Gosiame Thamara Sithole akiwa na mme wake
**
Mwanamke aitwayr Gosiame Thamara wa Afrika Kusini amejifungua watoto 10 kwa mpigo na kuvunja rekodi ya ulimwengu ambayo ilikuwa imewekwa na mwanamke kutoka Mali aliyepata watoto tisa miezi kadhaa iliyopita.
Gosiame Thamara Sithole mwenye umri wa miaka thelathini na saba alijifungua watoto hao kumi usiku wa Jumatatu, Juni 7,2021.
Mama huyo alikuwa akitarajia kujifungua watoto wanane kutokana na uchunguzi wa ujauzito uliofanyika awali, lakini watoto wengine wawili walipatikana wakati wa kujifungua. Kulingana na ripoti ya Pretoria News na vituo vingine vya habari, Thamara alijifungua wavulana saba na wasichana watatu kupitia upasuaji katika hospitali ya Pretoria.
Sasa ni mama wa watoto 12 kwani tayari ana pacha wa miaka sita. Mumewe, Teboho Tsotetsi, alisema ujauzito wa Thamara ulikuwa wa asili kabisa kwani hakuwa kwenye matibabu yoyote ya uzazi. "Sasa tuna wavulana saba na wasichana watatu.
Alizaa baada ya miezi saba na siku saba," baba huyo aliyejawa furaha alisema.
Katika mahojiano mwezi mmoja uliopita kabla ya kujifungua, mama huyo ambaye sasa ana watoto 12 alisema kuwa alishtuka kubaini kuwa huenda akajaliwa watoto wengi kwa wakati mmoja.
Awali alikuwa akitarajia kujaliwa watoto wanane lakini wawili zaidi walipatikana wakati akijifungua.
Mumewe, ambaye kwa sasa hana ajira, alisema alikuwa na furaha ya kuwakaribisha watoto wake ulimwenguni.
"Nilihisi kana kwamba nilikuwa mmoja wa watoto wa Mungu lakini bado sikuamini.
Nina hamu sana kuwashika watoto wangu mikononi mwangu," alisema.
Awali, iliripotiwa kuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 25 nchini Mali alijifungua watoto tisa kwa mpigo ambapo anaingia katika vitabu vya historia kwahi kujifungua idadi ya watoto kama hiyo.
Wizara ya Afya katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi ilisema mwanamke huyo, Halima Cisse alitarajia kujifungua watoto saba, lakini uchunguzi wa ultrasound haukugundua watoto wengine wawili ndani ya tumbo lake.
Wizara ilifichua kuwa Cisse alijaliwa wasichana watano na wavulana wanne kwa njia ya upasuaji.
0 comments:
Post a Comment