Saturday, 6 July 2019

Jeshi la Polisi lawanasa raia 3 wa kigeni wakisafirisha Madini

...
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu watatu raia wa kigeni kwa kosa la kusafirisha madini aina ya dhahabu bila kuwa na kibali.

Watuhumiwa hao walikuwa wakitokea Wilaya ya Chunya kuelekea Jijini Dar es salaam.Watuhumiwa hao ni 1: Clive Rooney (62)raia wa nchi ya Ireland 2: Ross Stephen Chertsey (34), raia wa nchini Uingereza pamoja na 3:Robert Charles 58, raia wa nchini Uingereza.

Tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 03.07. 2019  huko Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Songwe (SIA), Kata ya Nsalala,Tarafa ya Usongwe Wilaya ya Kipolisi Mbalizi. Watuhumiwa hao walikamatwa na maafisa wa usalama wa uwanja huo wa Songwe.

Madini hayo yalikuwa na uzito wa gramu 1,044.95. Ufuatiliaji unaendelea kufanywa na Kikosi kazi cha kamati ya usalama ya Mkoa.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger