Sauti kubwa ilisikika miongoni mwa wakaazi wa mji wa Puebla , katikati ya Mexico Jumamosi tarehe 29 mwezi Mei,2021.
Kutoka siku hiyo hadi sasa kile kilichoanza kuwa shimo la mviringo wa mita tano kiliendelea kuwa na mviringo wa mita 80 na kina cha mita 20.
Ukubwa wake uliendelea kuongezeka na muda na kutishia kumeza nyumba iliyopo karibu ambayo tayari mamlaka ya eneo hilo iliwahamishia wamiliki wake.
Shimo hilo kubwa lina ukubwa wa mita 80 na kina cha mita 20
Hii sio mara ya kwanza kitu kama hicho kimefanyika nchini Mexico ama hata duniani.
Katika siku za hivi karibuni ,ukweli ni kwamba kumekuwa na msusuru wa matukio kama haya ambayo yamesababisha maafa ya watu baada ya kutokea katika barabara.
Lakini unawezaje kuelezea tukio la shimo kubwa kama hilo?
Mashimo kama hayo hutokea wakati ardhi inapoanguka chini kutokana na tofauti ya unyevu nyevu.
Kulingana na Beatriz Manrique, katibu wa shirika la mazingira la Puebla, katika tukio hilo kuna tofauti mbili.
''Tunaamini inaweza kuwa mchanganyiko wa sababu mbili: Kulainika kwa ardhi, eneo lote ambalo lilikuwa likilimwa pamoja na kutolewa kwa maji ardhini hatua inayolainisha udongo wa chini'' , alisema.
Socavon Mexico
Baadhi ya wataalamu wanasema kwamba huenda kukawa kumesababishwa na utumiaji mbaya wa mito ya maji katika eneo hilo.
Ushirikiano wa pamoja wa mashirika ya kuwalinda raia katika eneo hilo pamoja na tume ya kitaifa ya maji ya Mexico utafanya uchunguzi kubaini chanzo chake.
Wakati huohuo, wakaazi wanaendelea kusubiri na kutazama kwa karibu shimo hilo litaongezeka kwa ukubwa gani.
CHANZO - BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment