Saturday, 6 July 2019

Isikupite Hii! ๐Ÿ‘‰Naitwa Chief Karim Wa Sultan.....Ni Bingwa Na Mtabiri Wa Nyota

Isikupite hii! ๐Ÿ‘‰Naitwa CHIEF KARIM WA SULTAN Kutoka- TANGA - TANZANIA: Ni Bingwa, Mnajimu na Mtabiri wa Nyota na Matatizo yote ya ndoa/mahusiano.

Natabiri nyota yako, Kung'alisha nyota, Kufungua nyota zako za mafanikio zilizo fungwa  na kusababisha usifanikiwe katika maisha yako, au unajikuta unafanya kazi/biashara unapata hela lakini pesa yako haikai yaani inapita tu katika mikono yako.

Nawezesha  NYOTA, ni UTAJIRI usio na kafara yoyote na ni UTAJIRI unaoendana na nyota yako tu.

Hakika watu wengi wanazidi kufanikiwa na kutimiza ndoto zao , Kulipwa haraka haki zako unazodai, Mvuto wa mapenzi, kumrudisha mpenzi, mme au mke aliyekuacha/kukutelekeza.

 Je unapata wapenzi/wachumba lakini wanakuacha bila kujua sababu? Nitakusaidia!

Kufungua kizazi chako kilichofungwa na kusababisha usipate mimba/mtoto au unashika mimba zinatoka/kuharibika na maumivu makali ya tumbo/chango.

 ๐Ÿ‘‰KWA TATIZO LOLOTE  LA KINYOTA WASILIANA NAMI ๐Ÿ‘‰WhatsApp : 0763 103 527
au
๐Ÿ‘‰PIGA SIMU  : 0716 681 318
๐Ÿ‘‰ 0688 745 790


NB ๐Ÿ‘‰(KWA MWANAUME YOYOTE MWENYE TATIZO LA KUISHIWA AU KUPUNGUKIWA NGUVU ZA KIUME AU KAMA UMEATHIRIKA NA TATIZO LA KUPIGA PUNYETO TUWASILIANE POPOTE ULIPO)*{ู„َุง ูŠُุคَุงุฎِุฐُูƒُู…ُ ุงู„ู„َّู‡ُ ุจِุงู„ู„َّุบْูˆِ ูِูŠ ุฃูŠْู…َุงู†ِูƒُู…ْ ูˆَู„َٰูƒِู†ْ ูŠُุคَุงุฎِุฐُูƒُู…ْ ุจِู…َุง ุนَู‚َّุฏْุชُู…ُ ุงู„ْุฃَูŠْู…َุงู†َ ۖ ูَูƒَูَّุงุฑَุชُู‡ُ ุฅِุทْุนَุงู…ُ ุนَุดَุฑَุฉِู…َุณَุงูƒِูŠู†َ ู…ِู†ْ ุฃَูˆْุณَุทِ ู…َุง ุชُุทْุนِู…ُูˆู†َ ุฃَู‡ْู„ِูŠูƒُู…ْ ุฃَูˆْ ูƒِุณْูˆَุชُู‡ُู…ْ ุฃَูˆْ ุชَุญْุฑِูŠุฑُ ุฑَู‚َุจَุฉٍ ۖ ูَู…َู†ْ ู„َู…ْ ูŠَุฌِุฏْ ูَุตِูŠَุงู…ُ ุซَู„َุงุซَุฉِ ุฃَูŠَّุงู…ٍ ۚ ุฐَٰู„ِูƒَ ูƒَูَّุงุฑَุฉُ ุฃَูŠْู…َุงู†ِูƒُู…ْ ุฅِุฐَุง ุญَู„َูْุชُู…ْ ۚ ูˆَุงุญْูَุธُูˆุง ุฃَูŠْู…َุงู†َูƒُู…ْ ۚ ูƒَุฐَٰู„ِูƒَ ูŠُุจَูŠِّู†ُ ุงู„ู„َّู‡ُ ู„َูƒُู…ْ ุขูŠَุงุชِู‡ِ ู„َุนَู„َّูƒُู…ْ ุชَุดْูƒُุฑُูˆู†َ }* ﴿ูจูฉ﴾ ✨WABILLAHHI TAWFIQ ASALLAM  ALAIKUM✨ 


Share:

Makamba Atoa Neno Mradi wa Magari ya Umeme Tanzania

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesema ni lazima athari za usafiri wa magari ya umeme kwenye mazingira ziangaliwe kabla ya huduma hiyo kuanzishwa.

Makamba ametoa mwongozo huo kupitia ukurasa wake wa Twitter kufuatia taarifa ya TANAPA jana Julai 5, 2019 kwamba inajipanga kuleta usafiri wa magari ya umeme ili kurahisisha utalii.

Taarifa ya TANAPA ilieleza hivi, ''Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), inatarajia kuanzisha usafiri mpya wa kutumia magari ya umeme yanayopita kwenye nyaya (Cable Cars), kupeleka watalii Mlima Kilimanjaro''.

Leo Julai 6, 2019 Waziri Makamba amesema ''Inabidi watu wa Mazingira tupitishe na kutoa cheti kwanza kabla hawajaanza. Na tutafanya studies ili kujua impact kwa mazingira na uthabiti wa mitigation measures''.


Share:

Mali za Freeman Mbowe Zapigwa Mnada

Mnada wa kuuza Vifaa na samani mbalimbali vya Kampuni ya Mbowe Limited, inayomilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, umeonekana kufanikiwa kwa kiasi baada ya baadhi ya vifaa hivyo kununuliwa na kusalia vichache.

Mnada huo ulioendeshwa na Kampuni ya udalali ya Fosters Auctioneer & General Traders ya Dar Es Salaam, umefanyika leo Julai 6, 2019 chini ya dalali wa mahakama Joshua Mwaituka, kwenye ghala la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lililopo maeneo ya Bandari.

Akizungumza kuhusu mnada huo, Mwaituka amesema mwitikio wa wateja umekuwa ni mzuri na kwamba asilimia kubwa ya vifaa hivyo vimepata wateja,ambapo amevitaja vifaa vilivyonunuliwa ikiwa ni pamoja na taa, jukwaa, viti, kreti za bia, genereta,Mashine za kupozea na samani mbalimbali.

''Vitu vyote vimeuzwa kasoro makochi, na bei zake ni za kawaida na mwitikio wa watu ni mzuri wamefika tangu saa 2:00 asubuhi''

Kwa upande wake Meneja wa ukusanyaji Madeni kutoka NHC amesema mnada huo ni mwendelezo wa shirika hilo katika kudai deni la zaidi ya shilingi bilioni 1 na kwamba fedha zitakazopatikana kupitia mnada huo, zitaingizwa katika deni la kampuni hiyo na kiasi cha deni kitakachosalia wahusika watalipa kwa mujibu wa sheria.

Vifaa vilivyopigwa mnada vilikuwa vikitumika katika klabu ya Bilicanas,  vilichukuliwa na NHC Septemba mwaka 2016, baada ya mmiliki wake kushindwa kulipa deni la zaidi ya shilingi bilioni 1 alilokuwa anadaiwa kwa kutokulipa kodi kwa muda wa miaka 20.


Share:

Amber Rutty Afunguka Baada ya Video yake Chafu Kusambaa Jana

Binti aliyejipatia umarufu baada ya kuvuja kwa picha na video za utupu mitandaoni, Amber Rutty ameandika ujumbe mzito, na kuwachana wale wanaondelea kumfanya aonekane mbaya mitandaoni.

Amber rutty ameandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instagram, baada ya kuendelea kuzagaa kwa video zake za faragha mitandaoni.

"๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญHabar nasikitishwa sana na baadhi ya vitu vinavyofanywa na watu wanaotumia matumizi mabaya ya mitandao kwanjia ya kutaka nionekane mkosefu kila leo  ingawa pia najiskia vibaya kuona hata watu wanaotuzunguka nao kushindwa kuchunguza kiundani jambo hili  na kukumbuka swalazima lililowahi kutokea mpaka kupelekea mamlaka husika kutuchukulia hatua na tukajisalimisha kituoni tukasota sana segerea nampaka leo bado kesi ipo mahakaman kupitia hizo izo picha /video chafu wanazo zisambaza tena kwa mara nyingine tena  

sipo hapa kwa jili yakutaka kujua anaefanya ivi kusudio lake ni nini  kwasababu hata ukitazama mionekano yetu ya sasa nahizo video ukianza na mikono ya mmewangu davil mpaka vidolen ambapo amechora tattoos toka mwaka jana mwezi wa 12 napia atamimi ukijalibu kuniangalia the way nilivyo sasa na hzo video kuna utafauti mkubwa sana  

pengine furaha ya mtu anaefanya haya yote ni kuona ndoto zetu zinapotelea gizani  au kutaka kuona mmoja kati yetu kapoteza uhai  ukizingatia swala tayar lipo mahakaman toka October mwaka jana lakin bado leo hii wanayarudia kuyafufua hayo hayo, 

 kiukweli tumechanganyikiwa kiakili mpaka kiafya atupo sawa  ombiletu ni kuomba anaeusika na ili jambo tunaomba aache maramoja kuendelea kwasababu sisi ni binadamu maumivu /mateso tunayoyapitia kwakipindi hiki ni makubwa mno please please.๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ"

Tukio la kuvuja kwa picha hizo mitandaoni zikimuonyesha Amber Rutty na mpenzi wake zilivuja mwezi wa kumi, mwaka jana.

Na siku ya jana ilisambaa tena video nyingine mitandaoni kati ya Amber Rutty na mume wake.


Share:

SBL yafanya ‘hafla kuipongeza Taifa Stars’ baada ya kurejea kutoka AFCON

Dar es Salaam, Julai 06, 2019: Kampuni inayoongoza kwa uzalishaji wa bia nchini Tanzania, Serengeti Breweries Limited (SBL), imeandaa hafla ya chakula cha mchana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuipongeza Timu ya Taifa ya mpira wa miguu (Taifa Stars) baada ya kurejea kutoka nchini Misri ilipokwenda kushiriki kwenye fainali zinazoendelea za kombe la mataifa barani Afrika (AFCON 2019).

Licha ya kupoteza mechi zake tatu za hatua ya makundi na hivyo kushindwa kusonga mbele kwenye hatua zinazofuata za mashindano hayo, Taifa Stars inayodhaminiwa na SBL inastahili pongezi kwa kuweza kufuzu kushiriki fainali hizo za mashindano makubwa ya mpira wa miguu barani Afrika baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa takribani miongo minne.

Akiongea kwenye hafla hiyo ambayo imefanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Anitha Rwehumbiza amewashukuru wachezaji na viongozi wa Taifa Stars kwa kutimiza ndoto ya Tanzania kushiriki katika fainali za AFCON.

“Kitendo cha kuweza kufuzu kushiriki fainali za mashindano haya ni hatua moja kubwa mbele ikizingatiwa tumejaribu mara kadhaa bila kufanikiwa, hivyo basi kwa hatua ambayo tumeweza kufika, kila mmoja aliyeshiriki kuifikisha hapa timu anastahili pongezi”. Alisema Anitha huku akiongeza kuwa kiwango walichoonyesha Taifa Stars kilionekana ‘kuimarika zaidi’ licha ya matokeo kutoridhisha.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF), Kidao Wilfred ameishukuru SBL kwa mchango wake mkubwa kwenye timu ya taifa na kuongeza kuwa udhamini wa SBL kwa Taifa Stars umekuwa na mchango kubwa katika kuiwezesha timu kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali yanayoikabili.

“Tutakutana na benchi la ufundi ili kufanya tathimini juu ya ushiriki wa timu yetu kwenye fainali za AFCON 2019, baada ya hapo tutakuja na mkakati kwa ajili ya mashindano yaliyoko mbele yetu ya kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN)”. Alisema Kidao huku akidokeza kuwa timu imepata ‘funzo kubwa’ kule Cairo.

Taifa Stars inayodhaminiwa na SBL imeweza kushiriki katika fainali za AFCON 2019 kwa mara ya kwanza tangu mara ya wisho ilipofanikiwa kufuzu kucheza fainali hizo takribani miaka 39 iliyopita.

Stars ilipangwa kwenye kundi C ambalo lilijumuisha magwiji wawili wa soka barani Afrika (Senegal na Algeria) pamoja na Kenya.

…Mwisho…

Kuhusu SBL

Ikiwa imeanzishwa kama Associated Breweries mwaka 1988, Kampuni ya Bia Serengeti (SBL) ni moja ya kampuni kubwa za bia nchini Tanzania, ambapo aina zake za bia zinachangia zaidi ya asilimia 20 ya bidhaa hizo katika soko. SBL inaendesha viwanda vitatu vilivyopo Dar es Salaam, Mwanza na Moshi.

Tangu kuanzishwa kwa SBL mwaka 2002 biashara yake imekua na kuimarika zaidi na asilimia 51 ya hisa mwaka 2010 zilizochukuliwa na Kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki (EABL) zimeshuhudia ongezeko la uwekezaji katika kukua zaidi na hivyo kusababisha kuongezeka kwa fursa zaidi za ajira kwa watu wa Tanzania.

Aina za bia zinazozalishwa na SBL ambazo zimepata tuzo kadhaa za kimataifa ni pamoja na Serengeti Premium Lager, Pilsner, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Guinness stout, Uhuru na Kick.

SBL pia ni wazalishaji vinywaji vikali vinavyofahamika duniani kama vile Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain Morgan Rum na Baileys Irish Cream. ………………………………………………………

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na; John Wanyancha SBL Corporate Relations Director Tel: 0692148857 Email: john.wanyancha@diageo.com
Share:

NCHI 13 ZILIZOENDELEA KUTOKA AFRIKA NA ASIA ZAMALIZA MAFUNZO YA SIKU SABA JUU YA HAKI ZA MILIKI BUNIFU NA USHAURI KWENYE UCHUMI WA UTANDAWAZI DAR


Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa shirika linaloshughulikia masuala ya Miliki bunifu Duniani (World Intellectual Property Organisation-WIPO) Bw. Kifle Shenkoru akitoa neno la shukrani
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Emmanuel Kakwezi akitoa neno la shukurani kwa washiliki wa mafunzo ya masuala ya miliki bunifu kutoka nchi kumi na tatu (13)
Afisa Mtendaji Mkuu wa chama cha Hakimiliki Tanzania Bi. Doreen A. Sinare akitoa neno la shukurani kwa washiliki wa mafunzo ya masuala ya miliki bunifu kutoka nchi kumi na tatu (13)
Mshiriki na mjumbe kutoka Uganda,Bwana Emmanuel Mutungi akitoa neno la shukurani kwa niaba ya washiriki kutoka nchi kumi na tatu (13)
Mshiriki wa mafunzo ya juu ya haki za miliki bunifu na ushauri kwenye uchumi wa utandawazi Kutoka Malawi Tikhale Magombo Chikanda akitoa neno la shukurani.
Washiriki wa mafunzo Washiriki kutoka nchi kumi na tatu (13) wa mafunzo ya juu ya haki za miliki Bunifu na ushauri wakifuatilia hitimisho la mafunzo yaliyochukua siku saba.
Mshiriki wa mafunzo ya juu ya haki za miliki bunifu na ushauri kwenye uchumi wa utandawazi akipokea zawadi kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa BRELA
Mshiriki wa mafunzo ya juu ya haki za miliki bunifu na ushauri kwenye uchumi wa utandawazi akipokea zawadi kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa BRELA
Mshiriki wa mafunzo ya juu ya haki za miliki bunifu na ushauri kwenye uchumi wa utandawazi akipokea zawadi kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa BRELA
Kamati ya maandalizi ya mafunzo ya siku saba ya nchi kumi na tatu (13) zinazoendelea kutoka Afrika na Asia iliyofanyika Juni 30,2019 hadi Julai 5, 2019 kwenye ukumbi wa Zanzibar ndani ya Hotel ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es salaam
Washiriki kutoka nchi kumi na tatu (13) wa mafunzo ya juu ya haki za miliki Bunifu na ushauri Kwenye uchumi wa utandawazi wakiwa wamemaliza mafunzo hayo ambayo yamechukua siku saba katika Hotel ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

Share:

Wizara ya Ardhi yaanza kusaka wadaiwa sugu kodi ya pango Dar

Na Munir Shemweta
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameanza operesheni maalum ya kuzibana Taasisi ambazo ni wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika jiji la Dara es Salaam kwa kutembelea ofisi moja hadi nyingine ili zilipe madeni yao katika muda uliopangwa ambapo katika ziara hiyo taasisi sita kati ya saba alizotembelea zimeahidi kulipa zaidi ya bilioni 4.5 kufikia Desemba 2019.

Dkt Mabula alizitembelea taasisi hizo juzi ikiwa ni mkakati wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhakikisha wadaiwa wote sugu wa kodi ya pango la ardhi wanalipa madeni yao kabla ya hatua za kuwafikisha kwenye Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya wale watakaokaidi kulipa ambapo adhabu yake ni kulipa ama kupigwa mnada kwa mali za taasisi husika kufidia deni la kodi ya pango la ardhi.

Taasisi alizotembelea Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi juzi ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linalodaiwa bilioni 3, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) bilioni 1.4, EPZA milioni 200, Shirika la Reli Tanzania (TRC) bilioni 2.5, Shirika la Masoko Kariakoo milioni 249 pamoja na Chuo cha Taifa cha Utalii milioni 26.8.

Akiwa katika Shirika la Masoko Kariakoo, Dkt Mabula alishangazwa na Shirika hilo kudaiwa zaidi ya milioni mia mbili huku likiomba kulipa deni lake katika kipindi cha miaka miwili jambo alilolieleza kuwa ni kinyume na taratibu za ulipajia madeni ya kodi ya pango la ardhi ambazo humtaka mdaiwa kulipa nusu ya deni.

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo Bw. Hetson Kipsi katika barua yake, Shirika lake liliahidi kulipa kwa awamu deni hilo katika kipindi cha miaka miwili kwa kutoa milioni saba kila mwezi jambo lililokataliwa na Dkt Mabula ambapo alieleza kuwa Shirika hilo linapaswa kulipa nusu ya deni kwanza ndipo liingia makubaliano ya kulipa kiasi kilichobaki kwa awamu. Hata hivyo Shirika la Masoko Kariakoo lilikubali kutoa milioni mia moja kufikia 29 Julai 2019 na kukamilisha kiasi kilichobaki desemba 2019.

Kwa upande wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mkurugenzi Mtendaji wake Masanja Kadogosa alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Mkazi Dkt Mabula kuwa Shirika lake halipingi kulipa deni inalodaiwa bali inachofanya ni kuhakiki upya deni hilo kwa kuwa kumekuwa na uhamisho wa umiliki wa mali za TRC kwenda TBA tangu mwaka 1999 sambamba na baadhi ya nyumba za Shirika kuuzwa kwa wananchi huku baadhi ya mali za TRC zikiwa hazina hati.

Kadogosa alisema, kiasi cha shilingi bilioni 2.4 wanachodaiwa ni kikubwa na hakilingani na uhalisia wa deni la TRC na kubainisha kuwa uhakiki utakapokamilika ana imani deni hilo litapungua kwa kiasi kikubwa. Dkt Mabula alimueleza kuwa, Shirika lake linapaswa kulipa robo ya tatu ya deni hilo wakati uhakiki ukiendelea na iwapo itaonekana deni limepungua basi kiasi cha fedha kilichozidi kitarudishwa.  Hata hivyo, Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TRC alikubali kulipa kiasi cha milioni 400 kwa awamu hadi kufikia oktoba 2019 wakati zoezi la uhakiki wa deni hilo unaohusisha Wataalamu wa Shirika hilo na Wizara ukiendelea.

Chuo cha Taifa cha Utalii kupitia kwa Kaimu Mkuu wa Chuo Boniface Mwaipaja kilikiri kudaiwa kiasi cha milioni 26.8 na kuahidi kulipa kwa awamu deni hilo ambapo Mkuu huyo wa Chuo aliahidi kulipa kiasi cha milioni saba kwanza na baadaye kulipa kwa awamu kiasi kilichobaki na kukamilisha deni hilo kufikia desemba 2019.

Taasisi nyingine zilizotembelewa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na kuahidi kulipa madeni yao baada ya uhakiki ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) inayodaiwa bilioni 1.4, na EPZA milioni 200 ambapo kwa upande wake TBA tayari imeandaa utaratibu wa kulipa deni hilo kwa awamu na tayari milioni 40 zimetengwa wakati EPZA ilihidi kutoa mchanganuo wa jinsi itakavyolipa deni hilo wiki hii.

Juni 11, 2019 Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi iliitisha kikao cha Taasisi ambazo ni wadaiwa Sugu wa kodi ya Pango la Ardhi takriban 200 kwa kuwapa taarifa ya kulipa madeni yao sambamba na kuhakiki madeni hayo kabla ya hatua za kisheria hazijachukuliwa kwa watakaokaidi kulipa madeni hayo. Ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ilikuwa ni kuangalia taasisi zinazodaiwa zimekwama wapi kutekeleza agizo lililotolewa.


Share:

Video Mpya: Dogo Janja – Kishada

Video Mpya: Dogo Janja – Kishada


Share:

Video Mpya: Vanessa Mdee - Moyo

Video Mpya: Vanessa Mdee - Moyo


Share:

Jeshi la Polisi lawanasa raia 3 wa kigeni wakisafirisha Madini

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu watatu raia wa kigeni kwa kosa la kusafirisha madini aina ya dhahabu bila kuwa na kibali.

Watuhumiwa hao walikuwa wakitokea Wilaya ya Chunya kuelekea Jijini Dar es salaam.Watuhumiwa hao ni 1: Clive Rooney (62)raia wa nchi ya Ireland 2: Ross Stephen Chertsey (34), raia wa nchini Uingereza pamoja na 3:Robert Charles 58, raia wa nchini Uingereza.

Tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 03.07. 2019  huko Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Songwe (SIA), Kata ya Nsalala,Tarafa ya Usongwe Wilaya ya Kipolisi Mbalizi. Watuhumiwa hao walikamatwa na maafisa wa usalama wa uwanja huo wa Songwe.

Madini hayo yalikuwa na uzito wa gramu 1,044.95. Ufuatiliaji unaendelea kufanywa na Kikosi kazi cha kamati ya usalama ya Mkoa.


Share:

Wazee wa CHADEMA watuma maombi ya Kuonana na Rais Magufuli

Baraza la Wazee Chadema limesema Rais Dk. John Magufuli anapaswa kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani kama alivyofanya kwa viongozi wa dini na wafanyabiashara.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Chadema, Hashim  Juma Issa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

Issa ambaye alizungumzia mambo mbalimbali ikiwamo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, matumizi fedha za umma na hali ya kisiasa nchini, alisema Rais aondoe wasiwasi na akutane na viongozi wa vyama vya upinzani wa juu kila chama ili aweze kubadilishana nao mawazo.

“Ameshakutana na viongozi wa dini alifanya jambo la maana sana…tunajua umekutana na wafanyabiashara hongera sana, hivyo ndivyo unavyotakiwa uwe kiongozi wa nchi.

“Lakini kwa bahati mbaya sana, sijui kwa nini hujakutana na viongozi wa vyama vya upinzani tangu umeingia madarakani, hapo unakuwa hutendi haki,”alisema Issa.

“Waambie kila chama angalau kije na viongozi 10 wa juu, tuje hapo, tukukosoe mbele yako, ndani  ya ikulu yako, tukueleze kasoro zako kama utaweza ujirekebishe,” alisema.

Mwenyekiti huyo wa Baraza la Wazee alikumbusha majibu yaliyowahi kutolewa na Rais Magufuli wakati akipokea ndege baada ya kushauriwa na kiongozi wa mmoja wa dini kuhusu kuonana na wapinzani, ambapo alisema hawezi kuonana nao kwa sababu wana njama za kumuhujumu.

 “Sisi kama Baraza la Wazee tukwambie, kitu kama hicho hakipo Chadema, na nina amini hata kwa vyama vingine hakipo ingawa mimi sio msemaji wa vyama vingine lakini naamini kitu kama hicho hakuna.

“Sisi Chadema hatuna nia ya kukudhuru wewe, hatuna nia ya kumdhuru mtu yoyote yule, wala hatuna kisasi chochote”

“Hata mfano ikitokea Mungu akijalia  tumeshinda uchaguzi 2020, sisi tunafuta mambo yote yaliyotokea nyuma, hatutomuhukumu mtu yoyote, hatutofukua makaburi yoyote wala hatuna kisasi na mtu yoyote,” alisema.

Kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwenyekiti huyo wa Baraza la Wazee alisema wamejiandaa kushiriki kwa asilimia 100.

“Tunamwambia Mwenyekiti wa CCM, Katibu Mkuu kuwa safari hii Baraza la Wazee tunakula kiapo hatutokubali kwa namna yoyote ile kuibiwa kura hata moja.

“Tunasikia Rais ameteua wakurugenzi na tunasikia tetesi kwamba baadhi ya vituo vitawekwa kwenye kambi za jeshi

“Sasa sisi kama Baraza la Wazee kwa sababu tunajiamini na tunadhamira safari hii kuingia kwenye uchaguzi hata waweke ma-DED  wa aina gani, vituo vyote vya Tanzania  viwe ndani ya kambi za jeshi, viwe ndani ya vituo vya  polisi,  viwe ndani jela za magereza na hata vingine vikiwekwa mochwari sisi tunaingia humo humo, tutapiga kura  tutashinda humo humo na hatutaibiwa kura hata moja”alisema.



Share:

Serikali Yaahidi Kufanya Kazi Na Vijana Katika Utekelezaji Wa Sera Ya Kilimo

Najma Khamis Salum, Afisa mawasilianao - Sahara Consulting
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imesema ipo tayari kufanya kazi na Vijana wabunifu katika utekelezaji wa Sera yake mpya ya Kilimo nchini ambapo suala la matumizi ya Teknolojia katika kilimo limepewa kipaumbele.

Hayo yamesemwa na Katibu MKuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe juzi tarehe 2 Julai 2019 wakati wa kikao maalumu kilicho itishwa na Wizara hiyo kupata ufahamu zaidi kuhusu mradi wa E-Kilimo Accelerator uliojikita katika kutafuta suluhu za teknolojia za kidijitali zinazosaidia kupambana na changamoto mbalimbali kwenye sekta ya kilimo.

Mradi huo wa E-Kilimo Accelerator umefadhiliwa na ubalozi wa Denmark nchini na kuendeshwa na Shirika la Sahara Consulting la jijini Dar es salaam.

Akizingumza katika kikao hicho kilichowahusisha wataalamu wa ngazi za juu wa Wizara ya Kilimo kutoka vitengo vyake vyote, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara hiyo Bw. Assery Obey amesema, Serikali ingependa kuona bunifu hizo zilizopatikana kupitia mradi huo zinatumika ipasavyo kwa kushirikiana na Wizara katika kutatua changamoto mbalimbali na ikiwezakana kufanya kazi na vitengo vyake katika kuziendeleza na kuzitumia katika maeneo yake ya utekelezaji.

“Nimefurahishwa na jinsi kampuni hizi zilivyokua zikiwakilisha bunifu zao hapa na vile walivyoweza kuchambua maeneo ya vipaumbele ya serikali na kupendekeza jinsi gani wanaweza kufanya kazi na Serikali”. Alisema  Assery.

Serikali pia imetoa wito wa ushirikwashaji wa serikali wakati wa uandaaji miradi hiyo na usimamiaji ili kuhakikisha inaleta matokeo makubwa zaidi na inajibu changamoto husika.

Nae Bwana Adam Mbyallu ambae ni Mkuregenzi wa Shirika la Sahara Consulting ambayo ni miongoni mwa taasisi tanzu ya Sahara Ventures ameishukuru Wizara ya Kilimo kwa utayari wake wa kufanya kazi na vijana na kuona bunifu zao zinaendelezwa.

“Sio lazima kila kijana ajihusishe na Kilimo kwa maana ya kulima moja kwa moja, Vijana kwa taaluma zao wanaweza wakabuni namna bora ya kusaidia Mnyororo wa Kilimo kupitia bunifu na teknolojia mbalimbali”. Alisema Bw, Mbyallu.

Mkutano huo, ulihudhuriwa pia na Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania Bw. Boniface Ihunyo.

Kwa upande wake Bw. Ihunyo amesema Ubalozi wa Denmark nchini uliamua kusaidia mradi huu katika juhudi zake za kuangalia ni kwa namna gani teknolojia inaweza kusaidia katika nyanja mbalimbali nchini ambapo kilimo ni moja ya nyanja kuu na hivyo basi kuona umuhimu wake.

Mradi huu ni wa kwanza na wa kipekee  unahusisha kusaidia ongezeko la kasi la biashara za kilimo. E-Kilimo ililenga kuongeza kasi katika ukuaji wa sekta ya bidhaa za chakula na mazao Tanzania kupitia matumizi ya teknolojia na uvumbuzi katika utatuzi wa changamoto zinazoikumba sekta hiyo na hivyo kuleta matokeo katika uzalishaji, ajira na fursa za maendeleo.

Jumla ya bunifu Tisa zimeweza kupatikana katika mradi huo na tano kati ya hizo ziliweza kuwasilisha bunifu hizo Wizarani.

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na yafuatayo;
●     Ni kwa namna gani kwa pamoja tunaweza kushirikiana ili kuweza kumsadia mkulima mdogo.
●     Ni kwa namna gani tunaweza kushirikiana kuandika na kuandaa miradi ya kilimo.
●     Na pia jinsi ya kuwasaidia vijana wanaokuja na mawazo mbalimbali ya kibunifu.


Share:

BASATA Watoa Tamko Baada ya Video Chafu ya Amber Rutty Kuvuja tena




Share:

Waziri Mkuu Majaliwa Atoa Rai Kwa Viongozi Wa Madhehebu Ya Dini Kuendelea Kutoa Malezi Ya Kiroho Ili Kuenzi Amani.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema viongozi wa dini waendelee kuimarisha malezi na mafundisho ya kiroho kwa vijana na kuepusha mmomonyoko wa maadili ili Taifa liendelee kung’ara, kuheshimika na kusifika duniani kwa utulivu, amani na umoja.

Amesema Serikali inatambua mchango wa madhehebu ya dini ikiwemo CCT katika kutengeneza mustakabali mwema na ustawi wa familia kupitia mahubiri ya injili na malezi ya kiroho kwa waamini. “Mtakubaliana nami kuwa siku zote Taifa imara msingi wake hujengwa na familia imara.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana (Ijumaa, Julai 5, 2019) wakati alipomwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya 53 ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ulioambatana na harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa kitegauchumi cha jumuiya hiyo. Mkutano huo umefanyika jijini Dodoma.

Amesema Serikali inatambua mchango wa malezi ya kiroho katika ustawi wa wananchi na Taifa kwa ujumla na mafundisho yake kwani yamesaidia kujenga watumishi wa umma ambao wamelelewa katika misingi bora ya kumcha Mwenyezi Mungu.   

Waziri Mkuu amesema Serikali inaamini kwamba watumishi wa namna hiyo watachapa kazi kwa bidii, uadilifu, uaminifu na kupiga vita vitendo vyote vya rushwa na ubadhilifu wa mali za umma. Serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi za kidini kwa ajili ya ustawi wa Taifa na watu wake.

Akizungumzia kuhusu harambee hiyo ambayo jumla ya sh. milioni 357.35 zilipatikana, Waziri Mkuu amesema ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa CCT wa miaka mitano (2017 – 2022) wenye lengo la kuiwezesha CCT kujitegemea kwa kuwa na vitega uchumi vyake ambavyo vitawawezesha kujiendesha kwa asilimia 80.

Waziri Mkuu ameipongeza CCT kwa kuanza kuchukua hatua za kujenga uwezo wa ndani wa kujitegemea kiuchumi kwani zinahitajika nguvu za pamoja katika kuhakikisha wanawahudumia Watanzania na kuwaletea maendeleo.

“Kujizatiti kwa CCT katika kufikia malengo yake ya kujitegemea kiuchumi ni muhimu katika kutimiza kusudio na agizo la Mungu la kuwahudumia wahitaji ambao ni Watanzania lakini pia mtakuwa mnajaliza juhudi za Serikali katika wajibu wake wa kuwahudumia wananchi.”

Waziri Mkuu amesema kwa msingi huo, Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za CCT na madhehebu mengine ya dini katika kuwahudumia Watanzania kupitia sekta za elimu, maji, afya na shughuli za ujasiriamali.

Amesema suala la kujitegemea ndiyo msingi wa uongozi wa Rais Dkt. Magufuli wa kujenga uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ifikapo mwaka 2025 na katika kufanikisha hilo, Serikali imeendelea kupunguza kiwango cha utegemezi.

Amesema kiwango cha utegemezi kutoka kwa Washirika wa Maendeleo katika bajeti kimepungua kutoka asilimia 12.5 mwaka 2017/2018 hadi asilimia nane 2019/2020. “Kuimarika huko kwa bajeti yetu kunakwenda sambamba na kuimarika kwa huduma za kijamii kama vile elimu, maji na kupungua kwa umaskini wa mahitaji muhimu.”

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CCT, Mchungaji Canon Moses Matonya, amesema jumuiya hiyo imeanzisha mkakati wa kuwa na vitegauchumu vyake kwa lengo kuondokana na utegemezi wa fedha za ufadhili ambazo zimekuwa zikipungua mwaka hadi mwaka.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Profesa Mbarawa akerwa na Wakandarasi wa maji wababaishaji Shinyanga, alazimika kuwasainisha makubaliano maalum.

NA SALVATORY NTANDU
Waziri wa Maji Prof, Makame Mbarawa amewaagiza wakandarasi wanaojenga mradi wa maji ya Ziwa victoria  kutoka kahama hadi  Isaka kwenda wa mkuu wa wilaya ya kahama kuandika makubaliano maalumu ambayo yataonesha ni lini watakamilisha miradi hiyo baada ya kushindwa kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.

Uamuzi huo umetolewa jana na Prof.Mbarawa baada ya kupokea taarifa za kutokamilika kwa mradi huo kutokamilika kwa wakati huku wakiendelea kutoa ahadi za uongo.

Mbarawa amefafanua kuwa Wakandarasi hao wameshindwa kutimiza mashariti ya mkataba walioingia na serikali hivyo hawatakuwa na nafasi tena ya kuendendelea kutokamilisha mradi huo licha ya kuwa fedha wameshalipwa na serikali.

Amesema serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais, Dk John Magufuli haitakubali kuendelea kuwakumbatia wakandarasi wazembe ambao wanakwamisha shughuli za maendeleo ya wananchi katika maeneo wanayoishi.

Kwa upande wake Ezekiel Maige ni mbunge wa jimbo la Msalala amemuomba  Waziri Mbarawa kuwabana wakandarasi hao ili mradi huo ukamilike kwa wakati ili kuwawezesha wananchi kupata maji safi na salama.

Nao baadhi ya wananchi Kurwa Kitunga na Kashindye Singu  wa Kata za Mwakata na Mwendakulima waliojitokeza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Waziri huyo wameomba kujengewa magati ya maji katika vijiji ambavyo kunashida ya maji ili kuwawezesha kuacha kutumia maji ambayo sio safi yanayotumika pamoja na wanyama.

Kampuni zilipewa dhabuni ya kujenga mradi huo ni pamoja na Oriental conslin limited na Changs ambazo zimepewa kandarasi hiyo yenye thamani ya zaidi ya bilioni 22 ambapo walitakiwa kukamilisha mradi huo mwezi june  mwaka huu.

Bado Waziri Mbarawa anaendelea na ziara yake ya kikazi ya siku 4 mkoani shinyanga kukagua miradi mbalimbali ya maji.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi 6 July



















Share:

Friday, 5 July 2019

Unahitaji Kufanya Service ya Gari Weekend Hii? Je wewe ni Mmiliki wa Gari? Ni Fundi Magari au Muuza Spea? ...Hapa Tunahabari Njema Inayokuhusu

Habari njema kwa wamiliki wa Magari, mafundi na Wauza Spea za Magari. EDRIVE PRO wamekeletea mfumo ambao unawaunganisha pamoja na pindi gari lako likiharibika popote ulipo hutapata tena tabu ya kuhangaika kutafuta fundi au maduka ya spea

www.edrivepro.co.tz ni mfumo wa kufanya na kusimamia utengenezaji wa magari online.

1. Katika mfumo huu wamiliki wa magari, maduka ya spare, na mafundi wanajisajiri ama wanaweza kusajiliwa kwa kuwasiliana na mtoa huduma wetu kwa e-mail edriveprotz@gmail.com

2. Baada ya kujisali kulingana nafasi yako [ mmiliki wa gari, muuza spare, fundi ama mwandika makala juu ya magari] msimamizi wa mfumo atakuthibitisha katika mfumo na utatumiwa e-mail na mfumo.

Baada ya kudhibitishwa utaweza kupata huduma za uuzaji wa spare, matengenezo ya magari kwa wamiliki wa magari na mafundi kupata fursa za mateja wapya mtandaoni nchi nzima.

3. Kutokana na wahusika wote katika mfumo huu kuwa wamesajiliwa, huduma katika mfumo huu ni nafuu na za uhakika.

Karibuni mjisajili katika www.edrivepro.co.tz


NB: Weekend hii kuna ofa kabambe kama unahitaji matengenezo ya Gari yako.  Hii si ya kukosa, Jisajili sasa.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger