Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kimesema kuwa Mkutano mkuu wa chama hicho utakaofanyika Mei 9 mwaka huu hautapitisha mgombea yeyote wa Urais kupitia chama hicho na badala yake kitampitisha Mgombea wa Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt.John Pombe Magufuli.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Chama hicho Agustino Latonga Mrema amesema kuwa jina Mgombea Urais lilishapitishwa na Halmashauri Kuu Chama na kilichobaki ni kudhibitisha jina la Mgombea huyo.
Amesema kuwa katika uchaguzi mkuu hakuna haja ya kuweka Mgombea wa Urais kutokana na Rais aliyopo kukidhi mahitaji ya watanzania.
Amesema vyama vingine vijifunze toka kwa Rais Magufuli namna Tanzania ilivyopata Maendeleo kwa kipindi kifupi ikiwamo kukomesha Rushwa.
0 comments:
Post a Comment