Saturday, 16 July 2016
Friday, 15 July 2016
NECTA Imezitaja Shule 10 Bora Kitaifa Pamoja na Shule 10 za Mwisho Kitaifa
Baraza
la mitihani Tanzania(NECTA) imetangaza matokeo ya kidato cha sita 2016,
na Kuzitaja shule zilizo fanya vizuri zaidi Kitaifa na zile ambazo
hazikufanya vizuri Kitaifa.
Ubora wa shule umepagwa kwa kutumia kigezo cha Wastani wa Pointi (Grade Point Average – GPA) ambapo A=1, B=2, C=3, D=4, E=5 na F=7.
Aidha, upangaji wa shule zilizofanya vizuri umezingatia shule zenye idadi ya watahiniwa wasiopungua 30 kama ifuatavyoa:
==>Shule 10 Bora Kitaifa
Aidha, upangaji wa shule zilizofanya vizuri umezingatia shule zenye idadi ya watahiniwa wasiopungua 30 kama ifuatavyoa:
==>Shule 10 Bora Kitaifa
1. Kisimiri (Government)
2. Feza Boys (Private)
3. Mwanza Alliance Girls (Private)
4. Feza Girls (Private)
5. Tabora Boys (Government)
6. Marian Boys (Private)
7. Kibaha (Government)
8. Mzumbe (Government)
9. Ilboru (Government)
10. Tandahimba (Private)
==>Shule 10 za Mwisho Kitaifa
1.Mpendae (Unguja)
2.Ben bella ( Unguja)
3.Tumekuja (Unguja)
4.Green Bird Boys (Kilimanjaro)
5.Jang'ombe (Unguja )
6.Kiembesamaki (Unguja )
7.Tanzania Adventist ( Arusha )
8.Al-Ihsan Girls ( Unguja )
9.Azania (Dar es salaam )
10: Lumumba (Unguja)
==>Shule 10 za Mwisho Kitaifa
1.Mpendae (Unguja)
2.Ben bella ( Unguja)
3.Tumekuja (Unguja)
4.Green Bird Boys (Kilimanjaro)
5.Jang'ombe (Unguja )
6.Kiembesamaki (Unguja )
7.Tanzania Adventist ( Arusha )
8.Al-Ihsan Girls ( Unguja )
9.Azania (Dar es salaam )
10: Lumumba (Unguja)
MPYA:ANGALIA HAPA MADARAJA YALIYOTUMIKA KUPANGA MATOKEO KIDATO CHA SITA 2016
Kama kawaida yangu,ninakupa kitu roho yako inapenda,je ungependa kujua GRADE A,B,C,D,E,S,F ULIZOPATA NI SAWA NA MAKSI NGAPI HADI NGAPI?Basi angalia hapo chini kujua maksi zako;
KAMA BADO HUJAONA MATOKEO KIDATO CHA SITA NA UALIMU 2016 BONYEZA HAPO CHINI KUANGALIA
>>>>>>>>BONYEZA HAPA
KAMA BADO HUJAONA MATOKEO KIDATO CHA SITA NA UALIMU 2016 BONYEZA HAPO CHINI KUANGALIA
>>>>>>>>BONYEZA HAPA
BREAKING NEWS:HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2016,UALIMU DSEE 2016,UALIMU GATCE 2016
"MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2016","MATOKEO YA
FORM 6 2016","NECTA RESULTS FORM 6 2016","NECTA RESULTS KIDATO CHA SITA
2016","MATOKEO YA KIDATO CHA 6 2016","MATOKEO YA FORM SIX 2016","NECTA RESULTS
KIDATO CHA 6 2016"
HAYA HAPA MATOKEO YA UALIMU DSEE 2016,NA GATCE 2016
BONYEZA HAPA KUANGALIA MATOKEO YA UALIMU 2016
KWA DSEE BONYEZA HAPO>>>>>>>DSEE RESULTS 2016
KWA GATCE BONYEZA HAPO>>>>>GATCE RESULTS 2016
Pingamizi la Tundu Lissu Kutaka Afutiwe Kesi ya Uchochezi Lagonga Mwamba
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya Mbunge
wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) ya kufutiwa mashitaka ya
uchochezi yanayomkabili na wenzake watatu.
Hakimu
Mkazi Mkuu, Emillius Mchauru alitoa uamuzi huo jana baada ya kukubali
pingamizi lililowasilishwa na upande wa Jamhuri waliodai mashitaka hayo
yasifutwe kwa kuwa hati ya mashitaka haina makosa.
Mbali
ya Lissu, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni mwandishi wa gazeti
la Mawio, Jabir Idrissa, Mhariri wa gazeti hilo, Simon Mkina na
Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob. Hata hivyo, uamuzi huo
ulitolewa jana bila Lissu kufika mahakamani hapo kwa kuwa anaumwa.
Akiieleza
mahakama, Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alidai Lissu ameshindwa
kufika mahakamani kwa kuwa anaumwa, lakini wadhamini wake akiwemo
Ibrahim Ahmed wamefika mahakamani na kueleza kuwa Lissu anaumwa malaria.
Aidha, ilielezwa kuwa mshtakiwa Idrissa anaumwa na yupo Zanzibar kwa
ajili ya matibabu.
Katika
maombi yao, washitakiwa kupitia kwa Wakili Kibatala waliiomba mahakama
ifute mashitaka hayo kwa kuwa hati ya mashitaka imekosewa kwa
kutokueleza makosa hayo wametenda wapi na pia mahakama hiyo haina
mamlaka ya kusikiliza masuala yanayohusu Zanzibar.
Akisoma
uamuzi, Hakimu Simba alisema baada ya mahakama kupitia hoja za pande
zote mbili katika kesi hiyo imejiridhisha kuwa hati ya mashitaka haina
makosa.
Aidha,
alisema mahakama hiyo ina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo kwa kuwa
makosa yaliyofanyika yanahusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hivi
karibuni, mahakama ilifuta mashitaka mawili ya uchochezi kati ya matano
yanayowakabili washitakiwa hao, baada ya upande wa jamhuri kuyaondoa
katika hati kwa kuwa hayana kibali cha Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).
Katika
mashitaka yao inadaiwa Januari 12 hadi 14, 2016, Dar es Salaam
washitakiwa walichapisha taarifa ya uchochezi yenye kichwa cha habari ‘
Machafuko yaja Zanzibar’.
Pia
inadaiwa Januari 14, 2016 Dar es Salaam walichapisha habari hizo ili
kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar. Inaendelea kudaiwa siku hiyo
hiyo, Lissu na wenzake bila ya kuwa na mamlaka yoyote yale waliwatisha
na kuwatia hofu wananchi wa Zanzibar ili wasikubali kuingia kwenye
marudio ya Uchaguzi Mkuu.
Rais Magufuli Afufua Safari ya Kuhamia Dodoma Kwa Kuwapeleka Mashujaa Dodoma
RAIS
John Magufuli ameonesha nia ya kuhamia Dodoma kwa kuanza kushughulikia
masuala muhimu, ikiwamo ya kuzindua awamu ya kwanza ya upanuzi wa Uwanja
wa Ndege wa Dodoma na kuhamishia maadhimisho ya Siku ya Mashujaa mkoani
Dodoma.
Akizungumza
juzi wakati wa mkutano wa kitaifa wa amani ulioandaliwa na Jumuiya ya
Ahamadiyya, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema katika
kuonesha dhamira ya kuhamia Dodoma ambao ulitangazwa kuwa Makao Makuu ya
Tanzania miaka ya 1970, Rais alielekeza fedha zilizobaki kwenye bajeti
iliyopita zitumike kwa ajili ya upanuzi wa uwanja wa ndege ambao pia
ujenzi wake utazinduliwa na Rais mwenyewe Julai 22, mwaka huu.
Aidha,
Rugimbana alisema Rais Magufuli pia ameagiza maadhimisho ya Siku ya
Mashujaa mwaka huu yahamie Dodoma ambapo kwa miaka mingi sasa yamekuwa
ikifanyika kwenye Viwanja vya Mashujaa, Mnazi Mmoja Dar es Salaam.
“Ndio
natoka kwenye kikao cha kuzungumzia maadhimisho hayo kufanyika Dodoma
hilo linadhihirisha wazi dhamira ya Rais kuhamia Dodoma,” alisema
Rugimbana na kuongeza kuwa Rais Magufuli atashiriki Mkutano Mkuu Maalumu
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) utakaoanza Julai 23, mwaka huu.
Akizungumzia
suala la amani, mkuu huyo wa mkoa alisema serikali itawachukulia hatua
kali viongozi wa taasisi mbalimbali ambao wamekuwa na tabia za kutumia
nafasi zao kuhubiri uchochezi na hivyo kutishia amani na utulivu wa
nchi.
Alisema
viongozi ambao wamekuwa na tabia za kutumia taasisi zao kama sehemu ya
kuhubiri masuala ya uovu, ikiwemo kushawishi vitendo vya uvunjifu wa
amani, serikali haitawafumbia macho.
Aliwataka
viongozi wa dini nchini kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa Katiba za
taasisi zao na siyo kufanya mambo kwa maslahi yao binafsi na tamaa.
Alisema pia serikali inaunga mkono jitihada za taasisi za dini katika
kuhubiri amani na utulivu wa nchi ambazo zimekuwa zikifanywa na viongozi
mbalimbali.
“Kama
serikali, tunaunga makono jitihada zenu mbalimbali ikiwemo kupinga
vitendo vya maovu pamoja na ufisadi ambao umekuwa ukilitafuna taifa
letu,” alisema.
Naye
Mwakilishi wa Jumuiya hiyo ya Ahmadiyya, Abdulrahman Ahmed akitoa mada
kuhusu amani, alisema Waislamu wanatakiwa kuzingatia miiko ambayo
imewekwa na dini hiyo katika kusaidia kudumisha amani na utulivu.
Wakati
huo huo, mapema wiki hii Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Profesa Makame Mbarawa alisema serikali inakarabati na kuongeza ukubwa
wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma ili upokee ndege kubwa za mizigo, abiria na
viongozi wa kitaifa na kimataifa, ikiwa ni maandalizi ya kuufanya mkoa
kuwa makao makuu ya nchi kivitendo.
Ujenzi
huo unatarajia kugharimu kiasi cha Sh bilioni 11.5 ambazo ni fedha za
ndani na utakamilika kwa muda mfupi ili kutoa fursa kwa mashirika ya
ndege kuanza huduma mkoani Dodoma, ikiwemo ndege kubwa zitakazonunuliwa
na serikali mwaka huu.
Profesa
Mbarawa akizungumza baada ya kukagua uwanja huo alisema uamuzi huo
unafikiwa kutokana na Serikali ya Awamu ya Tano kutaka kuufanya Dodoma
makao makuu ya nchi kivitendo, jambo linalotarajiwa kuongezeka shughuli
mbalimbali zikiwemo za kiutawala, uchumi, biashara na diplomasia
sambamba idadi ya wageni.
Kwa
upande wake, Meneja Mradi wa Upanuzi wa uwanja huo kutoka Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mbila Mdemu alisema mpaka sasa mita
900 zimekamilika kwa kuweka tabaka la kwanza lami katika eneo la kuruka
na kutua ndege na kazi ya kuchimba na kusawazisha eneo la kurefusha njia
imekamilika.
Alisema
wanatarajia kukamilisha kazi hiyo kwa muda mfupi. Upanuzi wa uwanja huo
unahusisha njia ya kuruka na kutua kwa ndege yenye urefu wa Km 2.5 na
mita 500 za taa za kuongozea ndege na usalama wa kuruka kwa ndege.
source:habari leo
source:habari leo
Nyaraka Feki za Serikali Zazagaa Kila Kona,Mpigachapa, Polisi Watoa Onyo kwa Wanaozimiliki
MPIGACHAPA
Mkuu wa Serikali, Cassian Chibogoyo amekiri kuwepo kwa nyaraka bandia
za serikali katika sekta mbalimbali, nyingi zikiwa za ukusanyaji wa
mapato ya serikali, vyeti vya kitaaluma, ndoa na nyinginezo.
Kutokana
na hali hiyo, amewaasa wananchi wanaofanya shughuli hizo za kutengeneza
nyaraka hizo bandia ambazo ni hatari kwa usalama wa nchi, kuacha kwani
wanaendesha oparesheni ya kudumu itakayowabaini na kuchukuliwa hatua
kali, ikiwemo kifungo cha miaka 20 jela.
Hivyo
amewataka watendaji na wasimamizi katika idara mbalimbali kufanya
uhakiki upya wa nyaraka za serikali, kwani zimezagaa sehemu mbalimbali
nchini hususan katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), vyuoni na katika
maeneo ya kazi.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Mpigachapa Mkuu Chibogoyo alisema nyaraka hizo
bandia ni pamoja na stakabadhi za malipo, vibali mbalimbali, hati za
makontena, leseni za magari pamoja na bima.
Alisema
katika oparesheni iliyofanyika mwaka jana ya ‘Okoa Pato la Taifa‘
katika kutafuta nyaraka bandia za serikali, walibaini kuwepo kwa nyaraka
za vyeti vya ukaazi au kuzaliwa vinavyomilikiwa na raia wa kigeni,
stakabadhi za mapato, leseni za biashara, vyeti bandia vya kitaaluma na
vinginevyo.
Alisema
nyaraka hizo walizikuta katika vituo vyao vya mauzo na wengine kwenye
nyumba zao za kutengenezea uhalifu huo na kubaini kuwa uhalifu huo ni
zaidi ya ujambazi kutokana na madhara yake kwa nchi.
Alisema
katika oparesheni hiyo walibaini kiwanda cha kutengeneza bidhaa hizo
maeneo ya Buguruni katika Manispaa ya llala, Dar es Salaam pamoja na
vyeti feki vya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU), vitambulisho vya ukaazi
ambako kuna raia wa kigeni amepewa cha ukazi akiishi Kariakoo, risiti za
usalama barabarani pamoja na shahada za ndoa za Kanisa Katoliki la
Mtakatifu Maria Magomeni jijini Dar es Salaam.
Alisema
pia walikamata boksi tatu za stika za bima zinazowekwa kwenye magari
zikiwa tayari kusafirishwa kwenda mkoani Tanga zikiwa zimewekwa kwenye
jokofu bovu lililochakaa karibu na mama ntilie katika maeneo ya
Salamander.
“Wananchi
wasio waaminifu wanaotaka kupoteza maisha ya wananchi wema na usalama
wa nchi ikiwemo kurudisha nyuma maendeleo na uchumi wa nchi, nawapa
salamu zangu kuwa mimi na timu yangu tumejipanga kutokomeza vitendo
hivyo na tutapigania nchi,” alisema Chibogoyo.
Alieleza
kuwa makatazo ya udhibiti wa nyaraka yapo katika Sheria ya Makosa ya
Jinai, Sheria ya Ngao ya Taifa, Sheria ya Ushahidi na Sheria ya Usalama
wa Taifa, hivyo ukikamatwa na katatasi inayokusudia kutumika kwa
udanganyifu, adhabu ni kufungwa miaka saba.
Aidha,
alifafanua kuwa Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1970 inakataza kuwa
na nyaraka, mihuri, karatasi maalumu na kumiliki taarifa za serikali
isivyo halali na sheria inasema kuwa ni mhalifu na adhabu yake ni miaka
20 jela.
Chibogoyo
aliwataka wananchi wema kutoa taarifa pale wanapowabaini watu hao
wanaotengeneza nyaraka bandia za serikali pale wanapohitaji nyaraka hizo
kwa haraka na ofisi yake itampatia nyaraka halali kwa haraka.
Akizungumzia
nyaraka hizo bandia za serikali, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam, Kamishna Simon Sirro alisema hali ya nyaraka hizo inatisha kwani
ni kubwa kwani nyaraka hizo zote muhimu zipo na zinatumika katika
maeneo mbalimbali.
Kamanda
Sirro alisema kuna watu wamenufaika kwa nyaraka hizo kama vyeti
kutumika kupata ajira hivyo watafuatilia na watawachukulia hata za
kisheria wanufaika wote wa nyaraka hizo bandia.
Alisema
katika oparesheni waliyoshirikiana na Mpigachapa Mkuu wa Serikali
walikamata watu watatu ambao inaonekaan ndiyo mabosi au wakurugenzi wa
kutengeneza nyaraka hizo huku wakiwa na mawakala wao katika mikoa
mbalimbali kama Mwanza na kwingineko.
Alisema wataendelea kufanya oparesheni ili kuhakikisha suala hilo linakoma kwa kuwakamata wahusika wote.
Picha ya Rais Zuma wa Afrika Kusini akimbusu msichana huyu yawa gumzo
Picha ya msichana akimbusu Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma imezua utata nchini humo.
Picha
hizo zilisambaa Jumatano hii baada ya msichana huyo kuziweka kwenye
mitandao ya kijamii. “We will check the matter,” alisema msemaji wa
serikali Bongani Ngqulunga alipoulizwa kuhusu picha hizo.
Msichana
huyo mwenye miaka 19 anaitwa Lindokuhle Dlamini. Kwenye picha hizo
aliandika: He is not just a blesser, we are inlove and I am grateful for
all that he has done for me, much love. Xo xo.”
Blesser inamaanisha ni mtu mzima anayehonga wasichana na kuwa na uhusiano nao. Akaunti yake ya Facebook imefutwa.
Hata
hivyo mtoto wa kiume wa rais huyo, Edward amedai kuwa msichana huyo ni
dada yake na kwamba akaunti iliyopost picha hizo ni feki. Baadhi ya
magazeti likiwemo Citizen‚ yamesema yaliambiwa na wasomaji wake kuwa ni
kweli binti huyo ni mtoto wa Zuma.
Hata
hivyo Makamu wa Rais wa Economic Freedom Fighters Floyd Shivambu
alikosoa kwa kutweet: Okay cool? What kind of Grand Fathers and Fathers
kiss their Grand Daughters & Daughters like this? Perverts??”
Serikali bado haijatoa majibu kama ilivyoahidi.
Picha 5 za Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe Alivyofunga ndoa jana Zanzibar
Thursday, 14 July 2016
Video MPYA: Joh Makini FT Chidinma -Perfect Combo
AUDIO: Mbwa adaiwa kuzaa nguruwe Iringa
Yawezekana
kabisa kuna matukio umeshawahi kuyasikia au hata kuyashuhuduia mwenyewe
na yakakushangaza, basi hii pia liongezee kwenye hayo mengine, Hili ni
tukio lililopata airtime kwenye Hekaheka ya Clouds fm leo July 14 2016.
Mbwa
mmoja Iringa amezaa mnyama aina ya Nguruwe, akielezea tukio hilo mwenye
mbwa amesema waligundua kwamba mbwa huyo amezaa ngurume tangu juzi,
baada ya mume na watoto wake kumjulisha hali hiyo na mara baada ya
kushuhudia tukio hilo alitoa taarifa kwa uongozi wa mtaa huo pamoja na
majirani huku akionesha kushtushwa na tukio hilo.
Daktari
wa mifugo, Anthony Mwangolombe mara baada ya kupata taarifa kuhusu
suala hilo walifika eneo la tukio na amesema kuwa jambo hilo hajawahi
kuliona likitokea kwa mbwa.
>> >>>>DOWNLOAD HAPA AUDIO
>> >>>>DOWNLOAD HAPA AUDIO