbo yao na kuzungumza na wananchi ili wazijue kero zao.

"Kaeni kwenye majimbo yenu ili muwe karibu na wapiga kura wenu, msikilize kero zao na mjue mahitaji yao". Amesema Balozi Seif.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji Mbunge wa viti maalum Mkoani Shinyanga,Mhe.Azza Hamad amesema kuwa jumla ya shilingi Milioni 130.8 zimetumika katika miradi ya sekta mbalimbali wilaya Kishapu ikiwemo afya, elimu na vikundi vya wanawake.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Mhe. Suleiman Nchambi
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad.
Share:

MKURUGENZI WA BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA APONGEZA MAFANIKIO YA TASAF


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe (aliyeshika mkoba) akilakiwa na Mmoja waMaafisa wa TASAF, Bi. Tatu Mwaruka wakati wa ziara ya kukutana na Walengwa wa TASAF katika Mtaa wa Keko Machungwa wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam. 
Bi. Anne Kabagambe (picha ya juu na chini) akiwa katika mkutano na walengwa wa TASAF katika mtaa wa Keko Machungwa ,wilaya ya Temeke, jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Walengwa wa TASAF wakiwa na bidhaa walizozitengeneza baada ya kupata ruzuku kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini-PSSN.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe akikagua bidhaa zilizotengenezwa na Walengwa wa TASAF mtaa wa Keko Machungwa,Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DuniaBi. Anne Kabagambe katika picha na Walengwa wa TASAF baada ya kukagua bidhaa wanazozitengeneza kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato kkupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. 
Na Estom Sanga -TASAF 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi.Anne Kabagambe amepongeza mafanikio ya Serikali ya Tanzania Kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF katika kuboresha maisha ya Wananchi wanaokabiliwa na Umaskini. 

Bi. Kabagambe ambaye yuko nchini kwa ziara ya Kikazi , ametoa pongezi hizo baada ya kukutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF,na kujionea bidhaa wanazozalisha katika Mtaa wa Keko Machungwa ,Wilaya Temeke, mkoani Dar es salaam. 

Amesema kutokana na ubora wa Utekelezaji wa Miradi ya TASAF, Benki ya Dunia imekubaliana na Serikali ya Tanzania kuidhinisha kiasi cha Shilingi Trilioni Moja kwa ajili ya Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Sehemu ya Pili , fedha ambazo amesema zitasaidia zaidi juhudi za Serikali katika kuwahudumia Wananchi wanaokabiliwa na Umaskini. 

‘’Tumejiridhisha pasi na mashaka kuwa utekelezaji wa Shughuli za TASAF katika awamu zote tatu umekuwa wa mafanikio makubwa hivyo Benki ya Dunia imeamua kuendelea kusaidia juhudi hizi’’ amesisitiza Bi.Kabagambe. 

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika amesema kiasi hicho cha fedha kitatolewa mwezi Ujao wa Septemba na kuwataka Walengwa na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kuendelea kuboresha miradi ya kiuchumi ili kuongeza tija na hatimaye waweze kuboresha zaidi maisha na kuondokana na umaskini wa kipato. 

Kwa Upande wao Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wameishukuru Serikali kupitia TASAF kwa jitihada za kuwaondolea kero ya umaskini wa kipato na kuomba juhudi zaidi zielekezwe katika kuwapatia elimu ya Ujasiriamali ili waweze kuboresha shughuli za uzalishaji mali na kukuza kipato chao. 

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF umekuwa ukitekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao unahudumia takribani Kaya Milioni Moja na Laki Moja Kote Tanzania Bara,Unguja na Pemba na hivi sasa uko katika maandalizi ya utekelezaji wa Sehemu ya Pili ya Mpango inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni baada ya taratibu muhimu kukamilika.
Share:

WALIOPATA SIFURI MTIHANI WA ‘MOCK’ KIDATO CHA NNE SIMIYU KUWEKWA KAMBI MAALUM YA KITAALUMA

Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka amesema wanafunzi kidato cha nne waliopata daraja sifuri katika mtihani wa Mkoa wa Kujipima ‘Mock’ watawekwa  katika kambi maalum ya kitaaluma na kufundishwa na walimu mahiri  kwa lengo la kuwasaidia kuongeza ufaulu na kufikia  daraja la nne na kuendelea,  katika mtihani wa Taifa mwaka huu 2019.

Mtaka ameyasema hayo Agosti 22, 2019  katika kikao cha tathmini ya matokeo ya mtihani wa Mock kwa wanafunzi wa kidato cha nne na matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha sita mwaka 2019, ambapo mkoa wa Simiyu umekuwa miongoni mwa mikoa kumi bora Kitaifa.

Mtaka amesema lengo la Mkoa ni kuona wanafunzi wote waanafanya vizuri na hakuna mwanafunzi wa kidato cha nne anapata daraja sifuri hivyo wanafunzi wote wenye daraja sifuri na wale walipata daraja la nne alama za mwisho watawekwa pamoja na kutafutiwa walimu mahiri ili wawasaidie kupanda kitaaluma na kupata ufaulu mzuri.

“ Tutaweka kambi ya wanafunzi wote waliopata sifuri kwenye mtihani wa ‘Mock’ lakini pia hata wale waliopata daraja daraja la nne alama zinazoashiria kuelekea kwenye sifuri, Siku sitini kabla ya mtihani wafundishwe masomo manne tu, Civics(Uraia), Kiswahili, Kiingereza na Historia ngalau wapate alama D ili wapate cheti; nia yetu kama mkoa ni kuona kila mwanafunzi anafanya vizuri" alisema

Katika hatua nyingine Mtaka amewahimiza wakuu wa shule kusimamia kwa karibu ufundishaji na kuhakikisha katika kipindi hiki kuelekea katika mitihani wa Taifa wa Kidato cha nne, kuongeza ufaulu kutoka nafasi ya tisa ya mwaka 2018 kwenda kwenye nafasi nzuri zaidi.

Afisa elimu wa mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju  amewataka wakuu wa shule na maafisa elimu kata na wilaya  kuendelea kusimamia ufundishaji ili wanafunzi waweze kufanya vizuri na wale ambao shule zao hazikufanya vizuri waimarishe usimamizi ili kuongeza ufaulu.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Itilima amezungumzia kambi maalum za kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata sifuri kwenye mtihani wa Mock ambao wapo takribani  2000 kati ya wanafunzi zaidi ya 9000, kwamba zitakuwa msaada kwao na wanatarajia kuzifanya kwa ufanisi ili mkoa uwe kati ya mikoa tisa bora Kitaifa mwaka 2019(Single digit).

Mkuu wa mkoa ameahidi kutoa shilingi elfu 30 kwa mwalimu katika kila alama A itakayopatikana kwenye somo lake, shilingi milioni tano kwa shule itakayoingia kumi bora kitaifa, Milioni tano kwa Halmashauri itakayoingia kumi bora kitaifa, na milioni mbili kwa mwanafunzi atakayepata ufaulu  daraja la kwanza pointi saba na kuwa katika kumi bora kitaifa na ikiwa hatakuwa miongoni mwa wanafunzi bora kitaifa atapewa shilingi milioni moja.

Mkutano wa tathimini ya matokeo ya kidato cha sita mkoani Simiyu unawakutanisha wakuu wa shule za sekondari,maafisa elimu wilaya ,wakurugenzi watendaji, wenyeviti wa halmashauri za wilaya na wenyeviti wa Kamati za Elimu za Halmashauri lengo likiwa ni kuangalia walipo na wanapoelekea katika maendeleo ya elimu mkoani Simiyu

MWISHO.


Share:

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UWEPO WA MALIKALE MADINI NA VITU VYA THAMANI

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) inapenda kuufahamisha umma na wadau wote wa sekta ya madini nchini kuwa kwa kipindi kirefu kumekuwepo na mitazamo mbalimbali juu ya uwepo wa malikale madini na vitu vya thamani  vilivyoachwa na wakoloni.


Kutokana na mitazamo hiyo, GST imekuwa ikifanya tafiti katika maeneo mbalimbali ili kubaini viashiria vya uwepo wa malikale madini ambazo zinasadikiwa kuwa zilifukiwa chini ya ardhi na wakoloni hasa wa Kijerumani baada ya vita ya pili ya dunia1939-1945. 

Baadhi ya maeneo yaliyofanyiwa utafiti ni:

•    Tarehe 16/1/2019 mpaka 21/1/2019, GST ilifanya utafiti katika  Kitongoji cha Ngarawani, kata ya Uwanja wa Ndege,Wilaya ya Serengeti, Mkoani Mara , juu ya kubaini viashiria vya uwepo wa malikale na vitu vya thamani vinavyosadikiwa kufichwa au kutunzwa ardhini.
.
•    Tarehe 27/2/2018 mpaka 7/3/2018, GST ilifanya utafiti katika Kijiji cha Vumba Kata ya Lugulu,wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro na Kitongoji cha Kakindu, kata ya Pongwe mtaa wa Pongwe Kusini Manispaa ya Tanga juu ya kubaini viashiria  vya uwepo wa malikale madini na vitu vya thamani  vinavyosadikiwa kufichwa au kutunzwa ardhini.

•    Tarehe 15/1/2016 GST ilifanya utafiti juu ya kusadikiwa kupotea kwa jiwe la thamani aina ya Almasi linalosadikiwa kufichwa katika shimo la Muhanga, katika kitongoji cha Manawa, kata ya Nkalalo, wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza.

Tafiti zote hizi zilitumia njia ya Jiolojia na Jiofizikia ambazo kisayansi zinaonesha mabadiliko ya asili ya sumaku ya dunia (magnetic survey), lengo la kutumia njia hizi ni kujua kama kweli malikale hizo zitakuwa zimehifadhiwa chini ya ardhi. Kwa kutumia njia tajwa hapo juu, kisayansi viashiria vya malikale vingekuwa katika maumbo madogo kulingana na vilipohifadhiwa kama vile umbo la mraba, mstatiri kuwakilisha sanduku au umbo la mviringo kuwakilisha pipa au chungu. Hata hivyo mahojiano ya kina yalifanyika ili kujua chanzo cha habari za malikale katika eneo hilo.

Matokeo ya tafiti  hizi yameonesha wazi kuwa maeneo yote yaliyofanyiwa utafiti, hayaoneshi viashiria vyovyote vya uwepo wa malikale madini wala vitu vya thamani. Sambamba na tafiti hizo mahojiano ya kina  yaliyofanyika miongoni mwa baadhi ya wanafamilia na jamii zinazozunguka maeneo husika  ili kujua sababu za  hisia za kuwepo malikale ambapo, majibu yote yalionesha ni usadikishwaji wa uwepo wa malikale katika maeneo hayo kwa kupewa hadithi (narrated stories) ambazo ndani yake zimejaa imani mbalimbali ikiwa ni pamoja na matambiko / ushirikina juu ya malikale.

Pamoja na imani hizo GST, itaendelea kufanya tafiti zake za Jiosayansi na kutoa elimu kwa jamii juu ya njia sahihi za  utafutaji madini katika makundi mbalimbali kwa lengo la  kuepusha jamii kupoteza muda, rasilimali fedha, mtaji na kuepusha kutokea kwa matukio yanayoendana na imani za kishirikina kama vile mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, watu wenye vipara na wanawake wenye ndevu.

IMETOLEWA NA;
TAASISI YA JIOLOJIA NA UTAFITI WA MADINI TANZANIA

23/08/ 2019


Share:

BALOZI SEIF AWAHAKIKISHIA WAKULIMA WA PAMBA KISHAPU KUWA YOTE KUNUNULIWA

Wakulima wa zao la Pamba wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wamehimizwa kuendelea kulima zao hilo kwa wingi kwani serikali inaendelea kusimamia na kuhakikisha Pamba yao inanunuliwa kwa bei nzuri na kuwanufaisha zaidi.

Hayo yamesemwa jana  na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipokuwa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Somagedi na kuwahakikishia kuwa serikali imeshaweka sawa mipango yote na pamba yote itanunuliwa.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM Mbunge wa Kishapu Mhe. Suleiman Nchambi amesema kuwa wakulima wa Pamba msimu huu wamepata shida kuuza Pamba yao kutokana na wanunuzi kutokwenda kununua Vijijini hali iliyowalazimu wakulima kuuza kwa bei ya hasara na Mbunge huyo kuiomba serikali kuwasaidi wakulima hasa suala la bei.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba amesema kuwa serikali imeshaongea na mabenki na tayari yameshatoa fedha kwa wanunuzi na Pamba imeshaanza kununuliwa kwa bei iliyopangwa hivyo wakulima wasiwe na wasi wasi.

Katika hatua nyingine Mbunge Nchambi ametoa mifuko 1,200 ya saruji na mabati 400 kwaajili ya kumalizia ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo shule, Zahanati na Vituo vya Afya, iliyoanzishwa na wananchi katika Kata zote 25 za Wilaya ya Kishapu.

Na Annastazia Paul - Malunde 1 blog
Share:

MBUNGE WA KISHAPU SULEIMAN NCHAMBI AWAONDOLEA HOFU YA MAJI WANANCHI

Wananchi katika wilaya ya Kishapu wanatarajiwa kunufaika na mradi wa maji safi na salama kutoka ziwa Victoria mradi ambao utawasaidia kuondokana na adha ya ukosefu wa huduma ya maji inayowakabili hivi sasa.

Hayo yamesemwa jana na Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mheshimiwa Suleiman Nchambi wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Somagedi.

Amesema kuwa tayari usanifu na michoro yote imeshakamilika hivyo ameiomba serikali itoe fedha kwaajili ya kukamilisha zoezi la usambazaji wa maji katika wilaya hiyo.

Kwa upande wake Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema kuwa atalifikisha suala hilo kwa Waziri Mkuu ili fedha zitolewe kwa ajili ya kukamilisha usambazaji wa maji safi na salama kwa matumizi ya wananchi na kwamba suala hilo ni muhimu hivyo litakekelezwa kwa haraka.
Na Annastazia Paul - Malunde1 blog
Share:

Wimbo Mpya wa Amber Lulu - Haters

Wimbo Mpya wa Amber Lulu - Haters


Share:

Video ya Darassa Ft. Maua Sama - Shika

Video ya Darassa Ft. Maua Sama - Shika


Share:

Mshindi wa Miss Tanzania kupatikana leo

Mrembo atakayeshikilia taji la Miss Tanzania 2019, anatarajiwa kupatikana leo katika kilele cha mashindano hayo katika ukumbi wa Millenium Tower, Makumbusho, Dar es Salaam.

Shindano hilo linawakutanisha warembo 20 kutoka kanda sita ambazo ni Nyanda za Juu Kusini, Kati, Mashariki, Ziwa, Dar es Salaam na Vyuo Vikuu.

Katika upande wa zawadi, mshindi atapewa shilingi 10,000,000.

Majaji wa shindano hilo ni Angela Damas (Miss Tanzania 2002), Shyrose Banji, Kenned The Remedy (Mtangazaji),  Miriam Ikoa na David Minja.


Share:

Mpango Wa RC Makonda Kuwashughulikia Matapeli Wa Mapenzi Wachukuwa Sura Mpya

Baada ya Mfumo wa Kupokea Malalamiko ya Wananchi dhidi ya utendajikazi wa watumishi wa Umma kuonyesha mafanikio makubwa ambapo hadi sasa umekamilika 99% na unatarajiwa kuzinduliwa Rasmi mwishoni mwa mwezi huu, sasa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaita tena Wataalamu wa ICT kufika ofisini kwake kwaajili ya Kuunda Mfumo wa Kusajili ndoa zote zilizofungwa kwa lengo la kuwalinda wanawake dhidi ya Wanaume walaghai wenye mchezo wa kutoa ahadi ya kuoa na mwisho wa siku wanaingia mitini.

RC Makonda amesema mfumo huo utasajili ndoa zote zilizofungwa kidini ikiwemo za Kikristo,Kislamu na zile zilizofungwa Kiserikali pamoja na kuchukuwa taarifa za Idadi ya watoto ndani ya ndoa.

Aidha RC Makonda amesema lengo la jitiada zote hizo ni kumlinda mwanamke dhidi ya Matapeli wa Mapenzi ambao wamekuwa na mchezo wa kuwachezea kinadada kwa kuwaahidi kuwa watawaoa na pindi wanapopata kile wanachokitaka wanaingia mitini jambo linalowaumiza wanawake na kupelekea baadhi yao kutaka kujiua, kupunguza ufanisi wa kazi na pia wengine kujikuta wanawachukia wanaume bila sababu yoyote.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema mpango huo pia unalenga kuzilinda ndoa zilizofungwa zisivunjike jambo litakalosaidia ustawi bora wa familia.

Mhe. Makonda amesema Mpango huo haulengi kuwatetea wanawake pekee bali hata wanaume waliowahi kuwagharamikia wanawake kwa kuwasomesha, kuwajengea nyumba, biashara na kuwapatia magari wanayo haki ya kurudishiwa gharama walizotumia.


Share:

Iran Yazindua rasmi mfumo wa makombora wa Bavar-373

Rais Hassan Rouhani wa Iran amepongeza kuongezeka kwa nguvu ya nchi hiyo dhidi ya shinikizo linaloongezeka la Marekani, na kusema nchi yake haijawahi kusikitishwa kutokana na njama za adui, bali imesimama dhidi yao kwa nguvu zaidi.

Rais Rouhani amesema hayo katika hafla ya kuzindua mfumo wa makombora ya ulinzi wa anga aina ya Bavar-373 iliyofanyika jana. 

Amesema shinikizo la Marekani dhihi ya Iran limeshindwa, na kuwapongeza wataalam wa Iran kwa kusanifu na kujenga mfumo huo.

Waziri wa ulinzi wa Iran ambaye pia alihudhuria hafla hiyo Bw. Amir Hatami amesema Iran imefanikiwa kutengeneza mfumo makini ambao sio tu unakabiliana na matishio ya anga, bali pia unatambua, kufuatilia, na kuharibu ndege na makombora yanayoweza kukwepa rada.

Mfumo huo wa makombora una uwezo wa kulenga shabaha hadi umbali wa kilomita 65 angani na kupiga umbali wa karibu kilomita 300 za nchi kavu. 


Share:

Serikali Ya Marekani Yaahidi Kusaidia Mapambano Dhidi Ya Ugonjwa Wa Seli Mundu (Sickle Cell) Nchini

Na WAJMW-Brazzaville
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amekutana na Waziri wa Afya wa Marekani Amiral Brett Giroir na kufanya mazungumzo na kuona namna gani nchi hizo mbili zinavyoweza kushirikiana katika kupambana na ugonjwa wa Sickle Cell (Seli Mundu) hasa kwa watoto wachanga na wale walio chini ya miaka mitano.

Waziri Ummy amemueleza Waziri huyo kuwa watoto wapatao 11,000 wanazaliwa na ugonjwa huo Tanzania na wengi hupoteza maisha kwa sababu ya kuchelewa kufanyiwa vipimo na kugundulika mapema.

Waziri Ummy amemueleza kuwa muelekeo wa nchi sasa ni kuhakikisha kuwa kila mtoto anayezaliwa anapimwa Sickle Cell na watakaogundulika matibabu yaanze mapema ili kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.

Mawaziri hao wamekubaliana kwa pamoja kushirikiana katika kudhibiti vifo vinavyoweza kutokea kwa sababu ya ugonjwa huo huku Waziri Amiral akiahidi kuimarisha upatikanaji wa vipimo, pamoja na matibabu kwa watoto wanaozaliwa na ugonjwa huo kuanzia ngazi ya zahanati na vituo vyote vya kutoa huduma za afya ya msingi nchini.

“Ni muhimu huduma hizi zikatolewa katika ngazi ya afya ya msingi mpaka taifa ili kuwapa huduma stahiki wananchi, hii ikiwa ni utekelezaji wa afya kwa wote. Suala la upimaji wa Seli Mundu, elimu kwa jamii na pia suala la matibabu katika ngazi zote za utoaji huduma ni muhimu vikapewa kipaumbele”. Aliongeza Waziri Ummy.

Hivi sasa huduma hii hapa nchini inapatikana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali za Rufa za Mikoa za Amana na Temeke pekee kwa nchi nzima.

Kwa upande wake Waziri Brett amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kwa kujenga viwanda vya dawa nchini ikiwa ni pamoja na za Sickle Cell. Pia ameahidi kutembelea Tanzania kuona na kujadiliana zaidi namna nchi hizi mbili zitavyoshirikiana katika kushughulikia ugonjwa huu nchini.

Mawaziri hao wanahudhuria mkutano wa 69 wa Shirika la Afya Duniani (WHO) unaojumuisha Mawaziri wa Afya toka nchi mbalimbali za Afrika unaoendelea jijini Brazzaville nchini Jamhuri ya Kongo.


Share:

TETESI ZA SOKA LEO IJUMAA AGOSTI 23,2019

Alexis Sanchez
Manchester United itakabiliwa na deni la mshahara la pauni milioni 12 kwa mchezaji Alexis Sanchez hata kama atasajiliwa na klabu ya Inter Milan. (ESPN)

Sanchez, 30, ambaye ni raia wa Colombia alikosa mazoezi ya Alhamisi na klabu yake ya Man United baada ya kwenda ubalozi wa Marekani jijini London. (Sun)

Mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke, 28, na mlinzi raia wa England James Tomkins, 30, wapo katika mazungumzo ya kuongeza mikataba yao na klabu ya Crystal Palace. (Guardian)

Barcelona wamekataa ofa ya klabu ya Inter Milan ambao wanataka kumsajili kiungo wa kimataifa wa Chile Arturo Vidal, 32, kwa mkopo. (Mundo Deportivo)Arturo Vidal
Man United wapo ukingoni kukubali mapatano ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Tottenham na Uhispania Fernando Llorente, 34. (Gazzetta dello Sport - via Star)

Lille wanaamini kuwa watafanikiwa kumng'oa kiungo Mreno Renato Sanches, 22, kutoka Bayern Munich. (L'Equipe)
Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer ataweza kutumia kitita cha pauni milioni 75 kwenye dirisha la usajili la mwezi Januari. Fedha hizo United walizipata baada ya kumuuza mshambuliaji raia wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, katika klabu ya Inter Milan mwanzoni mwa mwezi huu. (Talksport)

Kiungo Mreno wa klabu ya Leicester City Adrien Silva, 30, amesafiri kuelekea Monaco kwa ajili ya vipimo vya kiafya vitakavyofanyika leo Ijumaa. Silva anatarajiwa kujiunga na Monaco kwa mkopo. (Daily Telegraph)Willy Caballero
Kipa wa Chelsea Muargentina Willy Caballero, 37, anatakiwa na klabu Real Madrid. (Marca - in Spanish)

Ujumbe wa wawakilishi wa Real Madrid upo Ufaransa kufanya majadiliano juu ya uhamisho wa mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27 kutoka klabu ya Paris St-Germain. (Marca - in Spanish)Miamba ya Uhispania klabu za Real Madrid na Barcelona zinagombea saini ya Neymar kumng'oa PSG.

Winga raia wa Brazil anayekipiga na klabu ya Chelsea Kenedy, 23, anaangalia uwezekano wa kuihama moja kwa moja klabu hiyo kabla ya dirisha la usajili la ulaya kufungwa wiki ijayo. (Goal)

Miamba ya Uturuki klabu ya Fenerbahce imejitenga na harakati za uhamisho wa beki wa Manchester United na Argentina Marcos Rojo, 29. (Star)Fenerbahce wanasema hawataki tena kumsajiri mlinzi Rojo (katikati) kutoka Man United

Ombi la Barcelona la kumnunua kwa mkopo wa dau la £137m pamoja na kumpatia kandarasi ya kudumu mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27, limekataliwa na PSG huku mabingwa hao wa ligue 1 wakiitisha dau la £229m. (Marca)

Manchester United imemfanya winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19, lengo lao kubwa katika uhamisho wa mwezi Januari na wanajiandaa kutoa dau la £100m. (Sun)
Liverpool, Manchester City, Manchester United, Arsenal na Chelsea ni miongoni mwa klabu kuu barani Ulaya zinazomlenga mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 20, ambaye ana thamani ya £91m. (Sport1 - in German)

Tottenham imeanza mazungumzo ya kumuuza kiungo wa kati wa Kenya Victor Wanyama, 28, kuelekea klabu ya Bruges kwa dau la £11m.
Beki wa Liverpool na raia wa Croatia asiyehitajika sana Dejan Lovren, 30, anaivutia klabu ya Ujerumani ya Bayer Leverkusen baada ya kufeli kupata uhamisho kuelekea Roma. (Bild - in German)

Mshambuliaji wa Ubelgiji Michy Batshuayi, 25, anataka kusalia na kupigania nafasi yake Chelsea lakini ataitazama hali mwezi Januari. (Standard)

Manchester City inachunguza hali ya kiungo wa kati wa Argentina na klabu ya Velez Sarsfield Argentine Thiago Almada, 18, ambaye bado hajaandikisha upya kandarasi yake na klabu hiyo. (A Bola, via Manchester Evening News)
Chanzo - BBC
Share:

JAMAA MATATANI KWA KUREKODI VIDEO ZA UCHI WANAWAKE 550

Mwanaume mmoja amekamatwa jijini Madrid akishukiwa kuchukua video za uchi za wanawake zaidi ya 550 kinyume cha sheria.

Mwanaume huyo ana miaka 53 na ana asili ya Colombia, amerekodi video kupitia simu yake ya mkononi aliyoificha kwenye begi lake la mgongoni.

Polisi wamesema kuwa alizirusha mtandaoni video 283 katika tovuti za ngono na zikapata mamilioni ya watazamaji.

Wengi wa walengwa wa video hizo, baadhi ni watoto chini ya umri wa miaka 18, walilengwa maeneo ya usafiri wa treni.

Mwanaume huyo anashukiwa kuchukua video hizo tangu mwaka jana ambapo alianza kuziweka katika mitandao.

Alikua akirekodi pia katika maeneo kama masoko ya kisasa, kuna wakati alikua akijitambulisha kwa walengwa wake ili aweze kupata video nzuri.

Polisi walianza kumfatilia na kumkamata akirekodi mwanamke mmoja kwenye treni.

Katika video iliyowekwa katika mtandao wa Twitter , polisi wamemtaja kama mtu hatari zaidi kwa uhuru wa wanawake

Polisi walifanya upekuzi nyumbani kwake na kukuta kompyuta ikiwa na video zaidi ya mia moja, tovuti yake ina watumiaji 3,519.

Mshukiwa huyo bado anashikiliwa na polisi.

Nchini Uhispania kurekodi video za uchi bila ruhusa ni kosa la kijinsia kisheria na washatkiwa huweza kuhukumiwa kifungo.

Pia imekua kosa la kihalifu huko Uingereza na wales baada ya kampeni iliyofanywa na mwandishi Gina Martin.e.
Chanzo - BBC
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa 23 August























Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger