Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi Juni 19,2021 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilayanchini ambapo amewabadilisha vituo vya kazi baadhi, ameingiza sura mpya na kuwarudisha waliowahi kushika nafasi hizo.
Baadhi ya waliotoswa katika uteuzi huo ni pamoja na Lengai Ole Sabaya ambaye alikuwa mkuu wa wilaya ya Hai kabla ya kusimamishwa kwa tuhuma mbalimbali na Simon Odunga ambaye alikuwa mkuu wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Sambamba na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa mkoani Iringa, Richard Kasesela.
Mei 13, 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alimsimamisha kazi, Lengai Ole Sabaya ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili.
0 comments:
Post a Comment