Mabingwa wa Tanzania, Simba SC wameanza vyema hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, AS Vita Uwanja wa Marty's Jijini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo, Chriss Mugalu aliyeiadhibu timu ya nyumbani kwao kwa penalti dakika ya 61 baada ya beki wa AS Vita, Ousmane kuunawa mpira uliooigwa na kiungo Luis Miquissone, raia wa Msumbiji.
0 comments:
Post a Comment