Thursday, 14 May 2020

Jeshi La Polisi Dodoma Lakamata Magari 6 Ya Wizi......latangaza Dau La Milioni Moja Kwa Mtu Atakayesaidia Kutoa Taarifa Za Wizi Wa Magari

...
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linayashikilia magari sita  yanayodhaniwa kuwa ya wizi .

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Mei,14,2020 jijini Dodoma Kamanda wa Polisi mkoani hapa SACP Gilles Muroto amesema  mnamo tarehe 10/05/2020 majira ya saa 10  kijiji cha Mbande  ,kata ya Sejeli ,wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma   barabara kuu ya Morogoro –Dodoma , lilikamatwa gari Na.T.936 Toyota Land Cruiser VX Rangi nyeupe ,Chassis Na.HDJ800003615 na Engine Na.1HZ80-0019603.

Kamanda Muroto amebainisha kuwa katika uchunguzi wa awali gari limegundulika kutofautiana na taarifa zilizopo kwenye kadi inayoonesha Chassis Na.HZJ800019603  na Engine Namba 0111948  tofauti kabisa na uhalisia  na kutiliwa mashaka kuwa ni mali ya wizi.

Dereva Ramadhan Zaniel Sekiondo [31] mkazi wa Magomeni Mikumi Dar E s Salaam   alikuwa akilipeleka mkoani Tabora  kwa mtu asiyemfahamu akitokea Dar Es Salaam  baada ya kukabidhiwa na mtu asiyemfahamu  anayeishi  jiji Dar Es Salaam .

Katika tukio la pili Kamanda Muroto amefafanua kuwa mnamo  tarehe 11/5/2020 eneo la Area A  kata ya Kizota jijini Dodoma yalikamatwa magari mawili yaliyokuwa yamehifadhiwa kwa kufungiwa ndani ya nyumba yasiyo na Namba za usajili yakitumia Namba ya Chassis ambayo ni Toyota HARRIER Chassis Na.MCU310001691,Engine Na.1MZ1589700 na Toyota IST Chassis Na.NCP600209833 Engine Na.2MZ3578179.

Katika uchunguzi wa awali imegundulika kuwa hayana kumbukumbu zozote  na yaliingia nchini bila Uhalali huku  uchunguzi zaidi ukiendelea kwa kushirikiana na Interpol  na mtuhumiwa Omari Chilipachi [29] mkazi wa Sinza DSM anahojiwa na jeshi la Polisi.

Aidha,siku hiyohiyo,  Eneo la  Area A  Kata ya Kizota jijini hapa lilikamatwa gari aina ya Land Rover Discovery  lenye namba za usajili wanchi ya Afrika kusini  namba SJV576 GP  Chassis Na.SALLAAA135A339616 ambazo zinatofautiana na  zilizopo katika gari  049053121030305071757 ambalo halipo kwenye mfumo wa usajili wa magari  na mtuhumiwa Jamal Swalehe Rasidi [28] mkazi wa Area A anaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi.

Katika tukio jingine,Kamanda Muroto amesema mnamo tarehe 12/5/2020  eneo la Nzunguni jijini Dodoma lilikamatwa  gari aina ya Toyota Alphard lenye kadi Na.384 DMU lenye  Chassis Na. ANH100038956 Engine Na.2AZ1184313   ambapo katika uchunguzi wa awali ulibaniwa kuwa  chassis ANH100030547 na Engine ZNZ 0860988  halisi kwenye gari zinatofautiana na lililetwa Dodoma kwa matengenezo kutoka Mbeya  na Mtuhuiwa Gofrey Amos Sanga[37] mkazi wa Nzunguni anaendelea kuhojiwa.

Mnamo tarehe 13/5/2020  stand ya Daladala Sabasaba jijini Dodoma lilikamatwa gari  Na.T.589 BAD aina ya Toyota Hiace yenye  Chassis  LH1741000724,Engine  5L5091996  na baada ya ukaguzi wa awali liligundulika kutofautiana na namba halisi  ambazo ni chassis LH12330013812 na Engine 3L4538966.

Hata hivyo kamanda Muroto amesema wilayani Kondoa na Dodoma katika mwendelezo wa msako wa wezi wa pikipiki walikamatwa watuhumiwa wawili wa wizi wa pikipiki .

Pia,Kamanda Muroto amebainisha kuwa mnamo tarehe 13/5/2020  eneo la Medeli kata ya Tabuka Reli jijini Dodoma  alikamatwa Shaban Nyamhanga Wisandala [32] mkazi wa Medeli akijifanya afisa usalama wa taifa  na kuwatapeli watu  pamoja na kuwafanyia vitishio.

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limetoa dau la Tsh.milioni moja kwa mtu atakayesaidia kutoa taarifa ya wizi wa magari.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger