Bunge livunjwe tukawaombe radhi wananchi- Mjumbe
Laizer pia amewataka wajumbe wenzake kurudi katika
maeneo yao ili wakaombe radhi kwa Watanzania kutokana na ufujaji wa
fedha unaotokana na kuwepo kwao kwenye vikao vya Bunge.
Dodoma. Mivutano katika Bunge la Katiba
imemchukiza mmoja wa wajumbe wa chombo hicho, Michael Laizer ambaye
amemshauri mwenyekiti wake, Samuel Sitta amwombe Rais kuvunja Bunge.
Laizer pia amewataka wajumbe wenzake kurudi katika
maeneo yao ili wakaombe radhi kwa Watanzania kutokana na ufujaji wa
fedha unaotokana na kuwepo kwao kwenye vikao vya Bunge.
“Mwenyekiti narudia tena kama watu hawataki uamuzi
huu, nakushauri andika barua kwa Mheshimiwa Rais ili aje alivunje Bunge
na twende makwetu,” alisema Laizer.
Laizer alilishutumu Bunge hilo kuendelea kutafuna
fedha wakati watu wengine wanaishi maisha magumu zaidi kiasi cha
kushindwa kupata hata mlo mmoja kwa siku.
Alipinga muda ambao wametumia wajumbe hao kwa
ajili ya kujadili masuala ya kanuni pekee bila hata ya kufikia uamuzi,
akisema ndoto yake ni kuwa hadi wiki hii waanze kuchambua vifungu vya
katiba.
Aidha alisema watu wenye umri mkubwa kama yeye (Laizer) wanaogopa kuchangia hoja kutokana na tabia ya kuzomeana.
Aliwataka wajumbe kuwa wavumilivu ili kuruhusu wajumbe kuchangia mijadala kwa uhuru.
michango kwa uhuru.
na kuheshimiana kama ilivyotokea kwa baraza la
Wawakilishi Zanzibar ambako CCM ilikubali kugawa madaraka hata pale
ambapo hawakutaka kufanya hivyo.