Wednesday, 6 April 2016

MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRIL TAREHE 6.4.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRIL 06, 2016





Share:

Tuesday, 5 April 2016

MECHI ZA LEO JUMANNE UEFA TAREHE 5.4.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
UEFA TAR 5.4.3016
Share:

Watu wawili wafariki kwa kuangukiwa na Kifusi Geita

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Watu wawili wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa vibaya huku mama mmoja Felista Mganga (65) akivunjika miguu yote baada ya kuangukiwa na kifusi wakati wakichimba mawe yanayodaiwa kuwa na dhahabu.

Tukio hilo limetokea juzi katika kijiji cha Busaka tarafa ya Nyamilembe Wilayani Chato Mkoani Geita wakati watu hao walipokuwa ndani ya mashimo hayo.

Wakizungumza na Channel Ten katika eneo hilo likiwa limefungwa kwa ajili ya usalama huku walinzi wakiwa wanalinda, baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wanaeleza jinsi hali ilivyokuwa.

Pamoja na ajali hiyo,wachimbaji hao wamepaza sauti zao na kuiomba Serikal kuwapatia maeneo salama zaidi ya kuchimba dhahabu kama ilivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka jana.

Kaimu Afisa Madini Mkoa wa Geita Fabiani Mshai amesema wachimbaji hao walivamia eneo hilo baada ya kuvumbuliwa na mchoma mkaa kuhu jeshi la Polisi Mkoa wa Geita likithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Mwezi uliopita kijijini Mgusu Wilayani Geita watu wanane walifukiwa na kifusi huku watano wakipoteza maisha. 
Share:

VIDEO: Wezi wa Laptop kwenye magari wanalostisha sana… tazama walichowafanyia kina Master J kwa Sugu

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Rais Magufuli aombwa kuwa makini na uteuzi wa wakuu wa wilaya

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Watanzania wamemwomba Rais Magufuli kufanya mabadiliko katika Halmashauri za wilaya,manispaa na majiji nchini yakiwemo ya watendaji wake kwa madai kwamba zimejaa ufisadi wa kutisha pengine kuzidi ule wa bandarini.

Dereva taksi mjini Singida,Saad Mhando Mangala,amesema wakati huu Rais Dk.Magufuli akiwa kwenye maandalizi ya kuteua wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmshauri kwa nafasi za ukurugenzi auangalie kwa jicho la kipekee.

Akifafanua,alisema kwenye halmashauri hakuhitaji mtu awe na elimu kubwa ndipo aweze kuwa kiongozi, anatakiwa atambue jinsi rasimali za umma zikiwemo fedha zinavyotumika kinyume na makusudio yake.

“Watendaji katika halmashauri kuanzia mhudumu hadi mkurugenzi wapo vizuri ……wanamiliki mali mbalimbali zilizo nje ya uwezo wa mishahara yao, wakusanya mapato wana vitabu vya stakabadhi mbali mbali,kimoja cha halmashauri na kingine cha kwao na wakubwa wao waliowakabidhi stakabadhi hizo,” alisema.

Akifafanua zaidi, Mangala alisema kwa vile serikali ya awamu ya tano inahitaji watumishi waadilifu,waaminifu na wachapa kazi na upo umuhimu mkubwa safu ya watendaji kuanzia ukurugenzi ikafumuliwa au kufanyiwa mabadiliko makubwa.

“Kwenye halmashauri ambazo ndizo zipo karibu zaidi na wananchi wanatakiwa watendaji kuanzia nafasi ya ukurugenzi na kushuka chini, wawe ni watu watakaoendana na kasi ya utendaji ya Rais Magufuli usio na mzaha na wazembe na wabadhirifu wa mali za umma,” alisema dereva taksi huyo.

Aidha, Mangala alitumia fursa hiyo kumpongeza rais Magufuli kwa uteuzi wake makini wa kuteua wakuu wa mikoa na amemwomba aendeleze utamaduni wake huo wa kuchagua watu wenye elimu stahiki na wawajibikaji katika nafasi ya ukuu wa wilaya.

“Binafsi nisingependa urafiki, ushikaji au sura ya mtu apewe nafasi katia uteuzi wa wakuu wa wilaya. Achanguliwe mkuu wa wilaya mwenye elimu safi na ambaye atamudu kwenda na kasi ya rais wetu Magufuli,” alisema.

Kwa upande wake mkazi wa mjini hapa, Avi Mohammed, alisema wakuu wa wilaya waliopo ambao wameacha kuwatumikia wananchi wakisubiri uteuzi upite wao watumbuliwe na waonyeshwe mlango wa kutokea.

Avi alisema wakuu wa wilaya waliopo madarakani hivi sasa, wanalipwa mishahara kwa kazi ya kuwatumikia wananchi, hivyo kama wameacha kutekeleza majukumu yao ipasavyo watakuwa wanakwenda kinyume na mikataba yao ya kazi.

“Natarajia kuona uteuzi unazingatia watu wenye uwezo wa kukemea na kuwawajibisha watendaji wa chini yao wanao waonea wananchi. Pia wenye kutambua kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu kwa wakati. Wasiteuliwe watu wenye harufu ya rushwa na wavivu,” alisema.

Na Nathaniel Limu, Singida



Mkazi wa mji wa Singida, Avi Mohammed, amemshauri Rais Magufuli, asiwateue wakuu wa wilaya ambao kwa sasa hawatekelezi majukumu yao wakisubiri uteuzi.(Picha na Nathaniel Limu)



Dereva taksi mjini Singida, Saad Mhando Mangala, amshauri Rais Dk.Magufuli. 
Share:

Mbunge wa Moshi Mjini akutwa na mazito, namba yake yatumika kutapeli

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY



Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini Jafary Michael (Chadema) anatoa tahadhari kwa umma ya kuwa kuna baadhi ya watu wenye nia mbaya wanatumia namba yake ya simu ya mkononi ya mtandao wa Vodacom kufanya utapeli.
Watu hao wamekuwa wakituma ujumbe mfupi (SMS) kwa watu mbalimbali kwa lengo la kutapeli wakiomba kutumiwa fedha.

Wakati akishughulikia suala hilo katika vyombo vya dola ametoa ombi kwa yeyote atakayepata ujumbe huo kuupuza na kutoa taarifa kwa yeyote atakaye fikwa na kadhia hiyo.
Ukipata ujumbe huu mfahamishe na mwenzako.
Imetolewa na :
Japhary Michael
Mbunge wa Moshi mjini
Share:

Kuungua kwa Shule ya Iyunga Wanafunzi kidato cha sita waathirika

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari ya Ufundi Iyunga Mkoani Mbeya wamesema kuungua moto kwa shule hiyo, kumewaathiri kimasomo baada ya shule kufungwa, ambapo baadhi yao walilazimika kupanga vyumba na kuishi maisha ya geto ili waendelee kujisomea.

Wakizungumza na Channel Ten wanafunzi hao, ambao wanataraji kuanza mtihani wao wa mwisho mwanzoni wa mwezi Mei, wanasema walishindwa kurudi nyumbani kwao kutokana na umbali na gharama za nauli kuwa kubwa, lakini pia wakawashukuru wadau waliojitokeza kuchangia shule hiyo na kwamba kwa sasa imekuwa kwenye hali nzuri tofauti na awali kabla ya kuungua moto.

Aidha, Afisa elimu Sekondari Lidya Halbert anasema uongozi wa shule umejipanga ambapo wanafunzi wa kidato cha sita baada ya masomo ya kawaida, watasoma masomo ya jioni ili kuziba pengo la siku ambazo hawakuwepo shuleni.

Hata hivyo wadau mbalimbali wameendelea kujitokeza kuisaidia shule hiyo, ambapo Benki ya Axcess tawi la Mbeya imetoa msaada wa mifuko 56 ya sement.

Shule hiyo ambayo iliungua moto mara mbili katika kipindi cha juma moja pia ina uhitaji wa vitanda 250, hivyo kuomba wadau mbalimbali kujitokeza kuisaidia shule hiyo. 
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 5.4.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Magazetini Leo Jumanne April 5, 2016


20160405_044344
MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 5/4/2016
20160405_044357
20160405_044411
20160405_044421
20160405_044433
20160405_044449
20160405_044459
20160405_044515
20160405_044537
20160405_044555
20160405_044607
20160405_044618
20160405_044629
20160405_044638
20160405_044654
20160405_044705
20160405_044729
20160405_044740
20160405_044756
20160405_044806
20160405_044818
20160405_044831
20160405_044845
20160405_044854
20160405_044909
20160405_044919
20160405_044945
20160405_044953
Share:

Monday, 4 April 2016

MAGUFULI AFUTA SHEREHE ZA MUUNGANO TAREHE 26/4/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Share:

Msimamo wa Ligi Kuu England mpaka sasa

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

CfIuX3zWIAAhA1i.jpg large

Share:

HESLB: Tumejipanga kukusanya Tshs 8 bilioni kwa mwezi

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema imeanza kutekeleza mikakati mipya ya ukusanyaji wa mikopo ya elimu ya juu kutoka wadaiwa ambayo itaongeza wastani wa ukusanyaji wa Tshs 2.6 bilioni za sasa hadi kufikia Tshs 8 bilioni ifikapo mwezi Julai mwaka huu.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Jerry Sabi  ameyasema hayo leo (Jumatano, Machi 30, 2016) jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyotembelea ofisi za Bodi hiyo zilizopo Mwenge.

“Hadi mwezi uliopita (Februari, 2016) tulikuwa tunakusanya wastani wa shilingi bilioni 2.6 kwa mwezi, lakini sasa tumeongeza kasi na mikakati mipya ambayo itawezesha kukusanya shilingi bilioni 6 mwezi Aprili na shilingi bilioni 8 ifikapo mwezi Juni mwaka huu,” amesema Bw. Sabi aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo na miezi miwili iliyopita.

HESLB ilianzishwa ilianza kazi mwaka 2005 ili kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji na pia kukusanya mikopo kwa wanufaika. Hadi sasa, zaidi ya shilingi 2.1 trilioni zimetolewa kwa wanufaika na kati ya fedha hizi, mikopo iliyoiva na inayopaswa kukusanywa ni shilingi 258 bilioni ambazo wanufaika wake wamemaliza au kusitisha  masomo yao na vilevile kumaliza muda wa kujipanga kuanza kulipa (grace period).

Kwa mujibu wa Bw. Sabi, hadi sasa, HESLB imekusanya shilingi 91 bilioni kati ya shilingi 258 bilioni zilizoiva na hivyo kupaswa kukusanya.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo alikuwa akijibu hoja zilizotolewa na Wajumbe wa Kamati hiyo waliokutana na watendaji wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi na HESLB wakiongozwa na Waziri Prof. Joyce Ndalichako na Naibu wake Mhandisi Stella Manyanya.

Bw. Sabi alitaja mikakati mipya iliyobuniwa na HESLB kuwa ni pamoja na kuimarisha mtandao baina ya Bodi na waajiri kutoka sekta binafsi na umma ambao unalenga kubaini na kukusanya kiasi cha shilingi 7.02 bilioni kwa mwaka kutoka kwa  wanufaika 136,252.

“Tunapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa taasisi za Serikali na sasa tumejipanga kupitia upya mitandao ya waajiri kwa kushirikiano na taasisi kama Chama cha Waajiri (ATE), Mfuko wa Sekta Binafsi (TPSF) na Shirikisho la Asasi zisizo za Kiserikali (TANGO) ili kuhuisha takwimu zetu kuhusu waajiri ili kukusanya taarifa za wadaiwa wapya kwa haraka,” alifafanua Bw. Sabi.

Mikakati mingine ni kutoa elimu na kuimarisha ushirikiano na wadau mahsusi kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Usimamizi wa Mashirika ya Hifadhi za Jamii (SSRA), Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) na vyama vya kitaaluma.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini Bw. Peter Serukamba ameitaka HESLB kuongeza kasi ya kudai mikopo iliyoiva na kuutaka uongozi wa HESLB kuandaa orodha ya wadaiwa wote na kuiwasilisha kwa kamati ili ifanyiwe kazi.

“Ni lazima kuwe na fedha ili kuwezesha kutoa mikopo kwa wahitaji wengine ...haiwezekani mtu anapata mkopo halafu halipi...andaeni orodha ya wote walionufaika na mikopo ambayo itaonyesha nani halipi, nani analipa na nani amemaliza na tutaamua tufanye nini,” alisema Serukamba.

HESLB ilianzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai mwaka 2005 kwa lengo la kutoa mikopo kwa watanzania wahitaji waliopata nafasi za masomo katika vyuo vya elimu ya juu na kukusanya mikopo iliyoiva kutoka kwa wadaiwa walionufaika na mikopo tangu mwaka 1994.   

Mwisho.
Share:

MWANAFUNZI(DENTI) DARASA LA TANO AJINYONGA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Dada wa marehemu akilia baada ya mdogo wake kujinyonga.

STORI: Dustan Shekidele, Wikienda
Morogoro: Mshtuko! Mwanafunzi wa wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Mchikichini ‘B’ ya mjini hapa, Anosisye Gidion (12), ameacha viulizo kibao baada ya kujinyonga kwa kutumia kitenge cha mama yake, Judith Kilalu ‘Mama Kapipi’.

Tukio hilo la kuhuzunisha lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita, majira ya saa 1:00 asubuhi nyumbani kwao maeneo ya Mji Mpya mjini hapa.


Kitenge cha mama yake alichotumia kujinyongea.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Ashura na rafiki wa marehemu, Hussein walisema kuwa chanzo cha denti huyo kujinyonga kilidaiwa kuwa ni kitendo cha mama yake kumchapa na kumtishia kumpeleka polisi baada ya kuchukizwa na kitendo chake cha kurudi nyumbani saa 6:00 usiku huku akidaiwa kuonekana akiwa na kundi haramu la vibaka la Kizazi Jeuri.

Mama mzazi akilia kwa uchungu.

“Anosisye alichelewa kurudi nyumbani, ilipofika saa 4:00 usiku, mama yake aliamua kumtafuta akaambiwa alionekana akiwa na lile kundi lililokupora wewe (mwandishi wetu) maeneo ya Stendi ya Daladala ya Mji Mpya,” alisema mmoja wa mashuhuda hao huku akirekodiwa.

Mashuhuda wakifuatilia tukio hilo.

Kwa upande wake, mama mzazi wa denti huyo aliyeangushiwa zigo la lawama juu ya kifo cha mwanaye alisema: “Mwanangu alichelewa kurudi nyumbani usiku. Nilizunguka kumtafuta, nikaambiwa alionekana akiwa na Kizazi Jeuri hivyo nilimchapa sana na kumtisha kukicha nitampeleka polisi.

“Kulipokucha aliandaa nguo za shule, cha ajabu nimemkuta amejinyonga. Inauma sana jamani.”
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Makaburi B, Amiri Kombo aliyekuwepo eneo la tukio alithibitisha kutokea kwa tukio hilo katika mtaa wake.

Polisi wakichukua mwili wa marehemu kwaajili ya uchunguzi.

Wazazi wanahofia watoto wao kujiunga na kundi hilo lililomvamia mwandishi wetu na kumpora kamera na simu ambao aliwafungulia jalada la kesi namba MOR\RB\140\2016 hivyo wanasakwa na polisi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger