Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameshindwa kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mkutano mkuu wa jimbo hilo umefanyika leo Jumatatu tarehe 20 Julai 2020 katika ukumbi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere, Kuvukoni jijini humo ambapo wagombea walikuwa 78.
Mchuano ulikuwa mkali kati ya Makonda aliyeuacha ukuu wa mkoa ili kwenda kuwania ubunge kushindana na mbunge anayemaliza muda wake, Dk. Faustine Ndugulile.
Akitangaza matokeo, katibu mwenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Simon Mwakifamba amesema wapiga kura walikuwa 399 na hakuna kura zilizoharibika.
Amesema, Makonda amepata kura 122 huku Dk. Ndugulile akupata kura 190
0 comments:
Post a Comment