Sunday, 3 July 2016
Friday, 1 July 2016
Mtumishi wa umma atakayekwenda kusomea 'first degree' sasa kuchukua likizo isiyo na malipo
Mtumishi atakayekwenda kusomea FIRST DEGREE anatakiwa achukue LIKIZO
ISIYO NA MALIPO na hastahili kulipwa chochote na Mwajiri wake ikiwa ni
pamoja na kutolipwa Mshahara kwakuwa HAYUPO KAZINI.
Hakuna malipo yoyote ya UHAMISHO kwa Mtumishi atakayehamishwa umbali usiozidi kilometa 10.
Hakuna malipo yoyote ya UHAMISHO kwa Mtumishi atakayehamishwa umbali usiozidi kilometa 10.
MPYA: Serikali imezuia Benki kupandisha viwango vya tozo katika miamala yake
TRA wamesema taasisi za fedha wanapoongeza makato ya miamala ya fedha wanakosea kwa kupandishia wananchi kwa kuwa sheria hiyo inahusu fedha ambayo mwanachi alikuwa anakatwa na taasisi hizo ambayo hapo mwanzoni zilikuwa azilipiwi kodi kwa hiyo hizo ndizo zitakazokatwa 18%.
Mfano kama umetoa fedha ukakatwa 1000 na taasisi ya fedha ilikuwa haikatwi kodi lakini kwa sheria hiyo ada hiyo ndio itakatwa 18% na sio mwananchi kuongezewa makato kama ilivyofanyika kwa baadhi ya taasisi za fedha.
PICHA :Ajali Ya basi iliyotokea Mkoani Morogoro -imeua 11
Habari iliyoripotiwa hivi punde na kituo cha ITV ni kuhusu ajali ambayo imetokea eneo la Veta Dakawa mkoani Morogoro ikihusisha magari matatu ambayo ni lori la mafuta, kontena lililobeba mchele pamoja na basi.
Taarifa hiyo inasema kuwa watu 11 wamefariki dunia na wengine ambao idadi yao bado haijajulikana wamejeruhiwa.
Tunaendelea kufuatilia taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo.
Waziri Mkuu: Serikali Itatoa Waraka Juu Ya Ukusanyaji Mapato Kupitia Mawakala
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Halmashauri zitaelekezwa kwa waraka ni
vyanzo vipi vitahitaji kutumia wawakala wa ukusanyaji mapato kwani siyo
kila chanzo cha mapato ya Halmashauri kitakusanywa kwa ufanisi kwa
kutumia au kwa kutotumia mawakala.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo jana mchana (Alhamisi, Juni 30, 2016) wakati
akitoa hoja ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Alisema
katika ukusanyaji wa mapato, baadhi ya vyanzo vitapaswa kukusanywa na
Halmashauri zenyewe kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na Serikali.
“Moja
ya miongozo hiyo ni kwamba kuanzia sasa, iwe kwa kutumia mawakala au
Halmashauri zenyewe ni lazima fedha zinazokusanywa ziwekwe kwenye
akaunti ya Halmashauri na kutumia mifumo ya kielektroniki ili kupunguza
au kumaliza kabisa masuala ya kutumia malipo kwa fedha taslimu (cash
transactions),” alisema.
Alisema
katika kutekeleza agizo hilo, Halmashauri itabidi zikubaliane na wakala
ni kiasi gani cha asilimia ya makusanyo kitalipwa kwa wakala na malipo
yafanyike baada ya kukusanya na kuingizwa kwenye akaunti ya Halmashauri.
Alisema
Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura ya 290, inazipa uwezo Mamlaka
za Serikali za Serikali za Mitaa kutoza na kukusanya kodi, ushuru na
ada mbalimbali kama vyanzo vya mapato vya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
“Sheria
hiyo pia inazipa mamlaka hizo kuteua mawakala wa kukusanya mapato hayo
kwa niaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia sheria, kanuni
na taratibu. Lakini Serikali imebaini changamoto za kiufundi katika
kufanya tathmini ya vyanzo vya mapato; ugumu katika kupata mawakala
wenye weledi katika ukusanyaji mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato,
na wakati mwingine watumishi wenyewe kujipa uwakala kinyume na taratibu
zinazomzuia mtumishi kufanya biashara na taasisi yake,” alisema.
Alisema
hatua ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia mawakala ni miongoni mwa
mikakati ya kuboresha ukusanyaji mapato na pia kutoa muda mwingi zaidi
kwa watumishi wa mamlaka hizo kushughulika na majukumu ya msingi ya
Halmashauri na hasa utoaji wa huduma kwa wananchi na usimamizi wa miradi
ya maendeleo.
“Pamoja
na dhamira nzuri ya hatua hizo, tunayo mifano ya baadhi ya Halmashauri
kama vile Nzega ambayo baadhi ya wahusika wameshinikiza wakitaka zabuni
zote wapewe madiwani. Jambo hili halikubaliki na tena ni kinyume cha
maadili ya utumishi,” alisisitiza.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zote nchini kwamba
kuanzia Julai Mosi, 2016 zihakikishe zinatumia mifumo ya kielektroniki
katika kukusanya mapato, katika kulipa, kuweka na kutekeleza kikamilifu
mikakati madhubuti ya kuboresha makusanyo iwe yanakusanywa na
Halmashauri au na wakala.
Alisema
Mamlaka za Serikali za Mitaa zina wajibu wa kutoa taarifa kwa wananchi
kuhusu mapato na matumizi ya Serikali pamoja na michango ya wananchi
licha ya kuwa uzoefu unaonesha kuwa mamlaka hizo zina tatizo la kukaa na
fedha kwa muda mrefu kabla ya kuzielekeza kwenye matumizi
yaliyokusudiwa.
“Kuchelewesha
kutoa fedha zilizotengwa kwa shughuli zilizopangwa ni kuchelewesha
kufikisha huduma muhimu kwa wananchi. Napenda kuhimiza uzingatiaji wa
utaratibu wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu mapato na matumizi ya
fedha za Serikali katika ngazi zote ili kuongeza uwazi na uwajibikaji
katika sekta ya umma,” aliongeza.
Mkutano
huo wa tatu wa Bunge ulioanza Aprili 19, 2016 ulikuwa mahsusi kwa ajili
ya kujadili na kupitisha bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano
pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Bunge limeahirishwa hadi Septemba 6, mwaka huu litakapokutana tena mjini
Dodoma.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S.L. P. 980,
DODOMA.
ALHAMISI, JUNI 30, 2016