Tuesday, 20 August 2019

MAPOCHOPOCHO YA SHEREHE YA POSA YAUA WANNE....KADHAA WAPO HOI HOSPITALI


Wakazi katika kijiji cha Rodoma, Kieni, Kaunti ya Nyeri nchini Kenya wamekumbwa na mshtuko mkubwa baada ya watu wanne kuaga dunia baada ya kula chakula kinachodaiwa kuwa na sumu kwenye sherehe ya posa.

Familia hiyo ilikutana katika kijiji cha Rodoma, Kaunti ya Nyeri kwa ajili ya sherehe ya kulipa mahari.

 Miongoni mwa waliopoteza maish ni mama ya bwana mtarajiwa na wakwe wawili huku watu wengine kadhaa waliokula chakula kwenye sherehe hiyo wakilazwa hospitalini. 

Akizungumza na Citizen TV Jumatatu, Agosti 19,2019 Naibu Kamishna wa Kaunti ya Kieni Magharibi Samuel Kariuki alithibitisha kisa hicho na kusema wanne waliaga dunia na wengine kupelekwa hospitalini. 

Kulingana na Kariuki na wengine waliokuwa na ufahamu kuhusu mkasa huo, waliopika chakula hicho ni wapishi waliokodishwa kutoka soko la Gikomba, Nairobi. 

Baadhi ya walioaga dunia walidaiwa kuumwa na tmbo na kuendesha na wageni wengine walikimbizwa katika zahanati ya Kariminu baada ya kuanza kuhisi maumivu makali.
Share:

Mke na mume watupwa Jela miaka 5 kwa kuwakeketa watoto wao watatu

Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara imewahukumu kifungo cha miaka mitano jela, Thadei Parokwa (43) na mke wake Lowema Thadei (34) kwa kuwakeketa watoto wao watatu. 

Mwendesha mashitaka wa Polisi mahakama ya Wilaya ya Simanjiro, Mkaguzi wa Polisi, Hamilton Moses, alisema shitaka lililowakabili washitakiwa hao kuwa ni ukatili dhidi ya watoto.

Amesema kesi hiyo iliripotiwa kituo cha Polisi Orkesmet tarehe Machi 19, mwaka jana baada ya kukamatwa watuhumiwa hao ambao walidaiwa kuwakeketa watoto hao kwa bibi yao aliyekuwa Kitongoji cha Kangala Kijiji cha Lobosireti Wilayani humo.

Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro, Lugano Kasebele, baada ya kujiridhisha kwa pande hizo mbili, aliwatia hatiani wazazi hao kwenda jela miaka mitano ama faini ya laki sita na fidia ya laki tisa.


Share:

Mama Amuua Mwanae na Kisha na Yeye Kujinyonga

Binti wa miaka 22, Ephrazia Maneno, Mkazi wa Kijiji cha Nyaseke kata ya Bulela Mjini Geita anadaiwa kumuua kwa kumnyonga Mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu kisha naye kujinyonga.

Tukio hilo limetokea Jumapili August 18, 2019 saa saba mchana umbali wa mita 300 kutoka nyumba aliyokuwa akiishi, alitumia khanga kujinyonga katika mti wa mwembe.

Maneno Kapunda, Baba mzazi wa Efrazia amedai binti yake alikua akiishi na Babu na Bibi baada ya Wazazi kutengana na hakueleza tatizo lolote kabla ya kufanya uamuzi wa kujiua

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyaseke, John Maguta amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Polisi walifika eneo la tukio na kutoa mwili uliokuwa ukining’inia na kuruhusu familia kuendelea na taratibu za mazishi yaliyofanyika Jumatatu Kijijini hapo.


Share:

Kizimbani Kwa Tuhuma Za Kumkata Msichana Sehemu Za Siri Kwa Wembe

Mkazi wa Tandale kwa Mtogole wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam,  Siasa Samwel (30) amepandishwa katika mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jana Jumatatu Agosti 19, 2019 kwa tuhuma za kumkata msichana sehemu za siri na kumsababishia maumivu.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumkata mwanamke huyo sehemu za siri Novemba 15, mwaka jana na kumsababishia kupoteza bikra yake.

Akisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Boniface Lihamwike na Mwendesha Mashtaka wa Serikali Veronica Mtafya, amedai tukio hilo lilitokea eneo la Tandale Chama Wilayani Kinondoni jijini Dar es salaam.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo amekana shtaka hilo ambapo mwendesha mashtaka alidai upelelezi haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kusomwa kesi hiyo.

Hakimu Lihamwike amesema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu wenye barua za utambulisho, nakala ya vitambulisho na kusaini bondi ya Sh milioni moja.

Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya hayo na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakapokuja kusomwa tena Septemba 2, mwaka huu.


Share:

Picha : WAANDISHI WA HABARI MTANDAONI 'BLOGS & ONLINE TV' WAPEWA MAFUNZO KUHUSU HAKI ZA BINADAMU

Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media -  Blogs/ Online TV) nchini wametakiwa kujitafakari na kutimiza wajibu wao katika utetezi wa haki za binadamu.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne Agosti 20,2019 na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) Claud Gwandu wakati akifungua mafunzo ya Haki za Binadamu mjini Dodoma yanayoratibiwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kupitia ya Klabu Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC) kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT.

Gwandu alisema ni vyema waandishi wa habari wa vyombo vya habari wakatumia mafunzo wanayopewa na kuonesha kwa vitendo namna gani mafunzo ambayo wamekuwa wakipewa yanawasaidia katika kazi zao.

"Washiriki wa Work Group Three inayohusisha waandishi wa habari mtandaoni tutimize wajibu wetu kwa yaliyo ndani ya uwezo wetu, bado hatujaona habari za haki za binadamu na demokrasia kama ambavyo tunatakiwa kufanya",alisema.

"Tunaendelea kufuatilia kwa makini namna gani tutapunguza washiriki katika kundi hili, wafadhili wetu wameendelea kujiuliza na kuhoji kuhusu mafunzo tunayopewa na wajibu wetu",

"Nyinyi ni watu wazima mjitathimini mmesafiri kutoka kwenu kuja kushiriki mafunzo yanayogharamiwa kwa fedha nyingi,halafu hatuoni mabadiliko makubwa,hatutasita kupunguza washiriki ili tubaki na wale wanaozingatia kinachofundishwa",aliongeza Gwandu.

Naye Mwezeshaji wa mafunzo hayo Wakili Flodius Mtungi akizungumzia kuhusu haki alisema, haki za binadamu hazirithiwi wala kutolewa na mtu hivyo ni wajibu wa waandishi wa habari wana jukumu kubwa la kulinda haki za binadamu na kupaza sauti pale haki zinapovunjwa.

Mafunzo hayo ya Haki za Binadamu ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media).
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) Claud Gwandu wakati akifungua mafunzo ya Haki za Binadamu mjini Dodoma yaliyoshirikisha waandishi wa habari mtandaoni (Blogs/Online Tv ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media). Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) Claud Gwandu akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Haki za Binadamu.
Mwezeshaji wa mafunzo ya Haki za binadamu Wakili Flodius Mtungi akitoa mada kuhusu haki za binadamu.
Mwezeshaji wa mafunzo ya Haki za binadamu Wakili Flodius Mtungi akitoa mada kuhusu haki za binadamu.
Mwezeshaji wa mafunzo ya Haki za binadamu Wakili Flodius Mtungi akitoa mada kuhusu haki za binadamu.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

Wizara Ya Afya Yatoa Muda Zaidi Usajili NGO's

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii imetoa muda zaidi wa zoezi la usajili na uhuhishaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalijisajili kwa Sheria ya Makampuni, Bodi ya Wadhamini na sheria ya Jumuiya za Kiraia chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ambazo kwa sababu tofouti hazijakamilisha zoezi la uhuishaji kwa mujibu wa Sheria no. 3 ya mwaka 2019.
 
