Tuesday, 17 December 2019

MAENEO YALIYOJAA MAJI HAYAPITIKI KUTOKANA NA MAFURIKO DAR MUDA HUU

...

Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam zimesababisha baadhi ya maeneo kutopitika kutoka na maji kujaa sehemu hizo

Baadhi ya maeneo ambayo hali ya barabara siku ya leo  Jumanne Desemba 17,2019 sio shwari.


1. Jangwani.. Kutokea fire kwenda Magomeni na magomeni kwenda fire. Imefungwa.

2. Jangwani kwa nyuma kutokea Kariakoo to kigogo imejaa Maji.

3. Umoja wa mataifa. Kutokea Almuntazir mpaka Muhimbili primary kumajaa Maji.

4. Scout upanga barabara ya malik pamejaa maji kuja junction ya Muhimbili

5. Barabara ya Fire hapa katika hospitali ya Regency pamejaa Maji

6. Kamata ktk barabara ya nyerere katika fly over ya treni pamejaa Maji

7. Kamata kutokea kariakoo kuja barabara ya nyerere pamejaa Maji.

8. Waterfront hapa kuja central police pamejaa Maji
  
9. Barabara ya Mwamnyange kuja main road ya barabara ya whitesand pamejaa Maji

10. Barabara ya Whitesand kuja round about ya whitesand  hali si shwari

11. Basihaya kuja Nyaishozi hali sio nzuri

12. Junction ya barabara ya gonna katika Mataa Maji yamejaa

13. Mbozi road Chang'ombe Maji  kuna maji ya kutosha

14. Junction ya hapa kwa sokota napo pamejaa Maji

15. Sinza Legho darajani hapa pamejaa maji pia

 16. karibu na ofisi za kiwango kuna daraja nalo limejaa maji ya kutosha litanata kutema kabisa, huko Mburahati, Kigogo ni mwendo wa mafuriko tuu maji yamejaa ndani, ukija hapo mkwajuni kwenye mto napo pamejaa maji yamepita mpaka barabara




Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger