INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MKUU
WA JESHI LA KUJENGA TAIFA, MEJA JENERALI RAPHAEL MUHUGA ATAONGOZA KUTOA
HESHIMA ZA MWISHO KWA MIILI YA MAREHEMU ASKARI WAWILI PAMOJA NA VIJANA
WATANO WALIOKUWA WANAPATIWA MAFUNZO YA JKT KAMBI LA BULOMBORA
WALIOFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA GARI ILIYOTOKEA MKOANI KIGOMA.
TARATIBU
ZA KUAGA MIILI HIYO KWA HESHIMA ZOTE ZA KIJESHI ZINAFANYIKA LEO MCHANA
KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIJESHI JIJINI DAR ES SALAAM NA BAADAE
KUSAFIRISHWA KWA MAZISHI KATIKA MIKOA YA MTWARA, MOROGORO, TANGA,
SHINYANGA, KIGOMA NA DAR ES SALAAM.
MAJINA
YA ASKARI HAO WA KIKOSI CHA BULOMBORA JKT WALIOFARIKI DUNIA KATIKA
AJARI HIYO ILIYOTOKEA TAREHE 01 OKTOBA 2015 MAJIRA YA SAA 10 JIONI NI
SAJINI AMIDU ALLY KAMBANGA NA PRIVATE ABEL THADEI MAISHA. WENGINE NI
VIJANA WALIOKUWA WANAHUDHIRIA MAFUNZO YA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA
KUJITOLEA AMBAO NI SERVICEMAN SAID SADALA SAID NA SERVICEMAN EUGEN
STEPHANO BUTATI WALIOKUWA KATIKA MAFUNZO OPERESHENI KIKWETE.
MAKAO
MAKUU YA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA KUSHIRIKIA NA MAKAO MAKUU YA JESHI
LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA WAMESHAANDAA NDEGE KUBWA YA KIJESHI
ITAKAYOSAFIRISHA MIILI YA MAREHEMU HAO NA KULETWA DAR ES SALAAM.
AIDHA
KATIKA AJALI HIYO ASKARI WENGINE 23 WAMEJERUHIWA, KATI YAO WAWILI
WATAHAMISHIWA HOSPITALI KUU YA KIJESHI LUGALO KWA MATIBABU ZAIDI.
ASKARI
HAO WALIKUWA KWENYE GARI LA JESHI AINA YA IVECO 5717 JW09 AMBAPO
WALIPATA AJALI MAENEO YA MLIMA WA PASUA UMBALI WA KILOMITA 11 KUTOKA
KIGOMA MJINI, WALIKUWA WANAKWENDA KUBADILISHANA ZAMU YA ULINZI KATIKA
MOJA YA KITEULE CHA ULINZI KILICHOPO MKOANI KIGOMA.