Homa
ya kombe la dunia imeanza kupanda na timu kadhaa zimeanza kutangaza
vikosi vya wachezaji watakaoenda Brazil kushiriki michuano hiyo
inayotarajiwa kuanza June mwaka huu.
Jana usiku kocha wa timu ya taifa ya
Brazil Luis Fellipe Scolari alitangaza kikosi cha mwisho cha wachezaji
23 wataowawakilisha wabrazil kwenye fainali za kombe la dunia
zitakazofanyika nchi kwao – kikosi kilikuwa kama ifuatavyo: Goalkeepers: Jefferson (Botafogo), Julio Cesar (Toronto FC), Victor (Atletico MG).
Forwards: Bernard (Shakhtar Donetsk), Fred (Fluminense) Hulk (Zenit) Jo (Atletico MG), Neymar (Barcelona).
Leo hii kocha Joachim Loew wa Ujerumani
nae ametangaza kikosi cha awamu ya kwanza cha wachezaji 30 ambao
watachujwa na kubakia 23 watakaobeba dhamana ya wajerumani Brazil mwaka
huu: Goalkeepers : Manuel Neuer (Bayern Munich), Roman Weidenfeller
(Borussia Dortmund), Ron-Robert Zieler (Hannover) Defenders
: Jerome Boateng (Bayern Munich), Erik Durm (Borussia Dortmund), Kevin
Grosskreutz (Borussia Dortmund), Benedikt Howedes (Schalke), Mats
Hummels (Borussia Dortmund), Marcell Jansen (Hamburg), Philipp Lahm
(Bayern Munich), Per Mertesacker (Arsenal), Shkodran Mustafi
(Sampdoria), Marcel Schmelzer (Borussia Dortmund)
Midfielders : Lars Bender (Bayer
Leverkusen), Julian Draxler (Schalke), Matthias Ginter (Freiburg), Leon
Goretzka (Schalke), Mario Gotze (Bayern Munich), Andre Hahn (Augsburg),
Sami Khedira (Real Madrid), Toni Kroos (Bayern Munich), Max Meyer
(Schalke), Mesut Ozil (Arsenal), Bastian Schweinsteiger (Bayern Munich)
Attackers : Miroslav Klose (Lazio),
Kevin Volland (Hoffenheim), Lukas Podolski (Arsenal), Marco Reus
(Borussia Dortmund), Andre Schurrle (Chelsea), Thomas Muller (Bayern
Munich)
Mwanaume mmoja Mtanzania amekamwata
katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Nairobi Kenya akiwa amebeba
dawa za kulevya akiwa njiani kuelekea Antananarivo ambapo mzigo huo
ulitokea Tanga kisha ukapita Mombasa na baadae kwa ndege mpaka Nairobi. Mzigo
wenyewe ni wa cocaine na Heroin ambazo zote zina thamani ya zaidi ya
shilingi milioni 24 za Kitanzania na dawa hizo alikua ameziingiza
katika njia ya haja kubwa. Mkuu wa kitengo cha CID katika uwanja huo
Joseph Ngisa amesema mshukiwa alikamatwa JKIA na akawekwa kwenye chumba
cha uchunguzi na baadae akatoa tembe za cocain na tembe za Heroin na
tayari ameshapelekwa Mahakamani.
Mwezi
March mwaka huu watanzania wanne walikamatwa katika uwanja huohuo
walipopatikana na heroin yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 75
za Kitanzania na wote walifikishwa mahakamani na kukiri kosa. Wanawake
watatu na mwanaume mmoja kila mmoja akishtakiwa kando kwa kosa la
kusafirisha dawa za kulevya na walikua wameingia Kenya kupitia Namanga
na walikamtwa wakiwa njiani kuelekea Hong Kong. Kuanzia
March 2014 mpaka leo hii May ni jumla ya Watanzania watano wamekamatwa
kwenye kiwanja cha ndege Nairobi wakiwa kwenye pilika za kusafirisha
dawa za kulevya kwenda kwenye mataifa mengine.
Akichangia
jioni hii Mhe Sugu amesema kuwa Mhe Magufuli hafanyi kazi kitaalamu
bali anapiga siasa tuu ili kupumbaza watu. Amesema kuwa hizo barabara
anazojisifia na zinazotumia mabilioni mbona baada ya miezi michache
zinqumuka na kuhitaji matengenezo makubwa wakati kuna barabara za zamani
kama Makambako -Songea ni za zamani na bado zinahimili zaidi ya hizi? Pia
amezungumzia makampuni ya kigeni kama Strabag kuwazulumu vibarua wazawa
naye kukaa kimya kwa hilo zaidi ya kujisifia binafsi. Kamaliza na kusema kama anajipigia debe la urais huko asahau bali mahali panapo msahili ni jela kwa kushiriki kwake ubadhilifu
MUNGU mkubwa! Staa wa muziki wa
Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesimulia jinsi
alivyochungulia kifo baada ya kutikiswa na ugonjwa hatari na tishio
ulioibuka hivi karibuni wa Homa ya Dengue.
Akifunguka mbele ya gazeti hili juzi
baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini Mwananyamala, Dar alikokuwa
amelazwa, Ray C au Kiuno Bila Mfupa alisema kwamba kwenye maisha yake
hajawahi kushikwa na ugonjwa wenye mateso makali, tena ya muda mfupi
kama ilivyokuwa juzikati alipopata ugonjwa huo.
Alisema kwamba dakika chache tu baada ya
kuamka kitandani alikuwa akijisikia kichwa kikiuma kama kinataka
kuchomoka ambapo bila kuremba aliwasha gari lake na kukimbilia Hospitali
ya Mwananyamala.
Staa huyo wa Ngoma ya Na Wewe Milele alisema alipofika kwa kudra za muumba alilazwa tayari kwa kutundikwa dripu.
“Huwezi
kuamini baada ya madaktari kunipima na kugundua nina Ugonjwa wa Dengue,
walinishangaa sana hata namna nilipofika pale na kwamba sikutumia dawa
yoyote ya kutuliza maumivu kwa sababu maumivu yake huwa ni lazima
utatafuta tu dawa ya kukufanya upoze maumivu.
“Madaktari wengine wakatishika zaidi maana walisema kama ukimeza vidonge vya ‘Diclopa’ unaweza kupoteza maisha mara moja.
“Katika magonjwa ya ajabu na
yanayostahili kutafutiwa kinga mara moja basi huu ni ugonjwa wa kwanza
ambao serikali inatakiwa iwe macho sana maana haufai hata kidogo. “Tena
unatisha sana na wasipoangalia utapoteza maisha ya Watanzania kibao
kama hawatautafutia kinga au kuwapa Watanzania elimu ya kutosha.
“Mateso niliyoyapata kwa siku mbili
nilizolazwa Mwananyamala ni elimu tosha kabisa na kwamba ningekuwa na
uwezo wa kuzunguka au kupata nafasi ya kuongea na wakuu wa nchi basi
mara moja ningewaomba wafanye jitihada za haraka kuhakikisha wanapata
chanjo kwa ajili ya kuudhibiti mfumko wa gonjwa hilo.
“Dengue unaambukizwa na mbu tena wa mchana na dawa yake ni panadol tu!” alimalizia Ray C.
MTANGAZAJI aliyepata
kuwika katika vituo mbalimbali vya runinga Bongo, Maimartha Jesse,
amedaiwa kuwauzia mastaa wa mjini dawa za kuongeza makalio.Habari za
moto kutoka kwa sosi wa kuaminika, zinasema kuwa Maimartha ambaye pia
huitwa Mai amefikia hatua hiyo baada ya yeye kutumia na kufanikiwa.
Mtangazajialiyepata kuwika katika vituo mbalimbali vya runinga Bongo, Maimartha Jesse.
“Hamshangai siku hizi kila staa
anaonekana kuwa na makalio makubwa? Ni kazi ya Mai hiyo. Anafanya hiyo
biashara muda mrefu sana. Ni za kunywa na kupaka.
“Mbona hata yeye ametumia dawa hizo muda
mrefu sana? Ukimwangalia utagundua zamani hakuwa na hipsi za kiivyo. Ni
kwa sababu ya dawa,” alisema sosi huyo.
Akaongeza: “Hata Lulu Semagongo (Aunt
Lulu) ndiye aliyemsababishia kuwa na makalio makubwa kwani wakati wako
karibu alikuwa akimpa dawa hizo.”
Waandishi wetu walifika dukani kwa Mai
bila kujua kama ni waandishi na kuulizia bidhaa hizo ambapo zilitolewa,
wakapiga picha bila kugundulika.
Mai
akiwa hajui kuwa yupo mikononi mwa mapaparazi waliokuwa na njaa ya
habari, aliwaambia: “Ni dawa nzuri, mara moja zinarekebisha umbo na
unakuwa wa kuvutia. Kuna za shilingi 250,000 na 260,000 inategemea kama
ni vidonge au losheni.”
Mapaparazi wetu walipompigia simu Mai
baada ya kutoka dukani hapo na kumweleza kuhusu uuzaji wa dawa hizo
dukani kwake, alisema duka lake linauza urembo wa aina zote kwa mastaa
na wasio mastaa.
“Kama nimetumia dawa za kuongeza
makalio, nyie inawahusu nini? Kifupi duka langu linadili na urembo wa
aina zote,” alisema Mai akishindwa kufafanua zaidi.
Lulu alipovutiwa waya na kuulizwa kama
makalio yake ni matokeo mazuri ya dawa za Mai alisema: “Sijawahi kutumia
dawa za Mai kwa ajili ya kuongeza makalio.
Yangu ya asili lakini watu wakinipigia simu na kuniuliza dawa za kuongeza makalio huwa nawaelekeza kwa Mai.”
MWANADADA wa ‘long time’ kwenye
sanaa ya uigizaji amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukosa dili za
kazi za maana kutokana na tabia za kifuska kwa baadhi ya wasanii wa kike
wa Bongo Movie.
Msanii Nora.
Akipiga stori na paparazi wetu, Nora alisema amekuwa akitembelea katika ofi si mbalimbali na
kila anapojitambulisha kwamba ni msanii wa fi lamu watu wanashtuka na
sehemu nyingine anakosa dili za maana kutokana na uchafu wa baadhi ya
wasanii hasa wasagaji na wanaojiuza.
“Yaani naona aibu sana kujitambulisha
kwenye ofi si za watu kwani kila ninakoenda na kujitambulisha watu
wanaanza kunong’ona huku wakidai kwamba wasanii wa kike wa fi lamu wana
tabia chafu wakati tunachafuliwana watu wachache tu wasiojiheshimu,”
alisema Nora.
Rais
Jakaya Kikwete amemteua Rished Bade kuwa Kamishna mpya wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Harry Kitilya
aliyestaafu kazi akiwa katika nafasi hiyo, mwaka jana, Ikulu imesema leo
Huyu ndio dent ambaye ameamua kuweka wazi sehemu zake nyeti ....
Shariti lazima uwe mtu mzima umri kuanzia +18,ndipo uangalie hii picha,TUANGAZE BONGO atupo hapa kumzalilisha mtu ila tupo kwa ajili ya kukomesha vitendo vichafu vya kujiuza kupitia mitandao ya kijamii
Mahabusu
wa Gereza Kuu la Mkoa wa Arusha, jana walizua tafrani katika viwanja
vya Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini hapa, baada ya kuvua nguo na kugoma
kushuka kwenye basi wakipinga kitendo cha watuhumiwa wawili wa dawa za
kulevya kuachiwa kinyemela.
Watuhumiwa
wanaolalamikiwa ambao mashtaka yao yalibadilishwa mara mbili ili wapewe
dhamana ni Dharam Patel (26) na Nivan Patel (20) wanaodaiwa kukamatwa
na kete 173 za heroini na misokoto 300 ya bangi, Aprili mwaka huu.
Mahabusu
hao walikuwa wakipaza sauti kupinga madaraja kati ya wenye nacho na
wasio nacho kwa wengine kuachiwa na wengine kubaki ndani kwa kisingizo
cha ‘upelelezi haujakamilika’.
Huku
wakipaza sauti zao kwa nguvu, mahabusu hao wa kesi za mihadarati
ikiwamo mirungi na bangi, wizi wa kutumia silaha na mauaji, walisema
wamekaa mahabusu kwa zaidi ya miaka miwili, lakini hawajawahi hata
kusomewa maelezo ya awali na kuendelea kuteseka gerezani.
Sauti ilisikika kutoka ndani ya basi: “Wenzetu hata mwezi haujaisha wanafutiwa kesi, jamani sisi tumekosa nini? Tunataka haki itendeke kwa wote.”
Mahabusu hao walionekana wakiwa wamesimama ndani ya basi hilo bila nguo, huku umati wa watu waliofika mahakamani hapo ukitazama.
Baada
ya kuona umati wa watu unazidi kuongezeka kuwashangaa mahabusu hao,
askari wa magereza waliondoa basi hilo eneo la Mahakama.
Kuachiwa watuhumiwa
Taarifa
za kuachiwa kwa watuhumiwa hao wa dawa za kulevya waliokuwa na kesi
mbele ya Hakimu Mkazi Arusha, Mwakuga Gwanta zilidaiwa kuwa zilitokana
na Ofisi ya DPP Arusha, kubadilisha hati ya mashtaka.
Ilidaiwa
kuwa badala ya kudaiwa kuwa walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya,
iliandikwa kuwa walikutwa na dawa hizo mashtaka ambayo yana dhamana.
Kamanda
wa Kikosi cha Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa alisema
jana kuwa ofisi yake haina taarifa za watuhumiwa hao kupewa dhamana
lakini alisema kulikuwa na jaribio hilo.
“Ninachojua
kesi hii ilipangwa kutajwa Aprili 29, mwaka huu, lakini ikasogezwa
mbele hadi Mei 2 na kilichofanyika hati ya mashtaka ilibadilishwa na
kuandikwa wamepatikana na dawa za kulevya."
Alisema
kwa mujibu wa sheria, mtu ambaye anakamatwa na dawa za kulevya zenye
thamani chini ya Sh10 milioni anaweza kupewa dhamana, lakini kiwango
kikiwa zaidi ya hapo, hapati dhamana.
“Baada
ya kubainika kuna njama za mashtaka kubadilishwa, tulipinga kwa kuwa
kosa lipo wazi kwamba walikuwa wakisafirisha dawa hizo, sidhani kama
wamepewa dhamana... sidhani kama inawezekana ila tunafuatilia kwa karibu
tukio hili,” alisema Nzowa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema kazi ya polisi
ilikuwa ni kukamata watuhumiwa na kuwafikisha mahakamani tu.
Msajili
wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Wilibard Mashauri alisema hahusiki
katika malalamiko hayo kwa kuwa si mpelelezi wa kesi.
“Lakini
hawa mahabusu wanalalamikia kuachiwa kwa wale watuhumiwa wenye kesi ya
dawa za kulevya, kesi ambayo haipo kwangu wala sijui wameachiwa kwa
kifungu gani na inategemea na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DP)
amewaachia kwa kifungu gani,” alisema.
MWANAMKE aliyejulikana
kwa jina la Hadija Mohammed, mkazi wa Mchikichini, Ilala jijini Dar es
Salaam amekumbana na mkono wa sheria baada ya kufanya kitendo cha
kinyama kufuatia kujifungulia kwenye ndoo kisha kichanga kukitupa
chooni.
Hadija Mohammed, anayetuhumia kukitupa kichanga baada ya kuzaliwa.
Kwa mujibu wa chanzo, mwanamke huyo
alikuwa na ujauzito uliotimiza miezi tisa na kila mtu alikuwa akiuona,
lakini ghafla siku ya tukio baadhi ya ndugu waligundua kuwa hakuwa na
ujauzito tena!
NDUGU WAMBANA Chanzo
hicho kiliendelea kutiririka kuwa baadhi ya ndugu na majirani
walipomuona bila ujauzito walimbana kwa kumuuliza iliko mimba hiyo.
Hadija Mohammed akiwa chini ya ulinzi.
“Ndugu zake na majirani walipomuona hana
tumbo kama mwanzo walishangaa, wakaamua kumbana tena kwa vitisho kwamba
watampeleka polisi.
“Ndipo alipoamua kueleza ukweli kwamba, alijifungulia kwenye ndoo lakini mtoto alikwenda kumtupa chooni,” kilisema chanzo hicho.
POLISI WAAMBIWA, WAKOMAA NAYE Habari
zilizidi kudai kuwa baada ya majirani na ndugu kuambiwa hivyo
walikwenda kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Pangani kilichopo
Ilala, Dar ambapo walifika na kukiokoa kichanga hicho lakini walikuta
kimeshakata roho.
MAMA APELEKWA POLISI Mpashaji
wetu alizidi kudai kuwa, baada ya polisi kuuchukua mwili wa mtoto huyo
hawakumwacha mama mtu aendelee kuponda maisha uraiani, walimbeba mpaka
kituoni hapo na kumfungulia jalada lenye namba ILA/RB/1715/2014 kisha
kumpeleka kwenye Mahabusu ya Polisi Msimbazi huku mwili wa mtoto huyo
ukipelekwa Hospitali ya Amana na baadaye Hospitali ya Taifa Muhimbili.
NI FUNDISHO Afande
mmoja ambaye aliomba jina lake lisiandikwe, alisema ni lazima Hadija
apambane na mkono wa sheria ili iwe fundisho kwa wanawake wengine wenye
mchezo huo.
“Hii tabia imekua sana. Wanawake wengi
wanajifungua kisha wanawatupa watoto chooni au kokote kusikojulikana ili
wao waendelee kula raha mjini. Huyu lazima sheria ishike makali yake
ili iwe fundisho,” alisema afande huyo.
Askari wa Usalama barabarani eneo la
Makumbusho, Dar wakimpiga Dereva wa gari ambaye amejitambulisha kama
mwanajeshi! Tukio hili limetokea mida ya saa 9 mchana huu. Bado
haieleweki chanzo ni nini.
Je, unadhani hivi ndivyo askari wetu wanatakiwa kutekeleza majukumu yao?
MSANII wa
filamu na muziki, Snura Mushi ameingilia kati ugomvi wa wasanii
wenzake, Wema Sepetu na Kajala Masanja na kuwaagiza wamalize tofauti
zao.
Msanii wa filamu na muziki, Snura Mushi a.k.a mama majanga.
Wasanii hao ambao wameingia kwenye bifu
la kufa mtu kufikia hatua ya kuanikana kwenye vyombo vya habari huku
chanzo kikubwa kikitajwa ni shilingi milioni 13 ambazo Wema alimlipia
Kajala kama faini ya kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa rehani
kisheria iliyokuwa ikimkabili mahakamani.
Nyumba hiyo iliwekwa rehani kutokana na mume wa Kajala, Faraja Agustino kushitakiwa kwa kosa la kutakatisha fedha haramu.
Wema na Kajala.
Snura amewataka Wema na Kajala kutoangalia nani ana makosa, wamalize tofauti zao. “Nawashauri wenzangu wasigombane na kuwekeana vinyongo hiyo ni kama wanawapa watu faida,
nawaomba wamalize kwani haipendezi
kabisa kwa jinsi walivyokuwa wameshibana. Kama mmoja anaona amemkosea
mwenzake ajishushe na kuomba msamaha,” alisema Snura.
Afrika kama tunavyoifahamu, ilikuwa ni
sehemu ya Mila na Tamaduni bora kabisa, sehemu ambayo heshima adabu
vilikuwa ni msingi wa jamii yake, hasa kwenye jamii.
Ni sehemu ambayo masikini waliishi kwa
mlo mmoja lakini bado waliheshimiana, kuvumiliana na kupendana. Ni
sehemu ambayo binti angekutwa akifanya mambo ya aibu basi wazazi wake
wangenyooshewa vidole kwa malezi mabaya kwa binti yao. Vivyo hivyo kwa
vijana wa kiume. Mambo haya yalipatikana zaidi kwenye nchi nyingi za
kiafrika na Tanzania ni mojawapo.
Ila kwa sasa, Waafrika wengi, hasa
vijana wamezua mijadala mingi inayotokana na mienendo ya tabia zao
zinazopelekea kuvunjika kwa Mila na Tamaduni bara hili…. Kitu kinachozua
maswali juu ya nani wakulaumiwa kwa kuvunjika na kuharibika kwa Mila na
Tamaduni za Afrika…? Mfano mdogo uko kwenye hiyo picha hapo juu, huyu
binti anafunika nywele kwa imani lakini anafunua matiti. Dini, shule,
wazazi, walezi na walimu wameshindwa kukisaidia hiki kizazi. Ni nani wa
kulaumiwa? Kwangu mimi hiki bado ni kichekesho tu!