TANZANIA
YAPOKEA TUZO UMEME VIJIJINI
Jitihada za Wizara ya
Nishati na Madini za kuhakikisha umeme unafika na kusambaa maeneo ya vijijini
zimetambuliwa kimataifa hali iliyopelekea Serikali kupokea Tuzo ya Uwezeshaji
wa Mazingira Bora ya Upatikanaji wa Umeme Vijijini kwa Nchi zinazoendelea.
Serikali imetunukiwa
Tuzo hiyo mwezi Machi, 22 na Taasisi ya Kimataifa ya Alliance for Rural Electrification yenye Makao Makuu yake nchini Ubelgiji
ambayo ilipokelewa na Meneja Miradi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol, Prosper Magali
kwa niaba ya Serikali katika hafla ya utoaji tuzo iliyofanyika Lisbon, Ureno.
Magali pia ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA).