Friday, 16 August 2019

LIVE Kutoka Morogoro: Ziara Ya Rais Wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa....Tazama Hapa

Live Kutoka Morogoro: Ziara Ya Rais Wa Afrika Kusini  Mhe. Cyril Ramaphosa....Tazama Hapa


Share:

MWANAMUZIKI MBALAMWEZI WA KUNDI LA THE MAFIK AFARIKI DUNIA


Mwanamuziki Mbalamwezi ambaye ni mmoja wa Wasanii  wanaounda kundi la The Mafik amefariki dunia kutokana na majeraha ambayo yanahusishwa na kupigwa.

Baadhi ya ndugu wamesema taarifa za awali ni kwamba Mwili wake ulikutwa maeneo ya Africana Dar es salaam ukiwa hauna nguo ikiwa ni saa kadhaa zimepita toka msanii huyo atokomee bila kujulikana alipo. 

Msanii huyo ameshiriki katika kazi za kundi ambazo zimefanya vizuri kama Passenger, Sheba,Carola, Vuruga, na Dodo, pia ameshirikishwa katika nyimbo za Ruby na Ben Pol.




Share:

Ajali ya Basi na Lori Yaua Watu Wanne Morogoro

Watu 4 wamefariki dunia na wengine 26,  wamejeruhiwa kufuatia ajali iliyohusha basi la abiria na Lori  kugongana uso kwa uso katika eneo la nanenane Manispaa ya Morogoro.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo imehusisha basi la abiria lenye namba za usajili T212 DNU na Lori.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa,Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi ambaye alitaka kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua taadhari.

"Ni kweli usiku wa kuamkia leo Ijumaa August 16, saa saba na nusu usiku imetokea ajali eneo la Nanenane, Morogoro, basi mali ya kampuni ya Safari Njema ambayo ilikuwa inatokea DSM kwenda Dodoma imegongana kwa ubavu na lori mali ya Tumbaku Alliance, watu 4 wamefariki.

"Ingawa watu 4 wamefariki ila abiria wengine waliokuwa kwenye basi walikimbizwa Hospitali ya Mkoa Morogoro sababu ya mshtuko na wengi wametibiwa na kuruhusiwa, wamebakia abiria 3 wanaendelea na matibabu, dereva wa lori ni miongoni mwa waliofariki.

"Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa basi ambaye aliovertake pasipo kuchukua tahadhari na kukutana na gari nyingine mbele kisha ajali ikatokea, dereva wa basi ametoweka na tunamtafuta, kama hatopatikana tutamkamata mmiliki wa basi ili atuoneshe dereva alipo". Amesema Mutafungwa



Share:

Waziri Jafo Aingilia Kati sakata la watumishi wa Hospitali kulipishwa mashine ya Ultrasound iliyoibiwa

Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jafo ameingilia kata sakata la watumishi wa Hospitali ya Mji wa Bariadi  na kuamruru wasichangishwe fedha kufidia mashine ya Ultrasound iliyoibwa hospitalini hapo.

Jafo ametoa kauli hiyo jana Alhamisi Agosti 15, kauli ambayo inamuunga mkono Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini ya kutaka watumishi hao wasilipishwe fedha kama walioamriwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga  Jumatano Agosti 14.

Pamoja na mambo mengine, Jafo amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka kuunda tume ya uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na wizi wa mashine hiyo.

“Kulikuwa na maelekezo kuwa wale watumishi 137 walipie ile mashine kwa kukatwa kwenye mshahara yao, nielekeze kwamba watumishi wetu hawa wanafanya kazi katika mazingira magumu sana, na tukumbuke hata tulipopata janga pale Morogoro watumishi wetu wa idara ya afya muda mwingi ndiyo walikuwa kimbilio kuwasaidia wananchi.

“Kitendo kama hiki ni kuwakatisha tamaa na kuwaweka katika ya sintofahamu lakini kumbe inawezekana kuna watu walihusika. Lengo hapa ni kuwatafuta waliohusika, wabainishwe ni kina nani wachukuliwe hatua lakini pia wahakikishe mashine hii inarudi.

“Kwa hiyo nitoe maelekezo kuwa watumishi hawa wasichangishwe fedha ya aina yoyote kwa sababu siyo jukumu lao, ni jukumu la ulinzi kwa hiyo Mkuu wa Mkoa namuelekeza kwanza aunde tume ya uchunguzi kuwabaini wahusika na watumishi hao waachwe wafanye kazi kwa sababu tunawategemea sana haipaswi kuwabebesha mzigo usiowahusu,” amesema Jafo.

Mashine hiyo inadaiwa kuibiwa pamoja na kifaa chake cha kudurufu picha (printer) ambapo ilikua maalumu kwa matumizi ya wodi mpya ya akina Mama wajawazito na iliibiwa ikiwa katika wodi hiyo.


Share:

TPA YAKABIDHI MASHINE MBILI KWA AJILI YA KUHIFADHI WATOTO NJITI KWENYE HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO ZENYE THAMANI YA MILIONI 25

 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Witonde Philipo kulia akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto  mashine mbili za incubator kwa ajili ya kusaidia kuhifadhi watoto njiti zenye thamani ya Sh milioni 25 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga anayeshuhudia katikati ni Meneja wa Bandari ya Tanga Ajuaye Msese
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Witonde Philipo kulia akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto  mashine mbili za incubator kwa ajili ya kusaidia kuhifadhi watoto njiti zenye thamani ya Sh milioni 25 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga anayeshuhudia katikati ni Meneja wa Bandari ya Tanga Ajuaye Msese
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa  mashine mbili za incubator kwa ajili ya kusaidia kuhifadhi watoto njiti zenye thamani ya Sh milioni 25 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga vilivyotolewa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Witonde Philipo akifuatiwa na  Meneja wa Bandari ya Tanga Ajuaye Msese kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Abdiely Makange
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Witonde Philipo akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto ni Meneja wa Bandari ya Tanga Ajuaye Msese 
 Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Abdiely Makange akizungumza wakati wa hafla hiyo
 Meneja wa Bandari ya Tanga Ajuaye Msese akizungumza wakati wa halfa hiyo
 PRO wa Bandari ya Tanga Moni Jarufu akizungumza jambo wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano
 Sehemu ya msaada wa vifaa vilivyokabidhiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa ajili ya kuhifadhi watoto njiti zenye thamani ya Sh milioni 25 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Ta
 kuhifadhi watoto njiti zenye thamani ya Sh milioni 25 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Ta
 Sehemu ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakiwa kwenye halfa hiyo
  Sehemu ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakiwa kwenye halfa hiyo
  Sehemu ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakiwa kwenye halfa hiyo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati akisisitiza jambo kwa Meneja wa Bandari ya Tanga  Ajuaye Msese wakati alipowasili kwenye hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo kwa ajili ya kupokea msaada mashine mbili za incubator kwaajili ya kusaidia kuhifadhi watoto njiti zenye thamani ya Sh milioni 25 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga. uliotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Witonde Philipo



MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa mashine mbili za incubator kwaajili ya kusaidia kuhifadhi watoto njiti zenye thamani ya Sh milioni 25 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga.

Akikabidhi msaada huo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Witonde Philipo amesema kuwa mamlaka hiyo ilikuwa imetenga bajeti ya Sh milioni 50 kwa ajili ya kusaidia jamii katika sekta ya elimu na afya.

Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Mhandisi Witonde alisema kwamba wao wanashukuru kupewa nafasi ya kujumuika kwenye mkoa wa Tanga kusaidia kuboresha maisha ya wakazi wa mkoa huo.

Alisema kwamba walipata maombi ya kuwepo kwa changamoto hizo na wao wakaona wafanye jambo hilo hivyo wanaimani uongozi wa mkoa huu ungeweza kupata watu wengine lakini wakawaona wao.

Mhandisi Witonde alisema kwamba mamlaka hiyo imekuwa na utaratibu kila mwaka kutenga bajeti kwa ajili ya kusaidia jamii kwenye ameneo ya afya, elimu na maeneo mengine ya kijamii.

Alisema katika mwaka wa fedha walipanga kutumia kiasi cha milioni 50 kutoa huduma hizo huku akieleza kwamba vifaa hivyo vitasaidia kuokoa maisha ya watoto.

