INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Saturday, 12 July 2014
ANGALIA ZIARA YA MH.PINDA UINGEREZA
ANGALIA MATOKEO NA WAFUNGAJI WA MECHI ZOTE ZA KOMBE LA DUNIA LA MWAKA 2014 NCHINI BRAZIL
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
8th July 2014 World Cup 2014
5th July 2014 World Cup 2014
4th July 2014 World Cup 2014
KAJALA AFUNGUAKA,ASEMA KUWA RAFIKI YAKE WEMA NI MNAFIKI
MPENZI WA ZAMANI WA DIAMOND ,PENY ACHUMBIWA
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mtangazaji wa kipindi cha Genge cha EFM Radio, Penniel Mwingilwa 'VJ Penny'.
Friday, 11 July 2014
MAJINA YA WAOMBAJI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO CHA MISITU OLMOTONYI
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mkuu wa Chuo cha Misitu Olmotonyi, Arusha anayo furaha kuwataarifu wafuatao kuwa wamechaguliwa kujiunga na Chuo cha Misitu Olmotonyi, Arusha kwa udhamini wa binafsi, Wakala wa Huduma za Misitu na Mradi wa ECOPRC kwa mafunzo ya
Mkuu wa Chuo cha Misitu Olmotonyi, Arusha anayo furaha kuwataarifu wafuatao kuwa wamechaguliwa kujiunga na Chuo cha Misitu Olmotonyi, Arusha kwa udhamini wa binafsi, Wakala wa Huduma za Misitu na Mradi wa ECOPRC kwa mafunzo ya
SERIKALI YA TANZANIA YATANGAZA NAFASI ZA KAZI 1,324
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Sekretarieti
ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia Watanzania wenye sifa
na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 1,324 ambazo ni kwa ajili
ya waajiri mbalimbali Nchini.
Katibu
wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi amesema kuwa nafasi 1,334
zimeainishwa bayana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni
www.ajira.go.tz ili kuwawezesha wahitimu wote wenye sifa na uwezo
kutuma maombi kwa ajili ya kujaza nafasi hizo ajira Serikalini.
"Nadhani ni vizuri zaidi kwa kila
muhitimu anayetafuta kazi serikalini kufungua tovuti ya Sekretarieti ya
Ajira kuangalia nafasi za kazi zilizotangazwa na pale anapoiona kazi
inayoendana na sifa alizonazo kutuma maombi yake ili kuweza
kushindanishwa na wengine....maana ajira za Serikali hivi sasa ni za
ushindani hivyo inampasa kila anayetaka kupata kazi serikalini kujiandaa
vyema ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kuajiriwa katika
Utumishi wa Umma" alisema Daudi.
Alifafanua
kuwa kwenye tovuti hiyo kuna matangazo mawili tofauti ya kazi ambapo
moja liko katika lugha ya Kingereza likiwa na jumla ya nafasi za kazi
447 na tangazo lingine lipo kwa lugha ya Kiswahili ambalo lina jumla ya
nafasi za kazi 877.
Aidha,
alizitataja baadhi ya nafasi hizo za kazi zilizoko katika tangazo la
kazi kwa lugha ya Kiswahili kuwa ni Mhandisi kilimo (agro–engineers),
Afisa kilimo (agro–officers) Mkufunzi kilimo (aquaculture), Afisa kilimo
msaidizi (agricultural field officers), Daktari wa mifugo (veterinary
officers), Daktari utafiti mifugo (veterinary research officer), Daktari
mifugo mkufunzi (veterinary tutor), Mkufunzi mifugo (animal science),
Afisa mifugo (live stock officer), Afisa utafiti mifugo (livestock
research officer), Afisa Utumishi (human resources officer), Afisa ardhi
msaidizi, Dereva (driver).
AJALI YA BASI: BASI LA AMANI LAPATA AJALI MAENEO YA SALANDA MKOANI TABORA, MTOTO MMOJA AFARIKI DUNIA
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Basi la Amani Express likitokea Kigoma kuelekea Dar es salaam limepata
ajali usku wa kuamkia leo maeneo ya Salanda mkoani Tabora, ambapo mtoto
wa miaka mitatu amepoteza maisha na abiria kadhaa wamepata majeraha.
Mashuhuda wanahisi kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi. Pichani
abiria wakitafuta vitu vyao
MUDA WA NYONGEZA KWA WAOMBAJI MIKOPO AMBAO HAWAKUJAZA FOMU ZA MAOMBI YA MIKOPO KABLA YA JUNI WAONGEZWA
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawafahamisha waombaji wa
mikopo kwa mara ya kwanza na Umma kwa ujumla kwamba muda wa maombi ya
mikopo umeongezwa kwa mwezi mmoja kutoka Julai 1, 2014 hadi Julai 31,
2014.
Bodi ilianza rasmi kupokea maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao kuanzia
Aprili 23, 2014 ambapo tarehe ya mwisho wa kupokea maombi hayo ilikuwa
Juni 30, 2014.
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetoa muda wa nyongeza kwa
waombaji wa mikopo kukamilisha maombi ya mikopo katika kipindi cha siku
30, kupitia mtandao kwa anuani: http://olas.heslb.go.tz.
NYOTA SANCHEZ ATUA ARSENAL, KULAMBA PAUNI 140,000 KWA WIKI
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Nyota mpya wa Arsenal, Alexis Sanchez akiwa ndani ya 'uzi' mpya.
MSHAMBULIAJI mahiri wa Chile na Barcelona, Alexis Sanchez, amejiunga
na Klabu ya Arsenal kwa pauni milioni 30 na mkataba wa miaka miaka
minne.