Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi Safia Jongo
**
Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga limefanikiwa kuupata mguu wa mtu mwenye ulemavu wa ngozi, uliokatwa hivi karibuni na watu waliokwenda kufukua kaburi lake wilayani Lushoto kwa madai kuwa ukiwa na kiungo cha mtu mwenye ulemavu wa ngozi utajiri unakufuata.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi Safia Jongo, amesema kuwa hadi sasa jumla ya watu watatu wamekamatwa wakiwa na kiungo hicho.
Katika hatua nyingine, Jeshi hilo limewakamata watoto 117 wanaojiita watoto wa Ibilisi na wazazi kutokana na kujihusisha na matukio ya kihalifu na baadhi yao tayari wameshafikishwa mahakamani.
Chanzo - EATV
0 comments:
Post a Comment