JAMHURI
YAMUUGANO WA TANZANIA
OFISI
YA RAIS
TAWALA
ZA MIKOA NA SERIKALI ZAMITAA
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU AJIRA MPYA ZA
WALIMU WA MASOMO YA HISABATI NA SAYANSI
KWA MWAKA 2016/2017
Serikali kupitia
Ofisi ya Rais TAMISEMI imetangaza ajira mpya kwa Walimu wa masomo ya Hisabati
na Sayansi leo tarehe 12 Aprili, 2017.
Majina ya Walimu
yaliyotangazwa yanatokana na tangazo la nafasi ya kazi ya Ualimu lililotolewa
na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mnamo tarehe 01 Desemba, 2016.
Jumla ya Walimu
wapya wapatao 3,081 wakiwemo 1,544 ni wa ngazi ya Shahada na Walimu 1,537 ni wa
Stashahada.
Walimu hao
watatakiwa kuripoti kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri na baadaye
kwenye Shule walizopangiwa kuanzia tarehe 18 Aprili, 2017 hadi tarehe 25
Aprili, 2017. Walimu wote waripoti wakiwa na vyeti halisi vya taaluma vya
kidato cha nne (IV) na kidato cha sita (VI), vyeti halisi vya kitaalaam vya
kuhitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada na Shahada na Cheti cha
kuzaliwa.
Angalizo :
i.
Walimu waliopangiwa vituo ni wa masomo ya Hisabati na Sayansi
waliohitimu hadi mwaka 2014/2015.
1
ii.
Kituo cha kazi cha mwalimu ni shule aliyopangiwa na sio makao
makuu ya Halmashauri.
iii.
Mwalimu atakayeripoti na kuchukua posho ya kujikimu na baadae
kuondoka atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
iv.
Walimu wote watakiwa kuripoti katika vituo vyao kuanzia tarehe
18 Aprili, 2017 hadi 25 Aprili, 2017, watakaochelewa nafasi zao zitajazwa na
mwalimu mwingine.
v.
Hakutakuwa
na uhamisho ndani ya Mkoa au Halmashauri.
Majina ya Walimu
hao yanapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
Imetolewa na:
Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais TAMISEMI
2
3
0 comments:
Post a Comment