WAZIRI
wa mambo ya ndani ya nchi,Mwigulu Nchemba,amesema hawatokubaliana na
mtandao,kundi ama mtu anaehusika na kugharimu maisha ya askari ama
wananchi wasio na hatia.
Aidha
amebainisha kwamba kilichombele kwa sasa ,wanaendelea kuhakikisha kuwa
wanarudisha silaha zinazochukuliwa katika matukio mbalimbali ya mauaji
ya askari na kuendelea na mapambano na wahalifu hao.
Nchemba
ameyasema hayo ,wilayani Kibiti,mkoani Pwani,na kumtaka mwenyekiti wa
kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo
kupambana na matukio ya mauaji yanayoendelea katika baadhi ya wilaya
mkoani hapo.
Waziri huo wa mambo ya ndani ,alieleza kwamba,amepokea taarifa ya kuuwawa kwa askari nane wilayani Kibiti kwa mshituko mkubwa .
Nchemba aliwaomba watanzania kwa kipindi hiki wawe watulivu wakati jeshi la polisi likiendelea kukabiliana na mambo hayo.
“Hii
ni changamoto kwa wizara ya mambo ya ndani kuanza upya kuboresha mbinu
zake za ki intelensia zinazoendana na mazingira ya sasa kwa mahitaji ya
sasa”alisema.
Alibainisha kwamba,ni ngumu kuingia akili kwa watu wachache kuuwa hovyo askari ambao ndio walinzi wa raia na mali zao
“Kuna jambo lipo nyuma limejificha ambalo mwisho wake umefika kwani hatutoweza kulifumbia macho”alisisitiza.
Nchemba
aliomba jamii iendelee kulinda amani ya nchi na kuheshimu askari polisi
ambao wapo kwa ajili ya kuwalinda katika usalama wao.
0 comments:
Post a Comment