Waziri mkuu za zamani, Edward Lowassa amesema Rais Magufuli akiongoza nchi kwa miaka 10 itapiga hatua kubwa katika maendeleo.
Lowassa ametoa kauli hiyo katika maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika mjini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba.
"Amani ndio msingi anaoutumia mheshimiwa Magufuli leo kuongoza nchi yetu, kuleta mshikamano na umoja, nampongeza amefanya kazi nzuri sana…kama akiachiwa akapiga miaka yake kumi…kumi mheshimiwa nchi hii itabadilika,” – Amesema Lowassa
Lowassa alikihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015 na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambako alipitishwa kugombea urais mwaka 2015 na kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Magufuli katika uchaguzi mkuu, lakini baadaye Machi Mosi, 2019, alirejea CCM.
0 comments:
Post a Comment