Thursday, 7 April 2016

Serikali yabaini watumishi hewa 1855 nchini

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Serikali yabaini watumishi hewa 1855 nchini
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa George Simbachawene amewataka wakuu wa mikoa ambayo imekutwa na watumishi hewa kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi waliohusika kulipa na kupokea mishahara hewa.
Akizungumza na wakuu hao wa mikoa mara baada ya kukabidhiwa ripoti hizo, Waziri Simbachawene aliwataka viongozi hao kuhakikisha kuwa wanawakamata watumishi hao kwa makosa waliyobainika nayo na hatua stahiki.
"Wananchi wanataka kusikia hawa waliokuwa wanaiibia serikali wamechukuliwa hatua gani mara baada ya kutangazwa badala ya kuishia kuwatangaza kuwa ni watumishi hewa na wanalipwa mishahara," alisema.
Jumla ya watumishi hewa 1855 wamebainika kuwepo katika mikoa mbalimbali nchini huku mkoa wa Mwanza ukiwa na watumishi hewa 334, Arusha 270 na Sungida 202.
Mikoa ya Mwanza, Arusha na Singida inaongoza kwa kuwa na watumishi hewa wengi.
Kwa mujibu wa taarifa hizo kutoka kwa wakuu wa mikoa, watumishi waliobainika kuwa ni hewa ambao wamekuwa wakilipwa mishahara ni walimu na madaktari ambao ni marehemu na wastaafu.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Rais John Magufuli, kuwaagiza wakuu hao wa mikoa kuwasilisha ripoti ya watumishi hewa ambayo waliikabidhi kwa Simbachawene jana jijini Dar es Salaam kabla ya kuiwasilisha kwa Waziri wa Utumishi na kujumilisha na ripoti za sekta zote nchini na hatimaye kumfikishia Rais.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela alisema jumla ya watumishi hewa 334 walibainika kwenye mkoa huo hususani katika Halmashauri ya jiji la Mwanza ambalo lina watumishi hewa 72 pekee.
Katika mkoa wa Arusha jumla ya watumishi hewa 270 walibainika katika kipindi cha wiki mbili na kusababisha upotevu wa Sh. bilioni 1.188 kwa mwezi March pekee.
Katika mkoa wa Singida jumla ya watumishi hewa 202 walibainika na mkoa wa Kigoma wenye watumishi hewa 171 ambao wamesababisha hasara ya Sh. milioni 114.6 kwa mwezi.
Mikoa mingine ni Kilimanjaro wenye jumla ya watumishi hewa 111 ambao waliolipwa Sh. milioni 281.4 kwa mwezi mmoja na Dodoma watumishi hewa 101 waliolipwa Sh. bilioni 297 kwa muda wa miezi sita.
Pia katika mkoa wa Morogoro watumishi hewa waliobainika ni 122 ambao walilipwa Sh. milioni 450.79 kwa mwezi March pekee na mkoa wa Mara watumishi hewa 94 ambao walilipwa Sh. milioni 121.1 kwa mwezi mmoja.
Mkoa wa Mbeya ambao umeungana na mkoa mpya wa Songwe ulibainika kuwa na watumishi hewa 98 ambao walilipwa mishahara kiasi cha Sh. milioni 459.6.
Katika jiji la Dar es Salaam watumishi hewa waliobainika ni 73 ambao wamelipwa Sh. milioni 379 kwa mwezi mmoja.
Mikoa mingine ni mkoa wa Pwani uliobainika kuwa na watumishi hewa 150, Ruvuma watumishi hewa 37 ambao walilipwa Sh. milioni 58. 4, Njombe watumishi hewa 34 ambao walilipwa Sh. Milioni 20.107 na mkoa wa Rukwa wenye watumishi hewa 18 waliolipwa mishahara Sh. Milioni 55.64.
Watumishi wengine hewa walibainika katika mikoa ya Simiyu 33 ambao walilipwa Sh. Milioni 320.993 , Tabora jumla ya watumishi hewa 48 ambao walilipwa Sh. Milioni 118, Tanga watumishi hewa 24 na Lindi watumishi 57 waliolipwa Sh. Milioni 36.
Mikoa mingine ni Katavi wenye watumishi hewa 21 ambao walilipwa Sh. milioni 120 kwa miezi sita, kagera 14 ambao walilipwa Sh. milioni 49. 147 kwa mwezi, Geita wenye watumishi hewa nane na Manyara wenye watumishi hewa watano.
Aidha katika mkoa wa Shinyanga haukubainika kuwa na watumishi hewa kutokana na malengo waliyokuwa wamejiwekea tangu mwaka 2014, ikiwamo kukagua idadi ya watumishi walioko kazini na wanaotakiwa kulipwa mishahara kila mwezi.
Pia katika ripoti hizo walibainika watumishi watoro ambao walikuwa wakiendelea kulipwa mishahara licha ya kutokuwepo kazini kwa muda mrefu.
Katika mkoa wa Dodoma jumla ya watumishi watoro 38 walibainika, Iringa 145 na Kagera watumishi 248 ambao pia wanaendelea kuchunguzwa.
Mkoa wa Manyara jumla ya watumishi watoro 50, Mtwara watumishi 285 watoro, Mwanza watumishi watoro 205, Pwani watumishi watoro 50 , Rukwa watumishi watoro 139 na Simiyu watumishi watoro 62.
Mkoa wa Singida watumishi watoro 29 na Tanga jumla ya watumishi watoro 502.
Watumishi hao watoro ni wale walioacha kazi lakini wamekuwa wakiendelea kulipwa mishahara na wengine walio kwenye matatizo ya kiutumishi.
Share:

Waziri Simbachawene azipongeza halmashauri 10

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Waziri Simbachawene Azipongeza Halmashauri 10
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.George Simbachawene amezipongeza halmashauri 10 zilizofanya vizuri katika vigezo vya kutoa takwimu kwa usahihi, kupanga walimu katika shule zenye upungufu na kutuma ruzuku shuleni kwa wakati.
Aidha Waziri Simbachawene aliwataka wasimamizi wa mpango huo ambao umewekwa na serikali kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu nchini wahakikishe kuwa wanautekeleza kwa ufanisi wa hali ya juu ili uweze kufanikisha malengo yaliyo kusudiwa.
Akizungumza kwenye hafla maalum iliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa ajili ya kutoa motisha kwa halmashauri kumi bora zilizofanya vizuri Mhe.Simbachawene aliwataka viongozi wa Halmashauri 10 zilizofanya vizuri pamoja na halmashauri ambazo hazikufanya vizuri katika vigezo vilivyowekwa kujituma na kuhakikisha wanafanya kazi kwa ubunifu ili kuleta tija katika elimu nchini.
Aliongeza kuwa kuwa taifa linapaswa kujenga misingi imara ya elimu ya awali ili kuwa na wahitimu wa elimu ya juu ambao wameandaliwa vizuri na wanaoweza kukabiliana na changamoto za ajira za sasa.
Aliwataka kutekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa utakaoleta mabadiliko katika utoaji huduma na kufanya kazi kwa matokeo na kutekeleza malengo waliyojiwekea kwa wakati na kuzingatia viashiria vilivyoanishwa na kuvitekeleza ipasavyo.
Aidha, aliwakumbusha umuhimu wa kuweka takwimu na kutumia fedha zitakazoletwa kwa mujibu wa taratibu za serikali kwani huo ndio msingi wa kuleta tija katika maeneo yao ya kazi.
Halmashauri 10 kati ya 181 zilizopo nchini ambazo zimefanya vizuri katika vigezo vilivyowekwa na serikali ni halmashauri za Mbinga, Nkasi, Chato, Busega, Lushoto, Liwale, Sikonge, Mbarali, Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na Halmashauri ya Wilaya ya Tabora.
Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WATUMISHI WALIORUHUSIWA KUHAMA KUANZIA MWAKA 2012-2015

Share:

MATOKEO UEFA TAREHE 6.4.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 7.4.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Magazeti ya leo alhamisi april 7 2016
20160407_042520

20160407_042543
magazeti ya leo alhamis tarehe 7/4/2016
20160407_042559
20160407_042609
20160407_042836
20160407_042859
20160407_042624
20160407_042640
20160407_042650
20160407_042707
20160407_042723
20160407_042735
20160407_042747
20160407_042758
20160407_042913
20160407_042924
20160407_042937
20160407_042948
20160407_043004
20160407_043015
20160407_043043
20160407_043054
20160407_043141
20160407_043152
20160407_043209
20160407_043219
20160407_043235
20160407_043244
20160407_043255
20160407_043303
20160407_043323
20160407_043332
20160407_043343
20160407_043352
20160407_043405
20160407_043415
20160407_043449
20160407_043506
20160407_043606
20160407_043618
Share:

Wednesday, 6 April 2016

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ateketea kwa Moto Akiwa Ndani ya Gari Lake

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mhadhiri  wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Sayansi na Uhandisi wa Kompyuta (CoICT), Dk Richard Mgaya amefariki baada ya kuteketea ndani ya gari lake jijini Dar es Salaam juzi.

Gari la Dk Mgaya liliteketea baada ya kugongana na lori katika eneo la Mbezi Africana, Wilaya ya Kinondoni usiku wa kuamkia juzi na kuwaka moto uliosababisha kifo chake.

Juzi picha mbalimbali zilisambaa zikionesha gari aina ya Toyota Prado lililopata ajali eneo hilo la Africana baada ya kugongana na lori, baadaye ilibainika kuwa aliyekuwa katika gari hilo ni Dk Mgaya.

