Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Eleuther Alphone Mwangeni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kuanzia tarehe 08 Juni, 2021. Prof. Mwangeni ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) na anachukua nafasi ya Prof. Esther Ishengoma ambaye amemaliza muda wake.
Kufuatia uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo , ameteua wajumbe sita (6) wa Bodi hiyo kwa mujibu wa Sheria ya Chuo cha Elimu ya Biashara ya mwaka 1965 Sura 315 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2020.
Uteuzi wa Wajumbe hao utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 09, Juni, 2021. Wajumbe walioteuliwa ni kama ifuatavyo:
1. Dkt. Consolatha Deogratias Ishebabi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo, Wizara ya Viwanda na Biashara;
2. Dkt. Kenneth Hosea ambaye ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia;
3. Bi. Mwema Punzi ambaye ni Wakili wa Serikali Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
4. Bw. Zahoro Muhaji ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF);
5. CPA. Peter Lucas Mwambuja ambaye ni Rais wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA);
6. Waziri amemteua Prof. Wineaster Saria Anderson ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa Mjumbe wa Bodi ya CBE.
0 comments:
Post a Comment