Wednesday, 11 March 2020

CCM Waelekea Mahakamani Kumlipia Faini Dkt Vicent Mashinji...Alihukumiwa Jana Pamoja na Viongozi Wengine wa CHADEMA

...
Katibu wa itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole amewasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kufuata utaratibu, wa kulipa faini ya Sh milioni 30 ili kumnusuru DK Vicent Mashinji aliyetiwa hatiani jana.

Akizungumza katika viwanja vya mahakama akiwa ameambatana na wanachama wengine wa chama hicho pamoja na mke wa mfungwa huyo , Polepole amesema amefika kufuata utaratibu ili wamtoe Mashinji.

"Tunaishukuru CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wametusaidia tangu jana mpaka saa 4:00 usiku, tulikuwa tumekusanya kiasi chote kilichokuwa kinahitajika mahakamani ili kumnusuru ndugu yetu Mashinji, sisi hatuna mashaka na yeye na wala hatutomshikia bango kwamba tulimchangia na hata akiondoka wiki ijayo hatutohuzunika.

“Tayari tumeshapewa control namba, tunaenda kulipa kisha tutarudi Mahakama ya Kisutu ili tupewe utaratibu wa kwenda kumtoa gerezani,” amesema Polepole.

Dkt Vicent Mashinji pamoja na viongozi wengine wa CHADEMA, katika kesi yao ya uchochezi iliyokuwa ikiwakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jana walihukumiwa kulipa faini ama kwenda jela miezi mitano, ambapo faini ya Mashinji ni Milioni 30.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger