Saturday, 4 April 2020

WAZIRI MBARAWA ASEMA WATATUMIA WATAALAMU WA NDANI KUFUNGA PAMPU ZA MAJI IWAPO UGONJWA WA CORONA UTAENDELEA KUWEPO

...
 WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa akizungumza leo wakati wa ziara yake wilayani Pangani kushoto ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo
 WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa akizungumza mara baada ya kuangalia mradi wa maji Kijiji cha Ubangaa
 MKURUGENZI wa Bonde la Maji la Mto Pangani Segule Segule akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Pangani
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Pangani Seif Ally akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah katikati aliyekaa ni WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa

 MKURUGENZI wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akitolea ufafanuzi wakati wa ziara hiyo
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Pangani Seif Ally kushoto akimueleza jambo Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa wakati wa ziara hiyo katikati ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
 WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa katika akivuka kwenye kivuko Mto Pangani mara baada ya kumaliza ziara yake wilayani humo
 MKURUGENZI wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akivuka kivuko cha Mto Pangani leo wakati wa ziara hiyo
Mto Pangani kama unavyoonekana

WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa amesema miradi yote ya maji  ambayo pampu za kusukumia maji zimeletwa kutoka nje ya nchi lakini wataalamu wa kuzifunga wamekwama kutoka nchini Africa kusini kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona sasa watatumia wataalamu wa ndani kwa kibali.

Hatua hiyo inatajwa kwamba imekuwa ikikwamisha miradi mbalimbali ya maji kwa wananchi kutokana na wataalamu hao kushindwa kutoka kwenye nchi zao na kuja kuzifunga huku wananchi wakiendelea kukosa huduma hiyo muhimu.

Mbarawa aliyasema hayo leo wakati akihitimisha ziara yake kwenye wilaya za Pangani na Muheza ambapo alisema kwamba wakandarasi hao wataandikiwa barua huko ili watoe maelekezo na baadae watafutwe watu wengine wa kufanya kazi hiyo.

Alisema kwamba hawawezi kusema kwamba wanakaa kuwasubiri maana hawajui ugonjwa huo utaisha lini lakini lazima wawe na maamuzi mengine kwa kutumia wataalamu wa ndani kuweza kufunga pampu hizo ikiwemo makukabiliano kutoka kwa wataalamu hao.

Alisema kwamba hata kama wataalamu wangekuja wasingefunga pumpu hizo bali wangetoa maelekezo kwa wataalamu wa hapa nchini ndio wangeweaza kufanya kazi hiyo.

Aidha alisema wanachotaka kwa wakandarasi hao watoe kibali na maelekezo watu wafanye na hata ridhiki ya kazi wachukue ili kuweza kunusuru miradi isiendelee kukwama kutokana na uwepo wa ugonjwa huo.

“Naamini tukifanya hivyo miradi yote ya maji itakwenda na wananchi watapata huduma ya maji safi na salama kwa wakati na kuondokana na kero za kuifuata mbali”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba Corona ni ugonjwa umekuja lakini na dawa mojawapo ni maji hivyo ni wakati muafaka wizara ya maji wajitoe wafanye kazi kwa bidii kama walikuwa wanafanya kazi kwa spidi 80 sasa wanapaswa kwenda spidi 160 kutokana na hduuma yao kuhitajika kupita kiasi.

Hata hivyo Waziri Mbarawa alisema kwamba kwa wataalamu wa manunuzi nchini wizara ya maji imebaini kuwepo kwa changamoto kwao kutokana na kuzembea kufanya jambo kwa haraka.

“Utakuta jambo ni la kufanya miezi miwili anachukia miezio sita mfano mzuri ni hapa fedha ilikuja Novemba mpaka leo Aprili mabomba hayajafika wakati kuna baadhi ya mikoa Mbeya, Iringa na meeneo mengine kazi zipo asilimia 70 matenki yapo nusu”Alisema Waziri huyo.

Alisema lakini mkoani Tanga mpaka leo hawajafanya chochote sasa hao watu wa namna hiyo ataendelea kuwahamisha na kupelekea mwengine na wakishindwa kujirekebisha wataondoilewa kabisa.

Awali akizungumza wakati akitoa taarifa ya mradi wa maji Kijiji cha Ubangaa na Mkwajuni Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini wilaya ya Pangani (Ruwasa) Mhandisi Sande Batakanwa alimueleza Waziri Mbarawa kwamba changamoto kubwa kwa kuanzia ilikuwa ni uhitaji wa pampu,moto na Transfoma iliyoondolewa na Tanesco baada ya mradi kusimama.

Alisema kwamba kwa uhitaji huo kama pampu,mota na transfoma iliyoondolewa na Tanesco vingepatikana na wananchi wangeanza kupata huduma kama awali .


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger