Thursday, 15 August 2019
Wednesday, 14 August 2019
Jamii Yatakiwa Kuwatambua, Kuwatumia Wasaidizi Wa Kisheria Kupata Msaada Wa Kisheria
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Msajili wa Watoa Huduma ya Msaada wa Kisheria Tanzania, Bi. Felistas Joseph kutoka Wizara ya Katiba na Sheria ametoa wito kwa jamii kuwatambua na kuwatumia wasaidizi wa kisheria pindi wanapohitaji msaada katika masuala ya kawaida ya kisheria, ikiwemo migogoro ya ardhi, migogoro ya ndoa, utelekezaji wa familia na masuala mengine wanayokutana nayo siku kwa siku, ambao amesema wanatoa huduma hizo bila malipo yoyote.
Bi Felistas ameyasema hayo jana katika kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu wa Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi.
Amesema kada hii inatambuliwa kwa mujibu wa sheria ya msaada wa kisheria na wamefundishwa mafunzo ya awali ya sheria katika masuala ambayo wananchi wanakutana nayo siku kwa siku hivyo ni vema jamii na wadau wengine wakawatambua na kuwapokea kwa kuwa ni watu waliojitoa kuisaidia jamii bila malipo yoyote.
“Nia yetu ni kwamba jamii iweze kuwafahamu na kuwapokea wasaidizi wa kisheria, hawa ni watu wanaojitolea kwa dhati kufanya hii kazi bila kudai malipo, wanachohitaji ni ushirikiano na wadau wengine wa Serikali pamoja na wananchi; kada hii inatambuliwa rasmi chini ya sheria ya msaada wa kisheria na wameshapewa vigezo na mipaka ya kufanyia kazi” alisema.
Ameongeza kuwa Serikali imeandaa mtaala wa kufundisha wasaidizi wa huduma za kisheria na hadi sasa takribani wasaidizi wa kisheria 4500 wamefundishwa katika kipindi cha miaka mitatu nyuma ambao wamejiunga katika vikundi na kujisajili kama mashirika ambapo hadi sasa kuna jumla ya mashirika 200.
Awali akifungua kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani Simiyu, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema endapo wasaidizi wa kisheria watutumiwa vizuri kero nyingi za wananchi zitatatuliwa na kufikia mwisho, huku kutoa wito kwa Wakuu wa wilaya, wabunge, madiwani na viongozi wengine kuwashirikisha wasaidizi wa kisheria katika mikutano ya hadhara ambapo wananchi huwasilisha kero zao.
Aidha, Mtaka amesema ili kuongeza uewelewa wa masuala ya msaada wa kisheria mkoani Simiyu ni vema Wizara ya Katiba na Sheria ikaona haja ya kuendela kutoa elimu kwa jamii, ambapo amewaalika kutoa elimu hiyo katika kambi za kitaaluma mkoani hapa ambazo zinatarajia kuanza mwezi Septemba, 2019 kwa kidato cha nne..
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini amesema viongozi wa Mkoa watahakikisha kamati za uratibu wa huduma za kisheria ngazi ya wilaya zinaundwa na wasaidizi wa kisheria wanatumiwa ipasavyo.
Naye Sheikh wa Mkoa wa Simiyu, Mahamoud Kalokola amesema viongozi wa madhehebu ya dini wataendelea kutoa elimu kupitia makusanyiko ya ibada kwa waumini wao ili wananchi hususani wale ambao hawana na uwezo wa kifedha wa kuwalipa mawakili wajue kuwa wasaidizi wa kisheria wapo katika jamii na wanaweza kuwasaida kutatua changamoto zao.
Kamati ya Uratibu wa Shughuli za Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Simiyu imeundwa na kuzinduliwa chini ya Katibu Tawala wa Mkoa ambaye ni Mwenyekiti, Msajili msaidizi(Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa), mtaalamu wa ardhi, jeshi la polisi (dawati la jinsia) Magereza, TAKUKURU, Mahakama, Mwanasheria, Afisa wa dawati la malalamiko, viongozi wa dini na Afisa ustawi wa jamii na Afisa habari ngazi.
Wajumbe wengine ni mwakilishi wa vyombo vya habari, wawakilishi wa wadau wa maendeleo, wawakilishi wa taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria,Mwenyekiti wa baraza la ardhi na mwakilishi kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), ambapo kwa muundo huu huu kamati za wilaya zitaundwa ziweze kutekeleza jukumu la uratibu wa shughuli za huduma za kisheria wilayani
MWISHO
Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo
SUPER MORISIS; nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-85) Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wala kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 18-45
SUNUPER; Hurefusha na kunenepesha maumbire madogo ya uume uliosinyaa , matatizo haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguruma na kujaa gesi hatimae kinyesi kuwa km cha mbuzi, ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,
Pia nidawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno
ONDOA MATATIZOYAKO YOTE ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe) kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota, kuzuia majini wachafu, pete ya bahati, kurudisha mali iliyopotea au kuibiwa
Kwahuduma na msaada wasiliana na DR. GALIMBO 0759208637 / 0620510598
Tiba Halisi ya Tatizo la Nguvu za Kiume
√Ni dawa bora ya mitishamba yenye kuimarisha, kurefusha na kukufanya uwe imara hata kama umelala pia huimarisha na kukuza maumbile yaliyosinyaa na kuwa regevu
*📌SUPER GAFINA MIX*/
Ni dawabora ya nguvu za kiume yenye mchanganyiko wa miti shamba 10 yenye maajabu yafuatayo:/
🔖(1)Inatibu upungufu wa nguvu za kiume mara dufu na kuimarisha misuri ya uume ulio legea na kusinyaa wakati wa tendo la ndoa/
🔖(2)Kuongeza hamu ya tendo kukufanya uweze kurudia tendo hadi mara tatu bila kuchoka
🔖(3)Itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15-30 kwa tendo la Kwanza na utakuwa na uwezo wa Kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3-4 bila hamu kuisha na inatibu kabisa/
.
*MATATIZO HAYA HUSABABISHWA NA*/
🔖(1)Tumbo kujaa gesi, na kuunguruma chini ya kitovu/
🔖(2) Choo kuwa kama Cha mbuzi/
🔖(3)Ngiri/
🔖(4)Kama umejichua sana punyeto/
🔖(5)Kisukari/
🔖(6)Presha ya kupanda na kushuka/
🔖(7)Vidonda vya tumbo,/
Bado hujachelewa
Pia tuna tibu KISUKARI,PRESHA,VIDONDA VYA TUMBO N.K/
._______________________
ANAPATIKANA DAR ES SALAAM AU UNAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO SIMU NO:/
*📞0752723508*
RITA Majina ya waombaji waliohakikiwa kikamilifu – list of verified Students for HESLB 2019/2020
Majina ya waombaji waliohakikiwa kikamilifu RITA : The list of verified Students, who are applying for HESLB Loans 2019/20 – RITA Majina ya wanafunzi waliohakikiwa kikamilifu heslb 2019/2020, uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa rita 2019 – majibu ya uhakiki rita, majina ya uhakiki rita, majina yenye mapungufu rita, rita kuhakiki vyeti vya kuzaliwa, uhakiki wa vyeti rita 2019… Read More »
The post RITA Majina ya waombaji waliohakikiwa kikamilifu – list of verified Students for HESLB 2019/2020 appeared first on Udahiliportal.com.
#Kimataifa: Kiongozi Mkuu wa Iran akutana na waasi wa Houthi
Televisheni ya taifa ya Iran imeripoti kuwa kiongozi mkuu wa kidini nchini humo ametoa wito wa kuungwa mkono kwa waasi wa Houthi wa nchini Yemen dhidi ya muungano wa kijeshi unaongozwa na Saudi Arabia ambao amesema unalenga kuitenganisha nchi hiyo.
Ayatollah Ali Khamenei ametoa matamshi hayo wakati alipokutana hapo jana mjini Tehran na Mohamed Abdul Salam ambaye ni msemaji wa waasi wa Houthi.
Khamenei amesema Saudi Arabia, Muungano wa Falme za kiarabu na wale wanaowaunga mkono wanalenga kuiharibu Yemen ambayo ametaka isimame imara dhidi ya njama hizo.
Muungano wa kijeshi unaongozwa na Saudi Arabia ambao unajumuisha pia Falme za Kiarabu umekuwa ukipambana na waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran katika eneo la Kaskazini ya Yemen tangu Machi 2015 ili kuilinda serikali ya rais Abdo Rabbo Mansur Hadi.
#Kimataifa: Korea Kaskazini yaonya dhidi ya kupelekwa mifumo ya makombora Korea Kusini
Korea Kaskazini imesema leo kuwa jaribio lolote la Marekani la kupeleka mifumo ya makombora ya masafa ya kati nchini Korea Kusini litazusha zama mpya za vita baridi na kuzidisha mashindano ya kuunda silaha kwenye rasi ya Korea.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Mark Esper alisema mapema mwezi huu kuwa anaunga mkono kupelekea mifumo ya makombora ya masafa ya kati barani Asia, sikummoja baada ya Marekani kujitoa kutoka mkataba na Urusi wa kuzuia uundaji makombora ya nyuklia.
Korea Kaskazini imesema mpango huo wa Marekani unalenga kutanua nguvu zake kwenye eneo la Kaskazini Mashariki ya Asia na siyo kutoa ulinzi kwa Korea Kusini dhidi ya kitisho kutoka mataifa hasimu.
Korea Kusini kwa upande wake imesema hakujafanyika mazungumzo yoyote ya kuweka mifumo ya makombora ya Marekani nchini humo na hadi sasa hakuna mipango ya kufanya hivyo.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Mark Esper alisema mapema mwezi huu kuwa anaunga mkono kupelekea mifumo ya makombora ya masafa ya kati barani Asia, sikummoja baada ya Marekani kujitoa kutoka mkataba na Urusi wa kuzuia uundaji makombora ya nyuklia.
Korea Kaskazini imesema mpango huo wa Marekani unalenga kutanua nguvu zake kwenye eneo la Kaskazini Mashariki ya Asia na siyo kutoa ulinzi kwa Korea Kusini dhidi ya kitisho kutoka mataifa hasimu.
Korea Kusini kwa upande wake imesema hakujafanyika mazungumzo yoyote ya kuweka mifumo ya makombora ya Marekani nchini humo na hadi sasa hakuna mipango ya kufanya hivyo.
RUFAA YA MRAKIBU WA POLISI (SP) CHRISTOPHER BAGENI KUPINGA HUKUMU YA KUNYONGWA YATUPILIWA MBALI

Mahakama ya Rufani imetupilia mbali ombi la kuangaliwa upya hukumu ya kunyongwa, aliyohukumiwa Christopher Bageni, ambaye alifungua shauri hilo kutaka afutiwe adhabu hiyo, kwa kosa la mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini mkoani Morogoro.
Uamuzi wa kutupilia mbali maombi hayo ya Bageni ulioandaliwa na jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo waliosikiliza maombi hayo, umetolewa leo Jumatano, Agosti 14, 2019 na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani, Elizabeth Mkwizu.
Jopo la majaji hao waliosikiliza na kutoa uamuzi wa maombi hayo namba 63 ya mwaka 2016 ni Stella Mugasha (kiongozi), Ferdinarnd Wambali na Rehema Kerefu.
Kwa uamuzi huo ambao ndio wa mwisho, sasa Bageni hana namna nyingine ya kufanya kwani hakuna ngazi nyingine ya mahakama nchini wala hatua nyingine ambayo anaweza kuichukua kuupinga.
Kwa sasa atasubiri tu utekelezaji wake huku akiombea neema ya rais wa awamu ya sasa au awamu zijazo kumsamehe ama kumwachia huru au kumbadilishia adhabu pengine kuwa ya kifungo kwa mamlaka yake kikatiba kama ataguswa au kuona kuna sababu ya kufanya hivyo.
Picha : WFT YAKUTANA NA WADAU KUJADILI MBINU ZA KUKOMESHA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO SHINYANGA
Mratibu wa Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa haki za wanawake na watoto leo. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT) linalohusika na utetezi wa haki za wanawake,watoto na ujenzi wa tapo ya wanawake nchini Tanzania limekutana na wadau wa haki za wanawake na watoto halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili kujadili namna ya kutekeleza Mradi wa Kuwezesha Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkutano huo umefanyika leo Jumatano Agosti 14,2019 katika ukumbi wa Karena Hoteli na kukutanisha pamoja maafisa wa serikali ngazi ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na mkoa,viongozi wa dini,waandishi wa habari,wawakilishi wa baraza la watoto, na asasi za kiraia zinajishughulisha na utetezi wa haki za wanawake na watoto.
Mratibu wa Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia alisema lengo la mkutano huo ni kuwafahamisha wadau wa utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kuhusu mradi huo.
"Tumekutana hapa ili kuwafahamisha hatua tuliyofikia katika utekelezaji wa mradi huu ili tuweze kuunganisha jitihada za kuondoa ukatili kwa wanawake na watoto lakini pia kubaini na kujadili changamoto ambazo wadau wanakutana nazo katika utekelezaji wa MTAKUWWA",alisema Mbia.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa MTAKUWWA katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa kipindi cha Mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu,Afisa Ustawi wa Jamii wa halmashauri hiyo,Elizabeth Mweyo alisema tayari wameunda kamati za MTAKUWWA katika kata zote 26 na vijiji vyote 126 kati ya hizo kamati tano za ngazi ya kata zimejengewa uwezo.
Alisema kupitia vikundi hivyo wameendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya mila na desturi zinazochangia kuwepo kwa ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na kuhamasisha wananchi kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli za vikundi.
Nao wadau walioshiriki walizitaja baadhi ya changamoto zinazosababisha kuendelea kuwepo kwa vitendo vya ukatili katika jamii kuwa ni wananchi kutokuwa tayari kutoa ushahidi mahakamani kuhusu matukio ya ukatili huku wakiwanyooshea vidole baadhi ya Madaktari wasio waaminifu ambao wamekuwa hawatoi ushirikiano kwa kutofika mahakamani kutoa ushahidi mahakamani kuhusu matukio ya ukatili wanayopokea.
ANGALIA PICHA WAKATI WA MKUTANO
Mratibu wa Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akielezea lengo la mkutano wa wadau wa haki za wanawake na watoto uliofanyika leo katika ukumbi wa Karena Hoteli Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mratibu wa Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa Ustawi wa Jamii wa halmashauri ya Shinyanga ,Elizabeth Mweyo akizungumza katika mkutano wa wadau wa haki za wanawake na watoto.
Mkuu wa Progamu kutoka Women Fund Tanzania, Carol Francis Mango akiwasilisha mada kuhusu Mradi wa Kuwezesha Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa Progamu kutoka Women Fund Tanzania, Carol Francis Mango akiwasilisha mada kuhusu Mradi wa Kuwezesha Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini.
Mwakilishi wa BAKWATA Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Hemed Rashid akichangia hoja wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa Baraza la watoto kijiji cha Singita kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Stevi Peter Kienze akiomba taarifa za matukio ya ukatili zinapotolewa zifanyiwe kasi haraka ili kukomesha vitendo hivyo katika jamii.
Afisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga ,Lydia Kwesigabo akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGAPE ACP, John Myola akizungumza katika mkutano huo wa wadau wa haki za wanawake na watoto.
Mkutano unaendelea.
Rehema Katabi kutoka shirika la PWWCO akichangia hoja wakati wa mkutano huo.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kutoka Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Shinyanga,Victoria Maro akizungumza kwenye mkutano huo.
Mdau kutoka shirika la TAI, Jonathan Kifunda akichangia hoja wakati wa mkutano huo.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mkutano unaendelea.
Wadau wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Okoa Ndoa Yako Na Afya Yako Sasa Kwa Kutumia Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume Na Kisukari
Ni dawa zilizopimwa na mkemia na kupewa no 341/VOL,XV/36 na TFDA no 0127/F/F/1819/ MTINJETINJE ni dawa ya kisukari .....Hurudisha kongosho katika hali ya kawaidi hata kama limefeli haijalishi unatumia vidonge au sindano za insulin, itaifanya sukari kuwa normal
SUPER MAJINJA ni dawa inayotibu nguvu za kiume yani matatizo yafatayo (1) kushindwa kurudia tendo na mwili kuchoka (2)kuwai kufika kabla ya mwenzi wako (3)maumbile ya kiume kulegea na kusinyaa (4)maumbile ya kiume kuingia ndani na kuwa mafupi kwa wale walio jichua (5)miuungurumo ya tumbo,ngiri,kukosa choo,kiuno kuuma
ACHA KUONGOPEWA SASA DAWA HIZI NI TOFAUTI NA ULIZOWAI KUTUMIA
NJOO OFISINI KWANGU MBAGALA KARIBU NA BENK YA KCB NA mwanza yupo wakala piga simu ya DR AGU whatsapp 0783185060. 0620113431
Waziri Mkuu Azindua Mwongozo Wa Uwekezaji Kagera ....Azitaka Halmashauri Nchini Kuondoa Urasimu, Vikwazo Kwa Wawekezaji
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezindua Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Kagera wenye lengo la kutangaza fursa za Uwekezaji na hivyo, kukuza maendeleo ya mkoa huona ameziagiza halmashashauri zote za wilaya nchini ziondoe urasimu na kupunguza vikwazo kwa wawekezaji.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Agosti 14, 2019) wakati akizindua Kongamano la Wiki ya Kagera na Mwongozo wa Uwekezaji mkoani Kagera, lilifanyika Bukoba mjini.Amewataka Watanzania wahakikishe wanachangamkia fursa za biashara zilizopo.
Amesema Watanzania wanao uwezo wa kutumia fursa za uwekezaji na biashara zilizopo nchini kwa kushirikiana na taasisi za kifedha na kuwekeza katika miradi mbalimbali nchini, badala ya kuachia fursa hizo kuchukuliwa na wageni.
Amesema azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli ya kukuza uchumi kupitia sekta ya na kufikia wa kati ifikapo mwaka 2025 itaendelea kutekelezwa, hivyo, ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wa nje nao waje kuwekeza.
“Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda Awamu ya Tatu (2010/2020) na Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2015/2016 2020/2021) ambao lengo lake ni kuendeleza uchumi wa viwanda”.
Akizungumzia kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Uwekezaji Kagera, Waziri Mkuu amesema yamelenga kuwakutanisha wadau wa uwekezaji, ambao ni pamoja na Wafanyabiashara kutoka ndani ya mkoa na nchi jirani zinazozunguka Mkoa wa Kagera.
“Ni ukweli usiofichika kwamba tunahitaji wawekezaji watakaosaidia uchumi wa mkoa huu kukua kwa kasi kupitia fursa zilizopo kwenye nyanja za kilimo, mifugo, uvuvi, viwanda, maliasili na utalii”.
Waziri Mkuu amesema ukuaji mzuri wa uchumi wa mkoa utakuwa na manufaa katika kuongezeka kwa pato la mwananchi wa Kagera, pato la mkoa na hata pato la Taifa nalo litakuwa kwa kasi ndani ya kipindi cha muda mfupi.
Amesema mkoa wa Kagera ndiyo unaoongoza kwa uzalishaji wa kahawa nchini, ambapo zaidi ya nusu ya kahawa yote huzalishwa katika mkoa huo. Wastani wa uzalishaji wa kahawa kwa mwaka ni kati ya tani 50,000 hadi tani 65,000 kutegemea na hali ya hewa ya mwaka husika.
Hivyo, mkoa huo una fursa kubwa ya uwekezaji kwenye viwanda vya kukoboa na kusindika kahawa.Pia mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa michache Tanzania yenye fursa nyingi za uwekezaji ambazo kwa namna moja au nyingine hazipatikani katika mikoa mingine ya nchini. Miongoni mwa fursa hizo ni pamoja na soko kwani unapakana nan chi nne za Afrika Mashariki.
“Kagera imepakana na Uganda, Rwanda, Burundi na Kenya. Kupakana na nchi hizo zenye idadi kubwa ya watu katika ukanda huu wanaokadiriwa kufikia takriban milioni 190 ambapo kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2018 ni fursa ya uwepo wa soko kubwa la bidhaa zinazozalishwa au zinazoweza kuzalishwa katika mkoa wa Kagera”.
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ya usafiri ukiwemo wa anga na wa barabara ili kurahisisha usafiri kutoka Bukoba makao makuu ya mkoa wa Kagera kufika katika nchi hizo.
“Kwa mfano, umbali kutoka Bukoba hadi Kampala ni km. 340, Bujumbura km. 550 na Kigali km. 490. Kadhalika, itakuwa ni rahisi kufikia masoko ya nchi za Sudan Kusini pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC)”.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti alisema dhamira ya kuandaliwa kwa wiki ya uwekezaji mkoani Kagera ina lengo la kuhakikisha kwamba mkoa huo unafanya vizuri katika sekta ya uwezekezaji na biashara, hivyo kuchangia katika ukuaji wa pato la Taifa.
Alisema mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa 10 ambayo inamchango mdogo katika pato la Taifa, hivyo wanataka watoke kwenye kuchangia asilimia 3.9 hadi wafikie asilimia 10.
Kwa upande wao, viongozi mbalimbali wakiwemo Magavana kutoka na wafanyabiashara kutoka nchi za Rwanda na Burundi waliahidi kutumia fursa zilizopo nchini, pamoja na kuwakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania kwenda kuwekeza katika nchi zao.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, AGOSTI 14, 2019.




