Akizungumza  kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Christopher Fuime alisema gari la Dk Mgaya liliteketea na hata kushindwa kujulikana dereva wa gari hilo.

Alisema baadaye ndugu wa marehemu ndio walithibitisha kuwa gari hilo lililoteketea na dereva aliyekuwemo ni Dk Mgaya ambaye hata hivyo naye aliteketea ndani ya gari hilo.

“Lile gari liliungua na hakuna kitu kilichopatikana, hata wakati polisi wanafika eneo la tukio walikuta tayari dereva amekuwa majivu kutokana na kuteketea kwa moto… labda baada ya kupima vinasaba ndio itathibitika kama ilikuwa ni yeye,” alisema Kamanda Fuime.

Alisema hata gari hilo hawakuweza kulitambua mara moja na baada ya kufuatilia Mamlaka ya Mapato (TRA) ilibainika kuwa mmiliki wake ni Dk Mgaya.

Alisema “ndugu wa marehemu ndio wamesema kuwa ni ndugu yao.” 
Dk Mgaya alijiunga na idara hiyo miaka kadhaa iliyopita akitokea masomoni nchini Marekani na alikuwa ni mtaalamu wa artificial intelligence.
Share:

MECHI ZA LEO JUMATANO UEFA TAREHE 6.4.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
UEFA LEO TAREHR 6.4.2016
Share:

MATOKEO MECHI ZA UEFA JANA TAREHE 5.4.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Ezekiah Wenje Afunga ushahidi akiwa Shahidi pekee ......Ni baada ya Mahakama Kuu kukataa ombi la kutumia fomu alizotaka kuzitumia

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Upande wa madai katika kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa Nyamagana jana ulifunga ushahidi baada ya Mahakama Kuu kukataa ombi la kutumia fomu namba 21B kwa ajili ya mashahidi wengine.

Baada ya kufunga ushahidi katika kesi hiyo namba 5/2015, mbunge wa zamani wa jimbo hilo (Chadema), Ezekiah Wenje dhidi ya Stanslaus Mabula (CCM), upande wa utetezi leo unatarajiwa kuwasilisha hoja iwapo nao unafunga ushahidi au utaita mashahidi mahakamani.

Hatua hiyo imekuja jana baada ya Jaji Kakusilo Sambo kukubaliana na pingamizi lililowekwa na upande wa wajibu maombi wakipinga mleta maombi kutumia fomu hizo katika ushahidi wake. 
Katika pingamizi la mawakili wa utetezi, Vicent Tangoh anayemuwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Constantine Mutalemwa anayemuwakilisha Mabula, walidai mdai hakutoa fomu hizo kwa utetezi ili kuzihakiki kwa muda mwafaka kama alivyoagizwa na Mahakama, hivyo hazistahili kutumika mahakamani.

Upande wa utetezi ulidai licha ya kutowasilisha fomu hizo kwa muda mwafaka, pia mlalamikaji aliziwasilisha kwa kutumia vifungu tofauti bila kuieleza Mahakama sababu za msingi za kutaka aruhusiwe kuzitumia kama kielelezo.

“Fomu hizi ndizo kiini cha maombi haya na mdai alipewa siku 10 kuzikabidhi kwa upande wa utetezi ili kuzihakiki na kuandaa hoja za majibu, hakufanya hivyo na kushindwa kutoa sababu za msingi za kutofanya hivyo,” alidai wakili Tangoh.

Baada ya Mahakama kukubaliana na pingamizi hilo, wakili wa Wenje, Deya Outa aliomba kufunga ushahidi kwani hawataweza kuita shahidi mwingine kutokana na ushahidi wao wote kutegemea fomu zilizokataliwa.

Jaji Sambo alikubaliana na ombi hilo baada ya upande wa utetezi kutokuwa na pingamizi na kuahirisha kesi hiyo hadi leo mawakili hao wa utetezi watakapowasilisha hoja zao, iwapo wanafunga ushahidi au kuita mashahidi kupinga ushahidi wa Wenje ambaye ni shahidi pekee wa upande wa mlalamikaji
Share:

MWENYEKITI WA CHADEMA MKOANI IRINGA AFARIKI KWA AJALI YA GARI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mwenyekiti Wa Chadema Mkoa Wa Iringa Afariki Kwa Ajali


Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Iringa Vijijini  Ndg.Sinkala Mwenda amepata ajali jana  jioni  eneo la Tanangozi na kukimbizwa Hospitalini kwa ajili ya matibabu lakini bahati mbaya akafariki dunia muda mfupi wakati madaktari wakijitahidi kuokoa uhai wake. Pumzika kwa amani Kamanda Sinkara.!

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger