UTANGULIZI
Ndugu Waandishi wa habari, Karibuni kwenye mkutano huu mfupi ambao lengo
lake ni kutoa taarifa yetu fupi kuhusu ukweli uliojificha kuhusu
kitendo kilichopelekea Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi
wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga.
Tunaamini kwa uwezo mliona kama waandishi wa habari, taarifa hii itafikia umma wa Watanzania kama ilivyokusudiwa.
UFAFANUZI
Kama mnakumbuka mnamo tarehe 20 Mei mwaka huu, Rais Dk John Pombe
Magufuli alichukuwa uamuzi wa kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya
Ndani, Charles Kitwanga ambaye pia ni Mbunge wa Misungwi kwa kosa la
kwamba Mhe. Kitwanga aliingia bungeni akiwa amelewa.
Sisi wananchi wa Jimbo la Misungwi tumesikitishwa sana na taarifa na
uamuzi huu kwa kuwa tunaamini kuwa kuna dhamira iliyojifika iliyopelekea
Mhe Rais kufanya maamuzi haya. Ukweli ni kwamba huu ulikuwa mpango
wenye dhamira ovu na uliogubikwa na uongo mwingi ukilenga kumchonganisha
Mbunge wetu na Mhe. Raisi uliopangwa na waovu wachache ambao wamebanwa
na Serikali hii ya Awamu ya tano kupitia wizara hiyo nyeti kwa usalama
wa nchi.
Itakumbukwa kuwa, Mhe Charles kitwanga alinadiwa na Mhe Rais na wanaCCM
na baadae kupigiwa kura kwa wingi na wananchi wa Misungwi kwa ajili ya
uwezo wake na dhamira yake njema ya kulinda taifa letu. Sisi wananchi
wake, tunaamini katika uwexo wake, uadilifu wake na nidhamu ya kazi
aliyonayo, hatuna mashaka na hili.
Baada ya kuteuliwa na Mhe Raisi kama Waziri wa mambo ya ndani, amekuwa
muadilifu na kafanya mengi katika kuimarisha usalama na kufanya maamuzi
yengi mazuri kwa maslahi ya taifa. Hili lilimtengenezea maadui wengi
ndani ya serikali, ndani na nje ya CCM, mtandao wa dawa za kulevya,
walioachishwa kazi NIDA na Uhamiaji. Watu hawa ndio waliochochea na
kutengeneza mkakati wa kumchafua Mhe Kitwanga na walikuja dodoma
kuhakikisha dhamira yao ovu inatimia.
USHAHIDI WETU
Miongoni mwetu tulikuwa mjini Dodoma pamoja na madiwani wa Jimbo la
Misungwi ambao tulikwenda kumtembelea Mbunge wetu bungeni, tulizungumza
mengi kwa ajli ya jimbo letu na katika kikao chetu hapakuwa na chembe ya
kilevi chochote na hata kesho yake alipoinga bungeni alikuwa mzima wa
afya ya kimwili na akili timamu na tunawahakikishieni kuwa Kitwanga
hakuwa amelewa.
Ndugu waandishi wa habari asubuhi ya tarehe 20 tulielekea bungeni kwa
mwaliko wa Charles Kitwanga, tukiwa sehemu ya mualiko uliowajumuisha
Madiwani wa jimbo lake tukiwa tumeambatana naye tukaingia ndani ya
ukumbi wa bunge,tukashuhudia anajibu swali,baada ya kujibu swali la
mbunge Sakaya,tulitoka nje na kupiga picha na madiwani wote wa Misungwi
waliokuja kumtembelea Dodoma.
Baada ya zoezi la kupiga picha kukamilika pale nje ya ukumbi wa Bunge,
tulitoka na kuelekea Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa lengo la
kututembeza maeneo yote ya Dodoma , lakini ilipofika jioni wakati
tukirejea nyumbani tukiwa naye, ghafla tukaona habari zikisambazwa
kwenye mitandao ya kijamii kuwa Waziri Kitwanga amevuliwa uongozi kwa
kuwa alionekana na Waziri Mkuu akiwa amelewa.
Ndugu wanahabari , tulishangazwa wote kwani tulikuwa tumekaa naye pale
nyumbani kwake Dodoma (site 2) tukipata chakula cha usiku ,alionekana
kutoaamini na hata madiwani pia na wengine ambao tulikuwepo hapa
nyumbani kwake hatukuamini.
Tunachosema ni kwamba waziri Kitwanga hakulewa kama ambavyo imepotoshwa,
bali alikuwa ni mkakati wa kumchafua na kuhakikisha andavuliwa wadhifa
wake ili watu hawa waendelee kufanya maovu yao. Mtandao wa dawa za
kulevya, pamoja na wale waliokuwa wanamshutumu kwamba amehusika
kuondolewa kwao kazini wakiwemo Watu wa NIDA, Mbunge wa Jimbo la
Chalinze, Ridhiwani Kikwete, Mfanyabiashara Said Lugumi pamoja na kundi
mafisadi waliokwapua mabilioni ya fedha NSSF. Pia na baadhi ya wabunge
wa CCM na Upinzani ambao walikuwa hawafurahishwi na kasi ya utendaji
kazi wa Kitwanga katika Wizara ya Mambo ya ndani.
Kwa niaba ya wananchi wenzetu tunamuomba na kumtahadharisha Mhe. Rais
awe makini na makundi la wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, pamoja na
lile kundi la wanamtandao masalia ndani ya CCM na serikalini na kwenye
vyombo nyeti vya ulinzi na usalama, ambayo kwa ujumla yalikuwa na
mkakati kabambe wa kuhakikisha wanamtenganisha na kumpotosha Mhe Raisin a
kumjaza habari zisizo za kweli.
Ndugu waandishi wa habari, kilichotushangaza zaidi baada tu ya Kitwanga
kuvuliwa madaraka yake ya uwaziri, kuna watu walianza kufanya sherehe
wakishangilia hususani wale waliovuliwa madaraka NIDA pamoja na
NSSF,Uhamiaji na wale wanaotuhumiwa kuhusika na madawa ya kulevya.
Ndugu waandishi wa habari, tunajua namna kundi la Said Lugumi, Ridhiwani
Kikwete na kampuni yao walivyokuwa wanadhamini kwa mbinu za kifedha
katika vita hii ya kitwanga ili aondolewe, lakini baada ya kuondolewa,
wakajifanya kutoa taarifa ya kushangazwa kuondolewa kwake, Kitwanga
amekuwa mtumishi wa serikali akiwa mtumishi mwandamizi benki kuu
Tanzania (BOT),amekuwa mbunge na Naibu waziri kwa miaka 10,lakini hata
siku moja hakuwahi kuonekana amelewa.
Ni muadilifu na ana nidhamu ya kazi, na nidhamu hii ndiyo iliyomfanya aaminiwe na kupewa dhamana hii.
MAAZIMIO YETU
=Tunaliomba Bunge kumuomba radhi Mhe. Charles Kitwanga kwa kumdharirisha
mbele ya wapiga kura wake wa Jimbo la Misungwi familia yake pamoja na
watanzania wote waliokuwa wanaamini utendaji wake kupitia video
iliyochezewa na wataalamu wa IT katika studio za Bunge ili kufanikisha
lengo la kumuonyesha Kitwanga kuwa alikuwa amelewa bungeni.
=Tunamuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye ndiye Kiongozi Mkuu wa
Serikali bungeni atoe uthibitisho wa kikemia unaotanabaisha wazi kama
Kitwanga alikuwa katumia kilevi wakati akiwa bungeni maana hakuna kipimo
chochote kilichofanyika kudhibitisha uvumi huu.
=Tunaliomba Bunge lifanye uchunguzi na kubaini wale wote walisambaza ile
video inayoonyesha Kitwanga akiwa anaongea na kuonekana amelewa wakati
kiuhalisia hakulewa na alijibu maswali yote vizuri
=Tunaliomba Bunge kuchunguza idara ya habari ya Bunge pamoja na studio
ile ya Bunge ambao wamehusika na kuhariri ile picha ya video iliyokuwa
inasambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
=Tunahoji uhalali wa kumvua mtu madaraka kwa sababu ya ulevi bila
uthibitisho wa daktari ambaye kisheria ndiye mwenye mamlaka hayo
kugundua kilevi cha mtu.
= Tunaomba Watanzania wote waliosikitishwa na taarifa hizi wajue tu
kwamba ile video ambayo imemtia hatiani Kitwanga ilihaririwa kwa ustadi
mkubwa kupitia wafanyakazi wa Bunge ambao wanapitia zile asadi za bunge
pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa serikali kwenye vyombo vya ulinzi na
usalama ambao hawakupenda kitwanga aendelee kuwa pale ,kwa nia ya
kumhujumu na sasa wanasema kwenye vyombo vya habari ili kuhalalisha
uhujumu huo.
=Tunaomba mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuangalia picha
zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya Mhe Mbunge wa
Misungwi ambazo zinaonekana kumchafua wachukue hatua dhidi ya watu hao
kwani kisiasa zinaendelea kumchafua na kumharibia kwa wapigakura
wake,familia yake,mama yake mzazi ,ndugu zake .
=Tunajiandaa kuchukua hatua kwa Bunge za kisheria kama watashindwa
kuthibitisha tuhuma hizo dhidi ya Charles Kitwanga ambazo tunaamini
zimetengenezwa kwa maslahi ya makundi yanayompinga ndani ya Serikali
wakiwemo mtandao wa dawa za kulevya.
Pia tunamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa makini kundi
la wanamtandao walio ndani ya serikali ambalo linaongozwa wahafidhina
wasio taka mabadiliko ndani ya serikali .
Imeandaliwa na madiwani wa Jimbo la Misungwi pamoja na wakereketwa wa jimbo hilo.
Baraka Kingamkono,Gaudency Tungaraza na IDDY Majumuisho.
WAKONGWE kwa zaidi ya miaka kumi
kunako Muziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes, Inspector Haroun, Nature na
wengine kibao, Mei 28, mwaka huu wanatarajiwa kulitikisa jukwaa la
Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Juma Nature
Akichonga na Showbiz, Meneja wa Dar
Live, Juma Mbizo alisema kuwa mbali na wakali hao, wengine watakaoliteka
jukwaa ni Afande Sele, Jafarai, Sister P, Suma G, Abby Skillz na
wengineo.
“Hii ni moja ya shoo za kibabe kuwahi
kutokea Dar Live pekee. Ambapo niwaambie tu tutakuwa na makundi kibao ya
wakongwe ambayo ni Joint Mob, Zig Zag Crew, Solid Ground Family, Mabaga
Fresh, Manzese Crew na mengineyo,” alisema Mbizo na kumalizia kuwa
kiingilio kitakuwa 7,000 tu getini.
STAA
wa Muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Chura’ juzikati akiwa kwenye
shoo iliyofanyika Masasi, Mtwara alijikuta katika wakati mgumu baada ya
kutaka kupigwa na mashabiki kisa kikiwa eti ni kutokuimba Wimbo wa Chura
ambao umefungiwa.
Kwa mujibu wa chanzo, tukio hilo
lilijiri mida ya usiku katika ukumbi mmoja maarufu uliopo Masasi ambapo
Snura alikuwa akifanya shoo hapo na alipotaka kumaliza, mashabiki
walimtaka amalize na Wimbo wa Chura ndipo kizaazaa kilipoanzia na kutaka
kumpiga.
Baada ya kunyaka ubuyu huo, Over Ze
Weekend lilimnyanyulia simu Snura ambaye simu yake iliita bila
kupokelewa lakini alipopigiwa meneja wake, Hemed Kavu ‘HK’ alipokea na
kukiri kutokea kwa tukio hilo.
“Siyo tukio moja tu, tulishaenda shoo
zaidi ya mbili tunakutana na dhahama hizi. Tatizo lililopo, Snura hawezi
kupafomu wimbo ule kwa kuwa ulizuiliwa kutokana na video yake. Ni muda
umepita video mpya imetengenezwa na kupelekwa bodi ya filamu kukaguliwa
lakini hawajatoa jibu lolote zaidi ya kuzungushwa tu, mara TCRA mara
Basata,” alisema HK.
Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT), limechagua vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita
kwa mwaka 2016, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo
ya JKT kwa Mujibu wa Sheria. Sanjari na uchaguzi
huo, JKT limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda
wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01 - 05
Juni 2016. Vijana waliochaguliwa,
wamepangiwa katika Kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora,
JKT Ruvu – Pwani, JKT Makutupora – Dodoma, JKT Mafinga – Iringa, JKT
Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga, JKT Bulombora, JKT
Kanembwa na JKT Mtabila – Kigoma. Aidha, wahitimu wenye
ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) wanatakiwa
kuripoti Kambi ya JKT RUVU, iliyopo Mlandizi mkoani Pwani, ambayo ina
miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo. JKT linawataka vijana
hao kuripoti makambini wakiwa na nguo za michezo kama vile ‘track suit’,
bukta, raba pamoja na nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa kwenye
makambi yenye baridi kama JKT Makutupora, JKT Mafinga, JKT Mlale, JKT
Kanembwa na JKT Mtabila.
Ali Kiba baada ya kusaini mkataba na Kampuni ya Sonny.
HUKU mashabiki wa Ali Saleh Kiba
wakifurahia mafanikio ya msanii huyo kutokana na kulamba shavu la
kusaini mkataba na kampuni ya kimataifa ya Sony Music pamoja na kupewa
‘coverage’ na jarida maarufu la Marekani la The Source, mashabiki wa
Diamond Platnumz nao meno nje!
Diamond na Ne-Yo
Hiyo imefuatia baada ya Diamond naye
kutangazwa hivi karibuni kuwania Tuzo za Black Entertainment Television
(BET 2016) kwa mara ya pili mfululizo akiwa katika Kipendele cha Best
International Act: Africa, akichuana na wakali wengine wakiwemo Wizkid,
Yemi Alade (Nigeria), AKA, Cassper Nyovest na Black Koffie wote wa
Afrika Kusini.
Mafanikio ya mastaa hao yanawapa nguvu wasanii wengi wanaochipukia na waliopo kwenye gemu kuamini kuwa inawezekana.
Aibu yake! Mwigizaji wa kitambo
Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amen-aswa akikata ulabu hadi akawa
‘bwii’ huku akiwa amevaa kivazi ambacho kilimuacha nusu utupu hivyo
kuibua minong’ono kwa waliomshuhudia.
Tukio hilo la aibu lilijiri wikiendi
iliyopita kwenye ‘pub’ moja iliyopo Kijitonyama, Dar ambapo paparazi
wetu, akiwa kwenye ‘patroo’ ya matukio alimshuhudia Kabula akiwa
ametinga kipensi kifupi kilichoacha sehemu kubwa ya maungo yake nyeti
zikiwa wazi.
Paparazi wetu alitonywa kuwa wakati
Kabula anatia timu mahali hapo, waliomshuhudia akishuka kwenye Bajaj
walishikwa na butwaa baada ya kumuona dada huyo mrefu akiwa nusu utupu
huku mwenyewe akiwa hajali.
“Jamani sasa ni aibu…ndiyo tunafahamu
kuwa Kabula ni msanii lakini siyo wa kutuvalia vivazi kama hivi huku
mtaani. Sasa hapo ana tofauti gani na mtu aliyekaa uchi? Tunamuomba
Mungu atuepushe na balaa hili la maadili ya watoto wetu,” alisikika mzee
mmoja aliyekuwepo hapo.
Wikienda lilipombana Kabula akiwa tilalila na kumuuliza kulikoni kuvaa nusu utupu, Kabula alidai kwamba aachwe afanye yake.
CCM
imesema kitendo cha Rais John Magufuli kumvua uwaziri Charles Kitwanga
kutokana na kuingia bungeni akiwa amelewa, kimedhihirisha kuwa bado kuna
baadhi ya watumishi wanaokiuka maadili ya utumishi wa umma, lakini
hakitachukua hatua kwa kuwa ameshaadhibiwa.
Msemaji
wa CCM, Christopher Ole Sendeka jana alisema kitendo cha Kitwanga
kuingia bungeni akiwa amelewa kimewapa fundisho na sasa wanajua kuwa
kuna baadhi ya watumishi waliopewa dhamana na chama hicho, lakini
wanakiuka miiko ya maadili ya utumishi wa umma, jambo ambalo ni kinyume
na taratibu zao.
Sendeka
alisema licha ya kwamba Rais Magufuli amechukua hatua juu ya hilo na
kutoa adhabu, CCM itaendelea kufuatilia kwa ukaribu mienendo ya
wanasiasa waliopewa dhamana na chama hicho.
“Hatutasita kuchukua hatua endapo tutabaini kuna kada anayekiuka maadili ya viongozi wa umma,” alisema Sendeka.
Alisema
CCM inampongeza Rais Magufuli kwa uamuzi aliochukua dhidi ya Kitwanga
kwa kuwa hatua hiyo imedhihirisha kauli aliyowahi kusema kwamba
hataangalia mtu usoni wala kujali kabila au dini, ikiwa mtu huyo
atakiuka miiko ya uongozi.
Kuhusu CCM kumuadhibu Kitwanga, Sendeka alisema adhabu aliyopewa na Rais inatosha. “Hukumu haitolewi mara mbili,” alisema Sendeka.
Kitwanga
ambaye anatajwa kwenye sakata la utekelezaji mbovu wa mkataba wa
kufunga vifaa vya kuchukua alama za vidole baina ya Jeshi la Polisi na
kampuni ya Lugumi Enterprises, alivuliwa ukuu wa wizara hiyo nyeti baada
ya kutinga ndani ya ukumbi wa Bunge Ijumaa asubuhi na kujibu maswali
akiwa amelewa.
Hadi
jana jioni, Rais Magufuli alikuwa bado hajajaza nafasi hiyo nyeti huku
wananchi wakibashiri jina la mrithi wa Kitwanga kwa kuangalia jinsi
marais waliopita walivyokuwa wakijaza nafasi kama wa kumpandisha naibu
waziri wa wizara hiyo au nyingine, kumteua mtu anayemfahamu, kubadilisha
mawaziri na kumrejesha aliyewahi kuwa waziri ama kuteua kutoka kwenye
kanda anayotoka aliyetimuliwa.
Mara
nyingi katika uteuzi wa mawaziri, viongozi wakuu wa nchi wamekuwa na
utaratibu wa kuwapandisha baadhi ya manaibu kuwa mawaziri, kuwapa
uwaziri wabunge ambao amewateua au kuteua waziri kutoka katika mkoa
ambao anatokea waziri aliyeondolewa.
Mara zote saba ambazo Rais mstaafu Jakaya Kikwete alifanya mabadiliko ya baraza la mawaziri alifuata utaratibu huo.
Alipomuondoa
aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna
Tibaijuka ambaye ni mbunge kutoka mkoa Kagera alimteua mbunge mwingine
kutoka mkoa huo, Charles Mwijage kuwa Naibu Waziri wa Nishati na
Madini.Kwa sasa Mwijage ni Waziri wa Viwanda na Biashara.
Utaratibu
huo unaweza kunufaisha wabunge sita wa majimbo yaliyopo mkoa wa Mwanza
ambao ni Chalres Tizeba (Buchosa), Mansoor Hirani (Kwimba), Kiswaga
Boniventura (Magu), Stanslaus Mabula (Nyamagana), William Ngeleja
(Sengerema) na Richard Ndassa (Sumve).
Mbali
na Kitwanga ambaye aliteuliwa kuwa waziri kutoka mkoa huo, Rais pia
alimteua mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula kuwa Naibu Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Iwapo
Rais atatumia utaratibu wa kupandisha naibu waziri kuwa waziri, neema
huenda ikamuangukia mbunge wa Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani, Mhandishi Hamad Masauni au naibu mawaziri kutoka wizara nyingine.
Katiba pia inampa Rais fursa ya kuteua wabunge 10 na tayari ameshatumia
nafasi sita.
Diamond
Platnumz anaingia kwenye headlines nyingine baada ya jana kufanya show
ya kukata na shoka katika JEMBEKA FESTIVAL iliyofanyika mjini Mwanza,
ambapo yeye pamoja na NE-YO walitambulisha nyimbo yao mpya ambayo inasemekana inayoitwa I WILL MARY YOU.
Hapana nimekuwekea kipande kifupi cha wimbo huo ambao waliutumbuiz
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY Chiza Dastan (31), anayesadikiwa kuwa
mwizi wa pikipiki amefariki dunia Hospitali Wilaya ya Bukombe akipewa
matibabu baada ya kupigwa na nyundo kichwani wakati akijaribu kupora
pikipiki. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,
Mponjoli Mwabulambo alisema tukio hilo lilitokea Mei 20 saa 4.00 usiku
nje ya Baa ya Geen View, Kata ya Katente wilayani Bukombe.
Mwabulambo alisema Chiza ambaye ni
mkazi wa Kilimahewa, alifariki dunia wakati akitibiwa baada ya kujaribu
kupora pikipiki ya Nassoro Tadeo aliyemkodi kutoka mjini Ushirombo
kwenda kwenye baa hiyo.
Alisema wakiwa nje ya baa, ghafla
mhalifu alianza kuongea na watu wasiojulikana kwenye simu, mwendesha
bodaboda alishtuka na kutaka kuondoka.
Mwabulambo alisema wakati akijaribu
kuondoka, Chiza alichomoa nyundo na kuanza kumshambulia mwendesha
bodaboda na kumjeruhi kichwani.
Baada ya mwendesha bodaboda kupigwa
nyundo kichwani, aliachia pikipiki na kuanza kupambana naye
akig’ang’ania nyundo huku akiomba msaada.
Chiza alipanda pikipiki ili aondoke lakini mwendesha bodaboda, alifanikiwa kumnyang’anya nyundo na kuanza kumshambulia.
“Chiza alipoona kipigo kimezidi
aliiachia pikipiki na kukimbia kusikojulikana, mwendesha pikipiki
alichukua mali yake kwenda polisi ili kuandikiwa PF3 kwa ajili ya kwenda
Hospitali ya Wilaya ya Bukombe kupatiwa matibabu,” alisema.
Mwabulambo alisema mwendesha bodaboda
kupewa PF na kwenda kutibiwa, akiwa hospitalini hapo alishtuka kuona
Chiza akifikishwa na wasamaria wema saa 8.00 usiku akiwa na jeraha kubwa
kichwani.
“Lakini kabla polisi hawajatoa PF3 walimhoji na kubaini kuwa, ndiye aliyejaribu kuiba pikipiki,” alisema Mwabulambo.
Hata hivyo, Mwabulambo ametoa wito kwa
waendesha bodaboda kuwa makini wanapokuwa kwenye shughuli zao, hasa
nyakati za usiku na kwamba wanapomhisi mtu watoe taarifa kituo chochote
cha polisi.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk Mahona
Kaji alisema majeruhi alipokelewa akiwa na hali mbaya kutokana na
kupondwa na kitu kizito kichwani, fuvu la kichwa lilionekana limepasuka.
Dk Kaji alisema walijitahidi kuokoa maisha yake lakini ikashindikana.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtaka Rais John
Magufuli kuweka siasa kando na kuomba ushauri kwa waziri mkuu wa zamani,
Edward Lowassa ili kutatua tatizo la kuadimika kwa sukari.
Kauli hiyo ilitolewa na naibu katibu mkuu wa Chadema, Salim Mwalimu
juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Moto wilayani Monduli
Mkoa wa Arusha ambako Lowassa alizungumza na wananchi kuwashukuru kwa
kumpigia kura na akatangaza mpango wa kuzunguka nchi nzima kwa lengo
hilo.
Tangu Rais atangaze kudhibiti uagizaji sukari kutoka nje na baadaye
Bodi ya Sukari kutangaza bei elekezi, bidhaa hiyo muhimu imepanda bei
kutoka Sh1,800 hadi kufikia Sh5,000 kwa kilo na kwa sasa imeadimika
madukani, wakati Serikali ikisaka wafanyabiashara inaowatuhumu kuwa
wameificha kwenye maghala kwa lengo la kuihujumu.
Akizungumza kabla ya kumruhusu Lowassa kuongea na wananchi hao, Mwalimu
alisema inaonekana tatizo la sukari linaelekea kuishinda Serikali na
hivyo inahitaji msaada wa ushauri. “Tatizo la sukari kalianzisha yeye mwenyewe Magufuli na sasa anashindwa kulitatua,” alisema Mwalimu na kuongeza: “Mtu pekee atakayemsaidia ni Lowassa. Huyu alijipanga na alijiandaa kuongoza nchi.” Mwalimu alisema Lowassa amevumilia mengi kwa kuwa amenyanyaswa, ameonewa na kusimangwa lakini hakujibu.
“Amepitia kipimo cha mwisho cha utu, ni cha mwisho. Walimuonea mchana
kweupe akavumilia. Walimsimanga mchana kweupe mpaka watoto wadogo
walikuwa wakimuona Lowassa kama vile saizi yao, akavumilia,” alisema
Mwalimu.
“Ninajua vijana waliumia, mzee. Lakini leo warudi nyuma wafikirie
maisha yao. Ni nani angetoka nyumbani kwa kauli moja ya Lowassa,
kumshika mtoto wake mkono kumpeleka shule kama Lowassa angeangalia
ushetani na kumuacha Mungu,” alisema akirejea kauli ya Lowassa kuwa
alikuwa akipigiwa simu na watu kumtaka atoe kauli baada ya matokeo ya
Uchaguzi Mkuu mwaka jana kutangazwa, lakini akaawaambia watulie.
Lowassa, ambaye aligombea urais kwa tiketi ya Chadema baada ya
kuenguliwa CCM, alishika nafasi ya pili kwenye mbio hizo akipata kura
milioni 6.07 idadi ambayo ni rekodi kwa mgombea wa upinzani tangu siasa
za ushindani zirejeshwe mwaka 1992. Magufuli aliibuka mshindi kwa kupata
kura milioni 8.8.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Lowassa aliwataka wananchi kuendelea
kutulia, akisema mwaka 2020 hauko mbali na Chadema inaendelea kujipanga
upya ili kuhakikisha inashika dola na kuondoa kero zao.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa Chadema
kutoka makao makuu, mkoa pamoja na makada waliojiunga wakitokea CCM wa
wilaya ya Monduli, Lowassa alisema wafuasi wa ukawa wajiandae kwa
mikutano hiyo.
Huku akishangiliwa na wananchi hao waliokuwa wakimkatisha kwa kelele za
shangwe, Lowassa alisema kwa kushirikiana na viongozi wenzake
wamejipanga kufanya ziara ya kuijenga Chadema nchi nzima.
“Nina hakika tumewashika pabaya CCM na tumewaumiza sana. Sasa kwa
kushirikiana na viongozi wenzangu tutazunguka nchi nzima tunataka
kuiweka Chadema kwenye chama cha siasa na si uanaharakati,” alisema.
Akizungumzia Uchaguzi Mkuu uliomalizika Oktoba 25 mwaka jana, Lowassa
aliwashukuru wananchi kwa kumpa kura nyingi akisema hata walioiba kura
zake wanajua na dunia inajua kuwa alishinda.
“Niliamua kukaa kimya kwani najua ningesema jambo moja nchi yetu
ingeangamia. Na vijana kila kona ya nchi walikuwa wakinipigia simu
wakidai wanasubiri neno kutoka kwangu,” alisema.
“Sikufurahishwa na kwenda Ikulu kwa mikono iliyojaa damu. Kuna siku
nitakwenda Ikulu kwa mikono safi ya Watanzania, nina hakika na rafiki
zetu wanajua kabisa kwamba hawakushinda.”