Serikali
kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna
Tarish imevitaka vyuo vikuu 14 ambavyo havijatuma matokeo ya wanafunzi
wao ya mwaka uliopita kwa Bodi ya Mikopo kutuma mara moja ili kuwapatia
mikopo kwa walio katika utaratibu wa kupata mkopo wa serikali.
Taarifa
ambayo imetolewa na Tarish imevipa vyuo hivyo 14 siku mbili pekee
kuhakikisha vinatuma majina kwa Bodi ya Mikopo na kuagiza viweke mfumo
mzuri ambao utawawezesha kutuma matokeo kwa haraka.