Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Jumamosi Juni 19,2021 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilayanchini ambapo amewabadilisha vituo vya kazi baadhi, ameingiza sura mpya na kuwarudisha waliowahi kushika nafasi hizo.
Katika uteuzi huo ,Rais Samia amewateua pia waliokuwa viongozi wa upinzani wakahamia CCM. Wateule hao ni pamoja na aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji (Serengeti), aliyekuwa meya wa Arusha, Kalist Lazaro (Lushoto), aliyekuwa mwanasheria wa ACT Wazalendo, Albert Msando (Morogoro).
0 comments:
Post a Comment