“Kabla ya zoezi hili siku chache tulikwisha kukabidhi mabati 378 shule ya sekondari Tanga School yenye thamani ya milioni 15 na yamekarabati nyumba tano lakini pia tutaendelea kuona namna ya kuwasaidia kwa kadiri mungu atakavyowajalia”Alisema 

Awali akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella aliwashukuru TPA kwa kutenga fedha hizo milioni 50 kwenye mwaka wa fedha na kuwezesha kwenye katika mkoa wetu kuleta vifaa hvyo ambavyo vitakuwa ni chachu kuwasaidia kuboresha sekta ya afya.

Alisema kwani kutenga fedha ni jambo moja na kufanikisha ni jambo la pili hivyo niwapongeze TPA kwa kutekeleza wale walioyapanga na kuhaidi

“Nimshukuru MKurugenzi Mkuu wa TPA kwani Tanga imekuwa ni nyumbani kwenu kuja mara kwa mara na kuweza kuwasaidia tunatambua jitihada kubwa mnazofanya katika kuhakikisha mnasaidia jamii na watanzania kwa ujumla”Alisema

Alisema wanatambua jitihada kubwa mnazofanya TPA kuhakikisha mnasaidia jamii na watanzania kwa ujumla ukiacha suala la kusimamia mapato na kujenga mazingira mazuri ya kuwa lango kuu la kibiashara kati ya nchi yetu na jirahi bandari imekuwa ni msaada kuwasaidia shughuli mbalimbali za kijamii na maelezo yako ulioyayatoa yanadhihiridha

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa huo, Abdiel Makange, amesema mashine hizo zitaweza kusaidia kuokoa maisha ya watoto njiti ambao wanazaliwa katika hospitali hiyo.

“Hospitali ilikuwa ina mashine mbili tayari, hivyo uwepo wa nyingine za ziada kutawezesha kupunguza changamoto ya vifo kwa watoto hao” amesema.

Mwisho.
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa 16 August

























Share:

Thursday, 15 August 2019

Okoa Ndoa Yako Na Afya Yako Sasa Kwa Kutumia Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume Na Kisukari

Ni dawa zilizopimwa na mkemia na kupewa no 341/VOL,XV/36 na TFDA no 0127/F/F/1819/ MTINJETINJE ni dawa ya kisukari .....Hurudisha kongosho katika hali ya kawaidi hata kama limefeli haijalishi unatumia vidonge au sindano za insulin, itaifanya sukari kuwa normal

SUPER MAJINJA ni dawa inayotibu nguvu za kiume yani matatizo yafatayo (1) kushindwa kurudia tendo na mwili kuchoka (2)kuwai kufika kabla ya  mwenzi wako (3)maumbile ya kiume kulegea na kusinyaa (4)maumbile ya kiume  kuingia ndani na kuwa mafupi kwa wale walio jichua (5)miuungurumo ya tumbo,ngiri,kukosa choo,kiuno kuuma

ACHA KUONGOPEWA SASA DAWA HIZI NI TOFAUTI NA ULIZOWAI KUTUMIA

NJOO OFISINI KWANGU MBAGALA KARIBU NA BENK YA KCB NA mwanza yupo wakala piga simu ya DR AGU whatsapp 0783185060. 0620113431


Share:

Je, Wewe ni Mwathirika wa Kujichua?... Soma Hapa

🔖Asilimia 45-80 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kutowatimizia vyema wake au wapenz wao na kuwasababishia kutoka nje ya mahusiano yao.
------------------
🔖NINI CHANZO CHA HAYO?

📌Kupiga punyeto
,Ngiri,

Vidonda vya tumbo,

📌Korodani moja kuvimba,

📌 Msongo wa mawazo,

📌Presha, Magonjwa ya zinaa,

 ðŸ“ŒKufanyiwa tohara
ukiwa na umri mkubwa,

📌Kisukari.
------------------

💉DR. KHAFIZ Sasa anakuletea tiba sahihi ya tatizo la Nguvu za kiume.na maumbile mafupi
-------------------

💊MUJARABU :Hii hutibu na kuponya kabisa tatizo la Nguvu za kiume, utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka 
------------------
📌inazalisha homoni kwa mwingi na kuku fanya uwe nambegu nyingi zenye vimeleo vyauzazi vilivo koma
------------------
📌 itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20-45. Dawa hii imechanganywa na miti 18,Hata wazee wenye umri mkubwa wa zaidi ya miaka 85 wanapona kabisa okoa mahusiano yako, ndoa yako sasa.
------------------
📌TIBA YA KUDUMU

 -----------------
📌TUMIALEO UWONE MAJABU YAKE

------------------
🌠Pia tunadawa za Kupandisha nyota , Uzazi, Pumu, Malaria sugu, miguu kuwaka moto, Kaswende, Kisonono  na mvuto wa mpenzi.bishara na zindiko
--------------------
 ðŸ’‰DR.KHAFIZ ANAPATIKANA DAR-ES-SALAM SM 0716948950 kwa wale wa mikoani mingine huduma hii utaipata popote ulipo.


Share:

Nafasi za Kazi REDESO – Jobs at Staff at Relief to Development Society (REDESO)

Position: Programme Coordinator Location: Kigoma Reports to: Deputy Chief Executive Officer JOB SUMMARY The incumbent shall be responsible for providing assistance to DCEO on day to day business at field level and monitor the implementation of activities at field office.. Roles and responsibilities among others will be as follows; • Oversee operations team and program to ensure that… Read More »

The post Nafasi za Kazi REDESO – Jobs at Staff at Relief to Development Society (REDESO) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Nafasi za Kazi NMB Head; Centralized Operations – NMB bank vacancies 2019

nafasi za kazi nmb 2019, nafasi za kazi nmb july 2019, nafasi za kazi bank 2019, nmb bank vacancies 2019   Job Purpose Provide leadership and direction to Centralized Operations teams and be responsible for the development and maintenance of the Bank’s operations ensuring that it continually acquires and maintains a profitable business with minimum risk. Main Responsibilities… Read More »

The post Nafasi za Kazi NMB Head; Centralized Operations – NMB bank vacancies 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Yaliyojiri wakati Rais Magufuli na Rais Ramaphosa walipozungumza na wananchi wa Tanzania na Afrika Kusini kupitia vyombo vya habari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuomba Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Matamela Cyril Ramaphosa kuwahamasisha zaidi wafanyabiashara wa Afrika Kusini kuja kuwekeza hapa nchini kwa kuwa Tanzania inayo dhamira ya dhati ya kuongeza ushirikiano wake na nchi hiyo katika nyanja mbalimbali za kiuchumi.

Rais Magufuli amesema katika kutekeleza mipango yake ya maendeleo na dira ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 Tanzania inawakaribisha wawekezaji mbalimbali, kwa kuwa Afrika Kusini imepiga hatua kubwa katika viwanda amewaalika wafanyabiashara wa nchi hiyo kuja kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali zikiwemo dawa na vifaa tiba, kuchakata madini na kwamba Serikali itatoa ushirikiano wowote utakaohitajika.

Rais Magufuli pia amemuomba Rais Ramaphosa kuongeza ushirikiano na Tanzania katika utalii, hasa ikizingatiwa nchi hiyo inapokea watalii zaidi ya Milioni 10 kwa mwaka ikilinganishwa na Watalii Milioni 1.5 wanaoingia hapa nchini, na katika hilo ametoa wito kwa Afrika Kusini kuongeza safari za treni ya watalii na kwa wawekezaji wake kuja kuwekeza katika hoteli na fukwe za Tanzania.

Amempongeza Rais Ramaphosa kwa kuja na wafanyabiashara ambao wanajadiliana na wafanyabiashara wa Tanzania juu ya kushirikiana kibiashara, na amemhakikishia kuwa Tanzania itakuwa tayari kuhakikisha ushirikiano huo unafanikiwa.

“Sisi Tanzania tumeamua kuwa tunanunua bidhaa zetu Afrika Kusini badala ya kununua bidhaa hizo huko mbali, na kwa kuanzia pikipiki za kuongozea misafara ya viongozi tutakazotumia wakati huu wa Mkutano wa 39 wa SADC tumenunua Afrika Kusini” Rais Magufuli.

Kwa upande wake Rais Ramaphosa amemshukuru Rais Magufuli kwa kumwalika kufanya ziara ya Kitaifa hapa nchini na amemhakikishia kuwa wananchi Afrika Kusini wanaiona Tanzania ni nyumbani kwao na hivyo Serikali yake ipo tayari kuuendeleza na kuukuza uhusiano mzuri kati yake na Tanzania.

Rais Ramaphosa ameelezea kufurahishwa kwake na kuwepo kwa kampuni 228 za Afrika Kusini zilizowekeza nchini Tanzania na kuajiri wa zaidi ya watu 21,000 na ameahidi kwenda kuwahimiza zaidi wafanyabiashara na wawekezaji wa Afrika Kusini kuja kuwekeza nchini Tanzania huku akiwakaribisha wawekezaji wa Tanzania kwenda kuwekeza Afrika Kusini.

Aidha, Rais Ramaphosa amesema Afrika Kusini ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika nyanja nyingine mbalimbali zikiwemo afya, ulinzi na usalama, utalii na amekubaliana na mapendekezo ya Tanzania juu ya mpango wa kufundisha lugha ya Kiswahili nchini Afrika Kusini hasa wakati huu ambapo SADC inatarajia kuifanya kuwa lugha rasmi ya 4.

==Taarifa ya Ikulu


Share:

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH .....Anauwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani Mtabibu wa Nyota za Binadamu  Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Mohamed Buruani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO . Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie ..Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Mohamed Buruhan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN, Anatafsiri Ndoto. ,KUSAFISHA NYOTA, Mvuto wa Mwili na BIASHARA, ...MIGUU Kufa GANZI na mengi zaidi (+255  715971688 au (+255  756914036

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...


Share:

Rais Magufuli: Tutazidi Kufungua Milango Ya Biashara Na Uwekezaji Na Jamhuri Ya Afrika Kusini

Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
RAIS Dkt. John Magufuli amesema Tanzania itazidi kufungua milango ya ushirikiano na Jamhuri ya Afrika Kusini na kuwataka Wafanyabiashara na Wawekezaji wa nchi hizo kutumia fursa za vivutio mbalimbali vilivyopo ili kukuza uchumi kwa manufaa ya wananchi wa Mataifa hayo.

Akizungumza leo Alhamisi (Agosti 15, 2019) Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati wa mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, Rais Magufuli alisema Tanzania na Afrika Kusini ni mataifa rafiki yenye historia ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

Aliongeza kuwa Jamhuri ya Afrika Kusini ni miongoni mwa Mataifa yaliyopiga hatua kubwa za maendeleo ya kiuchumi katika Bara la Afrika, hivyo Tanzania itatumia fursa hiyo na mshirika wa karibu kwa ajili ya kupanua wigo wa sekta za kibiashara ikiwemo ununuzi na uuzaji wa bidhaa na mazao mbalimbali.

“Katika Nchi za SADC, mwaka 2018 Tanzania imeongoza katika ukanda wa SADC kwa thamani ya mauzo ya bidhaa zake Nchi ya Afrika Kusini iliyofikia thamani Dola Milioni 742.02, na biashara baina ya Mataifa haya ilifikia thamani ya Dola Bilioni 1.18 kutoka Dola Bilioni 1.11 mwaka 2017” alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alitoa wito kwa Wafanyabiashara na wawekezaji wa Afrika Kusni kuja kwa wingi nchini kwa ajili ya kuwekeza na kufanya biashara kwa kuwa Serikali imeendelea kuimarisha na kuweka mazingira wezeshi ikiwemo ujenzi wa miundombionu ya uhakika, pamoja na uimarishaji wa mifumo ya kitaasisi katika usimamizi wa kodi na biashara.

Akifafanua zaidi Rais Magufuli alisema Tanzania imejipanga kikamilifu katika kuimarisha mfumo imara wa uchumi wake ikiwemo kupitia ujenzi wa viwanda, ambayo ndiyo Dira na dhamira ya Serikali ya Awamu ya  Tanzania katika kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, hivyo aliwataka wawekezaji wa Afrika Kusini kuja nchini na kujenga viwand.

“Katika Bajeti ya Serikali kwa mwaka tunatenga kiasi cha Tsh Bilioni 270 kwa ajili ya ununuzi wa madawa nje ya nchi, tunawaomba wawekezaji wa Afrika Kusini waje Tanzania wajenge viwanda vya madawa kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tumepunguza gharama kubwa za uagizaji wa madawa kutoka nchi ya nchi” alisema Rais Magufuli.

Akifafanua zaidi Rais Magufuli alisema Serikali imekusudia miundombinu ya usafiri wa reli Tazara ili kuweza kutumika na Wafanyabiashara wa Afrika Kusini kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa mbalimbali pamoja na kutangaza fursa za vivutio vya utalii na fukwe za bahari zenye urefu wa takribani Kilometa 1400 zilizopo nchini.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli alisema Tanzania ipo tayari kufanya biashara na Jamhuri ya Afrika Kusini ikiwemo ununuzi wa vifaa mbalimbali ikiwemo magari, ambayo Tanzania imekuwa ikiyanunua katika nchi za mbali, huku akitolea mfano wa pikipiki zinazotumika katika Mkutano wa 39 wa SADC zimenunuliwa kutoka nchini Afrika Kusini.

Kwa upande wake Rais Cyril Ramaphosa alisema ziara yake nchini Tanzania ni kielelezo cha kuendelea kuimarika kwa ushirikiano baina ya Mataifa hayo na kusema Serikali yake itaweka mazingira wezeshi kwa Wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania kwenda nchini Afrika Kusini kufanya biashara na kutafuta fursa ya maeneo ya uwekezaji na biashara.

Aliongeza kuwa Serikali yake inatambua umuhimu wa sekta ya biashara na uwekezaji katika kukuza uchumi katika Nchi za SADC kupitia ajenda ya Maendeleo Endelevu ya jumuiya hiyo ya mwaka 2030 ambayo imedhamiria katika kujenga mazingira bora ya biashara katika Jumuiya hiyo.

MWISHO


Share:

Daktari FEKI Atiwa Mbaroni Mkoani Ruvuma

Polisi Mkoa wa Ruvuma linamshikilia Moses Lucas Masoud (34) mkazi wa Visiga mkoani Pwani  kwa tuhuma ya kujifanya daktari bingwa wa kutibu  magonjwa  mbalimbali ya binadamu.

Inadaiwa daktari huyo feki alikuwa akitoa huduma za kitabibu katika Kanisa la Jesus Miracle Church (JMC) lililopo maeneo ya Msamala kwa Gasa katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ambapo wananchi walimbaini na kutoa taarifa kwa Mganga Mkuu wa mkoa huo, Dk Jair  Khanga.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumatano Agosti 14, 2019 Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa alisema daktari huyo feki alikamatwa Agosti 13,2019 saa saba mchana katika maeneo ya Msamara kwa Gasa akiendelea na kutoa huduma za kitabibu kwa binadamu.

Alisema kabla ya kuanza kutoa huduma hiyo ya kitabibu aliingia kwenye kanisa hilo na kujitambulisha yeye ni daktari bingwa ana uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu na pia alijitambulisha yeye ni daktari anayetibu viongozi wakubwa wa Serikali ya Tanzania.

Kamanda Maigwa alidai daktari huyo feki  amekuwa akitoa huduma hiyo ya kitatibu kwa gharama kati ya Sh600,000 hadi Sh1.2 milioni kuligana na homa ya mteja wake, kitu ambacho kiliwashtua wananchi na kuanza kumtilia shaka kutokana na gharama ya matibabu ambayo anatoza kwa mgonjwa.

Alisema Polisi akishirikiana na Dk Khanga baada ya kupata taarifa  hiyo walikwenda kwenye kanisa hilo na kumkuta akiendelea kutoa huduma na alipohojiwa alikiri hana taaluma ya udaktari na hajahitimu mafunzo yoyote ya udaktari katika chuo chochote cha udaktari kinachotambulika na Serikali.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger