Tuesday, 17 August 2021

TAA ZA SHINYANGA MJINI ZAZUA GUMZO. ..KITINYA AHOJI KWANINI HAZIWAKI TENA

...

 


Diwani wa Kizumbi Manispaa ya Shinyanga Ruben Kitinya, akihoji hatma ya matengenezo ya Taa za Barabarani Mjini Shinyanga kwenye kikao cha Baraza la Madiwani


Na Marco Maduhu,Shinyanga

DIWANI wa Kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga Reuben Kitinya, amesikitishwa na ubovu wa Taa za Barabarani Mjini Shinyanga, ambapo sasa haziwaki na kusababisha giza.

Kitinya amebainisha hayo leo Jumanne Agosti 17,2021 kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa Manispaa ya Shinyanga, wakati wa ajenda ya kuuliza maswali ya papo kwa papo.

Amesema Taa hizo zimewekwa hivi karibuni na zilikuwa zikiupendezesha mji wa Shinyanga lakini sasa haziwaki tena na kusababisha mji kuwa na giza.

"Nauliza ni lini Halmashauri mtazifanyia matengenezo Taa za Barabarani ili ziwake kama zamani na kuupendezesha mji wetu," aliuliza Kitinya.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga John Tesha, ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, akijibu swali hilo, alisema matengenezo ya Taa hizo siyo la Halmashauri bali lipo chini ya Mkandarasi husika na.

Aidha, alisema Serikali ilishazungumza na Mkandarasi aliyeziweka Taa hizo awali, na zitafanyiwa matengenezo hivi karibuni, ambapo tayari zipo Bandarini.


Diwani wa Kizumbi Manispaa ya Shinyanga Ruben Kitinya, akihoji hatma ya matengenezo ya Taa za Barabarani Mjini humo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga John Tesha, akijibu maswali ya Papo kwa Papo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune, akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la madiwani.

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la madiwani.

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la madiwani.

Na Marco Maduhu- Shinyanga




Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger