Tuesday, 19 November 2024

RAIS SAMIA AMUAGIZA WAZIRI MKUU KUHARAKISHA UOKOAJI KARIAKOO

...

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na ajali ya kuporomoka kwa ghorofa, Kariakoo Mtaa wa Mchikichi na Kongo jijini Dar es Salaam, ambapo amemwagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa kushirikiana na timu za uokoaji kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa haraka na ufanisi.

Kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ikiwemo 'Instagram' na 'WhatsApp channel' Rais Samia ameandika: " Hivi punde nimezungumza kwa kirefu na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mbunge) kuhusiana na ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika Kata ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam, na kazi ya uokoaji inayoendelea. 

Nimempa maelekezo kuhakikisha kazi hii inafanyika kwa haraka na ufanisi, na niendelee kupata taarifa ya kila hatua ya maendeleo yake"

Akionesha masikitiko yake Rais Samia amesema: Nimesikitika kupokea taarifa ya ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika Kata ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam. 

Nimeuagiza Uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, na Idara ya Menejimenti ya Maafa kufanya kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi. 

Wakati hilo likiendelea na tukimuomba Mwenyezi Mungu awape pona ya haraka majeruhi, tuwaombee pia utulivu na subra ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wenzetu wanaotafuta riziki zao katika eneo hili muhimu kibiashara nchini ambao kwa namna mbalimbali wameathiriwa na ajali hii.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger