Sunday, 5 July 2020

Mgumba; Serikali Imetatua Changamoto Jimbo La Morogoro Kusini Mashariki

...
NAIBU waziri wa Kilimo Omary Mgumba  amesema kuwa serikali imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali maendeleo kwa  wananchi katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki tofauti na watu  baadhi ya watu  wanavyoeneza propaganda juu ya kile kilichotekelezwa katika jimbo hilo.

Mgumba ambae ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki ameyasema hayo wakati akizungumza na wajumbe wa kamati za siasa katika Kata ya Kidugalo na Ngerengere Mkoani Mkoani Morogoro.

Alisema kuwa wanaoeneza Propaganda hizo hawana nia njema na Chama cha Mapinduzi CCM kwani hivi sasa wananchi wamefunguliwa fursa mbalimbali ikiwemo miundombinu ya Barabara,elimu huduma za afya pamoja na huduma ya maji.

Aidha alisema kuwa hivi sasa wananchi pamoja viongozi wa CCM katika Jimbo hilo wanatakiwa watembee kifua mbele kutokana na yale yalitokelezwa na serikali ya awamu ya tano chini Dr John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yeye akiwa Mbunge wa Jimbo hilo la Morogoro Kusini Mashariki.

Akizungumzia kuhusu Barabara amesema kuwa hivi sasa barabara nyingi zinapitika amabzo zilikuwa changamoto hapo awali hali iliyaofanya wanachi kuteleza shughuli za zao za kimaendeleo licha ya kuwepo changamoto ndogongo katika baadhi ya barabara ambazo serikali imekuwa ikizitatua kwa kwa wakati.

Kuhusu Barabara ya Bigwa Kisaki amesema kuwa barabara hiyo hivi karibuni Itaanza kujengwa kwa Kiwango cha lami kwa Kilometa 60 na makandarasi ameshapatika.na hapo awali katika ilani ya CCM 2005 iliahidi kuifanyia upembuzi yanikini ili iweze kujengwa kwa lami

Sanjari na hayo alisema kuwa kwa kipindi cha uongozi wake amefanikiwa kutembelea takribani wa Vijiji na Kata Zote Kila mwaka tofauti na wasikuwa na nia njema wanaodai amekuwa Mbunge wa kata Moja ya Mkuyuni.

ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wa jimbo la Morogoro kusini Mashariki kwa ushirikiano wao walioutoa katika kipindi ambacho alikuwa mbunge wa Jimbo hilo

wajumbe hao wa kamati ya Siasa wamempongeza Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Omary Mgumba kwa kufanikwa kuteleza na kutatua changamoto mbalimbali ambazo hapo awali katika viongozi waliopita hazikuweza kutatuliwa.

Walisema kuwa hivi sasa ni faraja kwa serikali awamu ya tano chini Dr John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wanaimani nayo kutokana na miradi mikubwa ya kimkatati ambayo wameitekeleza kwa kipindi kiupi cha miaka miatano.

Waliongeza kuwa juhudi zao katika kusimamia shughuli za maendeleo ndizo zimeifanya sasa serikali hiyo kuingia katika uchumi wa kati.

Jimbo la Morogoro kusini Mashariki chini ya Mbunge wake Omary Mgumba katika kipindi cha awamu ya tano limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupokea fedha za miradi ya maendeleo kupitia mfuko wa Jimbo ambazo zimezaa matunda katika sekta mbalimbali.

Pia wamefanikiwa kudhibiti mapato ya halmsahauri ya Wilaya ya Morogoro ambayo yalikuwa yanapotea mikono mwa wachache,ujenzi wa Kiwanda cha kucahata mazao jamii ya mikunde ambacho ni pekee kwa Tanzania Nzima,pia kujengwa kwa kiwanda Kikubwa cha sukari cha Mkulazi kutafungua fursa kubwa ya ajira kwa wakazi wa jimbo hilo na maeneo mengine.
Ujenzi wa Hospital ya Wilaya,na kuhamishwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mogororo kwenda Mvua yote hayo ni moja ya mafanikio amabyo yamepatikana katika serikali ya awamu ya Tano
 


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger