Wednesday, 11 March 2020

Mgonjwa wa pili Apona Virusi Vya UKIMWI

...
Kwa mara ya pili katika historia , mgonjwa aliyekuwa na virusi vya ukimwi amepona kabisa mambukizi hayo, madaktari wamesema jana. 

Watafiti wa masuala ya afya nchini Uingereza wamethibitisha kuwa yule anayetambulika kama mgonjwa wa London, ambaye aliugua kutokana na virusi vinavyosababisha ukimwi, hana tena mambukizi hayo kwa muda wa miaka miwili sasa. 

Lakini wameonya dhidi ya kuzungumzia kuhusu dawa ya kuponya ugonjwa huo. 

Katika utafiti uliochapishwa na jarida la masuala ya afya la Lancet HIV, watafiti kutoka katika chuo kikuu cha Cambridge wamesema hakuna virusi vilivyopatikana kwa mgonjwa huyo karibu miaka miwili na nusu baada ya kufanyiwa matibabu ya uhamishaji wa seli . 

Castillejo amekuwa mtu wa pili kupona virusi vya HIV.

-DW


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger