TANZANIA
YAPOKEA TUZO UMEME VIJIJINI
Jitihada za Wizara ya
Nishati na Madini za kuhakikisha umeme unafika na kusambaa maeneo ya vijijini
zimetambuliwa kimataifa hali iliyopelekea Serikali kupokea Tuzo ya Uwezeshaji
wa Mazingira Bora ya Upatikanaji wa Umeme Vijijini kwa Nchi zinazoendelea.
Serikali imetunukiwa
Tuzo hiyo mwezi Machi, 22 na Taasisi ya Kimataifa ya Alliance for Rural Electrification yenye Makao Makuu yake nchini Ubelgiji
ambayo ilipokelewa na Meneja Miradi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol, Prosper Magali
kwa niaba ya Serikali katika hafla ya utoaji tuzo iliyofanyika Lisbon, Ureno.
Magali pia ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA).
Akikabidhi Tuzo hiyo Jijini
Dar es Salaam, kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia
Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo; Magali alisema Tuzo hiyo imetolewa kwa
kutambua mchango wa Serikali ya Tanzania wa kufikisha huduma ya umeme maeneo ya
vijijini pamoja na uwezeshaji wa mazingira bora na rafiki kwa wawekezaji wanaosambaza
umeme katika maeneo ya vijijini.
“Kwa mwaka huu,
Serikali yetu imetambuliwa kwa kufikisha umeme vijijini na juhudi zake za
kuhakikisha kunakuwa na mzingira rafiki kwa watoaji na wasambazaji wa huduma ya
umeme vijijini,” alisema Magali.
Kwa upande wake
Dkt.Mhandisi Pallangyo aliipongeza kampuni ya Ensol kwa kupokea tuzo kwa niaba
ya Serikali na kuahidi kuendeleza ushirikiano na kampuni zote zinazojihusisha
na usambazaji wa umeme maeneo ya vijijini.
Alisema Serikali
itaendelea kuandaa mazingira rafiki kwa wawekezaji ili kutimiza azma ya
kuhakikisha vijiji vyote vinafikiwa na huduma ya Nishati ya Umeme.
Aidha, Dkt. Mhandisi
Pallangyo alizitaka kampuni nyingine zinazoshughulika na uzalishaji na
usambazaji wa umeme vijijini kujiunga na Taasisi za Kimataifa ikiwemo ya Alliance
for Rural Electrification ili kunufaika na fursa zinazopatikana kwenye Taasisi
hizo.
Makabidhiano hayo
yalishuhudiwa na watendaji wa Wizara na Taasisi zake wakiongozwa na Kaimu
Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga na
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ensol, Hamis Mikate.
CAPTIONS
MOJA
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt.
Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akipokea Tuzo kutoka kwa Meneja Miradi wa
Kampuni ya Umeme ya Ensol, Prosper Magali.
MBILI
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Ensol, Hamis Mikate akizungumza wakati wa makabidhiano
ya Tuzo. Kulia ni Meneja Miradi wa kampuni hiyo, Prosper Magali na Afisa wa
Ensol, Magdalena Ally.
TATU
Watendaji
kutoka Wizara ya Nishati na Madini waliohudhuria tukio la upokeaji wa Tuzo. Wa
kwanza kushoto ni Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi
Innocent Luoga.
NNE
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt.
Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) katika picha ya pamoja na watendaji wa
Wizara na Taasisi zake na wawakilishi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol baada ya
kukabidhiwa Tuzo.
TANO
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt.
Mhandisi Juliana Pallangyo (wa nne kutoka kulia) katika picha ya pamoja na
watendaji wa Wizara na Taasisi zake na wawakilishi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol
baada ya kukabidhiwa Tuzo.
SITA
Meneja
Miradi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol, Prosper Magali (kushoto) akipokea Tuzo ya
Uwezeshaji wa Mazingira Bora ya Upatikanaji wa Umeme Vijijini kwa Nchi
zinazoendelea kwa niaba ya Serikali kutoka kwa Mwenyekiti wa Sera ya Mtandao wa
Kimataifa wa Nishati Mbadala (REN21) yenye makao makuu yake nchini Ufaransa,
Profesa Arthouros Zervos.
SABA
Meneja
Miradi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol, Prosper Magali pamoja na washiriki kutoka
nchi mbalimbali wakionesha Tuzo walizopokea kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa
ya Alliance for Rural Electrification
katika hafla ya utoaji tuzo iliyofanyika Lisbon, Ureno
0 comments:
Post a Comment