
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza Vyuo vyote vifunguliwe rasmi kuanzia Tarehe 01.06.2020
Rais Magufuli amesema hayo leo Alhamis Mei 21,2020 Ikulu Chamwino Dodoma wakati akiwaapisha viongozi aliowateua.
Pia amesema Vijana wanaosoma Form Six waliokuwa wanajiandaa kufanya mtihani wa Kumaliza kidato cha sita waanze masomo tarehe 01.06.2020.
Shule zingine za sekondari na msingi tujipe muda kidogo.
Michezo yote/Ligi zote nazo zifunguliwe Juni 1,2020.
Tarehe 27/28 Mei ,2020 ndege zote za watalii zianze kuingia Tanzania
0 comments:
Post a Comment