Akizungumza na vyombo vya habari jana  jijini Dodoma Msajili wa NGOs Nchini Bi. Vickness Mayao amesema kimsingi kazi hii inahusu yale mashirika ambayo hayajakamilisha zoezi la kuhuisha vyeti vyao kwa mujibu wa Sheria na Wizara imeona ni vyema kuendelea na zoezi hilo baada ya kuwa imefanya hivyo katika  Kanda tano hapa nchini.
 
“Tunaendelea na zoezi la usajili huu ambao kisheria unakamilika tarehe 30 Augusti 2019  kama Sheria no.3 ya mwaka 2019 inavyoelekeza ili kutoa nafasi zaidi kwa Mashirika yaliyosalia ambayo kwa namna moja au nyingine bado hayajakamilisha usajili wake na ifikapo mwisho wa mwezi huu kila Shirika litabaki katika Sheria yake”. Aliongeza Bi. Mayao. 
 
Aidha Bi. Mayao amesema kuwa Ofisi ya Msajili wa NGOs tayari imetoa orodha ya awali ya Mashirika ambayo yameondolewa kwenye Daftari la Msajili wa Mashirika Yasiyo kuwa ya Kiserikali ambayo pia yanatakiwa kuhamia katika Sheria nyingine akiongeza kuwa orodha hiyo tayari imewekwa kwenye tovuti ya Msajili wa NGOs.
 
Bi. Mayao ametaja idadi ya Mashirika hayo kuwa ni 158 na inatarajia kuongezeka kadili zoezi la kuyatambua Mashirika hayo linavyoendelea na kusisitiza kuwa orodha iliyopo ni ya wali na kuyataka Mashirika hayo kufanya haraka kuhuisha usajili wao kama Sheria mpya inavyosema kwani kushindwa kufanya hivyo maana yake shirika husika litakuwa limefutwa.

Msajili wa NGOs ameongeza kuwa zoezi la uhuishaji limefanikiwa kwa asilimia 85 baada ya kuwa limefanyika katika kanda tano ikiwemo Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati , Kanda ya Kaskazini, Pwani  na Nyanda za Juu Kusini na sasa zoezi hili linaendelea mjini Dodoma kwa ajili ya Mashirika ambayo bado yamesalia na zoezi hili linaendelea kwa kushirikiana na wale wanaosimamia Sheria nyingine.
 
Zoezi la uhuishaji Mashirika linafanyika kwa miezi miwili kwa mujibu wa Sheria no.3 ya mwaka 2019 na tayari limekamilika katika Kanda tano lakini linaendelea kukamilika Jjini Dodoma ili kutoa fursa ya ziada kwa Mashirika ambayo bado hajakamilisha zoezi la uhuishaji usajili kwake kabla ya kuondolewa usajili kama takwa la kisheria lilivyo katika Sheria hiyo.


Share:

Madereva Wa Daladala Kituo Cha Sabasaba Dodoma Waleta Mgomo Kisa Machinga Kuzagaa Kituoni Hapo.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Madereva  Wa  Daladala katika kituo cha daladala  sabasaba  jijini Dodoma  wamegoma kufanya safari wakishinikiza wamachinga kuondolewa kutokana na ufinyo wa nafasi katika eneo hilo.
 
Wakizungumza na waandishi wa habari hapo jana Agosti 19,2019  baadhi ya madereva wamesema kuwa,wamegoma kutokana na machinga kutokuwa na utaratibu mzuri wa kufanya biashara.
 
Baadhi ya abiria waliokuwa wakifanaya safari zao za kutoka na kuingia ndani ya stand hiyo wanaeleza athari za mgomo huo,kama anavyoeleza Franco James wakiwa na wenzake.
 
Akizungumza na madereva hao mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi mbali na kuomba madereva hao kuendelea kusafirisha, amepiga marufuku baadhi ya biashara ikiwemo uchomaji mshikaki .
 
Mgomo huo Ulimalizika na shughuli zikaendelea kama kawaida katika kituo cha daladala cha SABASABA jijini  Dodoma baada ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi kuingilia kati na kuamru wafanyabiashara hususan wakaanga mishikaki kutofanyia biashara katika kituo hicho.


Share:

APOTEZA BIKRA YA MWANAMKE KWA KUMCHANJA VIWEMBE SEHEMU ZA SIRI


Erick Mugisha, Dar es salaam
Mwanaume mmoja mkazi wa Tandale kwa Mtogole jijini Dar es Salaam, Siasa Samwel (30), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa kosa la kumjeruhi kwa kumkata kwa viwembe sehemu za siri mwanamke mmoja(jina linahifadhiwa).

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumkata mwanamke huyo sehemu za siri Novemba 15, mwaka jana na kumsababishia kupoteza bikra yake.

Akisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Boniface Lihamwike na Mwendesha Mashtaka wa Serikali Veronica Mtafya, amedai tukio hilo lilitokea eneo la Tandale Chama Wilayani Kinondoni jijini Dar es salaam.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo amekana shtaka hilo ambapo mwendesha mashtaka alidai upelelezi haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kusomwa kesi hiyo.

Hakimu Lihamwike amesema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu wenye barua za utambulisho, nakala ya vitambulisho na kusaini bondi ya Sh milioni moja.

Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya hayo na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakapokuja kusomwa tena Septemba 2, mwaka huu.
Chanzo -MTANZANIA
Share:

MSD Kufungua Kituo Cha Uuzaji Na Usambazaji Dawa Simiyu

Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya dawa (MSD)  Laurean Bwanakunu amesema Bohari ya dawa inatarajia kuanza ujenzi wa kituo cha mauzo na  usambazaji  dawa mkoani Simiyu ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa mkoa wa Simiyu na mikoa jirani.

Bwanakunu ameyasema hayo Agosti 19,2019 katika ufunguzi wa  mkutano wa tathmini ya utendaji  kazi wa menejimenti na mameneja wa kanda wa bohari ya dawa nchini.

Lengo likiwa   ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu.

Bwanakunu amesema wameamua kufanyia mkutano wa tathimini mkoani Simiyu ili kuweza kujionea eneo la ujenzi wa kituo cha mauzo ya dawa ikiwa ni moja ya kuongeza wigo mpana wa utoaji huduma.

“Tutakuwa na mkutano wa siku tatu hapa Simiyu kwa ajili kufanya tathmini ya utendaji kazi ulivyokuwa kwa mwaka mzima, tutawafanyia tathmini wakurugenzi wote na wenyewe watamfanyia Mkurugenzi Mkuu; lakini pia tutatumia fursa hii kutembelea mahali tulipoamua kujenga bohari kwa kuwa tunatarajia kujenga bohari hapa Simiyu”alisema Bwanakunu.

Akifungua mkutano huu, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema  maboresho ya usambazaji wa dawa yaliyofanywa na Bohari ya Dawa (MSD) yameongeza upatikanaji wa dawa mkoani Simiyu ambapo kwa sasa upatikananji wa dawa ni zaidi ya asilimi 88.

Aidha, Sagini ametoa wito kwa Taasisi zote za Umma zinazohitaji maeneo kwa ajili ya kujenga Ofisi zao kufika mkoani Simiyu, ambapo amewahakikishia upatikanaji wa maeneo lengo likiwa ni kuendelea kusogeza huduma mbalimbali karibu na wananchi.

Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa  Bohari ya Dawa(MSD), Bibi. Victoria Elangwa amesema uwepo wa kituo cha kusambaza dawa Simiyu kutapunguza umbali kwa Mkoa wa Simiyu na mikoa ya Mara na Shinyanga  kupata huduma za Bohari ambazo kwa sasa zinapatikana Mwanza.

Ameongeza kuwa ujenzi wa Kituo hicho unatarajia kuanza mara moja kwa kuwa tayari wataalam wameshaanza kushughulikia masuala ya ukamilifu wa mazingira na baada kukamilisha kazi hiyo atatafutwa mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi.


Share:

KAKA NA DADA WASHINDA KESI KUOANA WENYEWE KWA WENYEWE


James Banes (41) na Victoria Banes (38 ) ni ndugu wawili wa familia moja pia ni wapenzi kutoka New Jersey Marekani, wameshinda shauri la mahakama kuhusu kufunga ndoa.

Ndugu hao wameshinda shauri hilo baada ya kukaa miaka 10 kupambania kuhusu kupitishwa kwa sheria hiyo kwa kaka na dada kuona wenyewe kwa wenyewe.

James Banes ambaye ni kaka wa familia hiyo amesema, "alikuwa anaishangaa mahakama kukubali mtu kufunga ndoa na binamu yake na si mtu na dada yake ilihali kuwa hata Adam na Hawa walifanya hivyo kwa nini leo isiwe kwa sisi ndugu".

Pia Victoria Banes naye ameendelea kusema muda wote walikuwa na ndoto ya kuwa na familia kubwa na ndoto hizo zinakuja kuwa kweli baada ya kushinda kesi hiyo na kwa sasa ni mjamzito anategemea watoto mapacha.

Baada ya kushinda kwa kesi hiyo ndugu hao wamesema walifurahi sana kusikia hivyo na kupitia wao, watawahamasisha mamilioni ya wamerakani kuwa na mahusiano na ndugu zao.
Share:

TEDx OYSTERBAY YAKUTANISHA WADAU KUJADILI MAENDELEO NA CHANGAMOTO MBALI MBALI

Kongamano la kuongeza maarifa la TEDx Oysterbay, liilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wadau kutoka nyanja mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi. ambapo walipata fursa ya kusikiliza mada na kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusiana na masuala ya ubunifu, mapinduzi ya teknolojia,michezo na mada nyinginezo nyingi zenye kuelimisha zilizotolewa na wataalamu.Kampuni ya bia Tanzania (TBL) ilikuwa mmoja wa wadhamini wa kongamano hilo.
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada wakati wa kongamano la TEDx Oysterbay lililofanyika katika ukumbi wa The Little Theatre jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wakibadilishana mawazo wakati wa kongamano hilo
Baadhi ya washiriki wakifurahi katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kongamano hilo
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne August 20




Share:

Monday, 19 August 2019

Je, Wewe ni Mwathirika wa Kujichua?... Soma Hapa

🔖Asilimia 45-80 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kutowatimizia vyema wake au wapenz wao na kuwasababishia kutoka nje ya mahusiano yao.
------------------
🔖NINI CHANZO CHA HAYO?

📌Kupiga punyeto
,Ngiri,

Vidonda vya tumbo,

📌Korodani moja kuvimba,

📌 Msongo wa mawazo,

📌Presha, Magonjwa ya zinaa,

 ðŸ“ŒKufanyiwa tohara
ukiwa na umri mkubwa,

📌Kisukari.
------------------

💉DR. KHAFIZ Sasa anakuletea tiba sahihi ya tatizo la Nguvu za kiume.na maumbile mafupi
-------------------

💊MUJARABU :Hii hutibu na kuponya kabisa tatizo la Nguvu za kiume, utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka 
------------------
📌inazalisha homoni kwa mwingi na kuku fanya uwe nambegu nyingi zenye vimeleo vyauzazi vilivo koma
------------------
📌 itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20-45. Dawa hii imechanganywa na miti 18,Hata wazee wenye umri mkubwa wa zaidi ya miaka 85 wanapona kabisa okoa mahusiano yako, ndoa yako sasa.
------------------
📌TIBA YA KUDUMU

 -----------------
📌TUMIALEO UWONE MAJABU YAKE

------------------
🌠Pia tunadawa za Kupandisha nyota , Uzazi, Pumu, Malaria sugu, miguu kuwaka moto, Kaswende, Kisonono  na mvuto wa mpenzi.bishara na zindiko
--------------------
 ðŸ’‰DR.KHAFIZ ANAPATIKANA DAR-ES-SALAM SM 0716948950 kwa wale wa mikoani mingine huduma hii utaipata popote ulipo.


Share:

Okoa Ndoa Yako Na Afya Yako Sasa Kwa Kutumia Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume Na Kisukari

Ni dawa zilizopimwa na mkemia na kupewa no 341/VOL,XV/36 na TFDA no 0127/F/F/1819/ MTINJETINJE ni dawa ya kisukari .....Hurudisha kongosho katika hali ya kawaidi hata kama limefeli haijalishi unatumia vidonge au sindano za insulin, itaifanya sukari kuwa normal

SUPER MAJINJA ni dawa inayotibu nguvu za kiume yani matatizo yafatayo (1) kushindwa kurudia tendo na mwili kuchoka (2)kuwai kufika kabla ya  mwenzi wako (3)maumbile ya kiume kulegea na kusinyaa (4)maumbile ya kiume  kuingia ndani na kuwa mafupi kwa wale walio jichua (5)miuungurumo ya tumbo,ngiri,kukosa choo,kiuno kuuma

ACHA KUONGOPEWA SASA DAWA HIZI NI TOFAUTI NA ULIZOWAI KUTUMIA

NJOO OFISINI KWANGU MBAGALA KARIBU NA BENK YA KCB NA mwanza yupo wakala piga simu ya DR AGU whatsapp 0783185060. 0620113431


Share:

Uingereza Yafadhili Masomo Ya Watumishi Wizara Ya Fedha Na Mipango

Na. Peter Haule, WFM, Dar es Salaam
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amewataka Watumishi wa Wizara hiyo waliopatiwa ufadhili wa masomo na Serikali ya Uingereza kupitia Shirika lake la Maendeleo (DFID) katika vyuo vikuu vya nchi hiyo kusoma kwa bidii ili kuja kulitumikia taifa kwa umahili zaidi katika nyanja za  uchumi na uchambuzi wa masuala ya fedha.

Hayo yameelezwa na Waziri huyo wakati wa hafla ya kuwaaga rasmi watumishi watano wa Wizara hiyo waliopata udhamini huo, iliyofanyika katika Ofisi za British Council- Tanzania, jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mpango alisema kuwa, miaka miwili iliyopita aliiomba Serikali ya Uingereza kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (DFID), wasaidie kusomesha watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Vyuo vikuu vya Uingereza, kwa kuwa Wizara ya Fedha katika nchi yeyote ndio nguvu ya fikra katika Serikali, hivyo bila watumishi wenye ujuzi kutakua na wizara dhaifu.

“Ninawasisitiza sana vijana waliopata fursa ya kwenda kusoma Uingereza, wajue dhamana wanayokwenda nayo, watanzania takribani milioni 50 wanaimani nao, wanamatarajio kwamba watakapokwenda huko watazingatia kusoma kwa bidii, ili wakirudi wawe wataalam waliobobea katika masuala ya uchumi na uchambuzi wa masuala yote ya fedha ndani ya Wizara”, alieleza Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango alisema kuwa, pamoja na kuiomba Serikali ya Uingereza kutoa mafunzo kwa vijana hao aliwaomba pia iwapatie mafunzo kwa vitendo katika taasisi zinazojihusisha na masuala ya uchumi na fedha  nchini humo ili wapate udhoefu.

Alisema anaishukuru Serikali ya Uingereza kwa kukubali ombi hilo na sasa ni timu ya tatu kupelekwa masomoni, awamu ya kwanza na ya pili walipelekwa jumla ya vijana kumi, na sasa tumewaaga rasmi watumishi watano ambao wataenda mwezi ujao na kufikisha idadi ya watumishi 15.

Amewataka watumishi hao wakaitangaze vizuri Tanzania na wakirudi waje kuitumikia Tanzania ili taifa lipate maendeleo yanayotarajiwa baada ya hatua hiyo muhimu ya kuwekeza kwa vijana watanzania katika kupata ujuzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa Uingereza (DFID), Bi Beth Arthy, alisema kuwa  tangu mpango huo uanze Serikali yake imekwisha wasomesha wanafunzi kumi katika fani za uchumi na uchambuzi wa masuala ya fedha na idadi ya watumishi watano watakao kwenda kusoma nchini humo itafikisha idadi ya watumishi 15.

Alisema kuwa lengo la hatua hiyo ni  kuisaidia Serikali kuimarisha utawala wa fedha, masuala ya usimamizi wa kodi na mifumo ya kifedha.

Aidha amewapongeza waliofanikiwa kufuzu mitihani mbalimbali iliyowawezesha kupata nafasi hizo kwa watumishi wa Wizara hiyo kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na kuwataka kufanya bidii kwa kuzingatia masomo ili watakapomaliza masomo yao warudi kulitumikia Taifa la Tanzania.

Watumishi waliopata ufadhili wa masomo kupitia Shirika la DFID ni pamoja na Patricia Mlowe, Diana Ulomi, Alex Mwakisu, Martha Luanda na Hamad Bakar Said.

Kwa upande wa wanufaika kupitia wawakilishi wao, Bi. Diana Ulomi na Hamad Said waliishukuru Serikali ya Uingereza na Wizara ya Fedha na Mipango kwa jitihada za kufanikisha kuwapatia masomo kwa ngazi ya Uzamili ili kuongeza ujuzi wa kulitumikia taifa katika masuala ya uchumi hasa kipindi hiki ambacho Tanzania inaelekea katika uchumi wa kati uliojikita katika Viwanda na wameahidi kusoma kwa bidii ili kufikia malengo hayo.

Mwisho.


Share:

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa, Dalili zake Hizi Hapa..Makala
51 minutes ago

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kulundia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.


Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.


Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.


Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.


Ugojwa huu wa ngiri unaweza kutibika

Mpate mpenzi wako unayempenda na kumfunga mume,mke mpenzi asitoke kwa mwingine .

Kwa Ushauri na Msaada wa Wasaliana na  0714006521


Share:

Mkurugenzi TPDC Aliyerudishwa Kazini Na Rais Magufuli Aachiwa Huru Na Mahakama

Vigogo watano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC),akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo,James Mataragio wameachiwa huru leo August 19, 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP) kutokuwa na nia ya kuendelea na Mashitaka dhid yao.

Mataragio na wenzake walikuwa wakikabiliwa na shtaka moja la matumizi mabaya ya madaraka ambapo ilidaiwa kati ya Aprili 8, 2015 na Juni 3, 2016 walitenda kosa hilo wakiwa watumishi wa umma na waajiriwa wa TPDC.

Agosti 24, 2016 Bodi ya Wakurugenzi wa TPDC, ilimsimamisha Mkurugenzi huyo kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zikimkabili .

Hata hivyo, Julai 22, 2019 Rais Magufuli aliielekeza wizara ya nishati kumrejesha ofisini  katika wadhifa wake aliokuwa nao kabla ya kusimamishwa na kushtakiwa. 

Wengine waliofutiwa mashtaka ni George Seni, aliyekuwa Kaimu Meneja wa Uvumbuzi; Welington Hudson, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Utawala; Kelvin Komba, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mkondo wa Juu na Edwin Riwa aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mipango

Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Saimoni amedai leo Jumatatu Agosti 19,2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Kelvin Mhina kuwa shauri hilo limekuja kwaajili ya kusikilizwa lakini Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameonyesha nia ya kutoendelea na kesi hiyo.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger