***
Kumetokea na hali ya kushangaza katika makafani ya Hospitali ya Rufaa ya Bungoma nchini Kenya baada ya mwili wa Mwanamuziki Peter Oteng almaarufu Storm Dwarchild ulikataa kuingia katika jeneza duni hadi la bei ghali liliponunuliwa.
Oteng ambaye pia alikuwa afisa wa mawasiliano wa mbunge wa Kanduyi, Wafula Wamunyinyi, mwili wake ulikataa kutoshea kwenye jeneza hadi lingine la bei ghali liliponunuliwa.
Mmoja wa marafiki zake marehemu aliambia gazeti la Taifa Leo kuwa huenda alikataa kuwekwa katika sanduku kwa sababu pesa nyingi zilichangwa ili afanyiwe mazishi ya hadhi.
Swahiba huyo pia alidai kuwa huenda waliomuua Oteng walikuwepo katika mochwari hiyo na hivyo alikasirika kuwaona.
"Kunaweza kuwa na sababu nyingi za kufanya agome kuingia katika jeneza. Pengine familia yake na jamaa kutoka Uganda walikasirika na kufanya tambiko kuhakikisha kuwa wauaji wake hawatakuwa na amani maishani," rafiki huyo alisema.
Peter Oteng almaarufu Storm Dwarchild alipatikana ameuawa na mwili wake kutupwa kando ya viungani vya mji wa Bungoma.
Akizungumza na waandishi wa habari, Jumamosi, Agosti 7, Kamanda Mkuu wa polisi kata ndogo ya Bungoma Benjamin Kiwele alidhibitisha kifo cha Storm akisema mwili wa mwendazake ulipatikana na majeraha ya panga.
Kulingana na Kiwele ilibainika kwamba aliabiri bodaboda kuelekea nyumbani kwake baada ya kukutana na bosi wake mbunge Wamunyinyi.
Kiwele aliongeza kwamba polisi wameanzisha uchunguzi wakiwa tayari wamepata ujumbe muhimu kwenye simu unayoonyesha aliyemlipia nauli ya boda boda kumfikisha nyumbani.
Mbunge Wamunyinyi alikashifu mauaji hayo na akisema atahakikisha haki inatendeka kwa mwenda zake.
Chanzo - Tuko News
0 comments:
Post a Comment